وَٱلنَّـٰزِعَٰتِ غَرۡقٗا
Nina apa kwa [Malaika] wanaong’oa (roho) kwa nguvu
وَٱلنَّـٰشِطَٰتِ نَشۡطٗا
Na (kwa Malaika) wanaotoa (roho) kwa upole
وَٱلسَّـٰبِحَٰتِ سَبۡحٗا
Na ( kwa Malaika) wanaoogelea sana (katika anga kwa kupanda na kushuka wakitekeleza majukumu waliyopewa na Allah)
فَٱلسَّـٰبِقَٰتِ سَبۡقٗا
Kisha (Nina apa kwa Malaika) wenye kuongoza (katika kushidana wakati wa kutimiza wajibu wao)
فَٱلۡمُدَبِّرَٰتِ أَمۡرٗا
Kisha (Nina apa kwa Malaika) wenye kuendesha kila jambo (kwa maagizo ya Allah)
يَوۡمَ تَرۡجُفُ ٱلرَّاجِفَةُ
Siku kitakapotetemeka cha kutetemeka
تَتۡبَعُهَا ٱلرَّادِفَةُ
Na utafuatia mpulizo (mwingine wa pili wa baragumu)
قُلُوبٞ يَوۡمَئِذٖ وَاجِفَةٌ
Siku hiyo nyoyo zitapiga piga (mapigo ya haraka haraka kwa hofu)
أَبۡصَٰرُهَا خَٰشِعَةٞ
Macho yake yatainama chini
يَقُولُونَ أَءِنَّا لَمَرۡدُودُونَ فِي ٱلۡحَافِرَةِ
Wanasema: Je, hivi sisi kweli tutarudishwa kwenye hali ya kwanza?
أَءِذَا كُنَّا عِظَٰمٗا نَّخِرَةٗ
Je, hata tukiwa ni mifupa iliyosagika na kuoza?
قَالُواْ تِلۡكَ إِذٗا كَرَّةٌ خَاسِرَةٞ
Wanasema: Basi marejeo hayo, ni marejeo yenye hasara!
فَإِنَّمَا هِيَ زَجۡرَةٞ وَٰحِدَةٞ
Basi hakika huo ni ukelele mmoja tu
فَإِذَا هُم بِٱلسَّاهِرَةِ
Tahamaki hao watahudhurishwa kwenye ardhi ya mkusanyiko, (wakiwa macho baada ya kufa)
هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ مُوسَىٰٓ
Je, imekufikia habarii ya Mussa?
إِذۡ نَادَىٰهُ رَبُّهُۥ بِٱلۡوَادِ ٱلۡمُقَدَّسِ طُوًى
Mola wake alipo mwita katika bonde takatifu la Tuwaa, akamwambia;
ٱذۡهَبۡ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ
Nenda kwa Firauna, hakika yeye amepindukia mipaka
فَقُلۡ هَل لَّكَ إِلَىٰٓ أَن تَزَكَّىٰ
Umwambie: Je, unataka utakasike?
وَأَهۡدِيَكَ إِلَىٰ رَبِّكَ فَتَخۡشَىٰ
Na nikuongoze kwa Mola wako umuogope?
فَأَرَىٰهُ ٱلۡأٓيَةَ ٱلۡكُبۡرَىٰ
Basi akamuonyesha Ishara (muujiza) mkubwa kabisa
فَكَذَّبَ وَعَصَىٰ
Lakini aliikadhibisha na akaasi
ثُمَّ أَدۡبَرَ يَسۡعَىٰ
Kisha akageuka nyuma na kufanya juhudi, (ya kukanusha)
فَحَشَرَ فَنَادَىٰ
Akakusanya watu akatangaza
فَقَالَ أَنَا۠ رَبُّكُمُ ٱلۡأَعۡلَىٰ
Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mkuu kabisa
فَأَخَذَهُ ٱللَّهُ نَكَالَ ٱلۡأٓخِرَةِ وَٱلۡأُولَىٰٓ
Basi hapo Allah akamshika na kumuadhibu kwa adhabu ya mwisho na mwanzo.[1]
1- - Allah akampa adhabu kwa kauli yake ya mwisho, nayo ni vile kusema: “Mimi ndiye Mola wenu Mlezi aliye mkubwa kabisa. Na akampa adhabu kwa kauli yake ya mwanzo, nayo ni kumkadhibisha Musa”.
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبۡرَةٗ لِّمَن يَخۡشَىٰٓ
Hakika katika hayo bila shaka kuna funzo kwa yule anayeogopa
ءَأَنتُمۡ أَشَدُّ خَلۡقًا أَمِ ٱلسَّمَآءُۚ بَنَىٰهَا
Je! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga!
رَفَعَ سَمۡكَهَا فَسَوَّىٰهَا
Akainua kimo chake, na akaiten-geneza vizuri
وَأَغۡطَشَ لَيۡلَهَا وَأَخۡرَجَ ضُحَىٰهَا
Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake
وَٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ ذَٰلِكَ دَحَىٰهَآ
Na ardhi baada ya hayo Akai-tandaza