Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 1

سَبَّحَ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۖ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Vinamtakasa Allah (Pekee) vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi, Na yeye ndiye Mwenye nguvu kubwa, Mwenye hekima sana



Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 2

هُوَ ٱلَّذِيٓ أَخۡرَجَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ مِن دِيَٰرِهِمۡ لِأَوَّلِ ٱلۡحَشۡرِۚ مَا ظَنَنتُمۡ أَن يَخۡرُجُواْۖ وَظَنُّوٓاْ أَنَّهُم مَّانِعَتُهُمۡ حُصُونُهُم مِّنَ ٱللَّهِ فَأَتَىٰهُمُ ٱللَّهُ مِنۡ حَيۡثُ لَمۡ يَحۡتَسِبُواْۖ وَقَذَفَ فِي قُلُوبِهِمُ ٱلرُّعۡبَۚ يُخۡرِبُونَ بُيُوتَهُم بِأَيۡدِيهِمۡ وَأَيۡدِي ٱلۡمُؤۡمِنِينَ فَٱعۡتَبِرُواْ يَـٰٓأُوْلِي ٱلۡأَبۡصَٰرِ

Yeye Ndiye Aliyewatoa wale waliokufuru miongoni mwa waliopewa kitabu kutoka majumbani mwao wakati wa uhamisho wa kwanza. Nyinyi hamkudhani kwamba watatoka, na wao wakadhani kwamba ngome zao zitawakinga dhidi ya Allah. Lakini Allah akawafikia kwa namna ambayo hawakuitarajia, na akatia woga (kiwewe) katika nyoyo zao (wakawa) wanaziharibu nyumba zao kwa mikono yao na mikono ya Waumini. Basi zingatieni enyi wenye uoni wa kutia akilini



Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 3

وَلَوۡلَآ أَن كَتَبَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمُ ٱلۡجَلَآءَ لَعَذَّبَهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَاۖ وَلَهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ عَذَابُ ٱلنَّارِ

Na lau kama Allah Asingeliwaandikia kutoka, bila shaka Angeliwaadhibu duniani, na Akhira watapata adhabu ya moto



Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 4

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ شَآقُّواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥۖ وَمَن يُشَآقِّ ٱللَّهَ فَإِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ

Hivyo ni kwasababu wao wame-mpinga Allah na Mtume Wake. Na yeyote anayempinga Allah, basi hakika Allah ni Mkali wa kuadhibu



Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 5

مَا قَطَعۡتُم مِّن لِّينَةٍ أَوۡ تَرَكۡتُمُوهَا قَآئِمَةً عَلَىٰٓ أُصُولِهَا فَبِإِذۡنِ ٱللَّهِ وَلِيُخۡزِيَ ٱلۡفَٰسِقِينَ

Hamkukata aina yoyote ya mtende au mliouacha umesimama juu ya mashina yake, basi ni kwa idhini ya Allah na ili Awahizi (awadhalilishe) mafasiki



Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 6

وَمَآ أَفَآءَ ٱللَّهُ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ مِنۡهُمۡ فَمَآ أَوۡجَفۡتُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ خَيۡلٖ وَلَا رِكَابٖ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ يُسَلِّطُ رُسُلَهُۥ عَلَىٰ مَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Na ngawira yeyote ile Aliyoileta Allah Kwa Mtume Wake kutoka kwao; basi hamkuyaendea mbio Kwa farasi Na wala vipando vya ngamia. Lakini Allah Huwapa mamlaka na nguvu Mitume Wake dhidi ya Amtakaye. Na Allah juu ya kila kitu ni Muweza



Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 7

مَّآ أَفَآءَ ٱللَّهُ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡقُرَىٰ فَلِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينِ وَٱبۡنِ ٱلسَّبِيلِ كَيۡ لَا يَكُونَ دُولَةَۢ بَيۡنَ ٱلۡأَغۡنِيَآءِ مِنكُمۡۚ وَمَآ ءَاتَىٰكُمُ ٱلرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَىٰكُمۡ عَنۡهُ فَٱنتَهُواْۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۖ إِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ

Ngawira Aliyotoa Allah kwa Mtume Wake kutoka kwa watu wa hivi vijiji ni kwa ajili ya Allah na kwaajili ya Mtume na kwa ajili ya jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini na msafiri aliyeharibikiwa, ili isiwe yakizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu. Na lolote analokupeni Mtume basi lichukueni, na analokukatazeni, basi acheni. Na mcheni Allah. Hakika Allah ni Mkali wa kudhiabu



Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 8

لِلۡفُقَرَآءِ ٱلۡمُهَٰجِرِينَ ٱلَّذِينَ أُخۡرِجُواْ مِن دِيَٰرِهِمۡ وَأَمۡوَٰلِهِمۡ يَبۡتَغُونَ فَضۡلٗا مِّنَ ٱللَّهِ وَرِضۡوَٰنٗا وَيَنصُرُونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓۚ أُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلصَّـٰدِقُونَ

Wapewe (pia) mafakiri Waliohama ambao wametolewa (wamefukuzwa) kutoka majumbani mwao na mali zao kwa ajili ya kutafuta fadhila na radhi kutoka kwa Allah na wanainusuru (Dini ya) Allah na Mtume Wake hao ndio wa kweli.[1]


1- - Hapa wanatajwa Swahaba waliolazimishwa kuhama katika mji wa Makka. Walihama pamoja na Mtume huku wakiacha mali zao na kuwafanya kuwa maskini. Waliridhika kufanya hivyo ili kuinusuru dini ya Allah. Aya hii inawataja Swahaba hawa kuwa ni wakweli na waaminifu katika Imani yao. Aya hii na nyingine mbili baada ya hii ni hoja ya msingi wa itikadi ya Ahlisuna Waljmaa (Suni) katika kuwaheshimu Swahaba wakiongozwa na Abubakar, Umar, Uthman, Ali na wengine ambao wamehusika katika Aya hii kwa sababu walikuwa pamoja na Mtume kwenye harakati hizi za kuhama. Aya inawasifia kuwa ni wakweli, vipi mtu awatuhumu?


Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 9

وَٱلَّذِينَ تَبَوَّءُو ٱلدَّارَ وَٱلۡإِيمَٰنَ مِن قَبۡلِهِمۡ يُحِبُّونَ مَنۡ هَاجَرَ إِلَيۡهِمۡ وَلَا يَجِدُونَ فِي صُدُورِهِمۡ حَاجَةٗ مِّمَّآ أُوتُواْ وَيُؤۡثِرُونَ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ وَلَوۡ كَانَ بِهِمۡ خَصَاصَةٞۚ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفۡسِهِۦ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ

Na wale waliokuwa na masikani zao (Madiynah) na wakawa na imani yao kabla yao, wanawapenda wale walio hamia kwao, na wala hawahisi choyo yoyote vifuani mwao kwa yale waliyopewa (Muhaajiriyna), na wanawapendelea kuliko nafsi zao japokuwa wao wenyewe wanahitaji. Na yeyote anaye epushwa na ubakhili (na tamaa ya uchu) wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu



Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 10

وَٱلَّذِينَ جَآءُو مِنۢ بَعۡدِهِمۡ يَقُولُونَ رَبَّنَا ٱغۡفِرۡ لَنَا وَلِإِخۡوَٰنِنَا ٱلَّذِينَ سَبَقُونَا بِٱلۡإِيمَٰنِ وَلَا تَجۡعَلۡ فِي قُلُوبِنَا غِلّٗا لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ رَبَّنَآ إِنَّكَ رَءُوفٞ رَّحِيمٌ

Na wale waliokuja baada yao wanasema: Mola wetu! Tusamehe na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa imaan na wala Usijaalie katika nyoyo zetu mafundo ya chuki kwa wale walioamini; Rabb wetu! Hakika Wewe ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu



Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 11

۞أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ نَافَقُواْ يَقُولُونَ لِإِخۡوَٰنِهِمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ لَئِنۡ أُخۡرِجۡتُمۡ لَنَخۡرُجَنَّ مَعَكُمۡ وَلَا نُطِيعُ فِيكُمۡ أَحَدًا أَبَدٗا وَإِن قُوتِلۡتُمۡ لَنَنصُرَنَّكُمۡ وَٱللَّهُ يَشۡهَدُ إِنَّهُمۡ لَكَٰذِبُونَ

Je, Huwaoni wanao fanya unaafiki na wanawaambia ndugu zao walio kufuru katika Watu wa Kitabu: Mkitolewa na sisi lazima tutatoka pamoja nanyi, wala hatutamt’ii yeyote kabisa dhidi yenu. Na mkipigwa vita lazima tutakusaidieni. Na Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa hakika hao bila ya shaka ni waongo



Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 12

لَئِنۡ أُخۡرِجُواْ لَا يَخۡرُجُونَ مَعَهُمۡ وَلَئِن قُوتِلُواْ لَا يَنصُرُونَهُمۡ وَلَئِن نَّصَرُوهُمۡ لَيُوَلُّنَّ ٱلۡأَدۡبَٰرَ ثُمَّ لَا يُنصَرُونَ

Pindi wakitolewa hawatatoka pamoja nao, na wakipigwa vita hawatawasaidia. Na kama waki-wasaidia basi watageuza migongo; kisha hawatanusuriwa



Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 13

لَأَنتُمۡ أَشَدُّ رَهۡبَةٗ فِي صُدُورِهِم مِّنَ ٱللَّهِۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ قَوۡمٞ لَّا يَفۡقَهُونَ

Hakika nyinyi ni nitisho zaidi katika vifua vyao kuliko Allah. Hayo ni kwa kuwa hao ni watu wasio fahamu kitu



Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 14

لَا يُقَٰتِلُونَكُمۡ جَمِيعًا إِلَّا فِي قُرٗى مُّحَصَّنَةٍ أَوۡ مِن وَرَآءِ جُدُرِۭۚ بَأۡسُهُم بَيۡنَهُمۡ شَدِيدٞۚ تَحۡسَبُهُمۡ جَمِيعٗا وَقُلُوبُهُمۡ شَتَّىٰۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ قَوۡمٞ لَّا يَعۡقِلُونَ

Hawatapigana nanyi kwa mkusanyiko isipokuwa katika vijiji vilivyo zatitiwa kwa ngome, au nyuma ya kuta. Wao kwa wao vita vyao ni vikali. Utawadhania kuwa wako pamoja, kumbe nyoyo zao ni mbali mbali. Hayo ni kwa kuwa wao ni watu wasio na akili



Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 15

كَمَثَلِ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ قَرِيبٗاۖ ذَاقُواْ وَبَالَ أَمۡرِهِمۡ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ

Ni kama mfano wa wale walio kabla yao hivi karibuni tu walionja matokeo ya uovu wa mambo yao, na watapata adhabu iumizayo



Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 16

كَمَثَلِ ٱلشَّيۡطَٰنِ إِذۡ قَالَ لِلۡإِنسَٰنِ ٱكۡفُرۡ فَلَمَّا كَفَرَ قَالَ إِنِّي بَرِيٓءٞ مِّنكَ إِنِّيٓ أَخَافُ ٱللَّهَ رَبَّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

(Wanafiki) Ni kama mfano wa Shetani anapo mwambia mtu: Kufuru. Na akikufuru humwambia: Mimi si pamoja nawe. Hakika mimi namwogopa Allah, Mola wa walimwengu wote



Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 17

فَكَانَ عَٰقِبَتَهُمَآ أَنَّهُمَا فِي ٱلنَّارِ خَٰلِدَيۡنِ فِيهَاۚ وَذَٰلِكَ جَزَـٰٓؤُاْ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Basi ikawa mwisho wa wote wawili hao ni kuingia Motoni, wadumu humo daima; na hiyo ndiyo jazaa (malipo) ya madhaalimu



Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 18

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلۡتَنظُرۡ نَفۡسٞ مَّا قَدَّمَتۡ لِغَدٖۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ

Enyi mlio amini! Mcheni Allah, na kila nafsi iangalie inayo yatanguliza kwa ajili ya Kesho. Na mcheni Allah. Hakika Allah anazo khabari ya mnayo yatenda



Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 19

وَلَا تَكُونُواْ كَٱلَّذِينَ نَسُواْ ٱللَّهَ فَأَنسَىٰهُمۡ أَنفُسَهُمۡۚ أُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡفَٰسِقُونَ

Na wala msiwe kama wale waliomsahau Allah, Naye (Allah) Akawasahaulisha nafsi zao, hao ndio mafasiki



Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 20

لَا يَسۡتَوِيٓ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِ وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡجَنَّةِۚ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَنَّةِ هُمُ ٱلۡفَآئِزُونَ

Hawalingani sawa watu wa motoni na watu wa Peponi, watu wa Peponi ndio wenye kufuzu



Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 21

لَوۡ أَنزَلۡنَا هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانَ عَلَىٰ جَبَلٖ لَّرَأَيۡتَهُۥ خَٰشِعٗا مُّتَصَدِّعٗا مِّنۡ خَشۡيَةِ ٱللَّهِۚ وَتِلۡكَ ٱلۡأَمۡثَٰلُ نَضۡرِبُهَا لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمۡ يَتَفَكَّرُونَ

Lau kuwa tumeiteremsha hii Qur’ani juu ya mlima, basi bila ya shaka ungeli uona ukinyenyekea, ukipasuka kwa khofu ya Allah. Na hiyo mifano tunawapigia watu ili wafikiri



Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 22

هُوَ ٱللَّهُ ٱلَّذِي لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ عَٰلِمُ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِۖ هُوَ ٱلرَّحۡمَٰنُ ٱلرَّحِيمُ

Yeye ndiye Allah, ambaye hapana Mola isipokuwa Yeye tu. Mwenye kuyajua yaliyo fichikana na yanayo onekana. Yeye ndiye Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu



Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 23

هُوَ ٱللَّهُ ٱلَّذِي لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡمَلِكُ ٱلۡقُدُّوسُ ٱلسَّلَٰمُ ٱلۡمُؤۡمِنُ ٱلۡمُهَيۡمِنُ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡجَبَّارُ ٱلۡمُتَكَبِّرُۚ سُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يُشۡرِكُونَ

Yeye ndiye Allah ambaye hapana Mola isipokuwa Yeye tu. Mfalme, Mtukufu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo yake, Mwenye nguvu, Anaye fanya analolitaka, Mkubwa, Ametakasika Allah na hayo wanayo mshirikisha nayo



Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 24

هُوَ ٱللَّهُ ٱلۡخَٰلِقُ ٱلۡبَارِئُ ٱلۡمُصَوِّرُۖ لَهُ ٱلۡأَسۡمَآءُ ٱلۡحُسۡنَىٰۚ يُسَبِّحُ لَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Yeye ndiye Allah, Muumbaji, Mtengenezaji, Mtia sura, Mwenye majina mazuri kabisa. Kila kilichopo katika mbingu na ardhi kinamtakasa Yeye, naye ni Mwenye kushinda, Mwenye hekima