Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 121

قَالُوٓاْ ءَامَنَّا بِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Wakasema: Tumeamuamini Mola Mlezi wa walimwengu wote



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 122

رَبِّ مُوسَىٰ وَهَٰرُونَ

Mola Mlezi wa Musa na Haruna



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 123

قَالَ فِرۡعَوۡنُ ءَامَنتُم بِهِۦ قَبۡلَ أَنۡ ءَاذَنَ لَكُمۡۖ إِنَّ هَٰذَا لَمَكۡرٞ مَّكَرۡتُمُوهُ فِي ٱلۡمَدِينَةِ لِتُخۡرِجُواْ مِنۡهَآ أَهۡلَهَاۖ فَسَوۡفَ تَعۡلَمُونَ

Firauni akasema: Hivi mmemuamini kabla mimi sijakupeni idhini? Kwa hakika kabisa, hii ni njama mliyoipanga mjini ili muwatoe humo watu wake. Basi mtatambua (nitakachokufanyeni)!



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 124

لَأُقَطِّعَنَّ أَيۡدِيَكُمۡ وَأَرۡجُلَكُم مِّنۡ خِلَٰفٖ ثُمَّ لَأُصَلِّبَنَّكُمۡ أَجۡمَعِينَ

Kwa hakika kabisa, nitaikatakata mikono yenu na miguu yenu kwa kupishanisha, kisha nitakutundikeni misalabani nyote



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 125

قَالُوٓاْ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ

Wakasema: Hakika, sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 126

وَمَا تَنقِمُ مِنَّآ إِلَّآ أَنۡ ءَامَنَّا بِـَٔايَٰتِ رَبِّنَا لَمَّا جَآءَتۡنَاۚ رَبَّنَآ أَفۡرِغۡ عَلَيۡنَا صَبۡرٗا وَتَوَفَّنَا مُسۡلِمِينَ

Na hakuna kosa linalopelekea ututese isipokuwa tu huku kuamini kwetu Aya za Mola wetu Mlezi zilipotufikia. (Ewe) Mola wetu Mlezi, tujaze subira na tufishe tukiwa Waislamu



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 127

وَقَالَ ٱلۡمَلَأُ مِن قَوۡمِ فِرۡعَوۡنَ أَتَذَرُ مُوسَىٰ وَقَوۡمَهُۥ لِيُفۡسِدُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَيَذَرَكَ وَءَالِهَتَكَۚ قَالَ سَنُقَتِّلُ أَبۡنَآءَهُمۡ وَنَسۡتَحۡيِۦ نِسَآءَهُمۡ وَإِنَّا فَوۡقَهُمۡ قَٰهِرُونَ

Na mamwinyi katika watu wa Firauni wakasema (kumwambia Firauni): Hivi unamuacha Musa na watu wake wafanye uharibifu katika ardhi (nchi yetu) na akuache wewe na Miungu yako? (Firauni) Akasema: Tutawaua vibaya watoto wao wanaume na tutawaacha hai watoto wao wanawake, nasi tuna uwezo mkubwa wa kuwashinda!



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 128

قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِ ٱسۡتَعِينُواْ بِٱللَّهِ وَٱصۡبِرُوٓاْۖ إِنَّ ٱلۡأَرۡضَ لِلَّهِ يُورِثُهَا مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦۖ وَٱلۡعَٰقِبَةُ لِلۡمُتَّقِينَ

Musa akawaambia watu wake: Ombeni msaada kwa Allah na vumilieni[1]. Hakika, ardhi ni ya Allah tu anamrithisha amtakaye miongoni mwa waja wake. Na mwisho mwema ni wa wachaMungu tu


1- - Hapa kuna fundisho kwa Waislamu. Mtume Musa, kwa wakati huo, aliona udhaifu wa waumini na kutokuwa na maandalizi na uwezo wa kupambana. Kwa mantiki hiyo, hakuwashauri kuingia katika mapambano, lakini aliwaelekeza kuomba msaada kwa Allah na kuwa na Subira na uvumilivu na kuwaliwaza na pia kuwakumbusha ahadi ya Allah kuwa ushindi kwa waumini ni lazima pale Allah atakaporuhusu mazingira ya ushindi.


Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 129

قَالُوٓاْ أُوذِينَا مِن قَبۡلِ أَن تَأۡتِيَنَا وَمِنۢ بَعۡدِ مَا جِئۡتَنَاۚ قَالَ عَسَىٰ رَبُّكُمۡ أَن يُهۡلِكَ عَدُوَّكُمۡ وَيَسۡتَخۡلِفَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرَ كَيۡفَ تَعۡمَلُونَ

Wakasema: Tumefanyiwa maudhi kabla ya wewe kutujia na baada ya kutujia. (Musa) Akasema: Huenda Mola wenu Mlezi akamuangamiza adui yenu na akakuwekeni nyinyi badala yao katika ardhi ili aangalie: Mtafanya nini?



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 130

وَلَقَدۡ أَخَذۡنَآ ءَالَ فِرۡعَوۡنَ بِٱلسِّنِينَ وَنَقۡصٖ مِّنَ ٱلثَّمَرَٰتِ لَعَلَّهُمۡ يَذَّكَّرُونَ

Na kwa hakika kabisa, tuliwashika (tuliwatia adabu) watu wa Firauni kwa miaka ya shida mbali mbali na upungufu wa matunda (vyakula) ili waonyeke



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 131

فَإِذَا جَآءَتۡهُمُ ٱلۡحَسَنَةُ قَالُواْ لَنَا هَٰذِهِۦۖ وَإِن تُصِبۡهُمۡ سَيِّئَةٞ يَطَّيَّرُواْ بِمُوسَىٰ وَمَن مَّعَهُۥٓۗ أَلَآ إِنَّمَا طَـٰٓئِرُهُمۡ عِندَ ٱللَّهِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ

Basi linapowajia jambo zuri (mvua na rutuba) husema: Hili ni stahiki yetu, na likiwapata jambo baya (ukame na magonjwa) wanaamini kuwa ni nuksi ya Musa na walioko pamoja naye! Eleweni kwamba, mikosi yao inatoka kwa Allah na lakini wengi wao hawajui



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 132

وَقَالُواْ مَهۡمَا تَأۡتِنَا بِهِۦ مِنۡ ءَايَةٖ لِّتَسۡحَرَنَا بِهَا فَمَا نَحۡنُ لَكَ بِمُؤۡمِنِينَ

Na wakasema: Muujiza wowote utakaotuletea ili uturoge, basi sisi hatutakuamini



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 133

فَأَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمُ ٱلطُّوفَانَ وَٱلۡجَرَادَ وَٱلۡقُمَّلَ وَٱلضَّفَادِعَ وَٱلدَّمَ ءَايَٰتٖ مُّفَصَّلَٰتٖ فَٱسۡتَكۡبَرُواْ وَكَانُواْ قَوۡمٗا مُّجۡرِمِينَ

Basi tuliwapelekea tufani na nzige na chawa na vyura na damu ikiwa ni miujiza iliyowekwa wazi wakafanya kiburi na wakawa watu waovu



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 134

وَلَمَّا وَقَعَ عَلَيۡهِمُ ٱلرِّجۡزُ قَالُواْ يَٰمُوسَى ٱدۡعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِندَكَۖ لَئِن كَشَفۡتَ عَنَّا ٱلرِّجۡزَ لَنُؤۡمِنَنَّ لَكَ وَلَنُرۡسِلَنَّ مَعَكَ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ

Na adhabu ilipowashukia walisema: (Ewe Musa) Tuombee Mola wako Mlezi zile ahadi alizokuahidi. Kwa hakika kabisa, ukituondolea (hii) adhabu tutakuamini na tutawaachia Wana wa Israili waondoke pamoja nawe



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 135

فَلَمَّا كَشَفۡنَا عَنۡهُمُ ٱلرِّجۡزَ إِلَىٰٓ أَجَلٍ هُم بَٰلِغُوهُ إِذَا هُمۡ يَنكُثُونَ

Basi tulipowaondolea adhabu mpaka muda wao watakaoufikia, ghafla wao wakawa wanavunja ahadi



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 136

فَٱنتَقَمۡنَا مِنۡهُمۡ فَأَغۡرَقۡنَٰهُمۡ فِي ٱلۡيَمِّ بِأَنَّهُمۡ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَكَانُواْ عَنۡهَا غَٰفِلِينَ

Basi tuliwaadhibu tukawaza-misha baharini kwa sababu walikadhibisha Aya zetu na wali-kuwa wakizipuuza



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 137

وَأَوۡرَثۡنَا ٱلۡقَوۡمَ ٱلَّذِينَ كَانُواْ يُسۡتَضۡعَفُونَ مَشَٰرِقَ ٱلۡأَرۡضِ وَمَغَٰرِبَهَا ٱلَّتِي بَٰرَكۡنَا فِيهَاۖ وَتَمَّتۡ كَلِمَتُ رَبِّكَ ٱلۡحُسۡنَىٰ عَلَىٰ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ بِمَا صَبَرُواْۖ وَدَمَّرۡنَا مَا كَانَ يَصۡنَعُ فِرۡعَوۡنُ وَقَوۡمُهُۥ وَمَا كَانُواْ يَعۡرِشُونَ

Na tuliwarithisha watu waliokuwa wananyanyaswa mashariki ya ardhi (Shamu) na magharibi yake ambayo tumeibariki. Na neno zuri la Mola wako limetimia kwa Wana wa Israili kwa sababu walivumilia na tuliyaangamiza yote aliyotengeneza Firauni na watu wake, na (majumba ya kifahari) waliyokuwa wakiyajenga



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 138

وَجَٰوَزۡنَا بِبَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ ٱلۡبَحۡرَ فَأَتَوۡاْ عَلَىٰ قَوۡمٖ يَعۡكُفُونَ عَلَىٰٓ أَصۡنَامٖ لَّهُمۡۚ قَالُواْ يَٰمُوسَى ٱجۡعَل لَّنَآ إِلَٰهٗا كَمَا لَهُمۡ ءَالِهَةٞۚ قَالَ إِنَّكُمۡ قَوۡمٞ تَجۡهَلُونَ

Na tuliwavusha Wana wa Israili baharini, wakafika kwa watu wanaoabudu masanamu yao. (Wana wa Israili) Wakasema (kumwambia Mtume Musa): Ewe Musa, na sisi tufanyie Mungu kama hawa walivyo na Miungu. (Musa) Akasema: Hakika, nyinyi ni watu wajinga!



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 139

إِنَّ هَـٰٓؤُلَآءِ مُتَبَّرٞ مَّا هُمۡ فِيهِ وَبَٰطِلٞ مَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Hakika, hawa kimeangamizwa ambacho wanakifanya na ni batili yote ambayo waliyokuwa wakiyatenda



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 140

قَالَ أَغَيۡرَ ٱللَّهِ أَبۡغِيكُمۡ إِلَٰهٗا وَهُوَ فَضَّلَكُمۡ عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ

(Musa) Alisema: Hivi nikutakieni Mungu mwingine badala ya Allah na ilhali yeye ndiye aliyekufanyeni bora kuliko walimwengu wote (wa wakati wenu)?



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 141

وَإِذۡ أَنجَيۡنَٰكُم مِّنۡ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ يَسُومُونَكُمۡ سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِ يُقَتِّلُونَ أَبۡنَآءَكُمۡ وَيَسۡتَحۡيُونَ نِسَآءَكُمۡۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَآءٞ مِّن رَّبِّكُمۡ عَظِيمٞ

Na (kumbukeni) tulipokuokoeni kutoka kwa watu wa Firauni wakikupeni adhabu mbaya sana; wanawaua vibaya watoto wenu wanaume na kuwaacha hai watoto wenu wanawake. Na katika hayo kwenu kuna mitihani mikubwa kutoka kwa Mola wenu Mlezi



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 142

۞وَوَٰعَدۡنَا مُوسَىٰ ثَلَٰثِينَ لَيۡلَةٗ وَأَتۡمَمۡنَٰهَا بِعَشۡرٖ فَتَمَّ مِيقَٰتُ رَبِّهِۦٓ أَرۡبَعِينَ لَيۡلَةٗۚ وَقَالَ مُوسَىٰ لِأَخِيهِ هَٰرُونَ ٱخۡلُفۡنِي فِي قَوۡمِي وَأَصۡلِحۡ وَلَا تَتَّبِعۡ سَبِيلَ ٱلۡمُفۡسِدِينَ

Na tuliahidiana na Musa usiku (siku) thalathini na tukatimiza kwa (kuongeza) siku kumi. Basi ikatimia ahadi ya Mola wake siku arubaini. Na Musa alimwambia ndugu yake Haruna kwamba: Kuwa mrithi wangu kwa watu wangu na tengeneza (mambo yaliyoharibika) na usifuate njia ya waharibifu



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 143

وَلَمَّا جَآءَ مُوسَىٰ لِمِيقَٰتِنَا وَكَلَّمَهُۥ رَبُّهُۥ قَالَ رَبِّ أَرِنِيٓ أَنظُرۡ إِلَيۡكَۚ قَالَ لَن تَرَىٰنِي وَلَٰكِنِ ٱنظُرۡ إِلَى ٱلۡجَبَلِ فَإِنِ ٱسۡتَقَرَّ مَكَانَهُۥ فَسَوۡفَ تَرَىٰنِيۚ فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُۥ لِلۡجَبَلِ جَعَلَهُۥ دَكّٗا وَخَرَّ مُوسَىٰ صَعِقٗاۚ فَلَمَّآ أَفَاقَ قَالَ سُبۡحَٰنَكَ تُبۡتُ إِلَيۡكَ وَأَنَا۠ أَوَّلُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Na Musa alipokuja kwenye miadi yetu na Mola wake akamsemesha, alisema: Ewe Mola wangu Mlezi: Nioneshe nikuone. (Allah) Akasema: Katu hutaniona (hapa duniani), na lakini litazame jabali. Kama likibaki mahala pake basi utaniona. Basi Mola wake Mlezi alipojitokeza kwenye jabali, alilifanya likatike katike (na kusagika) na Musa akaanguka chini akiwa amezimia. (Musa) Alipozinduka alisema: Utakasifu ni wako, nimetubu kwako na mimi ni muumini wa wakwanza



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 144

قَالَ يَٰمُوسَىٰٓ إِنِّي ٱصۡطَفَيۡتُكَ عَلَى ٱلنَّاسِ بِرِسَٰلَٰتِي وَبِكَلَٰمِي فَخُذۡ مَآ ءَاتَيۡتُكَ وَكُن مِّنَ ٱلشَّـٰكِرِينَ

(Allah) Akasema: Ewe Musa, hakika ya mimi nimekuteua kwa watu kwa kukupa ujumbe wangu na maneno yangu. Basi chukua niliyokupa na uwe miongoni mwa wanaoshukuru



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 145

وَكَتَبۡنَا لَهُۥ فِي ٱلۡأَلۡوَاحِ مِن كُلِّ شَيۡءٖ مَّوۡعِظَةٗ وَتَفۡصِيلٗا لِّكُلِّ شَيۡءٖ فَخُذۡهَا بِقُوَّةٖ وَأۡمُرۡ قَوۡمَكَ يَأۡخُذُواْ بِأَحۡسَنِهَاۚ سَأُوْرِيكُمۡ دَارَ ٱلۡفَٰسِقِينَ

Na katika kila kitu tulimuandikia katika mbao (za Taurati) mawaidha na upambanuzi wa kila kitu. Basi zichukue (zishike na zifanyie kazi) kwa nguvu (na sio kimchezo mchezo na uvivu) na waamrishe watu wako na wazishike nzuri zake. Nitakuonesheni makazi ya waovu



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 146

سَأَصۡرِفُ عَنۡ ءَايَٰتِيَ ٱلَّذِينَ يَتَكَبَّرُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّ وَإِن يَرَوۡاْ كُلَّ ءَايَةٖ لَّا يُؤۡمِنُواْ بِهَا وَإِن يَرَوۡاْ سَبِيلَ ٱلرُّشۡدِ لَا يَتَّخِذُوهُ سَبِيلٗا وَإِن يَرَوۡاْ سَبِيلَ ٱلۡغَيِّ يَتَّخِذُوهُ سَبِيلٗاۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَكَانُواْ عَنۡهَا غَٰفِلِينَ

Nitawaondoa kwenye (ufahamu na utekelezaji wa) Aya zangu wale wanaofanya kiburi katika ardhi (dunia) bila ya haki. Na waonapo kila dalili (hoja) hawaiamini na waonapo njia ya uongofu hawaichukui kuwa ndio njia (sahihi), na waionapo njia ya upotevu wanaichukua kuwa ndio njia (sahihi). Hiyo ni kwa sababu wamezikanusha Aya zetu na wamekuwa wakizipuuza



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 147

وَٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَلِقَآءِ ٱلۡأٓخِرَةِ حَبِطَتۡ أَعۡمَٰلُهُمۡۚ هَلۡ يُجۡزَوۡنَ إِلَّا مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Na ambao wamekadhibisha Aya zetu na mkutano wa Akhera amali zao zimeporomoka (zimeharibika). Hawatalipwa isipokuwa yale tu waliyokuwa wakiyatenda



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 148

وَٱتَّخَذَ قَوۡمُ مُوسَىٰ مِنۢ بَعۡدِهِۦ مِنۡ حُلِيِّهِمۡ عِجۡلٗا جَسَدٗا لَّهُۥ خُوَارٌۚ أَلَمۡ يَرَوۡاْ أَنَّهُۥ لَا يُكَلِّمُهُمۡ وَلَا يَهۡدِيهِمۡ سَبِيلًاۘ ٱتَّخَذُوهُ وَكَانُواْ ظَٰلِمِينَ

Na watu Musa baada ya kuondoka kwake, walitengeneza kutokana na mapambo yao umbo la ndama lenye sauti (ya mlio wa ng’ombe). Hivi hawakuona kuwa (ndama yule) hawasemeshi na hawaongozi njia yoyote? Walimchukua (walimfanya kama Mungu) na walikuwa madhalimu



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 149

وَلَمَّا سُقِطَ فِيٓ أَيۡدِيهِمۡ وَرَأَوۡاْ أَنَّهُمۡ قَدۡ ضَلُّواْ قَالُواْ لَئِن لَّمۡ يَرۡحَمۡنَا رَبُّنَا وَيَغۡفِرۡ لَنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ

Na walipoangukia mikononi mwao (walipojuta) na kuona kuwa wameshapotea walisema: Ikiwa Mola wetu Mlezi hatatuhurumia na kutusamehe, bila shaka tutakuwa miongoni mwa wenye kupata hasara



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 150

وَلَمَّا رَجَعَ مُوسَىٰٓ إِلَىٰ قَوۡمِهِۦ غَضۡبَٰنَ أَسِفٗا قَالَ بِئۡسَمَا خَلَفۡتُمُونِي مِنۢ بَعۡدِيٓۖ أَعَجِلۡتُمۡ أَمۡرَ رَبِّكُمۡۖ وَأَلۡقَى ٱلۡأَلۡوَاحَ وَأَخَذَ بِرَأۡسِ أَخِيهِ يَجُرُّهُۥٓ إِلَيۡهِۚ قَالَ ٱبۡنَ أُمَّ إِنَّ ٱلۡقَوۡمَ ٱسۡتَضۡعَفُونِي وَكَادُواْ يَقۡتُلُونَنِي فَلَا تُشۡمِتۡ بِيَ ٱلۡأَعۡدَآءَ وَلَا تَجۡعَلۡنِي مَعَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Na Musa aliporudi kwa watu wake akiwa amekasirika na kuhuzunika alisema: Ubaya ulioje wa mliyoyafanya baada kuondoka kwangu! Hivi mmeharakia amri ya Mola wenu Mlezi? Na alizitupa mbao (za Taurati) na akakamata kichwa cha ndugu yake (Haruna) akimvutia kwake na kumwambia: Ewe mtoto wa mama yangu, hakika hawa watu wamenidharau na walikaribia kuniua. Basi usiwafurahishe maadui kupitia kwangu na usiniweke pamoja na watu madhalimu