فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni zipi neema za Mola wenu mnazikanusha?
Share :
وَمِن دُونِهِمَا جَنَّتَانِ
Na zaidi ya hizo mbili, ziko bustani mbili zingine
مُدۡهَآمَّتَانِ
Za rangi ya kijani iliyokoza
فِيهِمَا عَيۡنَانِ نَضَّاخَتَانِ
Mna humo chemchemu mbili zenye kububujika kwa nguvu mfululizo
فِيهِمَا فَٰكِهَةٞ وَنَخۡلٞ وَرُمَّانٞ
Mna humo matunda na mitende na makomamanga
فِيهِنَّ خَيۡرَٰتٌ حِسَانٞ
Mna humo wanawake wema wazuri
حُورٞ مَّقۡصُورَٰتٞ فِي ٱلۡخِيَامِ
weupe wakiwa na macho mapana waliotawishwa kwenye mahema
لَمۡ يَطۡمِثۡهُنَّ إِنسٞ قَبۡلَهُمۡ وَلَا جَآنّٞ
hawajaguswa na Mtu kabla yao wala Jini
مُتَّكِـِٔينَ عَلَىٰ رَفۡرَفٍ خُضۡرٖ وَعَبۡقَرِيٍّ حِسَانٖ
Wakiegemea kwenye matakia ya kijani na mazulia ya rangi mbalimbali ya hariri mazuri mno yasiyo na kifani
تَبَٰرَكَ ٱسۡمُ رَبِّكَ ذِي ٱلۡجَلَٰلِ وَٱلۡإِكۡرَامِ
Limetukuka jina la Mola wako mwenye utukufu na ukarimu