ٱلۡقَارِعَةُ
Inayo gonga!
Share :
مَا ٱلۡقَارِعَةُ
Nini Inayo gonga?
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡقَارِعَةُ
Na nini kitakacho kujuilisha nini Inayo gonga?
يَوۡمَ يَكُونُ ٱلنَّاسُ كَٱلۡفَرَاشِ ٱلۡمَبۡثُوثِ
Siku ambayo watu watakuwa kama nondo (vipepeo) walio tawanyika;
وَتَكُونُ ٱلۡجِبَالُ كَٱلۡعِهۡنِ ٱلۡمَنفُوشِ
Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa!
فَأَمَّا مَن ثَقُلَتۡ مَوَٰزِينُهُۥ
Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito,
فَهُوَ فِي عِيشَةٖ رَّاضِيَةٖ
Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza
وَأَمَّا مَنۡ خَفَّتۡ مَوَٰزِينُهُۥ
Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu,
فَأُمُّهُۥ هَاوِيَةٞ
Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya!
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا هِيَهۡ
Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo?
نَارٌ حَامِيَةُۢ
Ni Moto mkali!