Surah: AL-MULK 

Ayah : 1

تَبَٰرَكَ ٱلَّذِي بِيَدِهِ ٱلۡمُلۡكُ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Ametakasika (Allah) Ambaye ufalme umo mikononi Mwake yeye tu, Naye ni Muweza sana wa kila kitu



Surah: AL-MULK 

Ayah : 2

ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلۡمَوۡتَ وَٱلۡحَيَوٰةَ لِيَبۡلُوَكُمۡ أَيُّكُمۡ أَحۡسَنُ عَمَلٗاۚ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡغَفُورُ

Ambaye ameumba kifo na uhai ili akujaribuni; Ni nani miongoni mwenu mwenye kutenda (vitendo) vizuri zaidi? Na yeye (Allah) ndiye hasa Mwenye nguvu kubwa, Mwenye kusamehe sana



Surah: AL-MULK 

Ayah : 3

ٱلَّذِي خَلَقَ سَبۡعَ سَمَٰوَٰتٖ طِبَاقٗاۖ مَّا تَرَىٰ فِي خَلۡقِ ٱلرَّحۡمَٰنِ مِن تَفَٰوُتٖۖ فَٱرۡجِعِ ٱلۡبَصَرَ هَلۡ تَرَىٰ مِن فُطُورٖ

Ambaye ameumba mbingu saba zilizo tabaka tabaka. Huoni tofauti yoyote katika uumbaji wa Rahmani (Allah Mwingi wa rehema). Basi rudisha macho (uangalie uumbaji wa Allah); Je, unaona kasoro yoyote?



Surah: AL-MULK 

Ayah : 4

ثُمَّ ٱرۡجِعِ ٱلۡبَصَرَ كَرَّتَيۡنِ يَنقَلِبۡ إِلَيۡكَ ٱلۡبَصَرُ خَاسِئٗا وَهُوَ حَسِيرٞ

Halafu rudisha tena macho mara mbili (ili uhakikishe), macho yako yatakurudia yakiwa yametahayari na kunyong’onyea sana



Surah: AL-MULK 

Ayah : 5

وَلَقَدۡ زَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنۡيَا بِمَصَٰبِيحَ وَجَعَلۡنَٰهَا رُجُومٗا لِّلشَّيَٰطِينِۖ وَأَعۡتَدۡنَا لَهُمۡ عَذَابَ ٱلسَّعِيرِ

Na kwa hakika, tumeipamba mbingu ya karibu kwa mataa (nyota), na tumeyafanya ili kuwapigia mashetani, na tumewaandalia (hao mashetani) adhabu ya Moto uwakao kwa nguvu



Surah: AL-MULK 

Ayah : 6

وَلِلَّذِينَ كَفَرُواْ بِرَبِّهِمۡ عَذَابُ جَهَنَّمَۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ

Na kwa walio mkufuru Mola wao Mlezi ipo adhabu ya Jahanamu. Na ni marejeo maovu yalioje hayo!



Surah: AL-MULK 

Ayah : 7

إِذَآ أُلۡقُواْ فِيهَا سَمِعُواْ لَهَا شَهِيقٗا وَهِيَ تَفُورُ

Watakapotupwa humo watausikia mngurumo wake na huku inafoka



Surah: AL-MULK 

Ayah : 8

تَكَادُ تَمَيَّزُ مِنَ ٱلۡغَيۡظِۖ كُلَّمَآ أُلۡقِيَ فِيهَا فَوۡجٞ سَأَلَهُمۡ خَزَنَتُهَآ أَلَمۡ يَأۡتِكُمۡ نَذِيرٞ

Unakaribia kupasuka kwa hasira. Kila mara litakapotupwa humo kundi, walinzi wake watawauliza: Je, hakukufikieni muonyaji?



Surah: AL-MULK 

Ayah : 9

قَالُواْ بَلَىٰ قَدۡ جَآءَنَا نَذِيرٞ فَكَذَّبۡنَا وَقُلۡنَا مَا نَزَّلَ ٱللَّهُ مِن شَيۡءٍ إِنۡ أَنتُمۡ إِلَّا فِي ضَلَٰلٖ كَبِيرٖ

Watasema: Naam! Walitufikia waonyaji, lakini tuliwakadhibisha na tulisema: Allah hakuteremsha chochote. Nyinyi hammo Ila katika upotevu mkubwa tu



Surah: AL-MULK 

Ayah : 10

وَقَالُواْ لَوۡ كُنَّا نَسۡمَعُ أَوۡ نَعۡقِلُ مَا كُنَّا فِيٓ أَصۡحَٰبِ ٱلسَّعِيرِ

Na Watasema: Kama Tungalisikia Au Tungalikuwa Na Akili Hatungekuwa Katika Watu Wa Motoni



Surah: AL-MULK 

Ayah : 11

فَٱعۡتَرَفُواْ بِذَنۢبِهِمۡ فَسُحۡقٗا لِّأَصۡحَٰبِ ٱلسَّعِيرِ

Wakakiri dhambi zao. Basi kuangamia ni kwa watu wa Motoni!



Surah: AL-MULK 

Ayah : 12

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَخۡشَوۡنَ رَبَّهُم بِٱلۡغَيۡبِ لَهُم مَّغۡفِرَةٞ وَأَجۡرٞ كَبِيرٞ

Hakika wanao mwogopa Mola wao Mlezi kwa ghaibu, watapata msamaha na ujira mkubwa



Surah: AL-MULK 

Ayah : 13

وَأَسِرُّواْ قَوۡلَكُمۡ أَوِ ٱجۡهَرُواْ بِهِۦٓۖ إِنَّهُۥ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ

Na fanyeni siri kauli zenu, au zidhihirisheni, hakika Yeye ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani



Surah: AL-MULK 

Ayah : 14

أَلَا يَعۡلَمُ مَنۡ خَلَقَ وَهُوَ ٱللَّطِيفُ ٱلۡخَبِيرُ

Asijue aliyeumba, naye ndiye Mjua siri, au (Mwenye kuyaendesha mambo kwa upole), Mwenye khabari?



Surah: AL-MULK 

Ayah : 15

هُوَ ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلۡأَرۡضَ ذَلُولٗا فَٱمۡشُواْ فِي مَنَاكِبِهَا وَكُلُواْ مِن رِّزۡقِهِۦۖ وَإِلَيۡهِ ٱلنُّشُورُ

Yeye ndiye aliye idhalilisha ardhi kwa faida yenu, basi tembeeni katika pande zake, na kuleni katika riziki zake. Na kwake Yeye ndio kufufuliwa



Surah: AL-MULK 

Ayah : 16

ءَأَمِنتُم مَّن فِي ٱلسَّمَآءِ أَن يَخۡسِفَ بِكُمُ ٱلۡأَرۡضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ

Mnadhani mko salama kwa (Allah) alioko Mbinguni kuwa hatakudidimizeni kwenye ardhi, na tahamaki hiyo inatikisika!



Surah: AL-MULK 

Ayah : 17

أَمۡ أَمِنتُم مَّن فِي ٱلسَّمَآءِ أَن يُرۡسِلَ عَلَيۡكُمۡ حَاصِبٗاۖ فَسَتَعۡلَمُونَ كَيۡفَ نَذِيرِ

Au mnadhani mko katika amani na (Allah) Aliyeko mbinguni kwamba Hatokutumieni kimbunga chenye mawe ya changarawe? basi mtajua vipi maonyo Yangu



Surah: AL-MULK 

Ayah : 18

وَلَقَدۡ كَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ فَكَيۡفَ كَانَ نَكِيرِ

Na bila ya shaka walikwisha kanusha walio kuwa kabla yao; basi kulikuwaje kukasirika kwangu?



Surah: AL-MULK 

Ayah : 19

أَوَلَمۡ يَرَوۡاْ إِلَى ٱلطَّيۡرِ فَوۡقَهُمۡ صَـٰٓفَّـٰتٖ وَيَقۡبِضۡنَۚ مَا يُمۡسِكُهُنَّ إِلَّا ٱلرَّحۡمَٰنُۚ إِنَّهُۥ بِكُلِّ شَيۡءِۭ بَصِيرٌ

Je, hawawaoni ndege juu yao, wakiwa wakikunjua na kukunja (mbawa zao) hakuna anayewashikilia isipokuwa Allah mwingi wa Rehema, hakika Yeye ni Mwenye kuona kila kitu



Surah: AL-MULK 

Ayah : 20

أَمَّنۡ هَٰذَا ٱلَّذِي هُوَ جُندٞ لَّكُمۡ يَنصُرُكُم مِّن دُونِ ٱلرَّحۡمَٰنِۚ إِنِ ٱلۡكَٰفِرُونَ إِلَّا فِي غُرُورٍ

Au ni lipi hilo jeshi lenu linaloweza kukunusuruni badala ya (Allah) Mwingi wa Rehema? Makafiri hawamo isipokuwa katika udanganyifu



Surah: AL-MULK 

Ayah : 21

أَمَّنۡ هَٰذَا ٱلَّذِي يَرۡزُقُكُمۡ إِنۡ أَمۡسَكَ رِزۡقَهُۥۚ بَل لَّجُّواْ فِي عُتُوّٖ وَنُفُورٍ

Au ni nani huyo ambaye atakupeni riziki kama Yeye akizuia riziki yake? Bali wao wanaendelea (wanang’ang’ania) tu katika jeuri na chuki



Surah: AL-MULK 

Ayah : 22

أَفَمَن يَمۡشِي مُكِبًّا عَلَىٰ وَجۡهِهِۦٓ أَهۡدَىٰٓ أَمَّن يَمۡشِي سَوِيًّا عَلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

Je, anayekwenda kifudifudi kwa uso wake, ameongoka zaidi, au yule anayekwenda sawasawa kuelekea njia iliyonyooka?



Surah: AL-MULK 

Ayah : 23

قُلۡ هُوَ ٱلَّذِيٓ أَنشَأَكُمۡ وَجَعَلَ لَكُمُ ٱلسَّمۡعَ وَٱلۡأَبۡصَٰرَ وَٱلۡأَفۡـِٔدَةَۚ قَلِيلٗا مَّا تَشۡكُرُونَ

Sema: Yeye ndiye aliye kuumbeni tangu mwanzo, na akakupeni masikio na macho, na nyoyo. Ni kidogo kabisa shukrani zenu



Surah: AL-MULK 

Ayah : 24

قُلۡ هُوَ ٱلَّذِي ذَرَأَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَإِلَيۡهِ تُحۡشَرُونَ

Sema: Yeye Ndiye Yule Aliyekutawanyeni (Aliye waongozeni) kwenye ardhi, na Kwake mtakusanywa



Surah: AL-MULK 

Ayah : 25

وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَٰذَا ٱلۡوَعۡدُ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Na wanasema: Ni lini hiyo ahadi (ya kufufuliwa), mkiwa ni wasemao kweli?



Surah: AL-MULK 

Ayah : 26

قُلۡ إِنَّمَا ٱلۡعِلۡمُ عِندَ ٱللَّهِ وَإِنَّمَآ أَنَا۠ نَذِيرٞ مُّبِينٞ

Sema: Hakika ujuzi wake uko kwa Allah; na hakika mimi ni muonyaji tu mwenye kubainisha



Surah: AL-MULK 

Ayah : 27

فَلَمَّا رَأَوۡهُ زُلۡفَةٗ سِيٓـَٔتۡ وُجُوهُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَقِيلَ هَٰذَا ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تَدَّعُونَ

Basi watakapoiona (adhabu ya Kiyama) inakaribia, zitahuzunika nyuso za wale waliokufuru, na itasemwa: Hii ndio ambayo mliyokuwa mkiiomba



Surah: AL-MULK 

Ayah : 28

قُلۡ أَرَءَيۡتُمۡ إِنۡ أَهۡلَكَنِيَ ٱللَّهُ وَمَن مَّعِيَ أَوۡ رَحِمَنَا فَمَن يُجِيرُ ٱلۡكَٰفِرِينَ مِنۡ عَذَابٍ أَلِيمٖ

Sema Je, mnaonaje ikiwa Allah Ataniangamiza na walio pamoja nami, au Akiturehemu; basi ni nani atakaye wakinga makafiri na adhabu iumizayo?



Surah: AL-MULK 

Ayah : 29

قُلۡ هُوَ ٱلرَّحۡمَٰنُ ءَامَنَّا بِهِۦ وَعَلَيۡهِ تَوَكَّلۡنَاۖ فَسَتَعۡلَمُونَ مَنۡ هُوَ فِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٖ

Sema: Yeye Ndiye mwenye Huruma tumemwamini, na Kwake tunategemea, basi karibuni hivi mtakuja kujua ni nani ambaye yumo katika upotofu wa wazi



Surah: AL-MULK 

Ayah : 30

قُلۡ أَرَءَيۡتُمۡ إِنۡ أَصۡبَحَ مَآؤُكُمۡ غَوۡرٗا فَمَن يَأۡتِيكُم بِمَآءٖ مَّعِينِۭ

Sema: Niambieni, yakiwa maji yenu yamedidimia; basi ni nani atakayeweza kukuleteeni maji (ya chemchemu) yatiririkayo?