Surah: ANNISAI 

Ayah : 121

أُوْلَـٰٓئِكَ مَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُ وَلَا يَجِدُونَ عَنۡهَا مَحِيصٗا

Hao makazi yao ni Jahanamu na wala hawatakuwa na pa kuiepuka



Surah: ANNISAI 

Ayah : 122

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ سَنُدۡخِلُهُمۡ جَنَّـٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۖ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٗاۚ وَمَنۡ أَصۡدَقُ مِنَ ٱللَّهِ قِيلٗا

Na walioamini na wakatenda mema, tutawaingiza katika bustani zitiririkazo mito chini yake, watabaki humo milele. Ni ahadi ya Allah ya kweli, na ni nani mkweli zaidi wa kauli kuliko Allah?



Surah: ANNISAI 

Ayah : 123

لَّيۡسَ بِأَمَانِيِّكُمۡ وَلَآ أَمَانِيِّ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِۗ مَن يَعۡمَلۡ سُوٓءٗا يُجۡزَ بِهِۦ وَلَا يَجِدۡ لَهُۥ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلِيّٗا وَلَا نَصِيرٗا

Sio kwa matamanio yenu wala matamanio ya Watu wa Kitabu. Yeyote anayefanya uovu atalipwa kwa uovu huo, na wala hatapata yeyote wa kumlinda na wa kumnusuru badala ya Allah



Surah: ANNISAI 

Ayah : 124

وَمَن يَعۡمَلۡ مِنَ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ مِن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَأُوْلَـٰٓئِكَ يَدۡخُلُونَ ٱلۡجَنَّةَ وَلَا يُظۡلَمُونَ نَقِيرٗا

Na yeyote anayefanya mema awe mwanaume au mwanamke na ilhali ni Muumini, basi hao wataingia Peponi na hawatadhulumiwa (jema lolote) hata kama liwe ujazo wa uwazi wa tundu ya kokwa ya tende



Surah: ANNISAI 

Ayah : 125

وَمَنۡ أَحۡسَنُ دِينٗا مِّمَّنۡ أَسۡلَمَ وَجۡهَهُۥ لِلَّهِ وَهُوَ مُحۡسِنٞ وَٱتَّبَعَ مِلَّةَ إِبۡرَٰهِيمَ حَنِيفٗاۗ وَٱتَّخَذَ ٱللَّهُ إِبۡرَٰهِيمَ خَلِيلٗا

Na hakuna aliye na dini iliyo nzuri (sahihi) sana kuliko yule aliyeusalimisha uso wake kwa Allah (kwa kumtii), naye akawa mwenye kufanya mazuri na akafuata dini ya Ibrahimu akijitenga na Shirki. Na Allah amemfanya Ibrahimu kipenzi (chake)



Surah: ANNISAI 

Ayah : 126

وَلِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٖ مُّحِيطٗا

Na ni vya Allah tu vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na Allah ni mwenye kuvizunguka vitu vyote



Surah: ANNISAI 

Ayah : 127

وَيَسۡتَفۡتُونَكَ فِي ٱلنِّسَآءِۖ قُلِ ٱللَّهُ يُفۡتِيكُمۡ فِيهِنَّ وَمَا يُتۡلَىٰ عَلَيۡكُمۡ فِي ٱلۡكِتَٰبِ فِي يَتَٰمَى ٱلنِّسَآءِ ٱلَّـٰتِي لَا تُؤۡتُونَهُنَّ مَا كُتِبَ لَهُنَّ وَتَرۡغَبُونَ أَن تَنكِحُوهُنَّ وَٱلۡمُسۡتَضۡعَفِينَ مِنَ ٱلۡوِلۡدَٰنِ وَأَن تَقُومُواْ لِلۡيَتَٰمَىٰ بِٱلۡقِسۡطِۚ وَمَا تَفۡعَلُواْ مِنۡ خَيۡرٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِهِۦ عَلِيمٗا

Na wanakuuliza Fat’wa[1] kuhusu wanawake. Sema: Allah anakupeni Fat`wa kuhusu wao na (kuhusu) yale yanayosomwa kwenu katika kitabu (hiki) kuhusu Yatima wanawake ambao hamuwapi kile kilicho wajibu kupewa na mnatamani kuwaoa, na (Fat’wa kuhusu) wale wanyonge miongoni mwa watoto na kwamba muwasimamie Yatima kwa uadilifu. Na kheri yoyote mnayoifanya basi hakika Allah anaijua sana


1- - Fat’wa katika Uislamu ni kutoa maelezo ya hukumu ya sheria, kwa maana ya kufafanua na sio kulazimisha. Anayefanya hivi anaitwa Mufti. Kadhi na Mufti wanatofautiana kwamba kazi ya Kadhi ni kutoa hukumu na kulazimisha utekelezwaji wa hukumu hiyo wakati kauli ya Mufti na ufafanuzi wa hukumu yake sio lazima kutekelezwa. Rejea kitabu cha Al-Ahkaamus Sultwaaniyyah cha Imamu Almaawardi, Allah amrehemu.


Surah: ANNISAI 

Ayah : 128

وَإِنِ ٱمۡرَأَةٌ خَافَتۡ مِنۢ بَعۡلِهَا نُشُوزًا أَوۡ إِعۡرَاضٗا فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡهِمَآ أَن يُصۡلِحَا بَيۡنَهُمَا صُلۡحٗاۚ وَٱلصُّلۡحُ خَيۡرٞۗ وَأُحۡضِرَتِ ٱلۡأَنفُسُ ٱلشُّحَّۚ وَإِن تُحۡسِنُواْ وَتَتَّقُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٗا

Na iwapo mwanamke (mke) yeyote atachelea uasi kwa mumewe au kutojaliwa (kupuuzwa na kutelekezwa) basi si vibaya kwao kufanya suluhu baina yao, na suluhu ni jambo la kheri sana. Na nafsi zimehudhurishiwa (zimesogezewa) ubahili[1]. Na iwapo mtafanya mazuri na mkamcha Allah, basi hakika Allah anayajua vyema yote mnayoyafanya


1- - Hapa Aya inaelezea uhalisia wa nafsi ya mwanadamu wakati wa ugonvi na mivutano ambapo kila upande unakuwa na umimi, kujipendelea, kukataa kujishusha na kuwa na ugumu na uzito wa kukubali kosa, kujirudi au kusamehe haki ili kufikia suluhu na muafaka.


Surah: ANNISAI 

Ayah : 129

وَلَن تَسۡتَطِيعُوٓاْ أَن تَعۡدِلُواْ بَيۡنَ ٱلنِّسَآءِ وَلَوۡ حَرَصۡتُمۡۖ فَلَا تَمِيلُواْ كُلَّ ٱلۡمَيۡلِ فَتَذَرُوهَا كَٱلۡمُعَلَّقَةِۚ وَإِن تُصۡلِحُواْ وَتَتَّقُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ غَفُورٗا رَّحِيمٗا

Na hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wanawake (wake zenu) hata kama mtafanya jitihada. Basi (pamoja na hayo) msimili (msielemee) moja kwa moja (kwa mke mmoja), mkamuacha mwingine kama aliyetundikwa (aliyening’inizwa).[1] Na kama mtafanya usuluhishi na mkamcha Allah, hakika Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehem


1- - Waume wanakatazwa kutofanya uadilifu baina ya wake zao kwa kutotoa huduma stahiki kwa usawa au kwa kutelekeza baadhi. Hili halihusu mume mwenye wake zaidi ya mmoja tu, lakini linamhusu hata mume mwenye mke mmoja. Mume mwenye mke mmoja pia haruhusiwi kutomtendea uadilifu mkewe kwa kutompa haki zake au kwa kumtelekeza na kumuweka katika mazingira ya kutojitambua kwamba ni mke au sio mke. Uadilifu unaokusudia na sheria ni uadilifu wa huduma na sio hisia za mvuto, mahaba na mapenzi ya moyoni.


Surah: ANNISAI 

Ayah : 130

وَإِن يَتَفَرَّقَا يُغۡنِ ٱللَّهُ كُلّٗا مِّن سَعَتِهِۦۚ وَكَانَ ٱللَّهُ وَٰسِعًا حَكِيمٗا

Na iwapo (mke na mume) watatengana (kwa kuachana baada ya suluhu kushindikana), Allah atamtosheleza kila mmoja kutoka katika wasaa (ukarimu) wake. Na Allah ni Mwingi wa wasaa, Mwingi wa hekima



Surah: ANNISAI 

Ayah : 131

وَلِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ وَلَقَدۡ وَصَّيۡنَا ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ مِن قَبۡلِكُمۡ وَإِيَّاكُمۡ أَنِ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ وَإِن تَكۡفُرُواْ فَإِنَّ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ غَنِيًّا حَمِيدٗا

Na ni vya Allah tu vyote viliv-yomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na kwa hakika, tuliwausia waliopewa vitabu kabla yenu na nyinyi pia kwamba, mcheni Allah. Na kama mtapinga basi ni vya Allah tu vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na Allah ni Mkwasi sana, Mwenye kusifiwa



Surah: ANNISAI 

Ayah : 132

وَلِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَكِيلًا

Na ni vya Allah tu vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na Allah pekee anatosha kuwa Mtetezi



Surah: ANNISAI 

Ayah : 133

إِن يَشَأۡ يُذۡهِبۡكُمۡ أَيُّهَا ٱلنَّاسُ وَيَأۡتِ بِـَٔاخَرِينَۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ ذَٰلِكَ قَدِيرٗا

(Allah) Akitaka atakuondoeni enyi watu na ataleta wengine. Na Allah analiweza sana hilo



Surah: ANNISAI 

Ayah : 134

مَّن كَانَ يُرِيدُ ثَوَابَ ٱلدُّنۡيَا فَعِندَ ٱللَّهِ ثَوَابُ ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ سَمِيعَۢا بَصِيرٗا

Anayetaka malipo ya dunia, basi kwa Allah yapo malipo ya dunia na Akhera. Na Allah ni Mwenye kusikia sana, Mwenye kuona



Surah: ANNISAI 

Ayah : 135

۞يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُونُواْ قَوَّـٰمِينَ بِٱلۡقِسۡطِ شُهَدَآءَ لِلَّهِ وَلَوۡ عَلَىٰٓ أَنفُسِكُمۡ أَوِ ٱلۡوَٰلِدَيۡنِ وَٱلۡأَقۡرَبِينَۚ إِن يَكُنۡ غَنِيًّا أَوۡ فَقِيرٗا فَٱللَّهُ أَوۡلَىٰ بِهِمَاۖ فَلَا تَتَّبِعُواْ ٱلۡهَوَىٰٓ أَن تَعۡدِلُواْۚ وَإِن تَلۡوُۥٓاْ أَوۡ تُعۡرِضُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٗا

Enyi mlioamini, kuweni wasimamishaji uadilifu, wenye kutoa ushahidi kwa ajili ya Allah hata kama (uadilifu na ushahidi huo) ni dhidi ya nafsi zenu au wazazi na ndugu wa karibu. Ikiwa (anayetakiwa kutolewa ushahidi) ni tajiri au fukara (msipindishe ushahidi kwasababu) Allah ni bora zaidi kwao (kuliko nyinyi[1] Basi msifuate matamanio ya nafsi zenu mkaacha kutenda uadilifu. Na kama mtapotosha (ushahidi) au mtapuuza (kwa kuacha kuutoa) basi ni hakika Allah anayajua yote mnayotenda


1- - . Allah anasisitiza kuwa yeye ndiye Muumba wa Tajiri na maskini na anataka haki itendeke kwa wote. Ushahidi utolewe bila ya kuangalia utajiri wa mtu au umaskini wake.


Surah: ANNISAI 

Ayah : 136

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ ءَامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَٱلۡكِتَٰبِ ٱلَّذِي نَزَّلَ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ وَٱلۡكِتَٰبِ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ مِن قَبۡلُۚ وَمَن يَكۡفُرۡ بِٱللَّهِ وَمَلَـٰٓئِكَتِهِۦ وَكُتُبِهِۦ وَرُسُلِهِۦ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ فَقَدۡ ضَلَّ ضَلَٰلَۢا بَعِيدًا

Enyi mlioamini, endeleeni kumuaminini Allah na Mtume wake na kitabu (Qur’ani) alichokiteremsha kwa Mtume wake na vitabu alivyoviteremsha kabla yake (kabla ya Qur’ani). Na yeyote anayempinga Allah na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume wake na Siku ya Mwisho, basi amepotea upotevu wa mbali kabisa



Surah: ANNISAI 

Ayah : 137

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ثُمَّ كَفَرُواْ ثُمَّ ءَامَنُواْ ثُمَّ كَفَرُواْ ثُمَّ ٱزۡدَادُواْ كُفۡرٗا لَّمۡ يَكُنِ ٱللَّهُ لِيَغۡفِرَ لَهُمۡ وَلَا لِيَهۡدِيَهُمۡ سَبِيلَۢا

Hakika, wale walioamini kisha wakakufuru, kisha wakaamini kisha wakakufuru, kisha wakazidi ukafiri, Allah hakuwa mwenye kuwasamehe wala kuwaongoza njia (ya haki)



Surah: ANNISAI 

Ayah : 138

بَشِّرِ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ بِأَنَّ لَهُمۡ عَذَابًا أَلِيمًا

Wape bishara[1] wanafiki kwamba wanayo adhabu iumizayo mno


1- - Bishara ni taarifa ya jambo jema linaloleta faraja. Adhabu sio jambo jema la kutia faraja, lakini hapa limetumika kwa wanafiki kwa madhumuni ya kuwakejeli na kuwadhihaki.


Surah: ANNISAI 

Ayah : 139

ٱلَّذِينَ يَتَّخِذُونَ ٱلۡكَٰفِرِينَ أَوۡلِيَآءَ مِن دُونِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۚ أَيَبۡتَغُونَ عِندَهُمُ ٱلۡعِزَّةَ فَإِنَّ ٱلۡعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعٗا

(Wanafiki) Ambao wanawafanya makafiri kuwa marafiki badala ya Waumini (wenzao). Hivi wanatafuta heshima kwao? Basi hakika, heshima yote ni miliki ya Allah tu



Surah: ANNISAI 

Ayah : 140

وَقَدۡ نَزَّلَ عَلَيۡكُمۡ فِي ٱلۡكِتَٰبِ أَنۡ إِذَا سَمِعۡتُمۡ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ يُكۡفَرُ بِهَا وَيُسۡتَهۡزَأُ بِهَا فَلَا تَقۡعُدُواْ مَعَهُمۡ حَتَّىٰ يَخُوضُواْ فِي حَدِيثٍ غَيۡرِهِۦٓ إِنَّكُمۡ إِذٗا مِّثۡلُهُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ جَامِعُ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَٱلۡكَٰفِرِينَ فِي جَهَنَّمَ جَمِيعًا

Na kwa hakika, (Allah) amekuteremshieni katika kitabu (Qur’ani) kwamba msikiapo Aya za Allah zinakanushwa na zinafanyiwa kejeli, basi msikae pamoja nao (hao wafanyao hivyo), mpaka waingie katika mazungumzo mengine[1]. Hakika, mkikaa nao nanyi mtakuwa kama wao. Hakika, Allah atawakusanya Wanafiki na Makafiri wote katika Jahanamu


1- - Allah ametaja suala hili katika Aya ya 68 ya Sura Al-an-aam (6) inayosema kwamba “Na ukiwaona wanaozisema vibaya Aya zetu usikae nao…”.


Surah: ANNISAI 

Ayah : 141

ٱلَّذِينَ يَتَرَبَّصُونَ بِكُمۡ فَإِن كَانَ لَكُمۡ فَتۡحٞ مِّنَ ٱللَّهِ قَالُوٓاْ أَلَمۡ نَكُن مَّعَكُمۡ وَإِن كَانَ لِلۡكَٰفِرِينَ نَصِيبٞ قَالُوٓاْ أَلَمۡ نَسۡتَحۡوِذۡ عَلَيۡكُمۡ وَنَمۡنَعۡكُم مِّنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۚ فَٱللَّهُ يَحۡكُمُ بَيۡنَكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ وَلَن يَجۡعَلَ ٱللَّهُ لِلۡكَٰفِرِينَ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ سَبِيلًا

Ambao wanakuvizieni. Mkipata ushindi unaotoka kwa Allah wanasema: Si tulikuwa pamoja na nyinyi? Na ikiwa makafiri wamepata sehemu ndogo ya ushindi wanasema: Si tulikusimamieni na kukukingeni dhidi ya Waislamu? Basi Allah atahukumu baina yenu Siku ya Kiama. Na Allah hatawapa makafiri njia (ya kuwashinda) Waislamu



Surah: ANNISAI 

Ayah : 142

إِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ يُخَٰدِعُونَ ٱللَّهَ وَهُوَ خَٰدِعُهُمۡ وَإِذَا قَامُوٓاْ إِلَى ٱلصَّلَوٰةِ قَامُواْ كُسَالَىٰ يُرَآءُونَ ٱلنَّاسَ وَلَا يَذۡكُرُونَ ٱللَّهَ إِلَّا قَلِيلٗا

Hakika, wanafiki wanamhadaa Allah, naye ni mwenye kuwahadaa (pia). Na wanaposimama kwenda kuswali wanasimama wakiwa wavivu, wanajionyesha kwa watu (kwamba nao ni Waislamu) na hawamtaji Allah isipokuwa kidogo sana



Surah: ANNISAI 

Ayah : 143

مُّذَبۡذَبِينَ بَيۡنَ ذَٰلِكَ لَآ إِلَىٰ هَـٰٓؤُلَآءِ وَلَآ إِلَىٰ هَـٰٓؤُلَآءِۚ وَمَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَلَن تَجِدَ لَهُۥ سَبِيلٗا

Wanayumba yumba baina ya hayo (ya hali mbili za imani na unafiki). Hawako kwa hawa (Waislamu) na hawako kwa hawa (makafiri). Na yeyote ambaye Allah amempoteza hutampatia njia yoyote (ya kumuongoa)



Surah: ANNISAI 

Ayah : 144

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَّخِذُواْ ٱلۡكَٰفِرِينَ أَوۡلِيَآءَ مِن دُونِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَجۡعَلُواْ لِلَّهِ عَلَيۡكُمۡ سُلۡطَٰنٗا مُّبِينًا

Enyi mlioamini, msiwafanye makafiri marafiki wa ndani badala ya Waumini (wenzenu). Je, mnataka Allah awe na hoja iliyo wazi kwenu (kwamba nyinyi ni waovu na kustahiki adhabu kwa kuwapenda makafiri badala ya Waislamu wenzenu)?



Surah: ANNISAI 

Ayah : 145

إِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ فِي ٱلدَّرۡكِ ٱلۡأَسۡفَلِ مِنَ ٱلنَّارِ وَلَن تَجِدَ لَهُمۡ نَصِيرًا

Hakika, wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa la Moto, na hutampata yeyote wa kuwanusuru



Surah: ANNISAI 

Ayah : 146

إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُواْ وَأَصۡلَحُواْ وَٱعۡتَصَمُواْ بِٱللَّهِ وَأَخۡلَصُواْ دِينَهُمۡ لِلَّهِ فَأُوْلَـٰٓئِكَ مَعَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۖ وَسَوۡفَ يُؤۡتِ ٱللَّهُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ أَجۡرًا عَظِيمٗا

Isipokuwa wale waliotubu (unafiki wao) na wakatengeneza (wakarekebisha na kusahihisha itikadi na misimamo yao mibovu) na wakashikamana na (sheri za) Allah na wakaitakasa dini yao kwa ajili ya Allah. Basi hao watakuwa pamoja na waumini. Na Allah atawapa waumini ujira mkubwa sana



Surah: ANNISAI 

Ayah : 147

مَّا يَفۡعَلُ ٱللَّهُ بِعَذَابِكُمۡ إِن شَكَرۡتُمۡ وَءَامَنتُمۡۚ وَكَانَ ٱللَّهُ شَاكِرًا عَلِيمٗا

Allah hatakuadhibuni iwapo mtashukuru na kuamini, na Allah ndiye Mwenye kupokea shukurani na ndiye Mjuzi sana



Surah: ANNISAI 

Ayah : 148

۞لَّا يُحِبُّ ٱللَّهُ ٱلۡجَهۡرَ بِٱلسُّوٓءِ مِنَ ٱلۡقَوۡلِ إِلَّا مَن ظُلِمَۚ وَكَانَ ٱللَّهُ سَمِيعًا عَلِيمًا

Allah hapendi kudhihirisha kauli ovu isipokuwa kwa mwenye kudhulumiwa. Na Allah ni Mwenye kusikia sana, Mjuzi sana.[1]


1- - Aya inamkataza Muislamu kuwa na hulka na tabia ya kutoa kauli zisizofaa na zisizokuwa na staha. Lakini mbele ya mamlaka au mbele ya vyombo vya sheria na maamuzi, Muislamu ambaye amedhulumiwa haki yake anaruhusiwa kuwasilisha madai na, ikibidi kutamka maneno halisi ili madai yake yaeleweke, hata kama maneno ni makali. Anaruhusiwa kufanya hivyo ili apate haki yake na ili dhalimu aadhibiwe kwa kupewa adhabu anayostahiki.


Surah: ANNISAI 

Ayah : 149

إِن تُبۡدُواْ خَيۡرًا أَوۡ تُخۡفُوهُ أَوۡ تَعۡفُواْ عَن سُوٓءٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَفُوّٗا قَدِيرًا

Mkidhihirisha kheri au mkiificha au mkisamehe uovu, basi hakika Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye uwezo



Surah: ANNISAI 

Ayah : 150

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكۡفُرُونَ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦ وَيُرِيدُونَ أَن يُفَرِّقُواْ بَيۡنَ ٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦ وَيَقُولُونَ نُؤۡمِنُ بِبَعۡضٖ وَنَكۡفُرُ بِبَعۡضٖ وَيُرِيدُونَ أَن يَتَّخِذُواْ بَيۡنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا

Hakika, ambao wanamkufuru Allah na Mitume wake na wanataka kutenganisha kati ya Allah na Mitume wake, na wanasema: Tunaamini baadhi na tunakufuru baadhi, na wanataka kushika baina ya hayo njia (ya kati ambayo ni dini mseto inayochanganya baina ya Imani na ukafiri).[1]


1- - Aya inawakataza Waislamu kutofautisha baina ya Mitume ya Allah kama ilivyokuwa kwa Wayahudi ambao wamemuamini Mtume Mussa lakini wakataa kumuamini Mtume Isa na Mtume Muhammad, na kama ilivyo kwa Wakristo ambao wamemuamini Mtume Isa na kukataa kumuamini Mtume Muhammad. Pia aya inakataza kufanya ujanja wa kutaka kuunganisha dini zote hizo ili zionekane ni sahihi na zina mrengo mmoja unaopaswa kuwa pamoja.