لَآ أُقۡسِمُ بِيَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ
Nina apa kwa Siku ya Kiyama
Share :
وَلَآ أُقۡسِمُ بِٱلنَّفۡسِ ٱللَّوَّامَةِ
Na nina apa kwa nafsi inayolaumu sana
أَيَحۡسَبُ ٱلۡإِنسَٰنُ أَلَّن نَّجۡمَعَ عِظَامَهُۥ
Je, mwanadamu anadhani kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake?
بَلَىٰ قَٰدِرِينَ عَلَىٰٓ أَن نُّسَوِّيَ بَنَانَهُۥ
Ndio (tutaikusanya tu na) Tunao uwezo wa kuzifanya ziwe sawa sawa ncha za vidole vyake
بَلۡ يُرِيدُ ٱلۡإِنسَٰنُ لِيَفۡجُرَ أَمَامَهُۥ
Lakini mwanadamu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilizoko mbele yake
يَسۡـَٔلُ أَيَّانَ يَوۡمُ ٱلۡقِيَٰمَةِ
Anauliza: Ni lini hiyo Siku ya Kiyama?
فَإِذَا بَرِقَ ٱلۡبَصَرُ
Basi jicho litakapoduwaa (kwa kupatwa na bumbuwazi na fadhaa)
وَخَسَفَ ٱلۡقَمَرُ
Na mwezi utakapo patwa,
وَجُمِعَ ٱلشَّمۡسُ وَٱلۡقَمَرُ
Na vikakusanywa jua na mwezi ((Katika Kupatwa),
يَقُولُ ٱلۡإِنسَٰنُ يَوۡمَئِذٍ أَيۡنَ ٱلۡمَفَرُّ
Atasema Mwanadamu siku hiyo: Wapi pa kukimbilia?
كَلَّا لَا وَزَرَ
La! Hapana mahala pa kukimbilia!
إِلَىٰ رَبِّكَ يَوۡمَئِذٍ ٱلۡمُسۡتَقَرُّ
Kwa Mola wako siku hiyo ndio makazi ya (ya kutulia)
يُنَبَّؤُاْ ٱلۡإِنسَٰنُ يَوۡمَئِذِۭ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ
Siku hiyo ataambiwa Mtu yale aliyo yatanguliza na aliyo yakawiza
بَلِ ٱلۡإِنسَٰنُ عَلَىٰ نَفۡسِهِۦ بَصِيرَةٞ
Bali Mtu anajijua Vizuri Sana yeye mwenyewe
وَلَوۡ أَلۡقَىٰ مَعَاذِيرَهُۥ
Ingawa atatoa nyudhuru chungu nzima
لَا تُحَرِّكۡ بِهِۦ لِسَانَكَ لِتَعۡجَلَ بِهِۦٓ
Usiutikisie ulimi wako huu wahyi (ufunuo) kwa kuufanyia haraka
إِنَّ عَلَيۡنَا جَمۡعَهُۥ وَقُرۡءَانَهُۥ
Hakika ni juu Yetu kuikusanya na kukuwezesha kuisoma kwake
فَإِذَا قَرَأۡنَٰهُ فَٱتَّبِعۡ قُرۡءَانَهُۥ
Basi Tunapoisoma (kupitia Jibrili), fuata kusomwa kwake
ثُمَّ إِنَّ عَلَيۡنَا بَيَانَهُۥ
Kisha ni juu yetu kuubainisha
كَلَّا بَلۡ تُحِبُّونَ ٱلۡعَاجِلَةَ
Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani,
وَتَذَرُونَ ٱلۡأٓخِرَةَ
Na mnaacha maisha ya Akhera, (kwa kutoijali Akhera)
وُجُوهٞ يَوۡمَئِذٖ نَّاضِرَةٌ
Zipo Nyuso siku hiyo zitanawiri, (zitang’aa)
إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٞ
Zikimtazama Mola wake
وَوُجُوهٞ يَوۡمَئِذِۭ بَاسِرَةٞ
Na nyuso (nyenginezo) siku hiyo zitakunjana
تَظُنُّ أَن يُفۡعَلَ بِهَا فَاقِرَةٞ
Zikiwa na yakini kuwa zitafikiwa na msiba unaovunja uti wa mgongo
كَلَّآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلتَّرَاقِيَ
Sivyo! Itakapofika (roho) kwenye mafupa ya koo, (mitulinga)
وَقِيلَ مَنۡۜ رَاقٖ
Na itasemwa: Ni nani tabibu wa kumponya?
وَظَنَّ أَنَّهُ ٱلۡفِرَاقُ
Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki
وَٱلۡتَفَّتِ ٱلسَّاقُ بِٱلسَّاقِ
Na utakapo ambatanishwa muundi kwa muundi
إِلَىٰ رَبِّكَ يَوۡمَئِذٍ ٱلۡمَسَاقُ
Siku hiyo ndiyo (ya) kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako! (ama Peponi au Motoni)