Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 109

وَدَّ كَثِيرٞ مِّنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ لَوۡ يَرُدُّونَكُم مِّنۢ بَعۡدِ إِيمَٰنِكُمۡ كُفَّارًا حَسَدٗا مِّنۡ عِندِ أَنفُسِهِم مِّنۢ بَعۡدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ ٱلۡحَقُّۖ فَٱعۡفُواْ وَٱصۡفَحُواْ حَتَّىٰ يَأۡتِيَ ٱللَّهُ بِأَمۡرِهِۦٓۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Watu wa Kitabu wengi wanapenda laiti wakurudisheni muwe makafiri baada ya kuamini kwenu, kwa sababu ya husuda iliyomo nyoyoni mwao baada ya kuwa haki imewapambanukia. Basi sameheni na puuzeni mpaka Allah alete amri yake. Hakika, Allah ni Muweza sana wa kila jambo



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 178

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُتِبَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡقِصَاصُ فِي ٱلۡقَتۡلَىۖ ٱلۡحُرُّ بِٱلۡحُرِّ وَٱلۡعَبۡدُ بِٱلۡعَبۡدِ وَٱلۡأُنثَىٰ بِٱلۡأُنثَىٰۚ فَمَنۡ عُفِيَ لَهُۥ مِنۡ أَخِيهِ شَيۡءٞ فَٱتِّبَاعُۢ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَأَدَآءٌ إِلَيۡهِ بِإِحۡسَٰنٖۗ ذَٰلِكَ تَخۡفِيفٞ مِّن رَّبِّكُمۡ وَرَحۡمَةٞۗ فَمَنِ ٱعۡتَدَىٰ بَعۡدَ ذَٰلِكَ فَلَهُۥ عَذَابٌ أَلِيمٞ

Enyi mlioamini, mmeandikiwa kulipa kisasi katika waliouawa; muungwana kwa muungwana na mtumwa kwa mtumwa na mwanamke kwa mwanamke. Na aliyesamehewa jambo na ndugu yake (mtendewa jinai) basi fidia ifuatiliwe kwa wema na atekelezewe kwa uzuri. Hiyo ni tahafifu itokayo kwa Mola wenu na ni rehema. Na atakayekiuka baada ya hayo, basi yeye atapata adhabu iumizayo



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 237

وَإِن طَلَّقۡتُمُوهُنَّ مِن قَبۡلِ أَن تَمَسُّوهُنَّ وَقَدۡ فَرَضۡتُمۡ لَهُنَّ فَرِيضَةٗ فَنِصۡفُ مَا فَرَضۡتُمۡ إِلَّآ أَن يَعۡفُونَ أَوۡ يَعۡفُوَاْ ٱلَّذِي بِيَدِهِۦ عُقۡدَةُ ٱلنِّكَاحِۚ وَأَن تَعۡفُوٓاْ أَقۡرَبُ لِلتَّقۡوَىٰۚ وَلَا تَنسَوُاْ ٱلۡفَضۡلَ بَيۡنَكُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٌ

Na endapo mtawaacha kabla ya kuwaingilia na ilhali mmekwisha kadiria mahari, basi wapeni nusu ya mahari mliokadiria, isipokuwa kama wake wenyewe watasamehe au atasamehe yule ambaye kifungo cha ndoa kipo mikononi mwake. Na kama mtasamehe, hilo liko karibu zaidi na Ucha Mungu. Na msisahau utu kati yenu. Hakika, Allah ni Mwenye kuyaona myatendayo



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 134

ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ فِي ٱلسَّرَّآءِ وَٱلضَّرَّآءِ وَٱلۡكَٰظِمِينَ ٱلۡغَيۡظَ وَٱلۡعَافِينَ عَنِ ٱلنَّاسِۗ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

(Wacha Mungu) Ambao wanatoa (katika vile walivyopewa na Allah) katika hali ya wasaa na katika hali ya dhiki, na wenye kuzuia hasira (zao) na kusamehe watu (wanaowakosea). Na Allah anawapenda wafanyao mazuri



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 159

فَبِمَا رَحۡمَةٖ مِّنَ ٱللَّهِ لِنتَ لَهُمۡۖ وَلَوۡ كُنتَ فَظًّا غَلِيظَ ٱلۡقَلۡبِ لَٱنفَضُّواْ مِنۡ حَوۡلِكَۖ فَٱعۡفُ عَنۡهُمۡ وَٱسۡتَغۡفِرۡ لَهُمۡ وَشَاوِرۡهُمۡ فِي ٱلۡأَمۡرِۖ فَإِذَا عَزَمۡتَ فَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُتَوَكِّلِينَ

Basi ni kwa rehema za Allah umekuwa mpole kwao, na lau ungekuwa muovu wa tabia, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangekukimbia, basi samehe na uwaombee msamaha na watake ushauri katika jambo, na ukitia azma ya jambo basi mtegemee Allah, hakika Allah anawapenda wenye kumtegemea



Surah: ANNISAI 

Ayah : 149

إِن تُبۡدُواْ خَيۡرًا أَوۡ تُخۡفُوهُ أَوۡ تَعۡفُواْ عَن سُوٓءٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَفُوّٗا قَدِيرًا

Mkidhihirisha kheri au mkiificha au mkisamehe uovu, basi hakika Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye uwezo



Surah: AL-MAIDA 

Ayah : 13

فَبِمَا نَقۡضِهِم مِّيثَٰقَهُمۡ لَعَنَّـٰهُمۡ وَجَعَلۡنَا قُلُوبَهُمۡ قَٰسِيَةٗۖ يُحَرِّفُونَ ٱلۡكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِۦ وَنَسُواْ حَظّٗا مِّمَّا ذُكِّرُواْ بِهِۦۚ وَلَا تَزَالُ تَطَّلِعُ عَلَىٰ خَآئِنَةٖ مِّنۡهُمۡ إِلَّا قَلِيلٗا مِّنۡهُمۡۖ فَٱعۡفُ عَنۡهُمۡ وَٱصۡفَحۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Basi kwa sababu ya kuvunja kwao makubaliano yao, tuliwalaani na kuzifanya ngumu nyoyo zao; wanayapotosha maneno ya (Allah)[1] katika mahali pake na wameacha sehemu (kubwa) ya yale waliyokumbushwa. Na bado unaendelea kupata habari za khiyana yao isipokuwa wachache miongoni mwao. Basi wasamehe na wapuuze. Hakika, Allah anawapenda wafanyao mazuri


1- - Yaliyomo katika Torati na Injili.


Surah: YUSUF 

Ayah : 92

قَالَ لَا تَثۡرِيبَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡيَوۡمَۖ يَغۡفِرُ ٱللَّهُ لَكُمۡۖ وَهُوَ أَرۡحَمُ ٱلرَّـٰحِمِينَ

(Yusuf) Alisema: Leo hakuna lawama juu yenu. Allah atakusameheni, naye ni Mwenye huruma kuliko wenye huruma wote



Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 85

وَمَا خَلَقۡنَا ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَآ إِلَّا بِٱلۡحَقِّۗ وَإِنَّ ٱلسَّاعَةَ لَأٓتِيَةٞۖ فَٱصۡفَحِ ٱلصَّفۡحَ ٱلۡجَمِيلَ

Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake ila kwa ajili ya Haki. Na hakika Kiyama kitafika tu (wala hilo halina shaka). Basi (Ewe Mtume) samehe (watu wako) msamaha mzuri



Surah: ANNUUR 

Ayah : 22

وَلَا يَأۡتَلِ أُوْلُواْ ٱلۡفَضۡلِ مِنكُمۡ وَٱلسَّعَةِ أَن يُؤۡتُوٓاْ أُوْلِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينَ وَٱلۡمُهَٰجِرِينَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۖ وَلۡيَعۡفُواْ وَلۡيَصۡفَحُوٓاْۗ أَلَا تُحِبُّونَ أَن يَغۡفِرَ ٱللَّهُ لَكُمۡۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٌ

Na wale katika nyinyi wenye fadhila na wasaa wasiape kutowapa jamaa zao na masikini na walio hama katika Njia ya Allah. Na wasamehe, na waachilie mbali. Je! Nyinyi hampendi Allah akusameheni? Na Allah ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu



Surah: ASH-SHUURAA 

Ayah : 37

وَٱلَّذِينَ يَجۡتَنِبُونَ كَبَـٰٓئِرَ ٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡفَوَٰحِشَ وَإِذَا مَا غَضِبُواْ هُمۡ يَغۡفِرُونَ

Na wanayo yaepuka madhambi makubwa na mambo machafu, na wanapo kasirika wao husamehe,



Surah: ASH-SHUURAA 

Ayah : 40

وَجَزَـٰٓؤُاْ سَيِّئَةٖ سَيِّئَةٞ مِّثۡلُهَاۖ فَمَنۡ عَفَا وَأَصۡلَحَ فَأَجۡرُهُۥ عَلَى ٱللَّهِۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Na malipo ya uovu ni uovu mfano wa huo. Lakini mwenye kusamehe, na akasuluhisha, basi huyo malipo yake yapo kwa Allah. Hakika Yeye hawapendi wenye kudhulumu



Surah: ASH-SHUURAA 

Ayah : 43

وَلَمَن صَبَرَ وَغَفَرَ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمِنۡ عَزۡمِ ٱلۡأُمُورِ

Na anaye subiri, na akasamehe, hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa



Surah: AZZUKHRUF 

Ayah : 89

فَٱصۡفَحۡ عَنۡهُمۡ وَقُلۡ سَلَٰمٞۚ فَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ

Basi wasamehe, na uwambie maneno ya salama. Watakuja jua



Surah: AL-JAATHIYA 

Ayah : 14

قُل لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ يَغۡفِرُواْ لِلَّذِينَ لَا يَرۡجُونَ أَيَّامَ ٱللَّهِ لِيَجۡزِيَ قَوۡمَۢا بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ

Waambie walio amini wawa-samehe wale wasio zitaraji siku za Allah, ili awalipe kwa waliyo kuwa wakiyachuma



Surah: ATTAGHAABUN 

Ayah : 14

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِنَّ مِنۡ أَزۡوَٰجِكُمۡ وَأَوۡلَٰدِكُمۡ عَدُوّٗا لَّكُمۡ فَٱحۡذَرُوهُمۡۚ وَإِن تَعۡفُواْ وَتَصۡفَحُواْ وَتَغۡفِرُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ

Enyi walioamini! Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu ni maadui kwenu, basi tahadharini nao. Na mkisamehe na mkapuuza na mkayafutilia mbali, basi hakika Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu