عَبَسَ وَتَوَلَّىٰٓ
Alikunja paji lake la uso na akageuka
Share :
أَن جَآءَهُ ٱلۡأَعۡمَىٰ
Kwasababu alimjia kipofu
وَمَا يُدۡرِيكَ لَعَلَّهُۥ يَزَّكَّىٰٓ
Na nini kitakachokujulisha; huwenda akatakasika?
أَوۡ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ ٱلذِّكۡرَىٰٓ
Au akawaidhika na yakamnufaisha mawaidha?
أَمَّا مَنِ ٱسۡتَغۡنَىٰ
Ama yule ajionaye amejitosheleza (hana haja na mawaidha)
فَأَنتَ لَهُۥ تَصَدَّىٰ
Basi wewe ndio unamgeukia na kushughulika naye?
وَمَا عَلَيۡكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ
Na si juu yako wewe asipotakasika
وَأَمَّا مَن جَآءَكَ يَسۡعَىٰ
Na ama yule aliyekujia kwa kukukimbilia
وَهُوَ يَخۡشَىٰ
Na huku akiogopa (adhabu ya Allah)
فَأَنتَ عَنۡهُ تَلَهَّىٰ
Basi ndio wewe unampuuza?
كَلَّآ إِنَّهَا تَذۡكِرَةٞ
Sivyo hivyo! Hakika, hii [Qurani] ni mawaidha
فَمَن شَآءَ ذَكَرَهُۥ
Basi anayetaka, akumbushike kwayo
فِي صُحُفٖ مُّكَرَّمَةٖ
Nayo hii Qur’ani imo katika kurasa zilizo tukuzwa
مَّرۡفُوعَةٖ مُّطَهَّرَةِۭ
Zilizo inuliwa, zilizo takaswa
بِأَيۡدِي سَفَرَةٖ
Katika mikono ya Malaika waandishi
كِرَامِۭ بَرَرَةٖ
Walio watukufu, walio wema
قُتِلَ ٱلۡإِنسَٰنُ مَآ أَكۡفَرَهُۥ
Amelaaniwa na Kuangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha? [Au ukafiri ulioje alionao?]
مِنۡ أَيِّ شَيۡءٍ خَلَقَهُۥ
Hivi hakumbuki! Kwa kitu gani amemuumba?
مِن نُّطۡفَةٍ خَلَقَهُۥ فَقَدَّرَهُۥ
Kutokana na tone la manii, Amemuumba, Akamkadiria, [Akamuwezesha]
ثُمَّ ٱلسَّبِيلَ يَسَّرَهُۥ
Kisha akamsahilishia njia
ثُمَّ أَمَاتَهُۥ فَأَقۡبَرَهُۥ
Kisha akamfisha, akamtia kaburini
ثُمَّ إِذَا شَآءَ أَنشَرَهُۥ
Kisha Atakapotaka, Atamfufua
كَلَّا لَمَّا يَقۡضِ مَآ أَمَرَهُۥ
Si hivyo! Hakutimiza Aliyomuamuru (Allah)
فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَٰنُ إِلَىٰ طَعَامِهِۦٓ
Basi atazame mwanaadam chakula chake
أَنَّا صَبَبۡنَا ٱلۡمَآءَ صَبّٗا
Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu
ثُمَّ شَقَقۡنَا ٱلۡأَرۡضَ شَقّٗا
Kisha Tukaipasua ardhi mipasuko
فَأَنۢبَتۡنَا فِيهَا حَبّٗا
Kisha tukaotesha humo nafaka mbali mbali
وَعِنَبٗا وَقَضۡبٗا
Na mizabibu na mimea ya mboga (ikatwayo ikamea tena)
وَزَيۡتُونٗا وَنَخۡلٗا
Na mizaituni na mitende
وَحَدَآئِقَ غُلۡبٗا
Na mabustani yaliyositawi na kusongamana miti yake