سوره: QAAF 

آيه : 31

وَأُزۡلِفَتِ ٱلۡجَنَّةُ لِلۡمُتَّقِينَ غَيۡرَ بَعِيدٍ

Na Pepo italetwa karibu kwa kwaajili ya Wacha Mungu, haitakuwa mbali



سوره: QAAF 

آيه : 32

هَٰذَا مَا تُوعَدُونَ لِكُلِّ أَوَّابٍ حَفِيظٖ

(Itasemwa): Haya ndiyo yale mliyoahidiwa kwa kila mwenye kurejea kwa Allah, kwa kutubia, mwenye kuhifadhi vyema (amri za Allah)



سوره: QAAF 

آيه : 33

مَّنۡ خَشِيَ ٱلرَّحۡمَٰنَ بِٱلۡغَيۡبِ وَجَآءَ بِقَلۡبٖ مُّنِيبٍ

Anayemuogopa Allah (Mwingi wa Rehema) hali yakuwa hamuoni akaja na moyo ulioelekea kwake



سوره: QAAF 

آيه : 34

ٱدۡخُلُوهَا بِسَلَٰمٖۖ ذَٰلِكَ يَوۡمُ ٱلۡخُلُودِ

Ingieni kwa amani hiyo ndiyo siku ya kukaa milele



سوره: QAAF 

آيه : 35

لَهُم مَّا يَشَآءُونَ فِيهَا وَلَدَيۡنَا مَزِيدٞ

Humo watakuwa na kila wanachokitaka na kwetu sisi kuna ziada. (ya kumuona Allah)



سوره: QAAF 

آيه : 36

وَكَمۡ أَهۡلَكۡنَا قَبۡلَهُم مِّن قَرۡنٍ هُمۡ أَشَدُّ مِنۡهُم بَطۡشٗا فَنَقَّبُواْ فِي ٱلۡبِلَٰدِ هَلۡ مِن مَّحِيصٍ

Na Watu wa karne ngapi Tumewaaangamiza kabla yao ambao walikuwa wenye nguvu zaidi kuliko wao. Basi walitangatanga sana katika nchi nyingi. Je, kuna mahali popote pa kukimbilia?



سوره: QAAF 

آيه : 37

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَذِكۡرَىٰ لِمَن كَانَ لَهُۥ قَلۡبٌ أَوۡ أَلۡقَى ٱلسَّمۡعَ وَهُوَ شَهِيدٞ

Hakika katika hayo kuna ukumbusho kwa mtu mwenye moyo au ametega sikio nae yupo anashuhudia



سوره: QAAF 

آيه : 38

وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ وَمَا مَسَّنَا مِن لُّغُوبٖ

Na kwa yakini Tumeumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake katika siku sita, na wala Hauku-tugusa uchovu wowote



سوره: QAAF 

آيه : 39

فَٱصۡبِرۡ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ قَبۡلَ طُلُوعِ ٱلشَّمۡسِ وَقَبۡلَ ٱلۡغُرُوبِ

Basi vumilia kwa hayo wanayoyasema na mtakase Mola wako kwa kumhimidi kabla kuchomoza jua na kabla ya kuchwa



سوره: QAAF 

آيه : 40

وَمِنَ ٱلَّيۡلِ فَسَبِّحۡهُ وَأَدۡبَٰرَ ٱلسُّجُودِ

Na katika majira ya usiku pia mtakase yeye na baada ya kusujudu



سوره: QAAF 

آيه : 41

وَٱسۡتَمِعۡ يَوۡمَ يُنَادِ ٱلۡمُنَادِ مِن مَّكَانٖ قَرِيبٖ

Na sikiliza kwa makini Siku atakayonadi mwenye kunadi kutoka mahali pa karibu



سوره: QAAF 

آيه : 42

يَوۡمَ يَسۡمَعُونَ ٱلصَّيۡحَةَ بِٱلۡحَقِّۚ ذَٰلِكَ يَوۡمُ ٱلۡخُرُوجِ

Siku watakayosikia ukelele kwa haki. Hiyo ndio Siku ya kutoka (makaburini na kufufuka)



سوره: QAAF 

آيه : 43

إِنَّا نَحۡنُ نُحۡيِۦ وَنُمِيتُ وَإِلَيۡنَا ٱلۡمَصِيرُ

Hakika sisi ndiyo tunaohuisha na tunafisha na kwetu sisi tu ndiyo marejeo



سوره: QAAF 

آيه : 44

يَوۡمَ تَشَقَّقُ ٱلۡأَرۡضُ عَنۡهُمۡ سِرَاعٗاۚ ذَٰلِكَ حَشۡرٌ عَلَيۡنَا يَسِيرٞ

Siku itakayowapasukia ardhi (watoke) haraka haraka. Huo ndio mkusanyo, ni mwepesi kabisa kwetu



سوره: QAAF 

آيه : 45

نَّحۡنُ أَعۡلَمُ بِمَا يَقُولُونَۖ وَمَآ أَنتَ عَلَيۡهِم بِجَبَّارٖۖ فَذَكِّرۡ بِٱلۡقُرۡءَانِ مَن يَخَافُ وَعِيدِ

Sisi tunayajua wanayoyasema na wewe hukuwa mwenye kuwatenza nguvu, basi wakumbushe kwa Qur’ani yeyote mwenye kuogopa onyo langu