Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 86

إِنَّ رَبَّكَ هُوَ ٱلۡخَلَّـٰقُ ٱلۡعَلِيمُ

Hakika Mola wako Mlezi ndiye Muumbaji (wa kila kitu tena) Mjuzi sana



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 2

يُنَزِّلُ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةَ بِٱلرُّوحِ مِنۡ أَمۡرِهِۦ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦٓ أَنۡ أَنذِرُوٓاْ أَنَّهُۥ لَآ إِلَٰهَ إِلَّآ أَنَا۠ فَٱتَّقُونِ

Anateremsha Malaika (Jibrili) na wahyi kwa amri yake kwa amtakaye miongoni mwa waja wake (Mitume)(akiwaambia kuwa): Waonyeni watu, wajue kwamba: Hakika hakuna wa kuabudiwa kwa haki isipokuwa mimi tu; basi niogopeni



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 3

خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّۚ تَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ

Ameziumba mbingu na ardhi kwa haki. Ametukuka Allah na ametukuka (juu zaidi) ya vyote wanavyovishirikisha naye



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 4

خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ مِن نُّطۡفَةٖ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٞ مُّبِينٞ

Amemuumba mwanadamu kutokana na tone la manii, ghafla amekuwa mshindani aliye dhahiri mno



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 5

وَٱلۡأَنۡعَٰمَ خَلَقَهَاۖ لَكُمۡ فِيهَا دِفۡءٞ وَمَنَٰفِعُ وَمِنۡهَا تَأۡكُلُونَ

Na wanyama amewaumba kwa ajili yenu, katika hao mnapata joto na manufaa (mbali mbali), na baadhi yao mnawala



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 9

وَعَلَى ٱللَّهِ قَصۡدُ ٱلسَّبِيلِ وَمِنۡهَا جَآئِرٞۚ وَلَوۡ شَآءَ لَهَدَىٰكُمۡ أَجۡمَعِينَ

Na ni kwa Allah tu (kunako-bainishwa) njia iliyo sawa, na miongoni mwa njia zipo zisizo sawa. Na lau angependa (Mola wako mlezi), bila shaka angewaongozeni nyote



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 18

وَإِن تَعُدُّواْ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ لَا تُحۡصُوهَآۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na kama mkihesabu neema za Allah (kwenu) hamtaweza kuzidhibiti. Hakika Allah ni msamehevu sana mwenye rehema



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 19

وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعۡلِنُونَ

Na Allah anayajua zaidi yale mnayoficha na mnayotangaza



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 22

إِلَٰهُكُمۡ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞۚ فَٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ قُلُوبُهُم مُّنكِرَةٞ وَهُم مُّسۡتَكۡبِرُونَ

Mungu wenu ni Mungu mmoja; Basi walewasioiamini Akhera nyoyo zao zinapinga tu ilhali wao wanafanya kiburi (kuikubali haki.)



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 23

لَا جَرَمَ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعۡلِنُونَۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُسۡتَكۡبِرِينَ

Kweli kabisa kwa hakika Allah anajua wanayoficha na wanayotangaza. Kwa hakika yeye hawapendi wenye kiburi



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 28

ٱلَّذِينَ تَتَوَفَّىٰهُمُ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ ظَالِمِيٓ أَنفُسِهِمۡۖ فَأَلۡقَوُاْ ٱلسَّلَمَ مَا كُنَّا نَعۡمَلُ مِن سُوٓءِۭۚ بَلَىٰٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمُۢ بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Wale ambao Malaika wame-wafisha ilhali wamedhulumu nafsi zao. Nawakajisalimisha kwa Allah (wakisema): hatukuwa tukifanya uovu wowote. Naam, hakika Allah anajua sana mliyokuwa mkiyatenda



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 40

إِنَّمَا قَوۡلُنَا لِشَيۡءٍ إِذَآ أَرَدۡنَٰهُ أَن نَّقُولَ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ

Hakika si vingine ni kauli yetu tu tunapotaka kitu tunakiambia kuwa, basi kinakuwa



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 42

ٱلَّذِينَ صَبَرُواْ وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ

(Hao ni) wale waliosubiri na wakamtegemea Mola wao mlezi



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 51

۞وَقَالَ ٱللَّهُ لَا تَتَّخِذُوٓاْ إِلَٰهَيۡنِ ٱثۡنَيۡنِۖ إِنَّمَا هُوَ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞ فَإِيَّـٰيَ فَٱرۡهَبُونِ

Na amesema Allah: Kamwe msiwe na Miungu kuwa wawili, hakika sivingine Mungu ni mmoja tu: basi mimi tu niogopeni



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 53

وَمَا بِكُم مِّن نِّعۡمَةٖ فَمِنَ ٱللَّهِۖ ثُمَّ إِذَا مَسَّكُمُ ٱلضُّرُّ فَإِلَيۡهِ تَجۡـَٔرُونَ

Na neema yeyote mliyonayo imetoka kwa Allah. Kisha inapowaguseni dhara, basi yeye tu mnamlilia



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 61

وَلَوۡ يُؤَاخِذُ ٱللَّهُ ٱلنَّاسَ بِظُلۡمِهِم مَّا تَرَكَ عَلَيۡهَا مِن دَآبَّةٖ وَلَٰكِن يُؤَخِّرُهُمۡ إِلَىٰٓ أَجَلٖ مُّسَمّٗىۖ فَإِذَا جَآءَ أَجَلُهُمۡ لَا يَسۡتَـٔۡخِرُونَ سَاعَةٗ وَلَا يَسۡتَقۡدِمُونَ

Na lau Allah angewachukulia hatua watu kwasababu ya dhuluma yao, asingemuacha hata mnyama mmoja; Lakini anawasubirisha mpaka muda uliowekwa; Na utakapofika muda wao, hawataweza kuichelewesha saa moja na hawataweza kuiwahisha



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 65

وَٱللَّهُ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَحۡيَا بِهِ ٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ مَوۡتِهَآۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّقَوۡمٖ يَسۡمَعُونَ

Na Allah ameteremsha maji kutoka mbinguni na akahuisha kwa maji hayo ardhi baada ya kufa kwake (kwa ukame). Kwa hakika katika hayo (ya kuteremsha mvua na kuhuisha ardhi) kuna ishara ya wazi (juu ya uwepo wa Allah) kwa watu wanaosikia (na kuzingatia)



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 71

وَٱللَّهُ فَضَّلَ بَعۡضَكُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖ فِي ٱلرِّزۡقِۚ فَمَا ٱلَّذِينَ فُضِّلُواْ بِرَآدِّي رِزۡقِهِمۡ عَلَىٰ مَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُهُمۡ فَهُمۡ فِيهِ سَوَآءٌۚ أَفَبِنِعۡمَةِ ٱللَّهِ يَجۡحَدُونَ

Na Allah amewapa ubora (ziada) baadhi yenu kwa wengine katika riziki[1]. Lakini wale walio fadhilishwa hawarudishi riziki zao kwa wale walio wamiliki kwa mikono yao ya kuume ili wawe sawa katika (riziki) hiyo. Hivo basi, wanazipinga neema za Allah?


1- - Allah katika Aya hii anaelezea dhana ya Washirikishaji na ubaya wao,. Allah amewafadhilisha watu wao kwa wao akawafanya baadhi matajiri na wengine mafakiri, masikini, watumwa na walio huru. Kisha anawauliza matajiri walio washirikishaji hivi ni kwanini wanavishirikisha na yeye Allah katika kuviabudu hivyo kama wanavyo muabudu yeye ilhali wao hawawashirikishi watumwa wao katika matumizi ya mali wanazo zimiliki wakawa sawasawa anamalizia kwa kusema hii ni dhuluma kubwa ambayo wao wameikataa kwa watumwa wao na wameiridhia kwa Allah.


Surah: ANNAHLI 

Ayah : 74

فَلَا تَضۡرِبُواْ لِلَّهِ ٱلۡأَمۡثَالَۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ وَأَنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ

Na msimpigie Allah mifano. Hakika Allah anajua na ninyi hamjui (chochote)



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 81

وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّمَّا خَلَقَ ظِلَٰلٗا وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ ٱلۡجِبَالِ أَكۡنَٰنٗا وَجَعَلَ لَكُمۡ سَرَٰبِيلَ تَقِيكُمُ ٱلۡحَرَّ وَسَرَٰبِيلَ تَقِيكُم بَأۡسَكُمۡۚ كَذَٰلِكَ يُتِمُّ نِعۡمَتَهُۥ عَلَيۡكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تُسۡلِمُونَ

Na Allah amewafanyieni katika vile alivyoviumba, vitiavyo kivuli (kama miti na milima) na amewafanyieni milima kuwa sehemu ya kukimbilia, na amewafanyieni kanzu zinazowakingeni na joto, na dereya[1] zinazowakingeni katika vita vyenu. Hivi ndivyo (Allah) anatimiza neema zake kwenu ili mpate kutii


1- - Ni vazi la chuma linalovaliwa vitani kujikinga na mikuki na silaha zote (proof)


Surah: ANNAHLI 

Ayah : 83

يَعۡرِفُونَ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ ثُمَّ يُنكِرُونَهَا وَأَكۡثَرُهُمُ ٱلۡكَٰفِرُونَ

Wanazijua neema za Allah kisha wanazipinga na wengi wao ni makafiri



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 91

وَأَوۡفُواْ بِعَهۡدِ ٱللَّهِ إِذَا عَٰهَدتُّمۡ وَلَا تَنقُضُواْ ٱلۡأَيۡمَٰنَ بَعۡدَ تَوۡكِيدِهَا وَقَدۡ جَعَلۡتُمُ ٱللَّهَ عَلَيۡكُمۡ كَفِيلًاۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا تَفۡعَلُونَ

Na timizeni ahadi ya Allah mnapoahidi; na msivunje viapo baada ya kuvithibitisha, na hakika mlishamfanya Allah kuwa mdhamini wenu. Hakika Allah anayajua mnayoyafanya



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 93

وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَجَعَلَكُمۡ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗ وَلَٰكِن يُضِلُّ مَن يَشَآءُ وَيَهۡدِي مَن يَشَآءُۚ وَلَتُسۡـَٔلُنَّ عَمَّا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Na Allah angelitaka, kwa yakini angeliwafanyeni umma moja; lakini anayetaka (upotevu) anampoteza, na anayetaka (mwongozo) anamwongoza; na hakika mtaulizwa yale mliyokuwa mkiyafanya



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 99

إِنَّهُۥ لَيۡسَ لَهُۥ سُلۡطَٰنٌ عَلَى ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ

Hakika yeye hana nguvu juu ya wale walioamini na kwa Mola wao mlezi tu wanategemea



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 106

مَن كَفَرَ بِٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ إِيمَٰنِهِۦٓ إِلَّا مَنۡ أُكۡرِهَ وَقَلۡبُهُۥ مُطۡمَئِنُّۢ بِٱلۡإِيمَٰنِ وَلَٰكِن مَّن شَرَحَ بِٱلۡكُفۡرِ صَدۡرٗا فَعَلَيۡهِمۡ غَضَبٞ مِّنَ ٱللَّهِ وَلَهُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٞ

Hakika anayezusha uongo ni Yule aliyetamka neno la ukafiri baada ya imani isipokuwa tu yule aliyeshurutishwa, ilhali moyo wake unabaki imara katika imani. Lakini wale ambao mioyo yao imeridhika na ukafiri, basi ghadhabu za Allah zitawashukia, na watapata adhabu kubwa



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 110

ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ هَاجَرُواْ مِنۢ بَعۡدِ مَا فُتِنُواْ ثُمَّ جَٰهَدُواْ وَصَبَرُوٓاْ إِنَّ رَبَّكَ مِنۢ بَعۡدِهَا لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ

Kisha hakika Mola wako mlezi, kwa wale waliohama baada ya kuteswa, kisha wakajitahidi na wakasubiri, bila shaka Mola wako mlezi baada ya hayo ni msamehevu sana, mwenye rehema



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 114

فَكُلُواْ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ حَلَٰلٗا طَيِّبٗا وَٱشۡكُرُواْ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ إِيَّاهُ تَعۡبُدُونَ

Na kuleni katika vile alivyo-waruzukuni Allah, vilivyo halali na vizuri na shukuruni neema za Allah ikiwa nyinyi mnamuabudu yeye tu



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 115

إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡمَيۡتَةَ وَٱلدَّمَ وَلَحۡمَ ٱلۡخِنزِيرِ وَمَآ أُهِلَّ لِغَيۡرِ ٱللَّهِ بِهِۦۖ فَمَنِ ٱضۡطُرَّ غَيۡرَ بَاغٖ وَلَا عَادٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Kwa hakika (Allah) amewa-haramishia (katika wanyama) mzoga na damu (iliyomwagika baada ya mnyama kuchinjwa) na nyama ya nguruwe na (mnyama) aliyechinjwa si kwa ajili ya Allah (kama kuchinja kwa ajili ya mashetani). Lakini atakayelazimika (kula nyama hiyo kwa njaa asife kwa kukosa mbadala), bila kuasi wala kuchupa mipaka, basi hakika Allah ni msamehevu, mwenye rehema



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 116

وَلَا تَقُولُواْ لِمَا تَصِفُ أَلۡسِنَتُكُمُ ٱلۡكَذِبَ هَٰذَا حَلَٰلٞ وَهَٰذَا حَرَامٞ لِّتَفۡتَرُواْ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَفۡتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ لَا يُفۡلِحُونَ

Na msiseme (enyi washirikina), kwa uongo ambao usemwao na ndimi zenu kuwa, hii halali (kwanini Allah ameiharamisha) na hii haramu (kwanini ameihalalisha), ili kumzulia Allah uongo. Hakika wale wamzuliao Allah uongo hawatafaulu[1]


1- - Katika Aya hii Allah anabainisha kuwa uhalali wa kitu na uharamu hatokani na utashi wa mtu ama watu, bali ni msingi uliyowekwa na Allah mwenyewe kwa viumbe wake, hivyo anawakemea washirikishaji na Makafiri kwa ujumla, wasihalalishe au kuharamisha kitu kwa utashi wa nafsi zao. Kilicho halali ni kile alicha halalisha Allah, na haramu ni kile alicho kiharamisha Allah.


Surah: ANNAHLI 

Ayah : 119

ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ عَمِلُواْ ٱلسُّوٓءَ بِجَهَٰلَةٖ ثُمَّ تَابُواْ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ وَأَصۡلَحُوٓاْ إِنَّ رَبَّكَ مِنۢ بَعۡدِهَا لَغَفُورٞ رَّحِيمٌ

Kisha hakika Mola wako mlezi kwa wale waliofanya ubaya (dhambi) kwa kutokujua, kisha wakatubu baada ya hayo na waka-tenda mema, hakika bila shaka Mola wako baada ya hayo ni mwingi wa kusamehe, mwenye rehema