Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 85

ثُمَّ أَنتُمۡ هَـٰٓؤُلَآءِ تَقۡتُلُونَ أَنفُسَكُمۡ وَتُخۡرِجُونَ فَرِيقٗا مِّنكُم مِّن دِيَٰرِهِمۡ تَظَٰهَرُونَ عَلَيۡهِم بِٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡعُدۡوَٰنِ وَإِن يَأۡتُوكُمۡ أُسَٰرَىٰ تُفَٰدُوهُمۡ وَهُوَ مُحَرَّمٌ عَلَيۡكُمۡ إِخۡرَاجُهُمۡۚ أَفَتُؤۡمِنُونَ بِبَعۡضِ ٱلۡكِتَٰبِ وَتَكۡفُرُونَ بِبَعۡضٖۚ فَمَا جَزَآءُ مَن يَفۡعَلُ ذَٰلِكَ مِنكُمۡ إِلَّا خِزۡيٞ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۖ وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ يُرَدُّونَ إِلَىٰٓ أَشَدِّ ٱلۡعَذَابِۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ

Kisha nyinyi hao hao mnauana, na mnalitoa kundi kati yenu katika nyumba zao, mkisaidiana dhidi yao, kwa dhambi na uhasama. Na kama wakikujieni ilhali wakiwa mateka mnawakomboa wakati imeharamishwa kwenu kuwafukuza. Je, mnaamini baadhi ya maandiko na mengine mnayakataa? Basi hakuna malipo kwa mwenye kuyafanya hayo kati yenu isipokuwa tu hizaya katika maisha ya duniani, na Siku ya Kiyama watarejeshwa kwenye adhabu kali zaidi, na Allah si Mwenye kughafilika na yale mnayoyatenda



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 184

أَيَّامٗا مَّعۡدُودَٰتٖۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوۡ عَلَىٰ سَفَرٖ فَعِدَّةٞ مِّنۡ أَيَّامٍ أُخَرَۚ وَعَلَى ٱلَّذِينَ يُطِيقُونَهُۥ فِدۡيَةٞ طَعَامُ مِسۡكِينٖۖ فَمَن تَطَوَّعَ خَيۡرٗا فَهُوَ خَيۡرٞ لَّهُۥۚ وَأَن تَصُومُواْ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Ni siku chache za kuhesabika tu. Na atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu au safarini, basi[1] atimize hesabu katika siku nyingine. Na wale wasioiweza (funga), watoe fidia kwa kumlisha maskini. Na atakayefanya wema kwa ridhaa ya nafsi yake, basi ni bora kwake, na kufunga ni bora kwenu, ikiwa mnajua


1- - Anaruhusiwa kuacha kufunga na atimize.


Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 196

وَأَتِمُّواْ ٱلۡحَجَّ وَٱلۡعُمۡرَةَ لِلَّهِۚ فَإِنۡ أُحۡصِرۡتُمۡ فَمَا ٱسۡتَيۡسَرَ مِنَ ٱلۡهَدۡيِۖ وَلَا تَحۡلِقُواْ رُءُوسَكُمۡ حَتَّىٰ يَبۡلُغَ ٱلۡهَدۡيُ مَحِلَّهُۥۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوۡ بِهِۦٓ أَذٗى مِّن رَّأۡسِهِۦ فَفِدۡيَةٞ مِّن صِيَامٍ أَوۡ صَدَقَةٍ أَوۡ نُسُكٖۚ فَإِذَآ أَمِنتُمۡ فَمَن تَمَتَّعَ بِٱلۡعُمۡرَةِ إِلَى ٱلۡحَجِّ فَمَا ٱسۡتَيۡسَرَ مِنَ ٱلۡهَدۡيِۚ فَمَن لَّمۡ يَجِدۡ فَصِيَامُ ثَلَٰثَةِ أَيَّامٖ فِي ٱلۡحَجِّ وَسَبۡعَةٍ إِذَا رَجَعۡتُمۡۗ تِلۡكَ عَشَرَةٞ كَامِلَةٞۗ ذَٰلِكَ لِمَن لَّمۡ يَكُنۡ أَهۡلُهُۥ حَاضِرِي ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ

Na timizeni Hija na Umra kwa ajili ya Allah. Na ikiwa mmezuiwa[1], basi chinjeni wanyama watakaokuwa rahisi kupatikana. Na wala msinyoe vichwa vyenu, hadi mnyama afike mahali pake. Basi ambaye atakuwa mgonjwa miongoni mwenu, au ana tatizo kichwani kwake, basi atoe fidia ya kufunga au sadaka au mnyama. Na mtakapokuwa katika hali ya amani, atakayefanya Umra kabla ya Hija[2] basi afunge siku tatu katika Hija na siku saba mtakaporejea kwenu. Hizo ni siku kumi kamili. Hilo ni kwa ambaye familia yake sio wakazi wa (mji wa) Msikiti Mtukufu (wa Makka). Na mcheni Allah, na jueni kwamba, Allah ni mkali wa kuadhibu


1- - Kutimiza ibada hizo


2- - Bila kuunganisha Umra na Hija


Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 229

ٱلطَّلَٰقُ مَرَّتَانِۖ فَإِمۡسَاكُۢ بِمَعۡرُوفٍ أَوۡ تَسۡرِيحُۢ بِإِحۡسَٰنٖۗ وَلَا يَحِلُّ لَكُمۡ أَن تَأۡخُذُواْ مِمَّآ ءَاتَيۡتُمُوهُنَّ شَيۡـًٔا إِلَّآ أَن يَخَافَآ أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ ٱللَّهِۖ فَإِنۡ خِفۡتُمۡ أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ ٱللَّهِ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡهِمَا فِيمَا ٱفۡتَدَتۡ بِهِۦۗ تِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِ فَلَا تَعۡتَدُوهَاۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ ٱللَّهِ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ

Talaka ni mara mbili[1]. Basi (baada ya kumrejea) akae naye kwa wema au kumuacha kwa uzuri (aendelee kumaliza Eda yake). Na si halali kwenu kuchukua chochote katika vile mlivyowapa (wake zenu) isipokuwa kama wote wawili wataogopa kukiuka sharia za Allah. Basi kama mtaogopa kuwa hawatatekeleza sharia za Allah, hakuna ubaya kwa wawili (mke kurejesha mahari na mume kupokea) katika kile mwanamke alichojikombolea. Hiyo ni mipaka ya Allah, basi msiikiuke. Na watakaoikiuka mipaka ya Allah basi hao ni madhalimu hasa


1- - Ambazo mume ana haki ya kumrejea mkewe


Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 91

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَمَاتُواْ وَهُمۡ كُفَّارٞ فَلَن يُقۡبَلَ مِنۡ أَحَدِهِم مِّلۡءُ ٱلۡأَرۡضِ ذَهَبٗا وَلَوِ ٱفۡتَدَىٰ بِهِۦٓۗ أُوْلَـٰٓئِكَ لَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ وَمَا لَهُم مِّن نَّـٰصِرِينَ

Hakika, wale waliokufuru na wakafa wakiwa makafiri, kamwe hatakubaliwa mmoja wao hata kama atajikomboa kwa kutoa fidia ya dhahabu ujazo wa ardhi yote. Hao watapata adhabu yenye maumivu makali mno na hawatakuwa na watetezi (wowote)



Surah: AL-MAIDA 

Ayah : 36

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَوۡ أَنَّ لَهُم مَّا فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا وَمِثۡلَهُۥ مَعَهُۥ لِيَفۡتَدُواْ بِهِۦ مِنۡ عَذَابِ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ مَا تُقُبِّلَ مِنۡهُمۡۖ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ

Hakika ya wale waliokufuru, lau kama wangekuwa na yote yaliyomo duniani na mengine kama hayo ili watoe fidia ya kuepukana na adhabu ya Siku ya Kiyama, wasingekubaliwa, na watapata adhabu iumizayo



Surah: YUNUS 

Ayah : 54

وَلَوۡ أَنَّ لِكُلِّ نَفۡسٖ ظَلَمَتۡ مَا فِي ٱلۡأَرۡضِ لَٱفۡتَدَتۡ بِهِۦۗ وَأَسَرُّواْ ٱلنَّدَامَةَ لَمَّا رَأَوُاْ ٱلۡعَذَابَۖ وَقُضِيَ بَيۡنَهُم بِٱلۡقِسۡطِ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ

Na lau kama kila nafsi iliyodhu-lumu ingekuwa inamiliki vyote vilivyomo duniani, bila shaka yoyote ingevitoa fidia (ili kujikomboa isiadhibiwe). Na watakapoiona adhabu wataficha majuto na patahu-kumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawatadhulumiwa



Surah: AR-RA’D 

Ayah : 18

لِلَّذِينَ ٱسۡتَجَابُواْ لِرَبِّهِمُ ٱلۡحُسۡنَىٰۚ وَٱلَّذِينَ لَمۡ يَسۡتَجِيبُواْ لَهُۥ لَوۡ أَنَّ لَهُم مَّا فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا وَمِثۡلَهُۥ مَعَهُۥ لَٱفۡتَدَوۡاْ بِهِۦٓۚ أُوْلَـٰٓئِكَ لَهُمۡ سُوٓءُ ٱلۡحِسَابِ وَمَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمِهَادُ

Wale waliomuitikia Mola wao Mlezi watapata wema (Pepo). Na wale wasiomuitikia, hata wangelikuwa na vyote vilivyomo katika ardhi na mfano wa hivyo, bila ya shaka wangevitoa kujikomboa. Hao watakuwa na hesabu mbaya, na makao yao ni Jahanamu. Napo ni mahala pabaya mno



Surah: ASSWAAFFAAT 

Ayah : 107

وَفَدَيۡنَٰهُ بِذِبۡحٍ عَظِيمٖ

Basi tukamtolea fidia kwa dhabihu (mnyama wa kuchinja) mtukufu



Surah: AZZUMAR 

Ayah : 47

وَلَوۡ أَنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُواْ مَا فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا وَمِثۡلَهُۥ مَعَهُۥ لَٱفۡتَدَوۡاْ بِهِۦ مِن سُوٓءِ ٱلۡعَذَابِ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ وَبَدَا لَهُم مِّنَ ٱللَّهِ مَا لَمۡ يَكُونُواْ يَحۡتَسِبُونَ

Na lau kuwa walio dhulumu wangeli kuwa na vyote viliomo duniani na pamoja navyo vingine kama hivyo, bila ya shaka wangeli vitoa kujikomboa katika adhabu mbaya Siku hiyo ya Kiyama. Na yatawadhihirikia kwa Allah wasiyo kuwa wakiyatarajia



Surah: MUHAMMAD 

Ayah : 4

فَإِذَا لَقِيتُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فَضَرۡبَ ٱلرِّقَابِ حَتَّىٰٓ إِذَآ أَثۡخَنتُمُوهُمۡ فَشُدُّواْ ٱلۡوَثَاقَ فَإِمَّا مَنَّۢا بَعۡدُ وَإِمَّا فِدَآءً حَتَّىٰ تَضَعَ ٱلۡحَرۡبُ أَوۡزَارَهَاۚ ذَٰلِكَۖ وَلَوۡ يَشَآءُ ٱللَّهُ لَٱنتَصَرَ مِنۡهُمۡ وَلَٰكِن لِّيَبۡلُوَاْ بَعۡضَكُم بِبَعۡضٖۗ وَٱلَّذِينَ قُتِلُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ فَلَن يُضِلَّ أَعۡمَٰلَهُمۡ

Basi mnapo wakuta walio kufuru wapigeni shingoni mwao, mpaka mkiwadhoofisha wafungeni pingu. Tena waachilieni kwa hisani au wajikomboe, mpaka vita vipoe. Ndio hivyo. Na lau Allah angelitaka angeli washinda mwenyewe, lakini haya ni kwasababu akutieni mitihani nyinyi kwa nyinyi. Na waliouliwa katika njia ya Allah hatazipoteza amali zao



Surah: AL-HADIID

Ayah : 15

فَٱلۡيَوۡمَ لَا يُؤۡخَذُ مِنكُمۡ فِدۡيَةٞ وَلَا مِنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْۚ مَأۡوَىٰكُمُ ٱلنَّارُۖ هِيَ مَوۡلَىٰكُمۡۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ

Basi leo haitochukuliwa kutoka kwenu fidia na wala kutoka kwa waliokufuru. Makazi yenu ni moto, hayo ndio yanayostahiki kwenu, na ni marejeo mabaya yalioje



Surah: ALMA’RIJ 

Ayah : 11

يُبَصَّرُونَهُمۡۚ يَوَدُّ ٱلۡمُجۡرِمُ لَوۡ يَفۡتَدِي مِنۡ عَذَابِ يَوۡمِئِذِۭ بِبَنِيهِ

Watafanywa waonane. Mkosefu atatamani (kujikomboa) ajitolee fidia kutokana na adhabu Siku hiyo kwa kuwatoa watoto wake