عَمَّ يَتَسَآءَلُونَ
Wanaulizana nini?
Share :
عَنِ ٱلنَّبَإِ ٱلۡعَظِيمِ
Ni kuhusu habari kubwa sana
ٱلَّذِي هُمۡ فِيهِ مُخۡتَلِفُونَ
Ambayo wao wanatofautiana ndani yake
كَلَّا سَيَعۡلَمُونَ
Sihivyo! Karibu watakuja kujua
ثُمَّ كَلَّا سَيَعۡلَمُونَ
Tena si hivyo! Karibu watakuja kujua
أَلَمۡ نَجۡعَلِ ٱلۡأَرۡضَ مِهَٰدٗا
Je, kwani hatukuifanya ardhi (kama) tandiko?
وَٱلۡجِبَالَ أَوۡتَادٗا
Na milima kuwa (kama) vigingi?
وَخَلَقۡنَٰكُمۡ أَزۡوَٰجٗا
Na Tukakuumbeni kwa jozi; (wanaume na wanawake)?
وَجَعَلۡنَا نَوۡمَكُمۡ سُبَاتٗا
Na tukafanya kulala kwenu ni mapumziko?
وَجَعَلۡنَا ٱلَّيۡلَ لِبَاسٗا
Na tukaufanya usiku (ni kama) nguo (ya kukufunikeni)?
وَجَعَلۡنَا ٱلنَّهَارَ مَعَاشٗا
Na tukaufanya mchana ni wa kuchumia [kutafuta] maisha?
وَبَنَيۡنَا فَوۡقَكُمۡ سَبۡعٗا شِدَادٗا
Na Tukajenga juu yenu (mbingu) saba imara?
وَجَعَلۡنَا سِرَاجٗا وَهَّاجٗا
Na tukaifanya taa yenye mwanga na joto
وَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلۡمُعۡصِرَٰتِ مَآءٗ ثَجَّاجٗا
Na tukateremsha maji yanayo anguka kwa kasi kutoka mawinguni
لِّنُخۡرِجَ بِهِۦ حَبّٗا وَنَبَاتٗا
Ili tutoe [tuoteshe] kwayo nafaka na mimea
وَجَنَّـٰتٍ أَلۡفَافًا
Na mabustani yenye miti iliyo kamatana
إِنَّ يَوۡمَ ٱلۡفَصۡلِ كَانَ مِيقَٰتٗا
Hakika siku ya uamuzi,[hukumu] imewekewa wakati wake
يَوۡمَ يُنفَخُ فِي ٱلصُّورِ فَتَأۡتُونَ أَفۡوَاجٗا
Siku litakapopulizwa baragumu, nanyi mtakuja makundi kwa makundi
وَفُتِحَتِ ٱلسَّمَآءُ فَكَانَتۡ أَبۡوَٰبٗا
Na mbingu zitafunguliwa, ziwe kama milango
وَسُيِّرَتِ ٱلۡجِبَالُ فَكَانَتۡ سَرَابًا
Na milima itaondolewa na itakuwa kama sarabi, [mangati]
إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتۡ مِرۡصَادٗا
Hakika moto wa Jahannamu utakuwa ni wenye kuvizia
لِّلطَّـٰغِينَ مَـَٔابٗا
Kwa walioruka mipaka kwa kuasi ndio makaazi yao
لَّـٰبِثِينَ فِيهَآ أَحۡقَابٗا
Watabaki humo karne baada ya karne
لَّا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرۡدٗا وَلَا شَرَابًا
Hawatoonja humo cha baridi na wala kinywaji
إِلَّا حَمِيمٗا وَغَسَّاقٗا
Ila maji yamoto sana na usaha,
جَزَآءٗ وِفَاقًا
Ndio malipo yao muwafaka
إِنَّهُمۡ كَانُواْ لَا يَرۡجُونَ حِسَابٗا
Hakika wao walikuwa hawataraji kuhesabiwa
وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا كِذَّابٗا
Na wakikanusha Aya zetu kwa sana
وَكُلَّ شَيۡءٍ أَحۡصَيۡنَٰهُ كِتَٰبٗا
Na kila kitu Sisi tumekidhibiti kwa kukiandika
فَذُوقُواْ فَلَن نَّزِيدَكُمۡ إِلَّا عَذَابًا
Basi onjeni! Nasi hatutakuzidishieni ila adhabu!