سَأَلَ سَآئِلُۢ بِعَذَابٖ وَاقِعٖ
Muulizaji ameuliza kuhusu adhabu itakayotokea
Share :
لِّلۡكَٰفِرِينَ لَيۡسَ لَهُۥ دَافِعٞ
Kwa makafiri, hapana wa kuizuia
مِّنَ ٱللَّهِ ذِي ٱلۡمَعَارِجِ
Kutoka kwa Allah Mwenye madaraja ya juu (Mwenye mbingu za daraja)
تَعۡرُجُ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ وَٱلرُّوحُ إِلَيۡهِ فِي يَوۡمٖ كَانَ مِقۡدَارُهُۥ خَمۡسِينَ أَلۡفَ سَنَةٖ
Malaika na Roho (Jibrili) wanapanda kwenda kwake katika siku ambayo makadirio yake ni miaka hamsini elfu
فَٱصۡبِرۡ صَبۡرٗا جَمِيلًا
Basi subiri subira njema
إِنَّهُمۡ يَرَوۡنَهُۥ بَعِيدٗا
Hakika, wao wanaiona (siku hiyo) iko mbali
وَنَرَىٰهُ قَرِيبٗا
Nasi tunaiona iko karibu
يَوۡمَ تَكُونُ ٱلسَّمَآءُ كَٱلۡمُهۡلِ
Siku ambayo mbingu zitakuwa kama shaba iliyo yeyushwa
وَتَكُونُ ٱلۡجِبَالُ كَٱلۡعِهۡنِ
Na milima itakuwa kama sufi (iliyo chambuliwa)
وَلَا يَسۡـَٔلُ حَمِيمٌ حَمِيمٗا
Na rafiki hatomuuliza rafiki yake
يُبَصَّرُونَهُمۡۚ يَوَدُّ ٱلۡمُجۡرِمُ لَوۡ يَفۡتَدِي مِنۡ عَذَابِ يَوۡمِئِذِۭ بِبَنِيهِ
Watafanywa waonane. Mkosefu atatamani (kujikomboa) ajitolee fidia kutokana na adhabu Siku hiyo kwa kuwatoa watoto wake
وَصَٰحِبَتِهِۦ وَأَخِيهِ
Na mke wake na nduguye
وَفَصِيلَتِهِ ٱلَّتِي تُـٔۡوِيهِ
Na jamaa zake wa karibu ambao wanamlinda
وَمَن فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا ثُمَّ يُنجِيهِ
Na (pia atatamani kutoa fidia kwa kulipa) vyote vilivyomo ardhini (duniani) kisha (ili) vimuokoe
كَلَّآۖ إِنَّهَا لَظَىٰ
Sio hivyo (Hayawezekani hayo). Kwa hakika, huo ni Moto mkali kabisa
نَزَّاعَةٗ لِّلشَّوَىٰ
Unaobabua kwa nguvu ngozi ya kichwani na mwilini
تَدۡعُواْ مَنۡ أَدۡبَرَ وَتَوَلَّىٰ
Unamwita yule aliyegeuza mgongo (aliyepuuza muongozo wa Allah) na akakengeuka
وَجَمَعَ فَأَوۡعَىٰٓ
Na akakusanya (mali) kisha akayahifadhi (katika makasha)
۞إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ خُلِقَ هَلُوعًا
Hakika, mwanadamu ameumbwa akiwa mwenye pupa (mwenye kukosa subira)
إِذَا مَسَّهُ ٱلشَّرُّ جَزُوعٗا
Inapomgusa shari anakuwa mwingi wa kupapatika (kulalamika na kuhuzunika)
وَإِذَا مَسَّهُ ٱلۡخَيۡرُ مَنُوعًا
Na inapomgusa kheri (anakuwa) mwingi wa kuzuia (bahili)
إِلَّا ٱلۡمُصَلِّينَ
Isipokuwa wenye kuswali
ٱلَّذِينَ هُمۡ عَلَىٰ صَلَاتِهِمۡ دَآئِمُونَ
Ambao wenye kudumisha Sala zao
وَٱلَّذِينَ فِيٓ أَمۡوَٰلِهِمۡ حَقّٞ مَّعۡلُومٞ
Na wale ambao katika Mali zao kuna haki maalumu
لِّلسَّآئِلِ وَٱلۡمَحۡرُومِ
Kwa (Masikini) mwenye kuomba na anaye jizuilia kuomba
وَٱلَّذِينَ يُصَدِّقُونَ بِيَوۡمِ ٱلدِّينِ
Na ambao wanasadikisha Siku ya Malipo, (siku ya Kiyama)
وَٱلَّذِينَ هُم مِّنۡ عَذَابِ رَبِّهِم مُّشۡفِقُونَ
Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao
إِنَّ عَذَابَ رَبِّهِمۡ غَيۡرُ مَأۡمُونٖ
Hakika adhabu ya Mola wao si ya kusalimika nayo
وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِفُرُوجِهِمۡ حَٰفِظُونَ
Na ambao wanahifadhi tupu zao
إِلَّا عَلَىٰٓ أَزۡوَٰجِهِمۡ أَوۡ مَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُهُمۡ فَإِنَّهُمۡ غَيۡرُ مَلُومِينَ
Isipokuwa kwa wake zao, au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao si wenye kulaumiwa