Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 151

سَنُلۡقِي فِي قُلُوبِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱلرُّعۡبَ بِمَآ أَشۡرَكُواْ بِٱللَّهِ مَا لَمۡ يُنَزِّلۡ بِهِۦ سُلۡطَٰنٗاۖ وَمَأۡوَىٰهُمُ ٱلنَّارُۖ وَبِئۡسَ مَثۡوَى ٱلظَّـٰلِمِينَ

Tutazitia hofu nyoyo za wale waliokufuru kwasababu wamemshirikisha Allah na mambo ambayo hakuyateremshia hoja yoyote, na makazi yao ni Motoni tu, na mafikio mabaya ya madhalimuni hayo



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 152

وَلَقَدۡ صَدَقَكُمُ ٱللَّهُ وَعۡدَهُۥٓ إِذۡ تَحُسُّونَهُم بِإِذۡنِهِۦۖ حَتَّىٰٓ إِذَا فَشِلۡتُمۡ وَتَنَٰزَعۡتُمۡ فِي ٱلۡأَمۡرِ وَعَصَيۡتُم مِّنۢ بَعۡدِ مَآ أَرَىٰكُم مَّا تُحِبُّونَۚ مِنكُم مَّن يُرِيدُ ٱلدُّنۡيَا وَمِنكُم مَّن يُرِيدُ ٱلۡأٓخِرَةَۚ ثُمَّ صَرَفَكُمۡ عَنۡهُمۡ لِيَبۡتَلِيَكُمۡۖ وَلَقَدۡ عَفَا عَنكُمۡۗ وَٱللَّهُ ذُو فَضۡلٍ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Na ni hakika kabisa, Allah alitimiza ahadi yake kwenu, pale mlivyokuwa mnawafyeka kwa idhini yake hadi mliposhindwa na mkazozana (nyinyi kwa nyinyi) kuhusu amri ya (Mtume) na mkaasi baada ya Allah kuwaonesheni kile mnachokipenda. Kati yenu wapo wanaotaka dunia, na wapo miongoni mwenu wanaotaka Akhera. Kisha akakugeuzeni toka kwao ili akujaribuni, na kwa hakika ameshakusameheni. Na Allah ni Mwenye fadhila kwa Waumini



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 153

۞إِذۡ تُصۡعِدُونَ وَلَا تَلۡوُۥنَ عَلَىٰٓ أَحَدٖ وَٱلرَّسُولُ يَدۡعُوكُمۡ فِيٓ أُخۡرَىٰكُمۡ فَأَثَٰبَكُمۡ غَمَّۢا بِغَمّٖ لِّكَيۡلَا تَحۡزَنُواْ عَلَىٰ مَا فَاتَكُمۡ وَلَا مَآ أَصَٰبَكُمۡۗ وَٱللَّهُ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ

Kumbukeni mlipokuwa mkipanda Jabali kukimbia na hamumsikilizi yeyote, ilhali Mtume anawaiteni nyuma yenu. Basi Allah akakupeni huzuni juu ya huzuni, ili msisikitike kwa yaliyo kukoseni na kwa yaliyo kusibuni. Na Allah ni mwenye khabari juu ya yote myatendayo



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 154

ثُمَّ أَنزَلَ عَلَيۡكُم مِّنۢ بَعۡدِ ٱلۡغَمِّ أَمَنَةٗ نُّعَاسٗا يَغۡشَىٰ طَآئِفَةٗ مِّنكُمۡۖ وَطَآئِفَةٞ قَدۡ أَهَمَّتۡهُمۡ أَنفُسُهُمۡ يَظُنُّونَ بِٱللَّهِ غَيۡرَ ٱلۡحَقِّ ظَنَّ ٱلۡجَٰهِلِيَّةِۖ يَقُولُونَ هَل لَّنَا مِنَ ٱلۡأَمۡرِ مِن شَيۡءٖۗ قُلۡ إِنَّ ٱلۡأَمۡرَ كُلَّهُۥ لِلَّهِۗ يُخۡفُونَ فِيٓ أَنفُسِهِم مَّا لَا يُبۡدُونَ لَكَۖ يَقُولُونَ لَوۡ كَانَ لَنَا مِنَ ٱلۡأَمۡرِ شَيۡءٞ مَّا قُتِلۡنَا هَٰهُنَاۗ قُل لَّوۡ كُنتُمۡ فِي بُيُوتِكُمۡ لَبَرَزَ ٱلَّذِينَ كُتِبَ عَلَيۡهِمُ ٱلۡقَتۡلُ إِلَىٰ مَضَاجِعِهِمۡۖ وَلِيَبۡتَلِيَ ٱللَّهُ مَا فِي صُدُورِكُمۡ وَلِيُمَحِّصَ مَا فِي قُلُوبِكُمۡۚ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ

Kisha aliwateremshieni baada ya dhiki utulivu, usingizi ulifunika kundi moja kati yenu, na kundi lingine lilishughulishwa na nafsi zao hata wakamdhania Allah dhana isiyokuwa ya haki, dhana ya kijinga. Wakisema: Hivi sisi tuna jambo lolote katika hili? Sema: Mambo yote ni ya Allah. Wanaficha katika nafsi zao wasiyokubainishia. Wanasema: Lau ingelikuwa tuna lolote katika jambo hili tusingeuliwa hapa. Sema: Hata mngekuwa majumbani mwenu, basi wangetoka wale walioandikiwa kifo, wakaenda mahali pao pakuangukia wafe. Ili Allah ayajaribu yaliyomo vifuani mwenu, na asafishe yaliyomo nyoyoni mwenu. Na Allah anayajua yaliyomo vifuani



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 155

إِنَّ ٱلَّذِينَ تَوَلَّوۡاْ مِنكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡتَقَى ٱلۡجَمۡعَانِ إِنَّمَا ٱسۡتَزَلَّهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ بِبَعۡضِ مَا كَسَبُواْۖ وَلَقَدۡ عَفَا ٱللَّهُ عَنۡهُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ حَلِيمٞ

Hakika Wale waliorudi miongoni mwenu siku ambayo majeshi mawili yalipokutana, hakika shetani (ndiye) aliyewatelezesha kwa sababu ya baadhi ya makosa waliyoyafanya, na kwa hakika Allah amewasamehe. Hakika Allah ni Msamehevu sana Mpole Mno



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 156

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَكُونُواْ كَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَقَالُواْ لِإِخۡوَٰنِهِمۡ إِذَا ضَرَبُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ أَوۡ كَانُواْ غُزّٗى لَّوۡ كَانُواْ عِندَنَا مَا مَاتُواْ وَمَا قُتِلُواْ لِيَجۡعَلَ ٱللَّهُ ذَٰلِكَ حَسۡرَةٗ فِي قُلُوبِهِمۡۗ وَٱللَّهُ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ

Enyi mlioamini msiwe kama wale waliokufuru na wakasema kuhusu ndugu zao waliposafiri ardhini au walipokuwa vitani; kama wangekuwa kwetu wasingekufa na wasingeuwawa ili Allah afanye hilo kuwa ni majuto katika nyoyo zao, na Allah anahuisha na anafisha na Allah kwa munayoyatenda ni Mwenye kuyaona mno



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 157

وَلَئِن قُتِلۡتُمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ أَوۡ مُتُّمۡ لَمَغۡفِرَةٞ مِّنَ ٱللَّهِ وَرَحۡمَةٌ خَيۡرٞ مِّمَّا يَجۡمَعُونَ

Na ikiwa mtauliwa katika njia ya Allah au mkifa, hakika msamaha na rehema zitokazo kwa Allah ni bora kuliko yote wanayoyakusanya



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 158

وَلَئِن مُّتُّمۡ أَوۡ قُتِلۡتُمۡ لَإِلَى ٱللَّهِ تُحۡشَرُونَ

Na mkifa au mkiuliwa ni kwa Allah tu mtakusanywa



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 159

فَبِمَا رَحۡمَةٖ مِّنَ ٱللَّهِ لِنتَ لَهُمۡۖ وَلَوۡ كُنتَ فَظًّا غَلِيظَ ٱلۡقَلۡبِ لَٱنفَضُّواْ مِنۡ حَوۡلِكَۖ فَٱعۡفُ عَنۡهُمۡ وَٱسۡتَغۡفِرۡ لَهُمۡ وَشَاوِرۡهُمۡ فِي ٱلۡأَمۡرِۖ فَإِذَا عَزَمۡتَ فَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُتَوَكِّلِينَ

Basi ni kwa rehema za Allah umekuwa mpole kwao, na lau ungekuwa muovu wa tabia, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangekukimbia, basi samehe na uwaombee msamaha na watake ushauri katika jambo, na ukitia azma ya jambo basi mtegemee Allah, hakika Allah anawapenda wenye kumtegemea



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 160

إِن يَنصُرۡكُمُ ٱللَّهُ فَلَا غَالِبَ لَكُمۡۖ وَإِن يَخۡذُلۡكُمۡ فَمَن ذَا ٱلَّذِي يَنصُرُكُم مِّنۢ بَعۡدِهِۦۗ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ

Iwapo Allah atawanusuru, basi hakuna wa kuwashinda na endapo atakuacheni basi ni nani mwingine baada ya Yeye atakunusuruni? Na Waumini wategemee kwa Allah tu



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 161

وَمَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَغُلَّۚ وَمَن يَغۡلُلۡ يَأۡتِ بِمَا غَلَّ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفۡسٖ مَّا كَسَبَتۡ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ

Na haiwezekani kwa Nabii yeyote kufanya khiyana, na atakayefanya khiyana atayaleta aliyoyafanyia khiyana Siku ya Kiama kisha kila nafsi italipwa kwa iliyoyachuma kwa ukamilifu, nao hawatadhulumiwa



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 162

أَفَمَنِ ٱتَّبَعَ رِضۡوَٰنَ ٱللَّهِ كَمَنۢ بَآءَ بِسَخَطٖ مِّنَ ٱللَّهِ وَمَأۡوَىٰهُ جَهَنَّمُۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ

Je aliyefuata yanayomridhisha Allah, ni kama yule aliyestahiki ghadhabu kutoka kwa Allah na makazi yake kuwa jahannamu? Na hayo nimarejeo mabaya mno



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 163

هُمۡ دَرَجَٰتٌ عِندَ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ بَصِيرُۢ بِمَا يَعۡمَلُونَ

Hao wana vyeo mbalimbali kwa Allah, na Allah ni mwenye kuyaona yote wayatendayo



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 164

لَقَدۡ مَنَّ ٱللَّهُ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ إِذۡ بَعَثَ فِيهِمۡ رَسُولٗا مِّنۡ أَنفُسِهِمۡ يَتۡلُواْ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتِهِۦ وَيُزَكِّيهِمۡ وَيُعَلِّمُهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَإِن كَانُواْ مِن قَبۡلُ لَفِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٍ

kwa hakika Allah amewaneemesha Waumini pale alipomtuma kwao Mtume anayetokana na wao wenyewe, anawasomea Aya zake, anawatakasa na anawafundisha kitabu na hekima japokuwa kabla ya hapo walikuwa katika uovu wa wazi



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 165

أَوَلَمَّآ أَصَٰبَتۡكُم مُّصِيبَةٞ قَدۡ أَصَبۡتُم مِّثۡلَيۡهَا قُلۡتُمۡ أَنَّىٰ هَٰذَاۖ قُلۡ هُوَ مِنۡ عِندِ أَنفُسِكُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Hivi mlipopata msiba hakika mmekwishapatwa mara mbili ya huo, mlisema: umetoka wapi msiba huu? Sema huo umetoka kwenu wenyewe, hakika Allah juu ya kila kitu ni muweza



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 166

وَمَآ أَصَٰبَكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡتَقَى ٱلۡجَمۡعَانِ فَبِإِذۡنِ ٱللَّهِ وَلِيَعۡلَمَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Na yale yaliyokupateni siku yalipopambana majeshi mawili yalikuwa kwa idhini ya Allah na ili awajue waumini



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 167

وَلِيَعۡلَمَ ٱلَّذِينَ نَافَقُواْۚ وَقِيلَ لَهُمۡ تَعَالَوۡاْ قَٰتِلُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ أَوِ ٱدۡفَعُواْۖ قَالُواْ لَوۡ نَعۡلَمُ قِتَالٗا لَّٱتَّبَعۡنَٰكُمۡۗ هُمۡ لِلۡكُفۡرِ يَوۡمَئِذٍ أَقۡرَبُ مِنۡهُمۡ لِلۡإِيمَٰنِۚ يَقُولُونَ بِأَفۡوَٰهِهِم مَّا لَيۡسَ فِي قُلُوبِهِمۡۚ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا يَكۡتُمُونَ

Na ili awapambanue wanafiki, na wakaambiwa: njooni mpigane katika njia ya Allah au lindeni. Wakasema: lau tungejua kuwa kuna mapigano bila ya shaka tungelikufuateni. wao siku ile walikuwa wako karibu zaidi na ukafiri kuliko imani, wanasema kwa midomo yao yasiyokuwemo nyoyoni mwao, na Allah ni mjuzi zaidi kwa yale wanayoyaficha



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 168

ٱلَّذِينَ قَالُواْ لِإِخۡوَٰنِهِمۡ وَقَعَدُواْ لَوۡ أَطَاعُونَا مَا قُتِلُواْۗ قُلۡ فَٱدۡرَءُواْ عَنۡ أَنفُسِكُمُ ٱلۡمَوۡتَ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Hao ndio ambao walisema kuhusu ndugu zao na wao wakiwa wamekaa: Lau wangelitutii sisi wasingeuliwa sema: basi ziondoleeni nafsi zenu kifo ikiwa nyinyi ni wa kweli



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 169

وَلَا تَحۡسَبَنَّ ٱلَّذِينَ قُتِلُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ أَمۡوَٰتَۢاۚ بَلۡ أَحۡيَآءٌ عِندَ رَبِّهِمۡ يُرۡزَقُونَ

Na kamwe msiwadhanie waliouliwa katika njia ya Allah kuwa ni wafu, bali wako hai kwa Mola wao wanaruzukiwa



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 170

فَرِحِينَ بِمَآ ءَاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ مِن فَضۡلِهِۦ وَيَسۡتَبۡشِرُونَ بِٱلَّذِينَ لَمۡ يَلۡحَقُواْ بِهِم مِّنۡ خَلۡفِهِمۡ أَلَّا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Wanafurahia waliyopewa na Allah miongoni mwa fadhila zake, na wanawabashiria walio nyuma yao ambao bado hawajajiunga nao, ya kwamba: Hakutakuwa na khofu yoyote juu yao, na wala hawatahuzunika



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 171

۞يَسۡتَبۡشِرُونَ بِنِعۡمَةٖ مِّنَ ٱللَّهِ وَفَضۡلٖ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Wanawapa bishara ya neema zitokanazo kwa Mola wao na fadhila na hakika Allah hapotezi malipo ya waumini



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 172

ٱلَّذِينَ ٱسۡتَجَابُواْ لِلَّهِ وَٱلرَّسُولِ مِنۢ بَعۡدِ مَآ أَصَابَهُمُ ٱلۡقَرۡحُۚ لِلَّذِينَ أَحۡسَنُواْ مِنۡهُمۡ وَٱتَّقَوۡاْ أَجۡرٌ عَظِيمٌ

Ambao walimuitikia Allah na Mtume baada ya kupatwa na majeraha, kwa wale ambao waliofanya wema miongoni mwao na wakamcha Allah watakuwa na ujira mkubwa



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 173

ٱلَّذِينَ قَالَ لَهُمُ ٱلنَّاسُ إِنَّ ٱلنَّاسَ قَدۡ جَمَعُواْ لَكُمۡ فَٱخۡشَوۡهُمۡ فَزَادَهُمۡ إِيمَٰنٗا وَقَالُواْ حَسۡبُنَا ٱللَّهُ وَنِعۡمَ ٱلۡوَكِيلُ

Ambao watu waliwaambia wao: hakika kundi la watu limekukusanyikieni basi waogopeni, hilo likawazidishia imani na wakasema: Allah anatutosha na ndiye mbora wa wenye kutegemewa



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 174

فَٱنقَلَبُواْ بِنِعۡمَةٖ مِّنَ ٱللَّهِ وَفَضۡلٖ لَّمۡ يَمۡسَسۡهُمۡ سُوٓءٞ وَٱتَّبَعُواْ رِضۡوَٰنَ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ ذُو فَضۡلٍ عَظِيمٍ

Basi wakarudi na neema za Allah na fadhila zake, hakuna baya lililowagusa, na wakafuata yanayomridhi Allah, na Allah ni mwenye fadhila kubwa mno



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 175

إِنَّمَا ذَٰلِكُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ يُخَوِّفُ أَوۡلِيَآءَهُۥ فَلَا تَخَافُوهُمۡ وَخَافُونِ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Hakika huyo ni shetani anawatia khofu marafiki zake, basi msiwaogope wao, bali niogopeni mimi mkiwa nyinyi ni waumini



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 176

وَلَا يَحۡزُنكَ ٱلَّذِينَ يُسَٰرِعُونَ فِي ٱلۡكُفۡرِۚ إِنَّهُمۡ لَن يَضُرُّواْ ٱللَّهَ شَيۡـٔٗاۚ يُرِيدُ ٱللَّهُ أَلَّا يَجۡعَلَ لَهُمۡ حَظّٗا فِي ٱلۡأٓخِرَةِۖ وَلَهُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٌ

Wala wasikuhuzunishe ambao wanaharakisha kukimbilia ukafiri, hakika hao hawatamdhuru Allah, chochote anataka asiwawekee fungu lolote Akhera, nao watakuwa na adhabu kubwa mno



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 177

إِنَّ ٱلَّذِينَ ٱشۡتَرَوُاْ ٱلۡكُفۡرَ بِٱلۡإِيمَٰنِ لَن يَضُرُّواْ ٱللَّهَ شَيۡـٔٗاۖ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ

Hakika ya ambao wamenunua ukafiri dhidi ya imani hawatamdhuru Allah chochote, na wana adhabu chungu mno



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 178

وَلَا يَحۡسَبَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَنَّمَا نُمۡلِي لَهُمۡ خَيۡرٞ لِّأَنفُسِهِمۡۚ إِنَّمَا نُمۡلِي لَهُمۡ لِيَزۡدَادُوٓاْ إِثۡمٗاۖ وَلَهُمۡ عَذَابٞ مُّهِينٞ

Na kamwe wasidhani wale waliokufuru kwamba huu muda tunaowapa ni kheri kwao, hakika tunawapa muda ili wazidi kutenda dhambi, na wana adhabu yenye kudhalilisha



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 179

مَّا كَانَ ٱللَّهُ لِيَذَرَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ عَلَىٰ مَآ أَنتُمۡ عَلَيۡهِ حَتَّىٰ يَمِيزَ ٱلۡخَبِيثَ مِنَ ٱلطَّيِّبِۗ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُطۡلِعَكُمۡ عَلَى ٱلۡغَيۡبِ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ يَجۡتَبِي مِن رُّسُلِهِۦ مَن يَشَآءُۖ فَـَٔامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦۚ وَإِن تُؤۡمِنُواْ وَتَتَّقُواْ فَلَكُمۡ أَجۡرٌ عَظِيمٞ

Haiwi kwa Allah awaache waumini katika hali mliyonayo mpaka awapambanue wabaya kutokana na wema, na haikuwa kwa Allah akujulisheni mambo yaliyofichikana, lakini Allah humteua katika Mitume wake amtakaye, basi muaminini Allah na Mitume wake, na mkiamini na mkamcha Allah, basi mtakuwa na ujira mkubwa mno



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 180

وَلَا يَحۡسَبَنَّ ٱلَّذِينَ يَبۡخَلُونَ بِمَآ ءَاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ مِن فَضۡلِهِۦ هُوَ خَيۡرٗا لَّهُمۖ بَلۡ هُوَ شَرّٞ لَّهُمۡۖ سَيُطَوَّقُونَ مَا بَخِلُواْ بِهِۦ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۗ وَلِلَّهِ مِيرَٰثُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ

Na kamwe wasidhani ambao wanafanya ubakhili kwa kile alichowapa Allah katika fadhila zake kuwa ni kheri kwao, bali hiyo ni shari kwao watafungwa kongwa kwa vile walivyovifanyia ubakhili siku ya kiama na ni wa Allah pekee urithi wa Mbingu na Ardhi, na Allah ni mwenye khabari kwa yale mnayoyatenda