Surah: ATTAUBA 

Ayah : 123

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ قَٰتِلُواْ ٱلَّذِينَ يَلُونَكُم مِّنَ ٱلۡكُفَّارِ وَلۡيَجِدُواْ فِيكُمۡ غِلۡظَةٗۚ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلۡمُتَّقِينَ

Enyi mlioamini, piganeni na wale makafiri walio mbele yenu na wakute kwenu ukali (ujasiri na ushupavu). Na jueni ya kwamba Allah yupo pamoja na wachaMungu



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 124

وَإِذَا مَآ أُنزِلَتۡ سُورَةٞ فَمِنۡهُم مَّن يَقُولُ أَيُّكُمۡ زَادَتۡهُ هَٰذِهِۦٓ إِيمَٰنٗاۚ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ فَزَادَتۡهُمۡ إِيمَٰنٗا وَهُمۡ يَسۡتَبۡشِرُونَ

Na inapoteremshwa Sura wapo miongoni mwao wanaosema (kwa kebehi): Ni nani miongoni mwenu Sura hii imemzidishia Imani? Basi ama wale walioamini imewazidishia Imani, nao wanafurahia



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 125

وَأَمَّا ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ فَزَادَتۡهُمۡ رِجۡسًا إِلَىٰ رِجۡسِهِمۡ وَمَاتُواْ وَهُمۡ كَٰفِرُونَ

Na ama wale ambao nyoyoni mwao mna maradhi (ya unafiki), basi (Sura) imewazidishia uchafu (uovu) juu ya uchafu (uovu) wao; na wanakufa hali ya kuwa ni makafiri



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 126

أَوَلَا يَرَوۡنَ أَنَّهُمۡ يُفۡتَنُونَ فِي كُلِّ عَامٖ مَّرَّةً أَوۡ مَرَّتَيۡنِ ثُمَّ لَا يَتُوبُونَ وَلَا هُمۡ يَذَّكَّرُونَ

Je, hawaoni (wanafiki) ya kwamba wanatiwa mtihanini kila mwaka mara moja au mara mbili kisha hawatubu na hawakumbuki?



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 127

وَإِذَا مَآ أُنزِلَتۡ سُورَةٞ نَّظَرَ بَعۡضُهُمۡ إِلَىٰ بَعۡضٍ هَلۡ يَرَىٰكُم مِّنۡ أَحَدٖ ثُمَّ ٱنصَرَفُواْۚ صَرَفَ ٱللَّهُ قُلُوبَهُم بِأَنَّهُمۡ قَوۡمٞ لَّا يَفۡقَهُونَ

Na ikiteremshwa Sura wanata-zamana (wanakonyezana) wao kwa wao, (kana kwamba wanasema): Je, kuna mtu yeyote anayekuoneni (mkiamua kuondoka kwa Mtume)? Kisha huondoka (kwa Mtume kwa kuogopa aibu). Allah amezigeuza nyoyo zao kwa kuwa hao ni watu wasiofahamu



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 128

لَقَدۡ جَآءَكُمۡ رَسُولٞ مِّنۡ أَنفُسِكُمۡ عَزِيزٌ عَلَيۡهِ مَا عَنِتُّمۡ حَرِيصٌ عَلَيۡكُم بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ رَءُوفٞ رَّحِيمٞ

Kwa hakika kabisa, amekujieni Mtume anayetokana na nyinyi, kunamuumiza kutaabika kwenu, mwenye kukujalini sana (mwenye kuona mnafanikiwa) na kwa Waumini ni mpole sana, mwenye huruma sana



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 129

فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَقُلۡ حَسۡبِيَ ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ عَلَيۡهِ تَوَكَّلۡتُۖ وَهُوَ رَبُّ ٱلۡعَرۡشِ ٱلۡعَظِيمِ

Basi (wanafiki na washirikishaji) wakikengeuka (wakipinga), wewe sema: Allah ananitosheleza. Hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Yeye tu. Nimetegemea yeye tu, na Yeye tu ndiye Mola wa Arshi Tukufu



Surah: YUNUS 

Ayah : 1

الٓرۚ تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡحَكِيمِ

Alif laam raa. Hizo ni Aya za kitabu chenye hekima nyingi



Surah: YUNUS 

Ayah : 2

أَكَانَ لِلنَّاسِ عَجَبًا أَنۡ أَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ رَجُلٖ مِّنۡهُمۡ أَنۡ أَنذِرِ ٱلنَّاسَ وَبَشِّرِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَنَّ لَهُمۡ قَدَمَ صِدۡقٍ عِندَ رَبِّهِمۡۗ قَالَ ٱلۡكَٰفِرُونَ إِنَّ هَٰذَا لَسَٰحِرٞ مُّبِينٌ

Hivi, imekuwa ajabu kwa watu kwamba tumemshushia Wahyi (ufunuo) mtu miongoni mwao (na kumpa ujumbe kwamba): Waonye watu na wape bishara wale walioamini kwamba watakua na cheo cha juu kwa Mola wao? Makafiri walisema: “Hakika kabisa, huyu (Muhammad) ni Mchawi aliye dhahiri



Surah: YUNUS 

Ayah : 3

إِنَّ رَبَّكُمُ ٱللَّهُ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ يُدَبِّرُ ٱلۡأَمۡرَۖ مَا مِن شَفِيعٍ إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ إِذۡنِهِۦۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمۡ فَٱعۡبُدُوهُۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ

Hakika, Mola wenu Mlezi ni Allah ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha akalingana sawa juu ya Arshi, anaendesha mambo yote, hakuna muombezi yeyote (atakayekubaliwa uombezi wake) isipokuwa baada ya idhini yake tu. Huyo, kwenu nyie, ndiye Allah, Mola wenu mlezi, basi muabuduni. Hivi hamuonyeki?



Surah: YUNUS 

Ayah : 4

إِلَيۡهِ مَرۡجِعُكُمۡ جَمِيعٗاۖ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقًّاۚ إِنَّهُۥ يَبۡدَؤُاْ ٱلۡخَلۡقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥ لِيَجۡزِيَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ بِٱلۡقِسۡطِۚ وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَهُمۡ شَرَابٞ مِّنۡ حَمِيمٖ وَعَذَابٌ أَلِيمُۢ بِمَا كَانُواْ يَكۡفُرُونَ

Kwake tu ndio marejeo yenu nyote. Hii ni ahadi ya kweli ya Allah. Hakika yeye (Allah) anaanza kuumba kisha anarudisha (kuumba) ili awalipe kwa uadilifu wale walioamini na wakatenda mema. Na wale waliokufuru watapata kinywaji cha maji ya moto sana na adhabu iumizayo mno kwa sababu ya ukafiri waliokuwa wakiufanya



Surah: YUNUS 

Ayah : 5

هُوَ ٱلَّذِي جَعَلَ ٱلشَّمۡسَ ضِيَآءٗ وَٱلۡقَمَرَ نُورٗا وَقَدَّرَهُۥ مَنَازِلَ لِتَعۡلَمُواْ عَدَدَ ٱلسِّنِينَ وَٱلۡحِسَابَۚ مَا خَلَقَ ٱللَّهُ ذَٰلِكَ إِلَّا بِٱلۡحَقِّۚ يُفَصِّلُ ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ

Ni yeye ambaye amelifanya jua lenye kuangaza na mwezi kuwa na nuru na ameuwekea (mwezi) vituo ili (kwa kutumia mwezi) mjue idadi ya miaka na hesabu. Allah hakuviumba hivyo isipokuwa kwa haki tu, anazifafanua Aya (zake) kwa watu wanaojua



Surah: YUNUS 

Ayah : 6

إِنَّ فِي ٱخۡتِلَٰفِ ٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِ وَمَا خَلَقَ ٱللَّهُ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَتَّقُونَ

Hakika, katika kubadilishana kwa usiku na mchana na (katika vitu vingine) alivyoviumba Allah katika mbingu na ardhi kuna ishara (za wazi juu ya uwepo wake na uwezo wake) kwa watu wanao ogopa



Surah: YUNUS 

Ayah : 7

إِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يَرۡجُونَ لِقَآءَنَا وَرَضُواْ بِٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَٱطۡمَأَنُّواْ بِهَا وَٱلَّذِينَ هُمۡ عَنۡ ءَايَٰتِنَا غَٰفِلُونَ

Hakika, wale wasiotaraji kukutana nasi na wameridhika na maisha ya duniani na wamebweteka nayo, na wale ambao Aya zetu wameghafilika nazo,



Surah: YUNUS 

Ayah : 8

أُوْلَـٰٓئِكَ مَأۡوَىٰهُمُ ٱلنَّارُ بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ

Hao makazi yao ni motoni kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma



Surah: YUNUS 

Ayah : 9

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ يَهۡدِيهِمۡ رَبُّهُم بِإِيمَٰنِهِمۡۖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهِمُ ٱلۡأَنۡهَٰرُ فِي جَنَّـٰتِ ٱلنَّعِيمِ

Hakika, wale walioamini na wakatenda matendo mema, Mola wao Mlezi atawaongoza kwa imani yao (kwenda) kwenye pepo za neema mbali mbali ikipita mito mbele yao



Surah: YUNUS 

Ayah : 10

دَعۡوَىٰهُمۡ فِيهَا سُبۡحَٰنَكَ ٱللَّهُمَّ وَتَحِيَّتُهُمۡ فِيهَا سَلَٰمٞۚ وَءَاخِرُ دَعۡوَىٰهُمۡ أَنِ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Dua yao humo ni: “Utakatifu ni wako ewe Mola wetu Mlezi, na maamkizi yao humo (watasema): Amani (Assalaamu Alaykum), na mwisho Dua yao (watasema): Alhamdu Lillaahi Rabbil-aalamiin (Sifa zote njema anazistahiki Allah, Mola Mlezi wa walimwengu wote)



Surah: YUNUS 

Ayah : 11

۞وَلَوۡ يُعَجِّلُ ٱللَّهُ لِلنَّاسِ ٱلشَّرَّ ٱسۡتِعۡجَالَهُم بِٱلۡخَيۡرِ لَقُضِيَ إِلَيۡهِمۡ أَجَلُهُمۡۖ فَنَذَرُ ٱلَّذِينَ لَا يَرۡجُونَ لِقَآءَنَا فِي طُغۡيَٰنِهِمۡ يَعۡمَهُونَ

Na lau kama Allah angewaha-rakishia watu shari kama wao wanavyoharakisha kheri, bila shaka muda wao (wa kuishi) ungekatishwa (wangekuwa wameangamizwa zamani). Basi tunawaacha wale wasioamini kukutana nasi (Siku ya Kiyama) wakitangatanga katika upotevu wao



Surah: YUNUS 

Ayah : 12

وَإِذَا مَسَّ ٱلۡإِنسَٰنَ ٱلضُّرُّ دَعَانَا لِجَنۢبِهِۦٓ أَوۡ قَاعِدًا أَوۡ قَآئِمٗا فَلَمَّا كَشَفۡنَا عَنۡهُ ضُرَّهُۥ مَرَّ كَأَن لَّمۡ يَدۡعُنَآ إِلَىٰ ضُرّٖ مَّسَّهُۥۚ كَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلۡمُسۡرِفِينَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Na yanapomgusa (yanapompata) mtu madhara yoyote, anatuomba akiwa amelalia ubavu wake au akiwa amekaa au akiwa amesimama. Basi tunapo muondolea madhara yake hupita kana kwamba hakutuomba kutokana na madhara yaliyomgusa. Hivyo ndivyo wachupao mipaka walivyopambiwa yale waliyokuwa wakiyatenda



Surah: YUNUS 

Ayah : 13

وَلَقَدۡ أَهۡلَكۡنَا ٱلۡقُرُونَ مِن قَبۡلِكُمۡ لَمَّا ظَلَمُواْ وَجَآءَتۡهُمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ وَمَا كَانُواْ لِيُؤۡمِنُواْۚ كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡمُجۡرِمِينَ

Na kwa hakika kabisa, tuliangamiza (vizazi vya) karine nyingi kabla yenu pale walipofanya dhuluma, na walijiwa na Mitume wao kwa dalili za wazi na kamwe hawakuamini. Hivi ndivyo tunavyowalipa watu waovu



Surah: YUNUS 

Ayah : 14

ثُمَّ جَعَلۡنَٰكُمۡ خَلَـٰٓئِفَ فِي ٱلۡأَرۡضِ مِنۢ بَعۡدِهِمۡ لِنَنظُرَ كَيۡفَ تَعۡمَلُونَ

Kisha tumekufanyeni warithi (mnaopishana; wakiondoka hawa wanakuja wengine) ardhini baada yao, ili tuone jinsi mtakavyofanya



Surah: YUNUS 

Ayah : 15

وَإِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡ ءَايَاتُنَا بَيِّنَٰتٖ قَالَ ٱلَّذِينَ لَا يَرۡجُونَ لِقَآءَنَا ٱئۡتِ بِقُرۡءَانٍ غَيۡرِ هَٰذَآ أَوۡ بَدِّلۡهُۚ قُلۡ مَا يَكُونُ لِيٓ أَنۡ أُبَدِّلَهُۥ مِن تِلۡقَآيِٕ نَفۡسِيٓۖ إِنۡ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰٓ إِلَيَّۖ إِنِّيٓ أَخَافُ إِنۡ عَصَيۡتُ رَبِّي عَذَابَ يَوۡمٍ عَظِيمٖ

Na wakati wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, wale wasiotaraji (wasioamini) kukutana nasi wana-sema: “lete Qur’ani (nyingine) isiyokuwa hii au ibadilishe. Sema: “Haiwezekani kwangu kuibadili kwa utashi wangu. Sifuati isipokuwa tu yanayofunuliwa kwangu. Hakika mimi naogopa adhabu ya Siku iliyo kubwa sana ikiwa nitamuasi Mola wangu Mlezi



Surah: YUNUS 

Ayah : 16

قُل لَّوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا تَلَوۡتُهُۥ عَلَيۡكُمۡ وَلَآ أَدۡرَىٰكُم بِهِۦۖ فَقَدۡ لَبِثۡتُ فِيكُمۡ عُمُرٗا مِّن قَبۡلِهِۦٓۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ

Sema: Lau kama Allah angetaka nisingekusomeeni (hii Qur’ani), na (Allah) asingekujulisheni (kuwa hiyo Qur’ani ni haki), kwa sababu bila ya shaka yoyote nimekaa nanyi umri mwingi kabla yake (kabla ya kuletewa hii Qur’ani na wala sikukuambieni kuwa mimi nimeleta Qur’ani). Je, hamtumii akili?



Surah: YUNUS 

Ayah : 17

فَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوۡ كَذَّبَ بِـَٔايَٰتِهِۦٓۚ إِنَّهُۥ لَا يُفۡلِحُ ٱلۡمُجۡرِمُونَ

Basi ni nani aliye dhalimu (zaidi katika kuzua uongo) kuliko yule amtungiaye uongo Allah au anayekadhibisha Aya zake? Hakika, ilivyo ni kwamba watu waovu hawafaulu



Surah: YUNUS 

Ayah : 18

وَيَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَضُرُّهُمۡ وَلَا يَنفَعُهُمۡ وَيَقُولُونَ هَـٰٓؤُلَآءِ شُفَعَـٰٓؤُنَا عِندَ ٱللَّهِۚ قُلۡ أَتُنَبِّـُٔونَ ٱللَّهَ بِمَا لَا يَعۡلَمُ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَلَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ سُبۡحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ

Na wanaabudu badala ya Allah vitu visivyo wadhuru wala kuwanufaisha na wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allah”. Sema: Hivi mnamwambia Allah mambo asiyoyajua mbinguni na ardhini[1]? Utakasifu ni wake (Allah) na ametukuka na yuko mbali na vyote wanavyovishirikisha naye


1- - Allah hapa anamuamuru Mtume wake Muhammad, Allah amshushie rehema na amani, awaambie hawa makafiri washirikishaji kwamba: Allah Mtukufu ndiye mmiliki wa mbingu na ardhi hakifichikani kwake chochote humo. Hivi wanamfundisha na kumueleza vitu visivyokuwepo humo.


Surah: YUNUS 

Ayah : 19

وَمَا كَانَ ٱلنَّاسُ إِلَّآ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗ فَٱخۡتَلَفُواْۚ وَلَوۡلَا كَلِمَةٞ سَبَقَتۡ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيۡنَهُمۡ فِيمَا فِيهِ يَخۡتَلِفُونَ

Na hawakuwa watu isipokuwa ni Umma mmoja tu, basi wakatofautiana.[1] Na lau kama sio neno lililotangulia[2] kutoka kwa Mola wako Mlezi bila shaka wangekwisha hukumiwa kati yao katika yale wanayo tofautiana humo


1- - Aya hapa inaeleza kuwa binadamu wote walikuwa kitu kimoja wakiwa katika dini moja. Lakini baadae walitofautiana na baadhi yao kupotoka ndio Allah akatuma Mitume ili kuwarudisha katika dini sahihi.


2- - Neno lililokusudiwa hapa ni ule uamuzi wa Allah wa kutowahukumu watu hapa duniani kwa dhambi wanazofanya kama ilivyokuwa kwa mataifa yaliyopita. Amewapa muda hadi Siku ya Kiama. Uamuzi huu umetajwa katika Aya ya 14 ya Sura Ash-shuuraa (42).


Surah: YUNUS 

Ayah : 20

وَيَقُولُونَ لَوۡلَآ أُنزِلَ عَلَيۡهِ ءَايَةٞ مِّن رَّبِّهِۦۖ فَقُلۡ إِنَّمَا ٱلۡغَيۡبُ لِلَّهِ فَٱنتَظِرُوٓاْ إِنِّي مَعَكُم مِّنَ ٱلۡمُنتَظِرِينَ

Na wanasema: Si ingekuwa vyema lau kama angeteremshiwa Aya (muujiza) kutoka kwa Mola wake Mlezi? Sema: Mambo ya Ghaibu ni ya Allah tu. Basi subirini, hakika mimi pamoja nanyi ni miongoni mwa wenye kusubiri



Surah: YUNUS 

Ayah : 21

وَإِذَآ أَذَقۡنَا ٱلنَّاسَ رَحۡمَةٗ مِّنۢ بَعۡدِ ضَرَّآءَ مَسَّتۡهُمۡ إِذَا لَهُم مَّكۡرٞ فِيٓ ءَايَاتِنَاۚ قُلِ ٱللَّهُ أَسۡرَعُ مَكۡرًاۚ إِنَّ رُسُلَنَا يَكۡتُبُونَ مَا تَمۡكُرُونَ

Na tunapowaonjesha watu rehema yoyote baada ya shida iliyowagusa, ghafla huanza kufanya vitimbi katika Aya zetu. Sema: Allah ni mwepesi zaidi wa (kutengua hila na vitimbi). Hakika, wajumbe wetu (Malaika waandishi) wanaandika vitimbi mnavyovifanya



Surah: YUNUS 

Ayah : 22

هُوَ ٱلَّذِي يُسَيِّرُكُمۡ فِي ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِۖ حَتَّىٰٓ إِذَا كُنتُمۡ فِي ٱلۡفُلۡكِ وَجَرَيۡنَ بِهِم بِرِيحٖ طَيِّبَةٖ وَفَرِحُواْ بِهَا جَآءَتۡهَا رِيحٌ عَاصِفٞ وَجَآءَهُمُ ٱلۡمَوۡجُ مِن كُلِّ مَكَانٖ وَظَنُّوٓاْ أَنَّهُمۡ أُحِيطَ بِهِمۡ دَعَوُاْ ٱللَّهَ مُخۡلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ لَئِنۡ أَنجَيۡتَنَا مِنۡ هَٰذِهِۦ لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلشَّـٰكِرِينَ

Yeye (Allah) ndiye anaye-kuendesheni bara na baharini, mpaka mnapokuwa kwenye jahazi (mashua) na upepo mzuri ukatembea nao kwa kasi na wakaufurahia, upepo mkali uliijia jahazi hiyo na yakawapiga mawimbi kutoka kila upande, na wakadhani kuwa wamezingirwa, hapo walimuomba Allah wakim-takasia dini (utiifu wakisema kuwa, ewe Mola wetu Mlezi): “Kwa Yakini kabisa, endapo utatuokoa katika haya, bila shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru”



Surah: YUNUS 

Ayah : 23

فَلَمَّآ أَنجَىٰهُمۡ إِذَا هُمۡ يَبۡغُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّۗ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنَّمَا بَغۡيُكُمۡ عَلَىٰٓ أَنفُسِكُمۖ مَّتَٰعَ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۖ ثُمَّ إِلَيۡنَا مَرۡجِعُكُمۡ فَنُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Basi (Allah) alipowaokoa, ghafla wakawa wanafanya uovu katika ardhi bila ya haki. Enyi watu, hakika uasi wenu ni hasara kwenu; ni anasa (fupi) za maisha ya duniani. Kisha kwetu tu ndio marejeo yenu, kwa hiyo tutakuambieni yote mliyokuwa mkiyafanya