Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 151

۞قُلۡ تَعَالَوۡاْ أَتۡلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمۡ عَلَيۡكُمۡۖ أَلَّا تُشۡرِكُواْ بِهِۦ شَيۡـٔٗاۖ وَبِٱلۡوَٰلِدَيۡنِ إِحۡسَٰنٗاۖ وَلَا تَقۡتُلُوٓاْ أَوۡلَٰدَكُم مِّنۡ إِمۡلَٰقٖ نَّحۡنُ نَرۡزُقُكُمۡ وَإِيَّاهُمۡۖ وَلَا تَقۡرَبُواْ ٱلۡفَوَٰحِشَ مَا ظَهَرَ مِنۡهَا وَمَا بَطَنَۖ وَلَا تَقۡتُلُواْ ٱلنَّفۡسَ ٱلَّتِي حَرَّمَ ٱللَّهُ إِلَّا بِٱلۡحَقِّۚ ذَٰلِكُمۡ وَصَّىٰكُم بِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ

Sema: Njooni nisome yale Mola wenu aliyokuharamishieni (nayo ni) msikishirikishenaye kitu chochote na wazazi wawili wafanyieni yaliyo mazuri na msiwaue watoto wenu kwa sababu ya ufukara (umasikini kwa sababu) sisi tunakuruzukuni nyinyi na wao. Na msiyakaribie mambo machafu yaliyo dhihiri kati ya hayo na yaliyo ya siri. Na msiiue nafsi ambayo Allah ameharamisha (kuiua) ila kwa haki tu. Hayo amekuusieni (Allah) ili myatie akilini



Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 152

وَلَا تَقۡرَبُواْ مَالَ ٱلۡيَتِيمِ إِلَّا بِٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُ حَتَّىٰ يَبۡلُغَ أَشُدَّهُۥۚ وَأَوۡفُواْ ٱلۡكَيۡلَ وَٱلۡمِيزَانَ بِٱلۡقِسۡطِۖ لَا نُكَلِّفُ نَفۡسًا إِلَّا وُسۡعَهَاۖ وَإِذَا قُلۡتُمۡ فَٱعۡدِلُواْ وَلَوۡ كَانَ ذَا قُرۡبَىٰۖ وَبِعَهۡدِ ٱللَّهِ أَوۡفُواْۚ ذَٰلِكُمۡ وَصَّىٰكُم بِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ

Na msizisogelee mali za Yatima ila kwa njia iliyo nzuri sana hadi afikie utu uzima wake. Na timizeni vipimo na mizani kwa uadilifu. Hatuilazimishi nafsi (jambo lolote) isipokuwa kwa kadiri ya vile iwezavyo. Na msemapo semeni kwa uadilifu hata ikiwa (ni dhidi ya) ndugu. Na ahadi za Allah zitekelezeni. Hayo amekuusieni (Allah) ili mpate kukumbuka



Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 153

وَأَنَّ هَٰذَا صِرَٰطِي مُسۡتَقِيمٗا فَٱتَّبِعُوهُۖ وَلَا تَتَّبِعُواْ ٱلسُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمۡ عَن سَبِيلِهِۦۚ ذَٰلِكُمۡ وَصَّىٰكُم بِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ

Na kwa hakika, hii ni njia yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Na msifuate njia nyingine zikaku-farakanisheni muiache njia yake. Hayo amekuusieni (Allah) ili muwe wachaMungu



Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 154

ثُمَّ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ تَمَامًا عَلَى ٱلَّذِيٓ أَحۡسَنَ وَتَفۡصِيلٗا لِّكُلِّ شَيۡءٖ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٗ لَّعَلَّهُم بِلِقَآءِ رَبِّهِمۡ يُؤۡمِنُونَ

Kisha tulimpa Musa kitabu ikiwa ni kutimiza neema kwa aliyefanya mazuri na ni ufafanuzi zaidi wa kila kitu na ni muongozo na rehema ili wapate kuamini kukutana na Mola wao



Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 155

وَهَٰذَا كِتَٰبٌ أَنزَلۡنَٰهُ مُبَارَكٞ فَٱتَّبِعُوهُ وَٱتَّقُواْ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ

Na hii (Qur’ani) ni kitabu tulichokiteremsha, chenye baraka. Basi kifuateni na mcheni Allah ili mpate kushushiwa rehema



Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 156

أَن تَقُولُوٓاْ إِنَّمَآ أُنزِلَ ٱلۡكِتَٰبُ عَلَىٰ طَآئِفَتَيۡنِ مِن قَبۡلِنَا وَإِن كُنَّا عَن دِرَاسَتِهِمۡ لَغَٰفِلِينَ

(Allah amekuteremshieni Qur’ani) Ili msije kusema: Ilivyo ni kwamba, vitabu vimeteremshwa kwa makundi mawili ya (waliokuwepo) kabla yetu, na kwamba hakika tulikuwa hatuyajui kamwe waliyokuwa wakiyasoma



Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 157

أَوۡ تَقُولُواْ لَوۡ أَنَّآ أُنزِلَ عَلَيۡنَا ٱلۡكِتَٰبُ لَكُنَّآ أَهۡدَىٰ مِنۡهُمۡۚ فَقَدۡ جَآءَكُم بَيِّنَةٞ مِّن رَّبِّكُمۡ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٞۚ فَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّن كَذَّبَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَصَدَفَ عَنۡهَاۗ سَنَجۡزِي ٱلَّذِينَ يَصۡدِفُونَ عَنۡ ءَايَٰتِنَا سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِ بِمَا كَانُواْ يَصۡدِفُونَ

Au (msije) mkasema: Lau kama tungeteremshiwa sisi kitabu tungekuwa waongofu zaidi kuliko wao. Basi kwa hakika kabisa, umekujieni ubainifu kutoka kwa Mola wenu Mlezi na muongozo na rehema. Sasa ni nani dhalimu zaidi (katika suala zima la itikadi) kuliko yule aliyepinga Aya za Allah na akajitenga nazo? Tutawalipa wale wanaojitenga na Aya zetu adhabu mbaya kwa sababu ya yale waliyokuwa wakijitenga nayo



Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 158

هَلۡ يَنظُرُونَ إِلَّآ أَن تَأۡتِيَهُمُ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ أَوۡ يَأۡتِيَ رَبُّكَ أَوۡ يَأۡتِيَ بَعۡضُ ءَايَٰتِ رَبِّكَۗ يَوۡمَ يَأۡتِي بَعۡضُ ءَايَٰتِ رَبِّكَ لَا يَنفَعُ نَفۡسًا إِيمَٰنُهَا لَمۡ تَكُنۡ ءَامَنَتۡ مِن قَبۡلُ أَوۡ كَسَبَتۡ فِيٓ إِيمَٰنِهَا خَيۡرٗاۗ قُلِ ٱنتَظِرُوٓاْ إِنَّا مُنتَظِرُونَ

Hakuna wanacho kingoja isipokuwa tu wanangoja wawajie Malaika au aje Mola wako Mlezi au zije baadhi ya ishara za Mola wako. Siku zitakapokuja baadhi ya ishara za Mola wako haitamfaa mtu imani yake ikiwa hakuamini kabla ya hapo au hakuchuma kheri yoyote katika kuamini kwake. Sema: Ngojeni, nasi (pia) ni wenye kungoja



Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 159

إِنَّ ٱلَّذِينَ فَرَّقُواْ دِينَهُمۡ وَكَانُواْ شِيَعٗا لَّسۡتَ مِنۡهُمۡ فِي شَيۡءٍۚ إِنَّمَآ أَمۡرُهُمۡ إِلَى ٱللَّهِ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُواْ يَفۡعَلُونَ

Hakika, wale walioigawa dini yao na wakawa makundi makundi huna lawama yoyote kwao. Ilivyo ni kwamba, shauri lao liko kwa Allah kisha atawaambia yale waliyokuwa wakiyatenda



Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 160

مَن جَآءَ بِٱلۡحَسَنَةِ فَلَهُۥ عَشۡرُ أَمۡثَالِهَاۖ وَمَن جَآءَ بِٱلسَّيِّئَةِ فَلَا يُجۡزَىٰٓ إِلَّا مِثۡلَهَا وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ

Yeyote atendae (jambo) zuri atapata mfano wa zuri hilo mara kumi, na atendae baya hatalipwa isipokuwa mfano wake, na wao (waja) hawatadhulumiwa



Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 161

قُلۡ إِنَّنِي هَدَىٰنِي رَبِّيٓ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ دِينٗا قِيَمٗا مِّلَّةَ إِبۡرَٰهِيمَ حَنِيفٗاۚ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Sema: Kwa hakika, mimi ameniongoza Mola wangu Mlezi kwenye njia iliyo nyooka; dini iliyo sawa kabisa, mila ya Ibrahimu aliyeacha itikadi zote potofu na hakuwa miongoni mwa washirikina



Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 162

قُلۡ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحۡيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Sema: Hakika, Swala yangu na ibada zangu (zote) na uhai wangu na kifo changu ni kwa ajili ya Allah, Mola wa viumbe wote



Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 163

لَا شَرِيكَ لَهُۥۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرۡتُ وَأَنَا۠ أَوَّلُ ٱلۡمُسۡلِمِينَ

(Allah ambaye) Hana mshirika. Na hayo ndio niliyoamrishwa na mimi ni Muislamu wa kwanza (katika umma huu)



Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 164

قُلۡ أَغَيۡرَ ٱللَّهِ أَبۡغِي رَبّٗا وَهُوَ رَبُّ كُلِّ شَيۡءٖۚ وَلَا تَكۡسِبُ كُلُّ نَفۡسٍ إِلَّا عَلَيۡهَاۚ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٞ وِزۡرَ أُخۡرَىٰۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُم مَّرۡجِعُكُمۡ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ فِيهِ تَخۡتَلِفُونَ

Sema: Je nitafute Mola mlezi asiekuwa Allah! na ilhali yeye (Allah) ni Mola Mlezi wa kila kitu? Na kila nafsi haitachuma (jambo la kheri au la shari) isipokuwa litarudi kwake mwenyewe. Na hatabeba mtu yeyote mzigo wa (dhambi za) mwengine. Kisha (nyote) marejeo yenu ni kwa Mola wenu tu, na atakuelezeni yote mliyokuwa mkitofautiana



Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 165

وَهُوَ ٱلَّذِي جَعَلَكُمۡ خَلَـٰٓئِفَ ٱلۡأَرۡضِ وَرَفَعَ بَعۡضَكُمۡ فَوۡقَ بَعۡضٖ دَرَجَٰتٖ لِّيَبۡلُوَكُمۡ فِي مَآ ءَاتَىٰكُمۡۗ إِنَّ رَبَّكَ سَرِيعُ ٱلۡعِقَابِ وَإِنَّهُۥ لَغَفُورٞ رَّحِيمُۢ

Na yeye (Allah) ndiye aliyekufanyeni mnaopokezana duniani, na akawanyanyua baadhi yenu juu ya wengine kwa daraja ili akujaribuni katika yale aliyokupeni. Hakika, Mola wako Mlezi ni Mwepesi sana wa kuadhibu na, kwa hakika kabisa, yeye ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu