Surah: ATTAUBA 

Ayah : 91

لَّيۡسَ عَلَى ٱلضُّعَفَآءِ وَلَا عَلَى ٱلۡمَرۡضَىٰ وَلَا عَلَى ٱلَّذِينَ لَا يَجِدُونَ مَا يُنفِقُونَ حَرَجٌ إِذَا نَصَحُواْ لِلَّهِ وَرَسُولِهِۦۚ مَا عَلَى ٱلۡمُحۡسِنِينَ مِن سَبِيلٖۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Hakuna dhambi kwa wanyonge na wagonjwa na wasiokuwa na cha kutoa, iwapo wanamsafia nia Allah na Mtume wake. Hakuna njia ya kuwalaumu wanaofanya mazuri. Na Allah ni Mwenye kusamehe, mwenye Rehemu



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 92

وَلَا عَلَى ٱلَّذِينَ إِذَا مَآ أَتَوۡكَ لِتَحۡمِلَهُمۡ قُلۡتَ لَآ أَجِدُ مَآ أَحۡمِلُكُمۡ عَلَيۡهِ تَوَلَّواْ وَّأَعۡيُنُهُمۡ تَفِيضُ مِنَ ٱلدَّمۡعِ حَزَنًا أَلَّا يَجِدُواْ مَا يُنفِقُونَ

Na wala (hawana dhambi) wale (Answari) ambao walipokujia ili uwachukue (uwawezeshe na uwape vipando vya kwendea jihadi) ulisema: Sina kipando cha kukuchukueni (cha kukupeni) waliondoka na ilhali macho yao yanatiririka machozi kwa huzuni ya kukosa cha kutoa



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 93

۞إِنَّمَا ٱلسَّبِيلُ عَلَى ٱلَّذِينَ يَسۡتَـٔۡذِنُونَكَ وَهُمۡ أَغۡنِيَآءُۚ رَضُواْ بِأَن يَكُونُواْ مَعَ ٱلۡخَوَالِفِ وَطَبَعَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ

Kwa hakika kabisa, njia (ya kulaumu na kuwachukulia hatua) ipo kwa wale wanaokuomba ruhusa (ili wasiende vitani) na ilhali wao ni wakwasi. Wameridhia kuwa pamoja na wabakiao nyuma (kwa udhuru kama vile watoto, wagonjwa, wazee, wanawake, walemavu n.k.) na Allah amewapiga chapa kwenye nyoyo zao. Kwa hivyo hawajui (lililo na manufaa na wao)



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 94

يَعۡتَذِرُونَ إِلَيۡكُمۡ إِذَا رَجَعۡتُمۡ إِلَيۡهِمۡۚ قُل لَّا تَعۡتَذِرُواْ لَن نُّؤۡمِنَ لَكُمۡ قَدۡ نَبَّأَنَا ٱللَّهُ مِنۡ أَخۡبَارِكُمۡۚ وَسَيَرَى ٱللَّهُ عَمَلَكُمۡ وَرَسُولُهُۥ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَٰلِمِ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

(Wanafiki) Watakutoleeni udhuru mtakaporejea kwao. Sema (uwaambie): “Msitoe udhuru; hatutakuaminini tena. Allah ameshatueleza habari zenu. Na Allah na Mtume wake wataviona vitendo vyenu (kwamba mtatubu na kuacha unafiki au mtaendelea). Kisha mtarudishwa kwa (Allah) Mjuzi wa ya siri na ya dhahiri; naye atakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda”



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 95

سَيَحۡلِفُونَ بِٱللَّهِ لَكُمۡ إِذَا ٱنقَلَبۡتُمۡ إِلَيۡهِمۡ لِتُعۡرِضُواْ عَنۡهُمۡۖ فَأَعۡرِضُواْ عَنۡهُمۡۖ إِنَّهُمۡ رِجۡسٞۖ وَمَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُ جَزَآءَۢ بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ

Watakuapieni kwa Allah mtaka-porudi kwao ili msiwaulize. Basi wapuuzeni. Hakika hao ni Najisi (wa imani), na makazi yao ni Jahanamu ikiwa ni malipo kwa sababu ya waliyokuwa wanayachuma



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 96

يَحۡلِفُونَ لَكُمۡ لِتَرۡضَوۡاْ عَنۡهُمۡۖ فَإِن تَرۡضَوۡاْ عَنۡهُمۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يَرۡضَىٰ عَنِ ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡفَٰسِقِينَ

Wanakuapieni ili muwe radhi nao. Basi hata mkiwaridhia, kwa hakika Allah hawaridhii watu waovu



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 97

ٱلۡأَعۡرَابُ أَشَدُّ كُفۡرٗا وَنِفَاقٗا وَأَجۡدَرُ أَلَّا يَعۡلَمُواْ حُدُودَ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ عَلَىٰ رَسُولِهِۦۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ

Mabedui[1] ni washupavu mno katika ukafiri na unafiki (kuliko watu wa mijini) na ni kawaida sana (ya) kutoijua mipaka ya yale aliyoyateremsha Allah kwa Mtume wake[2]. Na Allah ni Mjuzi mno, Mwenye hekima sana


1- - Bedui ni mkazi wa mashambani; iwe jangwani au sehemu yoyote ya nje ya mji.


2- - Mabedui wamepewa sifa hizi kutokana na uchache wa maingiliano na kuchanganyika na watu wengine na pia kutokana na wao kuwa mbali na vyanzo vya elimu na maarifa. Aya pamoja na kuwa imetaja Mabedui kwa jumla yao lakini sio wote. Ni baadhi tu wenye sifa hizo. Katika lugha hii ni kawaida; kutaja jumla lakini ikakusudiwa baadhi, kama ilivyotajwa katika Aya ya 67 ya Sura Al-israi (17) kwamba “…na mwanadamu amekuwa kafiri sana (wa kumkataa Allah na kukanusha neema zake)”. Sio kwamba kila mwanadamu ana sifa hii. Ni baadhi tu. Na katika suala la Mabedui ni hivyo hivyo. Sio wote wana sifa za ukafiri na unafiki mkali. Ni baadhi tu. Ni kwa sababu hii, Allah katika Aya ya 99 ya Sura hii ya Attauba (9) ametaja kuwa wapo Mabedui wenye maadili mazuri na Imani sahihi.


Surah: ATTAUBA 

Ayah : 98

وَمِنَ ٱلۡأَعۡرَابِ مَن يَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ مَغۡرَمٗا وَيَتَرَبَّصُ بِكُمُ ٱلدَّوَآئِرَۚ عَلَيۡهِمۡ دَآئِرَةُ ٱلسَّوۡءِۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٞ

Na miongoni mwa Mabedui wapo wanaochukulia (wanadhani) vile wanavyovitoa (katika njia ya Allah) ni kazi bure (hasara), na wanakuvizieni mpate majanga. Majanga mabaya yawashukie wao. Na Allah ni Mwenye kusikia sana, Mwenye kujua mno



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 99

وَمِنَ ٱلۡأَعۡرَابِ مَن يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَيَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ قُرُبَٰتٍ عِندَ ٱللَّهِ وَصَلَوَٰتِ ٱلرَّسُولِۚ أَلَآ إِنَّهَا قُرۡبَةٞ لَّهُمۡۚ سَيُدۡخِلُهُمُ ٱللَّهُ فِي رَحۡمَتِهِۦٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na katika Mabedui wapo wanaomuamini Allah na Siku ya Mwisho na wanachukulia (wanaamini) kuwa wanavyovitoa (katika njia ya Allah) ni ibada zinazowasogeza kwa Allah na maombi ya Mtume. Zindukeni na mjue kwamba, hizo ni (ibada) zinazowasogeza (kwa Allah) kwa faida yao. Allah atawaingiza katika rehema zake. Hakika, Allah ni Mwenye kusamehe, mwenye kurehemu



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 100

وَٱلسَّـٰبِقُونَ ٱلۡأَوَّلُونَ مِنَ ٱلۡمُهَٰجِرِينَ وَٱلۡأَنصَارِ وَٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوهُم بِإِحۡسَٰنٖ رَّضِيَ ٱللَّهُ عَنۡهُمۡ وَرَضُواْ عَنۡهُ وَأَعَدَّ لَهُمۡ جَنَّـٰتٖ تَجۡرِي تَحۡتَهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ

Na wale Muhajirina na Answari wa mwanzo (kuamini) nawaliowafuata wao kwa uzuri, Allah ameridhika nao (kwa utiifu wao), na wao wameridhika naye (kwa malipo mazuri atakayowapa) na amewaandalia Pepo zipitazo mito mbele yake, wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa hasa.[1]


1- - Aya hii inatuonesha jinsi Allah alivyowapa Swahaba hadhi, heshima na taadhima kwa kuwatakasa na kuwaridhia. Ni Swahaba wakiongozwa na Abubakar, Umar, Uthman Ali na wengine, Tabiina na waliowafuata wao kwa wema na kwamba wote hao kwa ushahidi wa Aya hii ni Waumini na ni watu wa peponi. Na kwa upande wetu ni kuwaheshimu, kuwataja kwa wema, kuwatetea na kuwaombea dua njema. Allah anasema: “Na waliokuja baada yao wanasema: Ewe Mola wetu Mlezi, tusamehe na wasamehe ndugu zetu waliotutangulia katika imani na usitie ndani ya nyoyo zetu chuki dhidi ya yeyote miongoni mwa waumini. Ewe Mola wetu Mlezi, hakika wewe tu ndiye Mpole sana, Mwenye kurehemu”. Qur’ani 59: 10


Surah: ATTAUBA 

Ayah : 101

وَمِمَّنۡ حَوۡلَكُم مِّنَ ٱلۡأَعۡرَابِ مُنَٰفِقُونَۖ وَمِنۡ أَهۡلِ ٱلۡمَدِينَةِ مَرَدُواْ عَلَى ٱلنِّفَاقِ لَا تَعۡلَمُهُمۡۖ نَحۡنُ نَعۡلَمُهُمۡۚ سَنُعَذِّبُهُم مَّرَّتَيۡنِ ثُمَّ يُرَدُّونَ إِلَىٰ عَذَابٍ عَظِيمٖ

Na miongoni mwa Mabedui waliopo pembezoni mwenu (pembezoni mwa mji wa Madina) ni wanafiki. Na katika wenyeji wa Madina pia wapo (watu) waliobobea katika unafiki. Wewe huwajui, (lakini) sisi tunawajua. Tutawaadhibu mara mbili, kisha watarudishwa kwenye adhabu kubwa mno



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 102

وَءَاخَرُونَ ٱعۡتَرَفُواْ بِذُنُوبِهِمۡ خَلَطُواْ عَمَلٗا صَٰلِحٗا وَءَاخَرَ سَيِّئًا عَسَى ٱللَّهُ أَن يَتُوبَ عَلَيۡهِمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ

Na wapo wengine (miongoni mwa wakazi wa mji wa Madina waliohalifu kwenda jihadi) waliokiri dhambi zao; wamechanganya vitendo vyema na vingine viovu. Huwenda Allah akapokea Toba zao. Hakika, Allah ni Mwenye kusamehe, mwenye kurehemu



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 103

خُذۡ مِنۡ أَمۡوَٰلِهِمۡ صَدَقَةٗ تُطَهِّرُهُمۡ وَتُزَكِّيهِم بِهَا وَصَلِّ عَلَيۡهِمۡۖ إِنَّ صَلَوٰتَكَ سَكَنٞ لَّهُمۡۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

Chukua sadaka (Zaka) kutoka katika mali zao (waumini ili) uwasafishe na uwatakase kwazo na waombee rehema. Hakika dua yako ni (sababu ya) utuvu kwao. Na Allah ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 104

أَلَمۡ يَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ هُوَ يَقۡبَلُ ٱلتَّوۡبَةَ عَنۡ عِبَادِهِۦ وَيَأۡخُذُ ٱلصَّدَقَٰتِ وَأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ

Je, (waumini na wanaotubu) hawajui ya kwamba Allah (ndiye) anayekubali Toba za waja wake, na anazikubali sadaka, na kwamba Allah tu ndiye Mwingi wa kupokea Toba, Rahimu sana?



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 105

وَقُلِ ٱعۡمَلُواْ فَسَيَرَى ٱللَّهُ عَمَلَكُمۡ وَرَسُولُهُۥ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَۖ وَسَتُرَدُّونَ إِلَىٰ عَٰلِمِ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Na sema (uwaambie wanaotubu na wengineo): Tendeni amali (kwa ikhlasi). Allah, na Mtume wake, na Waumini wataziona amali zenu. Na mtarudishwa kwa (Allah) Mwenye kujua siri na dhahiri; Naye atakuambieni yote mliyokuwa mnayatenda



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 106

وَءَاخَرُونَ مُرۡجَوۡنَ لِأَمۡرِ ٱللَّهِ إِمَّا يُعَذِّبُهُمۡ وَإِمَّا يَتُوبُ عَلَيۡهِمۡۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ

Na wapo wengine wanangojeshwa (wanaosubirishwa) ili (kungojea) amri ya Allah ima awaadhibu au awasamehe. Na Allah ni Mwenye kujua mno, Mwenye hekima sana



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 107

وَٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ مَسۡجِدٗا ضِرَارٗا وَكُفۡرٗا وَتَفۡرِيقَۢا بَيۡنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَإِرۡصَادٗا لِّمَنۡ حَارَبَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ مِن قَبۡلُۚ وَلَيَحۡلِفُنَّ إِنۡ أَرَدۡنَآ إِلَّا ٱلۡحُسۡنَىٰۖ وَٱللَّهُ يَشۡهَدُ إِنَّهُمۡ لَكَٰذِبُونَ

Na (wapo wanafiki wengine ambao ni) wale waliotengeneza (waliojenga) msikiti kwa lengo la (kuleta) madhara na (kueneza) ukafiri na kuleta mfarakano baina ya Waumini na (kwa lengo la kulitumia jengo hilo kama kituo cha) kusubiria (na kupokea) wanaompiga vita Allah na Mtume wake hapo kabla.[1] Na bila ya shaka yoyote (wanafiki) wataapa kwamba: “Hatukukusudia (katika kuujenga msikiti huu) ila tu jambo zuri sana. Na Allah anashuhudia kuwa bila ya shaka yoyote wao ni waongo tu


1- - Hapa wanazungumziwa wanafiki waliojenga msikiti katika mji wa Madina wakiwa na lengo la kuudhoofisha msikiti aliojenga Mtume pale Madina kwa lengo la kuwafarakanisha Waislamu na pia kuufanya msikiti wao huo kituo cha kupangia mikakati ya kueneza unafiki, ukafiri na kupokea wapinzani wanaompinga Mtume na Waislamu kwa jumla.


Surah: ATTAUBA 

Ayah : 108

لَا تَقُمۡ فِيهِ أَبَدٗاۚ لَّمَسۡجِدٌ أُسِّسَ عَلَى ٱلتَّقۡوَىٰ مِنۡ أَوَّلِ يَوۡمٍ أَحَقُّ أَن تَقُومَ فِيهِۚ فِيهِ رِجَالٞ يُحِبُّونَ أَن يَتَطَهَّرُواْۚ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلۡمُطَّهِّرِينَ

(Ewe Mtume) Usisimame (usiswali) katika msikiti huo abadani. Kwa hakika kabisa, msikiti ulioasisiwa (uliojengwa) kwa msingi wa uchaMungu tangu siku ya mwanzo[1] una haki zaidi wewe kusimama (kuswali) humo (kuliko kuswali katika msikiti wa madhara). Humowamo watu wanaopenda kujitakasa, na Allah anawapenda wanaojitakasa.[2]


1- - Huu ni msikiti wa Kuba.


2- - Aya ya 107 -1110 zinakemea tabia mbaya ya kinafiki ya kuasisi na kujenga msikiti kwa lengo la kudhuru na kudhoofisha msikiti uliopo na pia kuwafarakanisha Waislamu.


Surah: ATTAUBA 

Ayah : 109

أَفَمَنۡ أَسَّسَ بُنۡيَٰنَهُۥ عَلَىٰ تَقۡوَىٰ مِنَ ٱللَّهِ وَرِضۡوَٰنٍ خَيۡرٌ أَم مَّنۡ أَسَّسَ بُنۡيَٰنَهُۥ عَلَىٰ شَفَا جُرُفٍ هَارٖ فَٱنۡهَارَ بِهِۦ فِي نَارِ جَهَنَّمَۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Hivi, mwenye kuasisi jengo lake katika kumcha Allah na (kutafuta) radhi (zake) ni bora au mwenye kuasisi jengo lake katika ukingo unaomomonyoka na likaporomoka naye katika moto wa Jahanamu? Na Allah hawaongoi watu madhalimu



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 110

لَا يَزَالُ بُنۡيَٰنُهُمُ ٱلَّذِي بَنَوۡاْ رِيبَةٗ فِي قُلُوبِهِمۡ إِلَّآ أَن تَقَطَّعَ قُلُوبُهُمۡۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

Jengo lao walilolijenga (ili kustawisha unafiki wao) linaendelea kuwa sababu ya kutia wasiwasi mioyoni mwao mpaka nyoyo zao zikatike katike (kwa kuuawa au kujuta). Na Allah ni Mwenye kujua mno, Mwenye hekima sana



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 111

۞إِنَّ ٱللَّهَ ٱشۡتَرَىٰ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ أَنفُسَهُمۡ وَأَمۡوَٰلَهُم بِأَنَّ لَهُمُ ٱلۡجَنَّةَۚ يُقَٰتِلُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ فَيَقۡتُلُونَ وَيُقۡتَلُونَۖ وَعۡدًا عَلَيۡهِ حَقّٗا فِي ٱلتَّوۡرَىٰةِ وَٱلۡإِنجِيلِ وَٱلۡقُرۡءَانِۚ وَمَنۡ أَوۡفَىٰ بِعَهۡدِهِۦ مِنَ ٱللَّهِۚ فَٱسۡتَبۡشِرُواْ بِبَيۡعِكُمُ ٱلَّذِي بَايَعۡتُم بِهِۦۚ وَذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ

Hakika, Allah amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwamba watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Allah; wanaua na wanauawa. Ni ahadi ya haki juu ya hilo katika Taurati na Injili na Qur’ani. Na ni nani atimizae ahadi zaidi kuliko Allah? Basi furahieni biashara yenu mliyofanya naye. Na huko ndiko hasa kufaulu kukubwa



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 112

ٱلتَّـٰٓئِبُونَ ٱلۡعَٰبِدُونَ ٱلۡحَٰمِدُونَ ٱلسَّـٰٓئِحُونَ ٱلرَّـٰكِعُونَ ٱلسَّـٰجِدُونَ ٱلۡأٓمِرُونَ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَٱلنَّاهُونَ عَنِ ٱلۡمُنكَرِ وَٱلۡحَٰفِظُونَ لِحُدُودِ ٱللَّهِۗ وَبَشِّرِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

(Miongoni mwa sifa za waumini wapiganao Jihadi na kuahidiwa pepo ni kwamba wao ndio) Wenye kutubu, wenye kuabudu, wenye kuhimidi, wenye kukimbilia heri, wenye kurukuu, wenye kusujudu, wenye kuamrisha mema na wenye kukataza maovu, na wenye kulinda mipaka ya Allah. Na wape Waumini bishara (habari njema)



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 113

مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَن يَسۡتَغۡفِرُواْ لِلۡمُشۡرِكِينَ وَلَوۡ كَانُوٓاْ أُوْلِي قُرۡبَىٰ مِنۢ بَعۡدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمۡ أَنَّهُمۡ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَحِيمِ

Haiwi (haifai) kwa Nabii na wale walioamini kuwaombea msamaha washirikina (makafiri), na hata kama watakuwa ni jamaa zao wa karibu, baada ya kuwabainikia kuwa hao ni watu wa Motoni



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 114

وَمَا كَانَ ٱسۡتِغۡفَارُ إِبۡرَٰهِيمَ لِأَبِيهِ إِلَّا عَن مَّوۡعِدَةٖ وَعَدَهَآ إِيَّاهُ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُۥٓ أَنَّهُۥ عَدُوّٞ لِّلَّهِ تَبَرَّأَ مِنۡهُۚ إِنَّ إِبۡرَٰهِيمَ لَأَوَّـٰهٌ حَلِيمٞ

Na msamaha wa Ibrahimu wa kumuombea baba yake (kafiri) haukuwa isipokuwa tu ni kwa sababu ya ahadi aliyomuahidi.[1] Basi ilipombainikia kwamba yeye ni adui wa Allah (na ni mtu wa motoni), alijiepusha naye. Hakika kabisa, Ibrahimu alikuwa mnyenyekevu sana (katika maombi), mpole mno


1- - Allah ameitaja ahadi hii ya Nabii Ibrahimu kwa baba yake katika Qur’an, Sura Almumtahina (60), Aya ya 4 pale Allah aliposema: “Kwa hakika kabisa, mmekuwa na kiigizo kizuri kwa Ibrahimu na waliokuwa pamoja naye, walipowaambia watu wao: Kwa yakini sisi tumejitenga nanyi na hayo mnayoyaabudu badala ya Allah; tumewapingeni, naumedhihiri uadui na chuki ya kudumu (kati yetu na yenu) mpaka mmuamini Allah peke yake, isipokuwa kauli ya Ibrahimu kwa baba yake (aliyomuambia kwamba): Hakika, nitakuombea msamaha…”.


Surah: ATTAUBA 

Ayah : 115

وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُضِلَّ قَوۡمَۢا بَعۡدَ إِذۡ هَدَىٰهُمۡ حَتَّىٰ يُبَيِّنَ لَهُم مَّا يَتَّقُونَۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٌ

Na Allah hakuwa akiwapoteza watu (hawaachi wapotee) baada ya kuwaongoa mpaka awabainishie yale yanayowafanya kuwa wachaMungu. Hakika, Allah ni Mwenye kukijua vyema kila kitu



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 116

إِنَّ ٱللَّهَ لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۚ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِن وَلِيّٖ وَلَا نَصِيرٖ

Hakika, Allah tu ndiye Mwenye ufalme wa mbinguni na ardhini; anahuisha na anafisha. Nanyi hamna Mlinzi wala Msaidizi minghairi (badala) ya Allah



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 117

لَّقَد تَّابَ ٱللَّهُ عَلَى ٱلنَّبِيِّ وَٱلۡمُهَٰجِرِينَ وَٱلۡأَنصَارِ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوهُ فِي سَاعَةِ ٱلۡعُسۡرَةِ مِنۢ بَعۡدِ مَا كَادَ يَزِيغُ قُلُوبُ فَرِيقٖ مِّنۡهُمۡ ثُمَّ تَابَ عَلَيۡهِمۡۚ إِنَّهُۥ بِهِمۡ رَءُوفٞ رَّحِيمٞ

Kwa hakika kabisa, Allah alishamsamehe Nabii (baada ya kuwaruhusu waliotoa udhuru wa uongo wa kutokwenda kupigana Jihadi) na (aliwasamehe pia) Muhajirina na Answari waliomfuata Mtume katika kipindi kigumu, baada ya nyoyo za baadhi yao kukaribia kugeuka (kwa kutamani kuacha kwenda vitani katika kipindi cha joto kali na mazingira magumu), kisha (Allah) akapokea Toba zao. Hakika, Yeye kwao ni Mpole mno, Mwenye kurehemu



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 118

وَعَلَى ٱلثَّلَٰثَةِ ٱلَّذِينَ خُلِّفُواْ حَتَّىٰٓ إِذَا ضَاقَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلۡأَرۡضُ بِمَا رَحُبَتۡ وَضَاقَتۡ عَلَيۡهِمۡ أَنفُسُهُمۡ وَظَنُّوٓاْ أَن لَّا مَلۡجَأَ مِنَ ٱللَّهِ إِلَّآ إِلَيۡهِ ثُمَّ تَابَ عَلَيۡهِمۡ لِيَتُوبُوٓاْۚ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ

Na (pia Allah amekubali Toba ya wale watu) watatu walioachwa nyuma (waliokataa kwenda Jihadi kwa uvivu[1] ambao Mtume hakuikubali toba yao kwa wepesi na aliwawekea vikwazo) mpaka dunia walipoiona finyu kwao pamoja na upana wake, na nafsi zao zikadhikika na wakawa na yakini kuwa hakuna pa kumkimbia Allah isipokuwa kwake Yeye tu. Kisha Allah aliwasamehe (baada ya kubainika ni waumini kweli aliwawezesha kujirudi) ili watubu. Hakika, Allah tu ndiye Mwenye kupokea sana Toba, Mwenye kurehemu


1- - Hawa ni Kaabi bin Malik, Hilal bin Umaya na Murara bin Rabii.


Surah: ATTAUBA 

Ayah : 119

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَكُونُواْ مَعَ ٱلصَّـٰدِقِينَ

Enyi mlioamini, mcheni Allah na kuweni pamoja na wakweli



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 120

مَا كَانَ لِأَهۡلِ ٱلۡمَدِينَةِ وَمَنۡ حَوۡلَهُم مِّنَ ٱلۡأَعۡرَابِ أَن يَتَخَلَّفُواْ عَن رَّسُولِ ٱللَّهِ وَلَا يَرۡغَبُواْ بِأَنفُسِهِمۡ عَن نَّفۡسِهِۦۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ لَا يُصِيبُهُمۡ ظَمَأٞ وَلَا نَصَبٞ وَلَا مَخۡمَصَةٞ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلَا يَطَـُٔونَ مَوۡطِئٗا يَغِيظُ ٱلۡكُفَّارَ وَلَا يَنَالُونَ مِنۡ عَدُوّٖ نَّيۡلًا إِلَّا كُتِبَ لَهُم بِهِۦ عَمَلٞ صَٰلِحٌۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Haikupasa kwa watu wa Madina na (Mabedui) walioko pembezoni mwao kubakia nyuma wasitoke na Mtume wa Allah, wala kujipendelea nafsi zao kuliko yeye. Hayo ni kwa sababu hawapati kiu, wala uchovu wala njaa katika Njia ya Allah, wala hawakanyagi mahali panapo wachukiza makafiri, wala hawapati chochote cha kupata kwa maadui (ngawira, kuuawa au kutekwa), ila kwa hayo huandikwa kuwa ni kitendo chema kwao. Hakika, Allah haupotezi ujira wa wanaofanya mazuri