۞قَالَ فَمَا خَطۡبُكُمۡ أَيُّهَا ٱلۡمُرۡسَلُونَ
Akasema basi Lipi Jambo Lenu Enyi Mliotumwa
Share :
قَالُوٓاْ إِنَّآ أُرۡسِلۡنَآ إِلَىٰ قَوۡمٖ مُّجۡرِمِينَ
Wakasema, Sisi Tumetumwa Kwenda Kwa Watu Waovu
لِنُرۡسِلَ عَلَيۡهِمۡ حِجَارَةٗ مِّن طِينٖ
Ili tuwatupie Juu Yao Mawe Yatokanayo Na Udongo
مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ لِلۡمُسۡرِفِينَ
Yaliyo wekwa Alama kutoka Kwa Bwana Wako Kwa Waliyochupa Mipaka
فَأَخۡرَجۡنَا مَن كَانَ فِيهَا مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Kwahivyo Tutawaondoa Waliyomo Humo Miongoni Mwa Waumini
فَمَا وَجَدۡنَا فِيهَا غَيۡرَ بَيۡتٖ مِّنَ ٱلۡمُسۡلِمِينَ
Lakini Hatukukuta Humo Isipokua Nyumba Moja Miongoni Mwa Waislamu
وَتَرَكۡنَا فِيهَآ ءَايَةٗ لِّلَّذِينَ يَخَافُونَ ٱلۡعَذَابَ ٱلۡأَلِيمَ
Na Tukaacha Humo Ishara Kwa Wale Ambao wanaoiogopa Adhabu Iumizayo
وَفِي مُوسَىٰٓ إِذۡ أَرۡسَلۡنَٰهُ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ بِسُلۡطَٰنٖ مُّبِينٖ
Na katika khabari za mussa pale tulipompeleka kwa Firauni kwa hoja za wazi
فَتَوَلَّىٰ بِرُكۡنِهِۦ وَقَالَ سَٰحِرٌ أَوۡ مَجۡنُونٞ
Lakini akakengeunka na jeshi lake na akasema mchawi au mwendawazimu
فَأَخَذۡنَٰهُ وَجُنُودَهُۥ فَنَبَذۡنَٰهُمۡ فِي ٱلۡيَمِّ وَهُوَ مُلِيمٞ
basi tukamchukua na jeshi lake tukawatupa baharini hali yakuwa yeye akilaumiwa
وَفِي عَادٍ إِذۡ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمُ ٱلرِّيحَ ٱلۡعَقِيمَ
Na katika khabari za Adi pale tulipowapelekea upepo wa kukata uzazi
مَا تَذَرُ مِن شَيۡءٍ أَتَتۡ عَلَيۡهِ إِلَّا جَعَلَتۡهُ كَٱلرَّمِيمِ
Haukuacha kitu chochote ulichokipitia ila hukigeuza kitu hicho kama jivu
وَفِي ثَمُودَ إِذۡ قِيلَ لَهُمۡ تَمَتَّعُواْ حَتَّىٰ حِينٖ
Na katika khabari za Thamud pale walipoambiwa stareheni hadi muda ufike
فَعَتَوۡاْ عَنۡ أَمۡرِ رَبِّهِمۡ فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّـٰعِقَةُ وَهُمۡ يَنظُرُونَ
Wakaasi amri ya bwana wao, basi ikawachukua adhabu ya moto hali yakuwa wao wakiangalia
فَمَا ٱسۡتَطَٰعُواْ مِن قِيَامٖ وَمَا كَانُواْ مُنتَصِرِينَ
Basi hawakuweza kusimama na hawakua wao wenye kushinda
وَقَوۡمَ نُوحٖ مِّن قَبۡلُۖ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَوۡمٗا فَٰسِقِينَ
Na Watu wa Nuhu hapo mbele. hakika wao walikua watu mafasiqi
وَٱلسَّمَآءَ بَنَيۡنَٰهَا بِأَيۡيْدٖ وَإِنَّا لَمُوسِعُونَ
Na mbingu tumeijenga kwa mikono na sisi ni wenye kuweza kuzitanua
وَٱلۡأَرۡضَ فَرَشۡنَٰهَا فَنِعۡمَ ٱلۡمَٰهِدُونَ
Na ardhi tumeitandika basi ni watengenezaji wazuri namna gani sisi!
وَمِن كُلِّ شَيۡءٍ خَلَقۡنَا زَوۡجَيۡنِ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ
Na kwa kila kitu tumekiumba kwa jozi (pea mbili) ili nyinyi mkumbuke
فَفِرُّوٓاْ إِلَى ٱللَّهِۖ إِنِّي لَكُم مِّنۡهُ نَذِيرٞ مُّبِينٞ
Basi kimbilieni kwa Allah hakika mimi kwenu ni muonyaji wa wazi
وَلَا تَجۡعَلُواْ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَۖ إِنِّي لَكُم مِّنۡهُ نَذِيرٞ مُّبِينٞ
Na msifanye kinyume cha Allah mungu mwingine mimi kwenu ni muonyaji mbainishaji kutoka kwake
كَذَٰلِكَ مَآ أَتَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا قَالُواْ سَاحِرٌ أَوۡ مَجۡنُونٌ
Na kama hivyo hakuwajia kwa ambao waliyokuwa kabla yao Mtume yeyote ila walisema mchawi au mwendawazimu
أَتَوَاصَوۡاْ بِهِۦۚ بَلۡ هُمۡ قَوۡمٞ طَاغُونَ
Hivi wameusiana hilo? bali wao ni watu wapotevu
فَتَوَلَّ عَنۡهُمۡ فَمَآ أَنتَ بِمَلُومٖ
Basi waachilie mbali hao, na si wewe kuwa ni mwenye kulaumiwa
وَذَكِّرۡ فَإِنَّ ٱلذِّكۡرَىٰ تَنفَعُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Na kumbusha hakika ukumbusho unawanufaisha waumini
وَمَا خَلَقۡتُ ٱلۡجِنَّ وَٱلۡإِنسَ إِلَّا لِيَعۡبُدُونِ
Na sikuwaumba majini na wanadamu ila kwa ajili ya kuniabudu
مَآ أُرِيدُ مِنۡهُم مِّن رِّزۡقٖ وَمَآ أُرِيدُ أَن يُطۡعِمُونِ
Na sihitaji toka kwao rizki na wala sihitaji kunilisha
إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلرَّزَّاقُ ذُو ٱلۡقُوَّةِ ٱلۡمَتِينُ
Hakika Allah ndiye yeye mtoa riziki mwenye nguvu kubwa
فَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُواْ ذَنُوبٗا مِّثۡلَ ذَنُوبِ أَصۡحَٰبِهِمۡ فَلَا يَسۡتَعۡجِلُونِ
Na hakika kwa wale ambao wamedhulumu wao wana adhabu mfano wa adhabu ya wenzao, basi wasiharakishe
فَوَيۡلٞ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن يَوۡمِهِمُ ٱلَّذِي يُوعَدُونَ
Basi adhabu kali kwa wale ambao wamekufuru katika siku yao ambayo wanayo ahidiwa