Surah: AN-FAL 

Ayah : 32

وَإِذۡ قَالُواْ ٱللَّهُمَّ إِن كَانَ هَٰذَا هُوَ ٱلۡحَقَّ مِنۡ عِندِكَ فَأَمۡطِرۡ عَلَيۡنَا حِجَارَةٗ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ أَوِ ٱئۡتِنَا بِعَذَابٍ أَلِيمٖ

Na (kumbuka) wakati (washirikina) waliposema: Ewe Allah, ikiwa ni kweli hii (Qur’an) inatoka kwako, basi tushushie (mvua ya) mawe kutoka mbinguni (kama ulivyowafanyia watu wa Nabii Luti) au tuletee adhabu (yoyote) inayoumiza sana



Surah: AN-FAL 

Ayah : 33

وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُعَذِّبَهُمۡ وَأَنتَ فِيهِمۡۚ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ مُعَذِّبَهُمۡ وَهُمۡ يَسۡتَغۡفِرُونَ

Na Allah hakuwa Mwenye kuwaadhibu (kuwaangamiza washirikina kama walivyoomba) ilhali nawe upo nao, na Allah si mwenye kuwaadhibu na ilhali wanaomba msamaha



Surah: AN-FAL 

Ayah : 34

وَمَا لَهُمۡ أَلَّا يُعَذِّبَهُمُ ٱللَّهُ وَهُمۡ يَصُدُّونَ عَنِ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ وَمَا كَانُوٓاْ أَوۡلِيَآءَهُۥٓۚ إِنۡ أَوۡلِيَآؤُهُۥٓ إِلَّا ٱلۡمُتَّقُونَ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ

Na (Washirikina) wana jambo gani (jema) hata Allah asiwaadhibu (asiwaangamize), na ilhali wanauwekea vikwazo Msikiti Mtukufu (kwa kuwazuia watu kwenda kutekeleza ibada) na wala wao hawakuwa waangalizi wake? Hawakuwa waangalizi wake ila wachaMungu tu, lakini wengi wao hawajui (kuwa hawana haki hiyo ya uangalizi wa Msikiti Mtukufu)



Surah: AN-FAL 

Ayah : 35

وَمَا كَانَ صَلَاتُهُمۡ عِندَ ٱلۡبَيۡتِ إِلَّا مُكَآءٗ وَتَصۡدِيَةٗۚ فَذُوقُواْ ٱلۡعَذَابَ بِمَا كُنتُمۡ تَكۡفُرُونَ

Na haikuwa (Swala) ibada yao kwenye Nyumba (Al Kaaba) ila ni kupiga miruzi na makofi tu. Basi (enyi Washirikina) onjeni adhabu (ya duniani kwa kupigwa kwenye vita vya Badri) (na adhabu ya huko Akhera inawangojeni) kwa vile mlivyokuwa mnakufuru



Surah: AN-FAL 

Ayah : 36

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يُنفِقُونَ أَمۡوَٰلَهُمۡ لِيَصُدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِۚ فَسَيُنفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيۡهِمۡ حَسۡرَةٗ ثُمَّ يُغۡلَبُونَۗ وَٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ إِلَىٰ جَهَنَّمَ يُحۡشَرُونَ

Hakika wale waliokufuru hutoa mali zao ili kuzuia (kuiwekea vikwazo) njia ya Allah (Uislamu usimakinike na watu wasiufuate). Basi watazitoa (mali zao hizo), kisha zitakuwa majuto kwao, kisha watashindwa. Na waliokufuru watakusanywa katika Jahanamu tu



Surah: AN-FAL 

Ayah : 37

لِيَمِيزَ ٱللَّهُ ٱلۡخَبِيثَ مِنَ ٱلطَّيِّبِ وَيَجۡعَلَ ٱلۡخَبِيثَ بَعۡضَهُۥ عَلَىٰ بَعۡضٖ فَيَرۡكُمَهُۥ جَمِيعٗا فَيَجۡعَلَهُۥ فِي جَهَنَّمَۚ أُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ

Allah (aliyafanya hayo) ili awapambanue waovu dhidi ya wema, na kuwaweka waovu juu ya waovu wengine warundikane wote pamoja, na kisha awatumbukize katika Jahanamu. Hao ndio waliohasirika (duniani na Akhera)



Surah: AN-FAL 

Ayah : 38

قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ إِن يَنتَهُواْ يُغۡفَرۡ لَهُم مَّا قَدۡ سَلَفَ وَإِن يَعُودُواْ فَقَدۡ مَضَتۡ سُنَّتُ ٱلۡأَوَّلِينَ

(Ewe Nabii Muhammad) Waambie waliokufuru kwamba: Iwapo watakoma (Washirikina, kuwafanyia uadui Waislamu na kuwapiga vita) watasamehewa yaliyokwishapita. Na wakirudi (kwenye maovu yao hayo) basi imekwishapita mifano (kama hii ya kuangamiza) kwa watu wa kale (nao wangoje kuangamizwa kama wenzao waliopita)



Surah: AN-FAL 

Ayah : 39

وَقَٰتِلُوهُمۡ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتۡنَةٞ وَيَكُونَ ٱلدِّينُ كُلُّهُۥ لِلَّهِۚ فَإِنِ ٱنتَهَوۡاْ فَإِنَّ ٱللَّهَ بِمَا يَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ

Na piganeni nao (Washirikina) mpaka fitina (mateso dhidi ya Waislamu) yasiwepo, na Dini yote iwe ya Allah. Basi wakiacha, hakika Allah anayaona wanayoyatenda



Surah: AN-FAL 

Ayah : 40

وَإِن تَوَلَّوۡاْ فَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ مَوۡلَىٰكُمۡۚ نِعۡمَ ٱلۡمَوۡلَىٰ وَنِعۡمَ ٱلنَّصِيرُ

Na kama wakigeuka (na kuamua kuendelea na uadui wao) basi jueni kwamba, Allah ndiye Mtetezi wenu. Mtetezi bora kabisa na Msaidizi bora kabisa ni yeye