ٱلرَّحۡمَٰنُ
(Allah) Mwingi wa rehma
Share :
عَلَّمَ ٱلۡقُرۡءَانَ
Amefundisha Qur’ani
خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ
Amemumba mwanadamu
عَلَّمَهُ ٱلۡبَيَانَ
Amemfundisha kusema (yaliyomo moyoni)
ٱلشَّمۡسُ وَٱلۡقَمَرُ بِحُسۡبَانٖ
Jua na mwezi (vinatembea) kwa hesabu (na mpangilio maalum)
وَٱلنَّجۡمُ وَٱلشَّجَرُ يَسۡجُدَانِ
Na nyota na miti vinasujudu
وَٱلسَّمَآءَ رَفَعَهَا وَوَضَعَ ٱلۡمِيزَانَ
Na mbingu ameinyanyua na ameweka mizani (kuthibitisha uadilifu na usawa)
أَلَّا تَطۡغَوۡاْ فِي ٱلۡمِيزَانِ
(Ameweka mizani) Ili msifanye dhulma katika upimaji
وَأَقِيمُواْ ٱلۡوَزۡنَ بِٱلۡقِسۡطِ وَلَا تُخۡسِرُواْ ٱلۡمِيزَانَ
Na simamisheni mzani kwa uadilifu na msipunguze mizani
وَٱلۡأَرۡضَ وَضَعَهَا لِلۡأَنَامِ
Na ardhi ameiweka kwa ajili ya viumbe
فِيهَا فَٰكِهَةٞ وَٱلنَّخۡلُ ذَاتُ ٱلۡأَكۡمَامِ
Humo mna matunda na mitende yenye makole
وَٱلۡحَبُّ ذُو ٱلۡعَصۡفِ وَٱلرَّيۡحَانُ
Na punje (nafaka ) zenye majani (makapi) na harufu nzuri
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni zipi neema za Mola wenu mnazikanusha?
خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ مِن صَلۡصَٰلٖ كَٱلۡفَخَّارِ
Amemuumba mwanadamu kutokana na udongo utowao sauti kama vyombo vya udongo vilivyochomwa
وَخَلَقَ ٱلۡجَآنَّ مِن مَّارِجٖ مِّن نَّارٖ
Na Akaumba majini kutokana na ulimi wa moto
Basi ni zipi neema za Molawenu mnazikanusha?
رَبُّ ٱلۡمَشۡرِقَيۡنِ وَرَبُّ ٱلۡمَغۡرِبَيۡنِ
Mola wa Mashariki mbili na Mola wa Magharibi mbili
مَرَجَ ٱلۡبَحۡرَيۡنِ يَلۡتَقِيَانِ
Ameziachilia bahari mbili zina-kutana
بَيۡنَهُمَا بَرۡزَخٞ لَّا يَبۡغِيَانِ
Baina yake kuna kizuizi; hazivu-kiani mipaka
يَخۡرُجُ مِنۡهُمَا ٱللُّؤۡلُؤُ وَٱلۡمَرۡجَانُ
Zinatoka humo lulu na marijani
وَلَهُ ٱلۡجَوَارِ ٱلۡمُنشَـَٔاتُ فِي ٱلۡبَحۡرِ كَٱلۡأَعۡلَٰمِ
Na ana yeye jahazi zilizoten-genezwa baharini kama milima
كُلُّ مَنۡ عَلَيۡهَا فَانٖ
Kila aliyekuwa juu yake (ardhini) ni mwenye kutoweka
وَيَبۡقَىٰ وَجۡهُ رَبِّكَ ذُو ٱلۡجَلَٰلِ وَٱلۡإِكۡرَامِ
Na atabakia Mwenyewe Mola wako mlezi mwenye utukufu na ukarimu
يَسۡـَٔلُهُۥ مَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ كُلَّ يَوۡمٍ هُوَ فِي شَأۡنٖ
Wanamuomba Yeye kila aliyeku-wepo mbinguni na ardhini, kila siku Yeye Yumo katika kujaalia mambo