سَنَفۡرُغُ لَكُمۡ أَيُّهَ ٱلثَّقَلَانِ
Tutakukusudieni kukuhesabuni enyi aina mbili ya viumbe; majini na wanaadamu
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni zipi neema za Mola wenu mnazikanusha?
يَٰمَعۡشَرَ ٱلۡجِنِّ وَٱلۡإِنسِ إِنِ ٱسۡتَطَعۡتُمۡ أَن تَنفُذُواْ مِنۡ أَقۡطَارِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ فَٱنفُذُواْۚ لَا تَنفُذُونَ إِلَّا بِسُلۡطَٰنٖ
Enyi jamii ya Majini na Watu kama mtaweza kupenya kutoka pande za mbinguni na ardhini, basi penyeni hamtoweza kupenya ila kwa nguvu na uwezo. (mamlaka)
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni zipi neema za Mola wenu mnazikanusha?
يُرۡسَلُ عَلَيۡكُمَا شُوَاظٞ مِّن نَّارٖ وَنُحَاسٞ فَلَا تَنتَصِرَانِ
Mtapelekewa muwako wa moto juu yenu na shaba iliyoyeyushwa, basi hamtoweza kujinusuru
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni zipi neema za Mola wenu mnazikanusha?
فَإِذَا ٱنشَقَّتِ ٱلسَّمَآءُ فَكَانَتۡ وَرۡدَةٗ كَٱلدِّهَانِ
Zitakapo pasuka mbingu zikawa nyekundu kama mafuta
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni zipi neema za Mola wenu mnazikanusha?
فَيَوۡمَئِذٖ لَّا يُسۡـَٔلُ عَن ذَنۢبِهِۦٓ إِنسٞ وَلَا جَآنّٞ
Basi Siku hiyo hatoulizwa kuhusu dhambi yake Binadamu na wala Jini
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni zipi neema za Mola wenu mnazikanusha?
يُعۡرَفُ ٱلۡمُجۡرِمُونَ بِسِيمَٰهُمۡ فَيُؤۡخَذُ بِٱلنَّوَٰصِي وَٱلۡأَقۡدَامِ
Watatambulikana wahalifu kwa alama zao, basi watachukuliwa kwa nywele za utosi na nyayo
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni zipi neema za Mola wenu mnazikanusha?
هَٰذِهِۦ جَهَنَّمُ ٱلَّتِي يُكَذِّبُ بِهَا ٱلۡمُجۡرِمُونَ
Huu hapa moto wa jahannamu ambao wanaukadhibisha Watu waovu
يَطُوفُونَ بَيۡنَهَا وَبَيۡنَ حَمِيمٍ ءَانٖ
Wataizunguka baina yake na baina ya maji yachemkayo yaliyo-fikia ukomo wa kutokota
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni zipi neema za Mola wenu mnazikanusha?
وَلِمَنۡ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِۦ جَنَّتَانِ
Na kwa mwenye kukhofu kusi-mamishwa mbele ya Mola wake atapata bustani mbili
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni zipi neema za Mola wenu mnazikanusha?
ذَوَاتَآ أَفۡنَانٖ
Zenye miti yenye matawi
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni zipi neema za Mola wenu mnazikanusha?
فِيهِمَا عَيۡنَانِ تَجۡرِيَانِ
Mna humo chemchemu mbili zinazopita
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni zipi neema za Mola wenu mnazikanusha?
فِيهِمَا مِن كُلِّ فَٰكِهَةٖ زَوۡجَانِ
Mna humo kila matunda ya aina mbili mbili
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni zipi neema za Mola wenu mnazikanusha?
مُتَّكِـِٔينَ عَلَىٰ فُرُشِۭ بَطَآئِنُهَا مِنۡ إِسۡتَبۡرَقٖۚ وَجَنَى ٱلۡجَنَّتَيۡنِ دَانٖ
Hali yakuwa wakiegemea kwenye matandiko mazito yaliyotengenezwa ndani yake kwa hariri nyepesi na matunda ya bustani hizo yapo karibu
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni zipi neema za Mola wenu mnazikanusha?
فِيهِنَّ قَٰصِرَٰتُ ٱلطَّرۡفِ لَمۡ يَطۡمِثۡهُنَّ إِنسٞ قَبۡلَهُمۡ وَلَا جَآنّٞ
Mna humo wanawake wenye staha wanaoinamisha macho, hawajaguswa na Mtu kabla yao wala Jini
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni zipi neema za Mola wenu mnazikanusha?
كَأَنَّهُنَّ ٱلۡيَاقُوتُ وَٱلۡمَرۡجَانُ
Kana kwamba hao wanawake ni yakuti na marijani
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni zipi neema za Mola wenu mnazikanusha?
هَلۡ جَزَآءُ ٱلۡإِحۡسَٰنِ إِلَّا ٱلۡإِحۡسَٰنُ
Haikua malipo ya wema ispokua wema