أَتَىٰٓ أَمۡرُ ٱللَّهِ فَلَا تَسۡتَعۡجِلُوهُۚ سُبۡحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ
Amri ya Allah imefika. Basi msiihimize. Utakasifu ni wake Allah, na ametukuka (juu) ya vyote wanavyovishirikisha naye
يُنَزِّلُ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةَ بِٱلرُّوحِ مِنۡ أَمۡرِهِۦ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦٓ أَنۡ أَنذِرُوٓاْ أَنَّهُۥ لَآ إِلَٰهَ إِلَّآ أَنَا۠ فَٱتَّقُونِ
Anateremsha Malaika (Jibrili) na wahyi kwa amri yake kwa amtakaye miongoni mwa waja wake (Mitume)(akiwaambia kuwa): Waonyeni watu, wajue kwamba: Hakika hakuna wa kuabudiwa kwa haki isipokuwa mimi tu; basi niogopeni
خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّۚ تَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ
Ameziumba mbingu na ardhi kwa haki. Ametukuka Allah na ametukuka (juu zaidi) ya vyote wanavyovishirikisha naye
خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ مِن نُّطۡفَةٖ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٞ مُّبِينٞ
Amemuumba mwanadamu kutokana na tone la manii, ghafla amekuwa mshindani aliye dhahiri mno
وَٱلۡأَنۡعَٰمَ خَلَقَهَاۖ لَكُمۡ فِيهَا دِفۡءٞ وَمَنَٰفِعُ وَمِنۡهَا تَأۡكُلُونَ
Na wanyama amewaumba kwa ajili yenu, katika hao mnapata joto na manufaa (mbali mbali), na baadhi yao mnawala
وَلَكُمۡ فِيهَا جَمَالٌ حِينَ تُرِيحُونَ وَحِينَ تَسۡرَحُونَ
Na nipambo kwenu pale mnapowarudisha jioni na mnapowapeleka malishoni asubuhi
وَتَحۡمِلُ أَثۡقَالَكُمۡ إِلَىٰ بَلَدٖ لَّمۡ تَكُونُواْ بَٰلِغِيهِ إِلَّا بِشِقِّ ٱلۡأَنفُسِۚ إِنَّ رَبَّكُمۡ لَرَءُوفٞ رَّحِيمٞ
Na (baadhi ya wanyama hao) wanawabebea mizigo yenu kupeleka kwenye mji msikoweza kufika isipokuwa kwa juhudi na taabu kubwa. Hakika Mola wenu mlezi ni mpole sana, mwenye kurehemu
وَٱلۡخَيۡلَ وَٱلۡبِغَالَ وَٱلۡحَمِيرَ لِتَرۡكَبُوهَا وَزِينَةٗۚ وَيَخۡلُقُ مَا لَا تَعۡلَمُونَ
Na (amewaumba) farasi na nyumbu na punda ili muwapande (katika safari zenu) na mapambo, na anaumba msivyovijua
وَعَلَى ٱللَّهِ قَصۡدُ ٱلسَّبِيلِ وَمِنۡهَا جَآئِرٞۚ وَلَوۡ شَآءَ لَهَدَىٰكُمۡ أَجۡمَعِينَ
Na ni kwa Allah tu (kunako-bainishwa) njia iliyo sawa, na miongoni mwa njia zipo zisizo sawa. Na lau angependa (Mola wako mlezi), bila shaka angewaongozeni nyote
هُوَ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗۖ لَّكُم مِّنۡهُ شَرَابٞ وَمِنۡهُ شَجَرٞ فِيهِ تُسِيمُونَ
Ni yeye ambaye ameteremsha kwa ajili yenu maji (mvua) kutoka mawinguni; baadhi yake mna-kunywa na baadhi yake anaoteshea miti (mnachungia wanyama wenu)
يُنۢبِتُ لَكُم بِهِ ٱلزَّرۡعَ وَٱلزَّيۡتُونَ وَٱلنَّخِيلَ وَٱلۡأَعۡنَٰبَ وَمِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّقَوۡمٖ يَتَفَكَّرُونَ
Anaotesha kwa ajili yenu kutokana na mvua mimea ya kila aina na mizaituni na mitende na mizabibu na kila matunda. Bila shaka katika hayo kuna ishara (kuhusu uweza wa Allah) kwa watu wenye kufikiri
وَسَخَّرَ لَكُمُ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَ وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَۖ وَٱلنُّجُومُ مُسَخَّرَٰتُۢ بِأَمۡرِهِۦٓۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَعۡقِلُونَ
Na amewadhalilishia usiku na mchana, na jua na mwezi, na nyota zimetiishwa kwa amri yake. Hakika katika hayo kuna ishara (juu ya uwepo wa Allah) kwa watu wenye akili
وَمَا ذَرَأَ لَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُخۡتَلِفًا أَلۡوَٰنُهُۥٓۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّقَوۡمٖ يَذَّكَّرُونَ
Na vyote alivyowaumbieni katika ardhi vyenye rangi mbalimbali (vinawatiini). Hakika katika hayo kuna ishara (za kuwepo kwa uweza wake) kwa watu wanaokumbuka
وَهُوَ ٱلَّذِي سَخَّرَ ٱلۡبَحۡرَ لِتَأۡكُلُواْ مِنۡهُ لَحۡمٗا طَرِيّٗا وَتَسۡتَخۡرِجُواْ مِنۡهُ حِلۡيَةٗ تَلۡبَسُونَهَاۖ وَتَرَى ٱلۡفُلۡكَ مَوَاخِرَ فِيهِ وَلِتَبۡتَغُواْ مِن فَضۡلِهِۦ وَلَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ
Na ni Yeye ambaye ameidhalilisha bahari ili (mvue) humo (samaki) mle nyama iliyombichi[1], na mtoe humo (lulu na marijani) mapambo mtakayovaa. Na utaona jahazi zikipasua humo (kuenda na kurudi), na ili mtafute fadhila zake na ili mpate kushukuru
1- - Maana ya mbichi hapa kinyume chake ni ukavu maana yake mle nyama ya samaki walio freshi na sio wabichi bila kupikwa.
وَأَلۡقَىٰ فِي ٱلۡأَرۡضِ رَوَٰسِيَ أَن تَمِيدَ بِكُمۡ وَأَنۡهَٰرٗا وَسُبُلٗا لَّعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ
Na akaweka ardhini milima (majabali) madhubuti ili ituliye (isiiname upande mmoja) isiwamwage, na mito na njia ilimpate kuongoka (njia iliyo sawa)
وَعَلَٰمَٰتٖۚ وَبِٱلنَّجۡمِ هُمۡ يَهۡتَدُونَ
Na (ameweka ardhini) alama, (mnazotumia kujua njia) na kwa nyota wao wanajiongoza
أَفَمَن يَخۡلُقُ كَمَن لَّا يَخۡلُقُۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ
Hivi, (mnamfanya) Allah anayeumba kuwa sawa na yule asiyeumba chochote?! Hivi, ham-kumbuki (hilo mkampwekesha)?
وَإِن تَعُدُّواْ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ لَا تُحۡصُوهَآۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ
Na kama mkihesabu neema za Allah (kwenu) hamtaweza kuzidhibiti. Hakika Allah ni msamehevu sana mwenye rehema
وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعۡلِنُونَ
Na Allah anayajua zaidi yale mnayoficha na mnayotangaza
وَٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ لَا يَخۡلُقُونَ شَيۡـٔٗا وَهُمۡ يُخۡلَقُونَ
Na wale wanaowaomba (Miungu wengine) badala ya Allah (Miungu hiyo) haina uwezo wakuumba chochote, bali wao ndio wameumbwa
أَمۡوَٰتٌ غَيۡرُ أَحۡيَآءٖۖ وَمَا يَشۡعُرُونَ أَيَّانَ يُبۡعَثُونَ
(Hivyo vyote) ni vitu visivyo na uhai, nahavijui lini Allah atawafufua wanaowaabudu (kisha kuwaingiza Motoni pamoja)
إِلَٰهُكُمۡ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞۚ فَٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ قُلُوبُهُم مُّنكِرَةٞ وَهُم مُّسۡتَكۡبِرُونَ
Mungu wenu ni Mungu mmoja; Basi walewasioiamini Akhera nyoyo zao zinapinga tu ilhali wao wanafanya kiburi (kuikubali haki.)
لَا جَرَمَ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعۡلِنُونَۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُسۡتَكۡبِرِينَ
Kweli kabisa kwa hakika Allah anajua wanayoficha na wanayotangaza. Kwa hakika yeye hawapendi wenye kiburi
وَإِذَا قِيلَ لَهُم مَّاذَآ أَنزَلَ رَبُّكُمۡ قَالُوٓاْ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ
Na pindi wanapoulizwa (Washirikina wa Makkah): Hivi nini ameteremsha Mola wenu mlezi (kwa Muhammad)? Wanasema: (Si chochote) ni hadithi tu za (watu) wa kale
لِيَحۡمِلُوٓاْ أَوۡزَارَهُمۡ كَامِلَةٗ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَمِنۡ أَوۡزَارِ ٱلَّذِينَ يُضِلُّونَهُم بِغَيۡرِ عِلۡمٍۗ أَلَا سَآءَ مَا يَزِرُونَ
Ili (mwisho) wabebe madhambi yaokamili Siku ya Kiyama, na sehemu ya madhambi ya wale wanaowapoteza bila ya kujua. Sikilizeni! Ni mabaya sana wanayobeba
قَدۡ مَكَرَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ فَأَتَى ٱللَّهُ بُنۡيَٰنَهُم مِّنَ ٱلۡقَوَاعِدِ فَخَرَّ عَلَيۡهِمُ ٱلسَّقۡفُ مِن فَوۡقِهِمۡ وَأَتَىٰهُمُ ٱلۡعَذَابُ مِنۡ حَيۡثُ لَا يَشۡعُرُونَ
Hakika walifanya vitimbi wale waliokuwa kabla yao, na Allah akawapelekea adhabu kuanzia katika misingi ya nyumba zao, basi dari zikawaangukia juu yao; na ikawafika adhabu bila wao kuhisi
ثُمَّ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ يُخۡزِيهِمۡ وَيَقُولُ أَيۡنَ شُرَكَآءِيَ ٱلَّذِينَ كُنتُمۡ تُشَـٰٓقُّونَ فِيهِمۡۚ قَالَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡعِلۡمَ إِنَّ ٱلۡخِزۡيَ ٱلۡيَوۡمَ وَٱلسُّوٓءَ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ
Kisha Siku ya Kiyama atawa-fedhehesha na atawauliza: Wako wapi washirika wangu ambao kwa ajili yao mlikuwa mkigombana (na Manabii)? Watasema wale waliopewa elimu: Hakika leo fed-heha na ubaya vitawafika makafiri,
ٱلَّذِينَ تَتَوَفَّىٰهُمُ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ ظَالِمِيٓ أَنفُسِهِمۡۖ فَأَلۡقَوُاْ ٱلسَّلَمَ مَا كُنَّا نَعۡمَلُ مِن سُوٓءِۭۚ بَلَىٰٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمُۢ بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Wale ambao Malaika wame-wafisha ilhali wamedhulumu nafsi zao. Nawakajisalimisha kwa Allah (wakisema): hatukuwa tukifanya uovu wowote. Naam, hakika Allah anajua sana mliyokuwa mkiyatenda
فَٱدۡخُلُوٓاْ أَبۡوَٰبَ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَاۖ فَلَبِئۡسَ مَثۡوَى ٱلۡمُتَكَبِّرِينَ
Basi ingieni katika milango ya Jahannamu mtakaa humo milele. Na niubaya ulioje wamafikio kwa wafanyao kiburi
۞وَقِيلَ لِلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ مَاذَآ أَنزَلَ رَبُّكُمۡۚ قَالُواْ خَيۡرٗاۗ لِّلَّذِينَ أَحۡسَنُواْ فِي هَٰذِهِ ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٞۚ وَلَدَارُ ٱلۡأٓخِرَةِ خَيۡرٞۚ وَلَنِعۡمَ دَارُ ٱلۡمُتَّقِينَ
Na wakaaulizwa wale waliomcha (Allah): Hivi ni kipi ameteremsha Mola wenu mlezi? Watasema: Ni kheri tupu. Ama wale waliofanya wema katika hii dunia watapata wema, na hakika nyumba ya Akhera ni nzuri zaidi; na hakika ni nyumba bora ya Wacha Mungu