يَـٰٓأَيُّهَا ٱلۡمُدَّثِّرُ
Ewe mwenye kujigubika
Share :
قُمۡ فَأَنذِرۡ
Simama uonye
وَرَبَّكَ فَكَبِّرۡ
Na Mola wako Mlezi mtukuze
وَثِيَابَكَ فَطَهِّرۡ
Na nguo zako zisafishe
وَٱلرُّجۡزَ فَٱهۡجُرۡ
Na (mambo) machafu yahame (yaache)
وَلَا تَمۡنُن تَسۡتَكۡثِرُ
Wala usitoe (usifanye hisani) kwa kutaraji kuzidishiwa (kupata kingi Zaidi)
وَلِرَبِّكَ فَٱصۡبِرۡ
Na kwa ajili ya Mola wako tu kuwa na subira (kuwa mvumilivu)
فَإِذَا نُقِرَ فِي ٱلنَّاقُورِ
Basi litakapopulizwa baragumu (Tarumbeta)
فَذَٰلِكَ يَوۡمَئِذٖ يَوۡمٌ عَسِيرٌ
Basi siku hiyo itakuwa ni siku ngumu sana
عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ غَيۡرُ يَسِيرٖ
Kwa makafiri haitakuwa nyepesi
ذَرۡنِي وَمَنۡ خَلَقۡتُ وَحِيدٗا
Niache Mimi peke yangu na yule niliye muumba
وَجَعَلۡتُ لَهُۥ مَالٗا مَّمۡدُودٗا
Na nikamjaalia awe na mali nyingi
وَبَنِينَ شُهُودٗا
Na watoto wanao onekana
وَمَهَّدتُّ لَهُۥ تَمۡهِيدٗا
Na nikamtengenezea mambo vizuri kabisa
ثُمَّ يَطۡمَعُ أَنۡ أَزِيدَ
Kisha anatumai Nimuongezee!
كَلَّآۖ إِنَّهُۥ كَانَ لِأٓيَٰتِنَا عَنِيدٗا
Hasha! Kwani hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi (Na umpinzani) Aya zetu!
سَأُرۡهِقُهُۥ صَعُودًا
Nitamtesa kwa mateso yasio wezekana
إِنَّهُۥ فَكَّرَ وَقَدَّرَ
Kwani hakika yeye alifikiri na akapima
فَقُتِلَ كَيۡفَ قَدَّرَ
Basi ameangamia! Namna alivyo pima
ثُمَّ قُتِلَ كَيۡفَ قَدَّرَ
Tena ameangamia! Namna alivyo pima!
ثُمَّ نَظَرَ
Kisha akatazama
ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ
Kisha akakunja paji (la uso) na akafinya uso kwa ghadhabu
ثُمَّ أَدۡبَرَ وَٱسۡتَكۡبَرَ
Kisha akageuka nyuma, na akaipa kisogo haki, na akatakabari
فَقَالَ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٞ يُؤۡثَرُ
Na akasema: Hii (Qurani) si chochote ila ni uchawi ulio nukuliwa
إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا قَوۡلُ ٱلۡبَشَرِ
Hii si chochote isipokuwa ni kauli ya binadamu
سَأُصۡلِيهِ سَقَرَ
Nitamuingiza (na kumuunguza) kwenye Moto wa saqar
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا سَقَرُ
Na ni nini kitakujuulisha nini huo Moto wa Saqar?
لَا تُبۡقِي وَلَا تَذَرُ
Haubakishi wala hauachi, (kitu chochote)
لَوَّاحَةٞ لِّلۡبَشَرِ
Wenye kubabua vikali ngozi, (iwe nyeusi)
عَلَيۡهَا تِسۡعَةَ عَشَرَ
Juu yake wako (walinzi) kumi na tisa