وَبُرِّزَتِ ٱلۡجَحِيمُ لِلۡغَاوِينَ
Na Jahannamu itadhihirishwa kwa wapotovu
Share :
وَقِيلَ لَهُمۡ أَيۡنَ مَا كُنتُمۡ تَعۡبُدُونَ
Na wataambiwa: Wako wapi mlio kuwa mkiwaabudu
مِن دُونِ ٱللَّهِ هَلۡ يَنصُرُونَكُمۡ أَوۡ يَنتَصِرُونَ
Badala ya Allah? Je! Wanaku-saidieni, au wanajisaidia wenyewe?
فَكُبۡكِبُواْ فِيهَا هُمۡ وَٱلۡغَاوُۥنَ
Basi watavurumizwa humo wao na hao wakosefu,
وَجُنُودُ إِبۡلِيسَ أَجۡمَعُونَ
Na majeshi ya Ibilisi yote
قَالُواْ وَهُمۡ فِيهَا يَخۡتَصِمُونَ
Watasema, na hali ya kuwa wanazozana humo:
تَٱللَّهِ إِن كُنَّا لَفِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٍ
Wallahi! Kwa yakini tulikuwa katika upotovu ulio dhaahiri
إِذۡ نُسَوِّيكُم بِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Tulipo kufanyeni ni sawa na Mola Mlezi wa walimwengu wote
وَمَآ أَضَلَّنَآ إِلَّا ٱلۡمُجۡرِمُونَ
Na hawakupoteza ila wale wakosefu
فَمَا لَنَا مِن شَٰفِعِينَ
Basi hatuna waombezi
وَلَا صَدِيقٍ حَمِيمٖ
Wala rafiki wa dhati
فَلَوۡ أَنَّ لَنَا كَرَّةٗ فَنَكُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Laiti tungelipata kurejea tena tungeli kuwa katika Waumini
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ
Hakika katika haya ipo Ishara, lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu
كَذَّبَتۡ قَوۡمُ نُوحٍ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Kaumu ya Nuhu waliwakadhibisha Mitume
إِذۡ قَالَ لَهُمۡ أَخُوهُمۡ نُوحٌ أَلَا تَتَّقُونَ
Alipowaambia ndugu yao, Nuhu: Je! Hamumuogopi Allah?
إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٞ
Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu
فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
Basi Mcheni Allah, na nitiini mimi
وَمَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Na sikutakini juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote
۞قَالُوٓاْ أَنُؤۡمِنُ لَكَ وَٱتَّبَعَكَ ٱلۡأَرۡذَلُونَ
Wakasema: Je! Tukuamini wewe, hali wanaokufuata ni watu wa chini?
قَالَ وَمَا عِلۡمِي بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Akasema: Nayajuaje waliyo kuwa wakiyafanya?
إِنۡ حِسَابُهُمۡ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّيۖ لَوۡ تَشۡعُرُونَ
Hesabu yao haiko ila kwa Mola wao Mlezi, laiti mngeli tambua!
وَمَآ أَنَا۠ بِطَارِدِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Wala mimi si wa kuwafukuza Waumini
إِنۡ أَنَا۠ إِلَّا نَذِيرٞ مُّبِينٞ
Mimi si chochote ila ni Muonyaji wa dhahiri
قَالُواْ لَئِن لَّمۡ تَنتَهِ يَٰنُوحُ لَتَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمَرۡجُومِينَ
Wakasema: Ikiwa huachi, ewe Nuhu, bila ya shaka utapigwa mawe
قَالَ رَبِّ إِنَّ قَوۡمِي كَذَّبُونِ
Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikanusha
فَٱفۡتَحۡ بَيۡنِي وَبَيۡنَهُمۡ فَتۡحٗا وَنَجِّنِي وَمَن مَّعِيَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Basi hukumu baina yangu na wao kwa hukumu yako, na uniokoe mimi na walio pamoja nami, Waumini
فَأَنجَيۡنَٰهُ وَمَن مَّعَهُۥ فِي ٱلۡفُلۡكِ ٱلۡمَشۡحُونِ
Kwahivyo tukamwokoa yeye na walio kuwa pamoja naye katika marikebu iliyo sheheni
ثُمَّ أَغۡرَقۡنَا بَعۡدُ ٱلۡبَاقِينَ
Kisha tukawazamisha baadaye walio bakia