فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni zipi neema za Mola wenu mnazikanusha?
Share :
وَلِمَنۡ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِۦ جَنَّتَانِ
Na kwa mwenye kukhofu kusi-mamishwa mbele ya Mola wake atapata bustani mbili
ذَوَاتَآ أَفۡنَانٖ
Zenye miti yenye matawi
فِيهِمَا عَيۡنَانِ تَجۡرِيَانِ
Mna humo chemchemu mbili zinazopita
فِيهِمَا مِن كُلِّ فَٰكِهَةٖ زَوۡجَانِ
Mna humo kila matunda ya aina mbili mbili
مُتَّكِـِٔينَ عَلَىٰ فُرُشِۭ بَطَآئِنُهَا مِنۡ إِسۡتَبۡرَقٖۚ وَجَنَى ٱلۡجَنَّتَيۡنِ دَانٖ
Hali yakuwa wakiegemea kwenye matandiko mazito yaliyotengenezwa ndani yake kwa hariri nyepesi na matunda ya bustani hizo yapo karibu
فِيهِنَّ قَٰصِرَٰتُ ٱلطَّرۡفِ لَمۡ يَطۡمِثۡهُنَّ إِنسٞ قَبۡلَهُمۡ وَلَا جَآنّٞ
Mna humo wanawake wenye staha wanaoinamisha macho, hawajaguswa na Mtu kabla yao wala Jini
كَأَنَّهُنَّ ٱلۡيَاقُوتُ وَٱلۡمَرۡجَانُ
Kana kwamba hao wanawake ni yakuti na marijani
هَلۡ جَزَآءُ ٱلۡإِحۡسَٰنِ إِلَّا ٱلۡإِحۡسَٰنُ
Haikua malipo ya wema ispokua wema
وَمِن دُونِهِمَا جَنَّتَانِ
Na zaidi ya hizo mbili, ziko bustani mbili zingine
مُدۡهَآمَّتَانِ
Za rangi ya kijani iliyokoza
فِيهِمَا عَيۡنَانِ نَضَّاخَتَانِ
Mna humo chemchemu mbili zenye kububujika kwa nguvu mfululizo
فِيهِمَا فَٰكِهَةٞ وَنَخۡلٞ وَرُمَّانٞ
Mna humo matunda na mitende na makomamanga
فِيهِنَّ خَيۡرَٰتٌ حِسَانٞ
Mna humo wanawake wema wazuri
حُورٞ مَّقۡصُورَٰتٞ فِي ٱلۡخِيَامِ
weupe wakiwa na macho mapana waliotawishwa kwenye mahema
لَمۡ يَطۡمِثۡهُنَّ إِنسٞ قَبۡلَهُمۡ وَلَا جَآنّٞ
hawajaguswa na Mtu kabla yao wala Jini