ءَاخِذِينَ مَآ ءَاتَىٰهُمۡ رَبُّهُمۡۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَبۡلَ ذَٰلِكَ مُحۡسِنِينَ
Hali Wakichukua Yale Ambayo Aliyowapa Wao Bwana Wao Hakika Wao Walikua Kabla Ya Haya wakifanya mema
Share :
كَانُواْ قَلِيلٗا مِّنَ ٱلَّيۡلِ مَا يَهۡجَعُونَ
Walikuwa Sehemu Ndogo Ya Usiku Wanalala
وَبِٱلۡأَسۡحَارِ هُمۡ يَسۡتَغۡفِرُونَ
Na Usiku Wa Manane (Kabla ya Alfajiri) Wanafanya Istighifari
وَفِيٓ أَمۡوَٰلِهِمۡ حَقّٞ لِّلسَّآئِلِ وَٱلۡمَحۡرُومِ
Na Katika Mali Zao Kuna Fungu Kwa Ajili Ya Mwenye Kuomba Na Asiye omba
وَفِي ٱلۡأَرۡضِ ءَايَٰتٞ لِّلۡمُوقِنِينَ
Na Katika Ardhi Kuna Ishara Nyingi Kwa Walio Na Yakini
وَفِيٓ أَنفُسِكُمۡۚ أَفَلَا تُبۡصِرُونَ
Na Katika Nafsi Zenu Hivi Hamuoni?
وَفِي ٱلسَّمَآءِ رِزۡقُكُمۡ وَمَا تُوعَدُونَ
Na Katika Mbingu Rizki Yenu Na Yote Mnayoahidiwa
فَوَرَبِّ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ إِنَّهُۥ لَحَقّٞ مِّثۡلَ مَآ أَنَّكُمۡ تَنطِقُونَ
Naapa Kwa Bwana Wa Mbingu Na Ardhi Hakika Hilo Ni Haki Kama Ambavyo Nyinyi Mnavyotamka
هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ضَيۡفِ إِبۡرَٰهِيمَ ٱلۡمُكۡرَمِينَ
Je Imewafikia Habari Za Wageni Wa Ibrahimu Walio Wema (wanao heshimiwa?)
إِذۡ دَخَلُواْ عَلَيۡهِ فَقَالُواْ سَلَٰمٗاۖ قَالَ سَلَٰمٞ قَوۡمٞ مُّنكَرُونَ
Pale Walipoingia Kwake Wakasema Salama, Akasema Salama nyinyi ni Watu nisio kujueni
فَرَاغَ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ فَجَآءَ بِعِجۡلٖ سَمِينٖ
Akaenda Kwa Ahli Yake Na Akaja Na Nyama Ya Ndama Aliye nona
فَقَرَّبَهُۥٓ إِلَيۡهِمۡ قَالَ أَلَا تَأۡكُلُونَ
Akawakaribisha na akasema Mbona Hamli?
فَأَوۡجَسَ مِنۡهُمۡ خِيفَةٗۖ قَالُواْ لَا تَخَفۡۖ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَٰمٍ عَلِيمٖ
Akahisi Kuwaogopa katika Nafsi Yake Kuhusu Wao, Wakasema Usiogope Na Wakampa Bishara Kwa Kijana mwenye elimu
فَأَقۡبَلَتِ ٱمۡرَأَتُهُۥ فِي صَرَّةٖ فَصَكَّتۡ وَجۡهَهَا وَقَالَتۡ عَجُوزٌ عَقِيمٞ
Ndipo Mkewe akawaelekea na huku akisema Hali Ya kupiga Kelele Na Kujipigapiga Usoni (kwa kustaajabu) Na Akasema Kikongwe Tasa!!
قَالُواْ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡحَكِيمُ ٱلۡعَلِيمُ
Wakasema Hivyo Ndivyo Alivyosema Bwana Wako Hakika Yeye Ni Mwingi Wa Hekima Na Mjuzi