قُتِلَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡأُخۡدُودِ
Wameangamizwa watu wa mahandaki
Share :
ٱلنَّارِ ذَاتِ ٱلۡوَقُودِ
Yenye moto wenye kuni nyingi,
إِذۡ هُمۡ عَلَيۡهَا قُعُودٞ
Walipo kuwa wamekaa hapo,
وَهُمۡ عَلَىٰ مَا يَفۡعَلُونَ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ شُهُودٞ
Na wao ni mashahidi wa yale waliyo kuwa wakiwafanyia Waumini
وَمَا نَقَمُواْ مِنۡهُمۡ إِلَّآ أَن يُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَمِيدِ
Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Allah, Mwenye nguvu, Msifiwa,
ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدٌ
Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Allah ni shaahidi wa kila kitu
إِنَّ ٱلَّذِينَ فَتَنُواْ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ ثُمَّ لَمۡ يَتُوبُواْ فَلَهُمۡ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمۡ عَذَابُ ٱلۡحَرِيقِ
Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua
إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ لَهُمۡ جَنَّـٰتٞ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡكَبِيرُ
Hakika walio amini na wakatenda mema watapata Bustani zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa
إِنَّ بَطۡشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ
Hakika kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali
إِنَّهُۥ هُوَ يُبۡدِئُ وَيُعِيدُ
Yeye ndiye anaye anzisha na ndiye anaye rejesha tena,
وَهُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلۡوَدُودُ
Naye ni Mwenye kusamehe, Mwenye mapenzi,
ذُو ٱلۡعَرۡشِ ٱلۡمَجِيدُ
Mwenye Kiti cha Enzi,
فَعَّالٞ لِّمَا يُرِيدُ
Atendaye ayatakayo
هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلۡجُنُودِ
Je! Zimekufikia khabari za majeshi?
فِرۡعَوۡنَ وَثَمُودَ
Ya Firauni na Thamudi?
بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فِي تَكۡذِيبٖ
Lakini walio kufuru wamo katika kukadhibisha
وَٱللَّهُ مِن وَرَآئِهِم مُّحِيطُۢ
Na Allah nyuma yao amewazunguka
بَلۡ هُوَ قُرۡءَانٞ مَّجِيدٞ
Bali hii ni Qur’ani tukufu
فِي لَوۡحٖ مَّحۡفُوظِۭ
Katika Ubao Ulio Hifadhiwa
وَٱلسَّمَآءِ وَٱلطَّارِقِ
Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku!
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلطَّارِقُ
Na nini kitakacho kujuulisha ni nini hicho Kinachokuja usiku?
ٱلنَّجۡمُ ٱلثَّاقِبُ
Ni Nyota yenye mwanga mkali
إِن كُلُّ نَفۡسٖ لَّمَّا عَلَيۡهَا حَافِظٞ
Hapana nafsi ila inayo mwangalizi
فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَٰنُ مِمَّ خُلِقَ
Hebu na ajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani?
خُلِقَ مِن مَّآءٖ دَافِقٖ
Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa,
يَخۡرُجُ مِنۢ بَيۡنِ ٱلصُّلۡبِ وَٱلتَّرَآئِبِ
Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu
إِنَّهُۥ عَلَىٰ رَجۡعِهِۦ لَقَادِرٞ
Hakika Yeye ana uwezo wa kumrudisha
يَوۡمَ تُبۡلَى ٱلسَّرَآئِرُ
Siku zitakapo dhihirishwa siri
فَمَا لَهُۥ مِن قُوَّةٖ وَلَا نَاصِرٖ
Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi
وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلرَّجۡعِ
Naapa kwa mbingu yenye marejeo!