وَجَآءَ فِرۡعَوۡنُ وَمَن قَبۡلَهُۥ وَٱلۡمُؤۡتَفِكَٰتُ بِٱلۡخَاطِئَةِ
Na Firauni na wale waliokuwepo kabla yake na (watu wa) miji iliyopinduliwa (chini juu kwa sababu ya madhambi yao) walikuja kufanya makosa pia
Share :
فَعَصَوۡاْ رَسُولَ رَبِّهِمۡ فَأَخَذَهُمۡ أَخۡذَةٗ رَّابِيَةً
Wakamuasi Mtume wa Mola wao Mlezi, ndipo Yeye (Allah) akawakamata (na kuwaadhibu) kwa mkamato wa nguvu sana
إِنَّا لَمَّا طَغَا ٱلۡمَآءُ حَمَلۡنَٰكُمۡ فِي ٱلۡجَارِيَةِ
Maji Yalipofurika Hakika Sisi Tuliwapandisheni Katika Merikebu
لِنَجۡعَلَهَا لَكُمۡ تَذۡكِرَةٗ وَتَعِيَهَآ أُذُنٞ وَٰعِيَةٞ
Ili tuifanye kuwa ni ukumbusho kwenu, na ibakie kumbukumbu katika sikio linalobakisha kumbukumbu
فَإِذَا نُفِخَ فِي ٱلصُّورِ نَفۡخَةٞ وَٰحِدَةٞ
Na litakapo pulizwa barugumu mpulizo mmoja tu,
وَحُمِلَتِ ٱلۡأَرۡضُ وَٱلۡجِبَالُ فَدُكَّتَا دَكَّةٗ وَٰحِدَةٗ
Na ardhi na majabali ikaondolewa kisha ika pondwa pondwa mpondo mmoja
فَيَوۡمَئِذٖ وَقَعَتِ ٱلۡوَاقِعَةُ
Basi siku hiyo ndio litatokea tukio la kutokea
وَٱنشَقَّتِ ٱلسَّمَآءُ فَهِيَ يَوۡمَئِذٖ وَاهِيَةٞ
Na mbingu zitapasuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu kabisa
وَٱلۡمَلَكُ عَلَىٰٓ أَرۡجَآئِهَاۚ وَيَحۡمِلُ عَرۡشَ رَبِّكَ فَوۡقَهُمۡ يَوۡمَئِذٖ ثَمَٰنِيَةٞ
Na Malaika Watakuwa Wame-simama Kandoni Mwake, Na Siku Hiyo Juu Yao Malaika Wanane Watakibeba Kiti Cha Enzi Cha Mola Wako
يَوۡمَئِذٖ تُعۡرَضُونَ لَا تَخۡفَىٰ مِنكُمۡ خَافِيَةٞ
Siku hiyo mtahudhurishwa - haitafichika kwenu siri yoyote yenu
فَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ فَيَقُولُ هَآؤُمُ ٱقۡرَءُواْ كِتَٰبِيَهۡ
Basi ama atakaye pewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema: Haya someni kitabu changu!
إِنِّي ظَنَنتُ أَنِّي مُلَٰقٍ حِسَابِيَهۡ
Hakika mimi niliyakinisha kuwa hakiki mimi ni mwenye kukutana na hesabu yangu!
فَهُوَ فِي عِيشَةٖ رَّاضِيَةٖ
Basi Yeye Atakuwa Katika Maisha Ya Raha
فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٖ
Katika Bustani (Pepo) Iliyo Juu,
قُطُوفُهَا دَانِيَةٞ
Vishada Vyake (vya matunda) Vitakuwa Karibu:
كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ هَنِيٓـَٔۢا بِمَآ أَسۡلَفۡتُمۡ فِي ٱلۡأَيَّامِ ٱلۡخَالِيَةِ
(Wataambiwa): Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyoyatanguliza katika siku nyingi zilizopita
وَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِشِمَالِهِۦ فَيَقُولُ يَٰلَيۡتَنِي لَمۡ أُوتَ كِتَٰبِيَهۡ
Na ama yule atakayepewa kitabu chake kushotoni mwake; atasema: Ee! Laiti nisingelipewa kitabu changu!
وَلَمۡ أَدۡرِ مَا حِسَابِيَهۡ
Wala nisingeli jua nini hesabu yangu
يَٰلَيۡتَهَا كَانَتِ ٱلۡقَاضِيَةَ
Ee! Laiti yangelikuwa (mauti) ndio kumalizika kwangu
مَآ أَغۡنَىٰ عَنِّي مَالِيَهۡۜ
Haikunifaa mali yangu
هَلَكَ عَنِّي سُلۡطَٰنِيَهۡ
Madaraka yangu yamenitoweka
خُذُوهُ فَغُلُّوهُ
(Ataambiwa): Mchukueni, na mfungeni pingu
ثُمَّ ٱلۡجَحِيمَ صَلُّوهُ
Kisha kwenye moto uwakao vikali mtupeni humo!
ثُمَّ فِي سِلۡسِلَةٖ ذَرۡعُهَا سَبۡعُونَ ذِرَاعٗا فَٱسۡلُكُوهُ
Mkamateni Na Mtieni Minyororo Shingoni Mwake,
إِنَّهُۥ كَانَ لَا يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ ٱلۡعَظِيمِ
Kwani huyo hakika alikuwa hamuamini Allah Mtukufu
وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ
Wala Hakuhimiza Juu Ya Kulisha Maskini
فَلَيۡسَ لَهُ ٱلۡيَوۡمَ هَٰهُنَا حَمِيمٞ
Basi Leo Hapa Hana Rafiki Mpenzi ( wa kumwonea uchungu)
وَلَا طَعَامٌ إِلَّا مِنۡ غِسۡلِينٖ
Na wala hana chakula isipokuwa maji ya usaha ya vidonda vilivyooshwa (vya watu wa motoni)
لَّا يَأۡكُلُهُۥٓ إِلَّا ٱلۡخَٰطِـُٔونَ
Hawakili chakula hicho isipokuwa wakosefu
فَلَآ أُقۡسِمُ بِمَا تُبۡصِرُونَ
Basi Naapa kwa yale mnayoyaona