Surah: ALMUNAAFIQUUN 

Ayah : 7

هُمُ ٱلَّذِينَ يَقُولُونَ لَا تُنفِقُواْ عَلَىٰ مَنۡ عِندَ رَسُولِ ٱللَّهِ حَتَّىٰ يَنفَضُّواْۗ وَلِلَّهِ خَزَآئِنُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَلَٰكِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ لَا يَفۡقَهُونَ

Wao ndio wale wasemao: Msitoe mali kwa ajili ya walioko kwa Mtume wa Allah mpaka waondokelee mbali. Na ni za Allah Pekee hazina za mbingu na ardhi, lakini wanafiki hawafahamu



Surah: ALMUNAAFIQUUN 

Ayah : 8

يَقُولُونَ لَئِن رَّجَعۡنَآ إِلَى ٱلۡمَدِينَةِ لَيُخۡرِجَنَّ ٱلۡأَعَزُّ مِنۡهَا ٱلۡأَذَلَّۚ وَلِلَّهِ ٱلۡعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِۦ وَلِلۡمُؤۡمِنِينَ وَلَٰكِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ لَا يَعۡلَمُونَ

Wanasema: Tutakaporudi Madinah, mwenye hadhi zaidi atamfukuza humo aliye dhalili. Na hali utukufu ni wa Allah na wa Mtume Wake na wa Waumini, lakini wanafiki hawajui



Surah: ALMUNAAFIQUUN 

Ayah : 9

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تُلۡهِكُمۡ أَمۡوَٰلُكُمۡ وَلَآ أَوۡلَٰدُكُمۡ عَن ذِكۡرِ ٱللَّهِۚ وَمَن يَفۡعَلۡ ذَٰلِكَ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ

Enyi mlio amini! Yasikusa-haulisheni mali zenu, wala watoto wenu, kumkumbuka Allah. Na wenye kufanya hayo ndio walio pata khasara



Surah: ALMUNAAFIQUUN 

Ayah : 10

وَأَنفِقُواْ مِن مَّا رَزَقۡنَٰكُم مِّن قَبۡلِ أَن يَأۡتِيَ أَحَدَكُمُ ٱلۡمَوۡتُ فَيَقُولَ رَبِّ لَوۡلَآ أَخَّرۡتَنِيٓ إِلَىٰٓ أَجَلٖ قَرِيبٖ فَأَصَّدَّقَ وَأَكُن مِّنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ

Na toeni katika tulicho kupeni kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti, tena hapo akasema: Ee Mola wangu! Naomba uniachilie angalau muda kidogo tu, ili nipate kutoa sadaka, na niwe katika watu wema?



Surah: ALMUNAAFIQUUN 

Ayah : 11

وَلَن يُؤَخِّرَ ٱللَّهُ نَفۡسًا إِذَا جَآءَ أَجَلُهَاۚ وَٱللَّهُ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ

Wala Allah hatoichelewesha nafsi yoyote ile (muda wake wa kufa) pale inapo fika ajali yake; na Allah anazo khabari za mnayo yatenda



Surah: ATTAGHAABUN 

Ayah : 1

يُسَبِّحُ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۖ لَهُ ٱلۡمُلۡكُ وَلَهُ ٱلۡحَمۡدُۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Vinamsabihi Allah (viumbe) vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Ni wake yeye tu ufalme na ni zake yeye tu sifa njema. Na Yeye ni Mwenye uwezawa kila kitu



Surah: ATTAGHAABUN 

Ayah : 2

هُوَ ٱلَّذِي خَلَقَكُمۡ فَمِنكُمۡ كَافِرٞ وَمِنكُم مُّؤۡمِنٞۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٌ

Yeye ndiye ambaye amekuumbeni. Basi miongoni mwenu yupo aliye kafiri na miongoni mwenu yupo aliye Muumini. Na Allah ni Mwenye kuyaona vyema myatendayo



Surah: ATTAGHAABUN 

Ayah : 3

خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّ وَصَوَّرَكُمۡ فَأَحۡسَنَ صُوَرَكُمۡۖ وَإِلَيۡهِ ٱلۡمَصِيرُ

Ameumba mbingu na ardhi kwa haki, na amekuumbeni katika sura, kisha akazifanya nzuri sura zenu, na marejeo ni kwake



Surah: ATTAGHAABUN 

Ayah : 4

يَعۡلَمُ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَيَعۡلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعۡلِنُونَۚ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ

Anajua yale yaliyomo mbinguni na ardhini, na anayajua yale mnayofanya kwa siri na mnayoyafanya hadharani. Na Allah ni Mjuzi sana wa yaliyomo vifuani



Surah: ATTAGHAABUN 

Ayah : 5

أَلَمۡ يَأۡتِكُمۡ نَبَؤُاْ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن قَبۡلُ فَذَاقُواْ وَبَالَ أَمۡرِهِمۡ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ

Je, haijakufikieni habari ya wale waliokufuru kabla wakaonja matokeo mabaya ya jambo lao (uovu wa ukafiri)? Na (bila ya shaka yoyote) watapata adhabu iumizayo sana



Surah: ATTAGHAABUN 

Ayah : 6

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُۥ كَانَت تَّأۡتِيهِمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَقَالُوٓاْ أَبَشَرٞ يَهۡدُونَنَا فَكَفَرُواْ وَتَوَلَّواْۖ وَّٱسۡتَغۡنَى ٱللَّهُۚ وَٱللَّهُ غَنِيٌّ حَمِيدٞ

Hayo ni kwa sababu ilikuwa wakiwafikia Mitume wao kwa hoja zilizo wazi, lakini walisema: Ah! Hivi binaadamu ndio watuongoze? Basi walikufuru na wakakengeuka; na Allah Akawa hana haja nao. Na Allah ni Mkwasi (si mhitaji), ni Mwenye kusifiwa



Surah: ATTAGHAABUN 

Ayah : 7

زَعَمَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَن لَّن يُبۡعَثُواْۚ قُلۡ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتُبۡعَثُنَّ ثُمَّ لَتُنَبَّؤُنَّ بِمَا عَمِلۡتُمۡۚ وَذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٞ

Waliokufuru wamedai kwamba hawatofufuliwa kamwe. Sema: Bali hapana! Naapa Kwa Mola wangu, bila shaka mtafufuliwa, kisha mtajulishwa Kwa yale mliyoyatenda, na hayo kwa Allah ni mepesi



Surah: ATTAGHAABUN 

Ayah : 8

فَـَٔامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَٱلنُّورِ ٱلَّذِيٓ أَنزَلۡنَاۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ

Basi muaminini Allah na Mtume Wake na Nuru (Qurani) Tuliyoiteremsha, na Allah anazo khabari za mnayo yatenda



Surah: ATTAGHAABUN 

Ayah : 9

يَوۡمَ يَجۡمَعُكُمۡ لِيَوۡمِ ٱلۡجَمۡعِۖ ذَٰلِكَ يَوۡمُ ٱلتَّغَابُنِۗ وَمَن يُؤۡمِنۢ بِٱللَّهِ وَيَعۡمَلۡ صَٰلِحٗا يُكَفِّرۡ عَنۡهُ سَيِّـَٔاتِهِۦ وَيُدۡخِلۡهُ جَنَّـٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ

Siku Atakayokukusanyeni kwaajili ya Siku ya mkusanyiko. Hiyo ndio Siku ya kupata na kukosa. Basi yeyote anayemuamini Allah na akatenda mema (Allah) Atamfutia maovu yake na Atamuingiza katika Mabustani yapitayo chini yake mito, watadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa



Surah: ATTAGHAABUN 

Ayah : 10

وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَآ أُوْلَـٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِ خَٰلِدِينَ فِيهَاۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ

Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Aya (na ishara, dalili) Zetu hao ndio watu wa motoni, watadumu humo milele. Na hayo ndiyo mafikio mabaya



Surah: ATTAGHAABUN 

Ayah : 11

مَآ أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۗ وَمَن يُؤۡمِنۢ بِٱللَّهِ يَهۡدِ قَلۡبَهُۥۚ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٞ

Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Allah. Na mwenye kumuamini Allah huuongoa moyo wake. Na Allah ni Mjuzi wa kila kitu



Surah: ATTAGHAABUN 

Ayah : 12

وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَۚ فَإِن تَوَلَّيۡتُمۡ فَإِنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ

Na mtiini Allah, na mt’iini Mtume. Mkigeuka, basi hakika juu ya Mtume wetu ni kufikisha (Ujumbe wake) kwa uwazi tu



Surah: ATTAGHAABUN 

Ayah : 13

ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ

Allah, hapana Mungu wa Kuabudiwa kwa haki ila Yeye tu. Na juu ya Allah pekee nawategemee Waumini



Surah: ATTAGHAABUN 

Ayah : 14

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِنَّ مِنۡ أَزۡوَٰجِكُمۡ وَأَوۡلَٰدِكُمۡ عَدُوّٗا لَّكُمۡ فَٱحۡذَرُوهُمۡۚ وَإِن تَعۡفُواْ وَتَصۡفَحُواْ وَتَغۡفِرُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ

Enyi walioamini! Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu ni maadui kwenu, basi tahadharini nao. Na mkisamehe na mkapuuza na mkayafutilia mbali, basi hakika Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu



Surah: ATTAGHAABUN 

Ayah : 15

إِنَّمَآ أَمۡوَٰلُكُمۡ وَأَوۡلَٰدُكُمۡ فِتۡنَةٞۚ وَٱللَّهُ عِندَهُۥٓ أَجۡرٌ عَظِيمٞ

Hakika Mali zenu na watoto wenu ni jaribio. Na Kwa Allah upo ujira mkubwa



Surah: ATTAGHAABUN 

Ayah : 16

فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ مَا ٱسۡتَطَعۡتُمۡ وَٱسۡمَعُواْ وَأَطِيعُواْ وَأَنفِقُواْ خَيۡرٗا لِّأَنفُسِكُمۡۗ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفۡسِهِۦ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ

Basi mcheni Allah muwezavyo, na sikilizeni; na tiini na toeni (kwa ajili ya Allah) itakuwa kheri kwa ajili ya nafsi zenu. Na yeyote anayeepushwa na ubakhili (tamaa ya uchu wa nafsi yake), basi hao ndio wenye kufaulu (kufanikiwa)



Surah: ATTAGHAABUN 

Ayah : 17

إِن تُقۡرِضُواْ ٱللَّهَ قَرۡضًا حَسَنٗا يُضَٰعِفۡهُ لَكُمۡ وَيَغۡفِرۡ لَكُمۡۚ وَٱللَّهُ شَكُورٌ حَلِيمٌ

Mkimkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mzuri, atakuzidishieni maradufu, na atakusameheni. Na Allah ni Mwenye kupokea shukurani, Mpole, (Mvumilivu)



Surah: ATTAGHAABUN 

Ayah : 18

عَٰلِمُ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Mwenye kujua ghaibi (siri) na dhahiri, Mwenye nguvu, Mwenye hekima



Surah: ATTWALAAQ 

Ayah : 1

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ إِذَا طَلَّقۡتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ وَأَحۡصُواْ ٱلۡعِدَّةَۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ رَبَّكُمۡۖ لَا تُخۡرِجُوهُنَّ مِنۢ بُيُوتِهِنَّ وَلَا يَخۡرُجۡنَ إِلَّآ أَن يَأۡتِينَ بِفَٰحِشَةٖ مُّبَيِّنَةٖۚ وَتِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ ٱللَّهِ فَقَدۡ ظَلَمَ نَفۡسَهُۥۚ لَا تَدۡرِي لَعَلَّ ٱللَّهَ يُحۡدِثُ بَعۡدَ ذَٰلِكَ أَمۡرٗا

Ee Nabii, mnapotaka kuwapa talaka wanawake (wake zenu), basi wapeni talaka (katika wakati wa Twahara) kwenda kwenye Eda zao.[1]. Na hesabuni barabara eda na mcheni Allah Mola wenu Mlezi. Msiwatoe katika nyumba zao, na wala wao wasitoke isipokuwa wakileta uchafu ulio wazi. Na hiyo ndio mipaka ya Allah. Na yeyote atakayevuka mipaka ya Allah basi kwa yakini amedhulumu nafsi yake. Hujui; huwenda Allah akaibua (akaleta) jambo (jingine) baada ya hayo


1- - (Yaani wakati wakiwa twahara kabla ya kuwaingilia)


Surah: ATTWALAAQ 

Ayah : 2

فَإِذَا بَلَغۡنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمۡسِكُوهُنَّ بِمَعۡرُوفٍ أَوۡ فَارِقُوهُنَّ بِمَعۡرُوفٖ وَأَشۡهِدُواْ ذَوَيۡ عَدۡلٖ مِّنكُمۡ وَأَقِيمُواْ ٱلشَّهَٰدَةَ لِلَّهِۚ ذَٰلِكُمۡ يُوعَظُ بِهِۦ مَن كَانَ يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۚ وَمَن يَتَّقِ ٱللَّهَ يَجۡعَل لَّهُۥ مَخۡرَجٗا

Na watakapokaribia kufikia muda wao, basi wazuieni kwa wema, au farikianeni nao kwa wema, na mshuhudishe mashahidi wawili wenye uadilifu miongoni mwenu, na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Allah. Hivyo ndivyo anavyo waidhiwa (anavyo agizwa) anaye mwamini Allah na Siku ya Mwisho. Na yeyote anayemcha Allah; humtengenezea njia ya kutokea (kwenye shida)



Surah: ATTWALAAQ 

Ayah : 3

وَيَرۡزُقۡهُ مِنۡ حَيۡثُ لَا يَحۡتَسِبُۚ وَمَن يَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِ فَهُوَ حَسۡبُهُۥٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ بَٰلِغُ أَمۡرِهِۦۚ قَدۡ جَعَلَ ٱللَّهُ لِكُلِّ شَيۡءٖ قَدۡرٗا

Na humruzuku kwa njia asiyo tazamia. Na anaye mtegemea Allah Yeye humtosha. Hakika Allah anatimiza amri yake. Hakika Allah Amejaalia kwa kila kitu na makadirio yake



Surah: ATTWALAAQ 

Ayah : 4

وَٱلَّـٰٓـِٔي يَئِسۡنَ مِنَ ٱلۡمَحِيضِ مِن نِّسَآئِكُمۡ إِنِ ٱرۡتَبۡتُمۡ فَعِدَّتُهُنَّ ثَلَٰثَةُ أَشۡهُرٖ وَٱلَّـٰٓـِٔي لَمۡ يَحِضۡنَۚ وَأُوْلَٰتُ ٱلۡأَحۡمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعۡنَ حَمۡلَهُنَّۚ وَمَن يَتَّقِ ٱللَّهَ يَجۡعَل لَّهُۥ مِنۡ أَمۡرِهِۦ يُسۡرٗا

Na wale wanawake ambao wanaokoma hedhi miongoni mwa wanawake wenu, mkiwa mna shaka, basi eda yao ni miezi mitatu, pamoja na wale wanawake wasiopata hedhi. Na wenye mimba muda wao (wa eda) watakapozaa mimba zao. Na yeyote anayemcha Allah Atamjaalia wepesi katika jambo lake



Surah: ATTWALAAQ 

Ayah : 5

ذَٰلِكَ أَمۡرُ ٱللَّهِ أَنزَلَهُۥٓ إِلَيۡكُمۡۚ وَمَن يَتَّقِ ٱللَّهَ يُكَفِّرۡ عَنۡهُ سَيِّـَٔاتِهِۦ وَيُعۡظِمۡ لَهُۥٓ أَجۡرًا

Hiyo ni amri ya Allah Amekuteremshieni; na yeyote anayemcha Allah, Atamfutia maovu yake, na atampa ujira ulio mkubwa



Surah: ATTWALAAQ 

Ayah : 6

أَسۡكِنُوهُنَّ مِنۡ حَيۡثُ سَكَنتُم مِّن وُجۡدِكُمۡ وَلَا تُضَآرُّوهُنَّ لِتُضَيِّقُواْ عَلَيۡهِنَّۚ وَإِن كُنَّ أُوْلَٰتِ حَمۡلٖ فَأَنفِقُواْ عَلَيۡهِنَّ حَتَّىٰ يَضَعۡنَ حَمۡلَهُنَّۚ فَإِنۡ أَرۡضَعۡنَ لَكُمۡ فَـَٔاتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ وَأۡتَمِرُواْ بَيۡنَكُم بِمَعۡرُوفٖۖ وَإِن تَعَاسَرۡتُمۡ فَسَتُرۡضِعُ لَهُۥٓ أُخۡرَىٰ

Wawekeni wanawake (mlio-wataliki) kwenye majumba mnayokaa nyinyi kwa kadiri ya kipato chenu, na wala msiwadhuru ili muwatie dhiki. Na wakiwa ni wenye mimba, basi wapeni matumizi mpaka wazae mimba zao. Na wakikunyonyesheeni (Watoto wenu), basi wapeni ujira wao. Na shaurianeni baina yenu kwa wema. Na mkiona uzito kati yenu, basi amnyonyeshee mwanamke mwingine



Surah: ATTWALAAQ 

Ayah : 7

لِيُنفِقۡ ذُو سَعَةٖ مِّن سَعَتِهِۦۖ وَمَن قُدِرَ عَلَيۡهِ رِزۡقُهُۥ فَلۡيُنفِقۡ مِمَّآ ءَاتَىٰهُ ٱللَّهُۚ لَا يُكَلِّفُ ٱللَّهُ نَفۡسًا إِلَّا مَآ ءَاتَىٰهَاۚ سَيَجۡعَلُ ٱللَّهُ بَعۡدَ عُسۡرٖ يُسۡرٗا

Ili mwenye wasaa agharimu kwa wasaa wake, na aliyebaniwa riziki yake, basi agharimie katika kile Alichompa Allah. Allah Hamkalifishi mtu yeyote yule isipokuwa kwa kile Alichompa. Allah Atajaalia baada ya ugumu kuwa wepesi