وَمَن يَرۡغَبُ عَن مِّلَّةِ إِبۡرَٰهِـۧمَ إِلَّا مَن سَفِهَ نَفۡسَهُۥۚ وَلَقَدِ ٱصۡطَفَيۡنَٰهُ فِي ٱلدُّنۡيَاۖ وَإِنَّهُۥ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ لَمِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ
Na hakuna anayeichukia dini ya Ibrahimu isipokuwa yule anayejitia upumbavu. Na bila shaka tumemteua duniani, na hakika akhera atakuwa miongoni mwa watu wema
وَقَالُواْ كُونُواْ هُودًا أَوۡ نَصَٰرَىٰ تَهۡتَدُواْۗ قُلۡ بَلۡ مِلَّةَ إِبۡرَٰهِـۧمَ حَنِيفٗاۖ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ
Na wamesema: Kuweni Wayahudi au Wanaswara mtaon-goka. Sema: Bali (tunafuata) dini ya Ibrahimu aliyeacha dini zote potevu na kufuata Uislamu, na hakuwa miongoni mwa washirikina
قُولُوٓاْ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيۡنَا وَمَآ أُنزِلَ إِلَىٰٓ إِبۡرَٰهِـۧمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ وَإِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَ وَٱلۡأَسۡبَاطِ وَمَآ أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَمَآ أُوتِيَ ٱلنَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمۡ لَا نُفَرِّقُ بَيۡنَ أَحَدٖ مِّنۡهُمۡ وَنَحۡنُ لَهُۥ مُسۡلِمُونَ
Semeni: Tumemuamini Allah na tulichoteremshiwa na alichoteremshiwa Ibrahimu na Ismaili na Isihaka na Yakubu na watoto wa Yakubu na alichopewa Musa na Isa, na walichopewa Manabii kutoka kwa Mola wao. Hatumbagui yeyote kati yao, na sisi ni wenye kujisalimsha kwake
مَا كَانَ إِبۡرَٰهِيمُ يَهُودِيّٗا وَلَا نَصۡرَانِيّٗا وَلَٰكِن كَانَ حَنِيفٗا مُّسۡلِمٗا وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ
Ibrahimu hakuwa Myahudi na wala (hakuwa) Mnaswara, lakini alikuwa Muongofu, Muislamu na hakuwa miongoni mwa Washirikina
قُلۡ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَمَآ أُنزِلَ عَلَيۡنَا وَمَآ أُنزِلَ عَلَىٰٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ وَإِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَ وَٱلۡأَسۡبَاطِ وَمَآ أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَٱلنَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمۡ لَا نُفَرِّقُ بَيۡنَ أَحَدٖ مِّنۡهُمۡ وَنَحۡنُ لَهُۥ مُسۡلِمُونَ
Sema: Tumemuamini Allah na kile tulichoteremshiwa na alichoteremshiwa Ibrahimu na Ismaili na Is-haka na Yakubu na Asbaati (watoto wa Yakubu) na alichopewa Musa na Isa na Manabii (wengine) kutoka kwa Mola wao. Hatumbagui yeyote kati yao. Nasisi tumejisalimisha kwake tu
وَمَن يَبۡتَغِ غَيۡرَ ٱلۡإِسۡلَٰمِ دِينٗا فَلَن يُقۡبَلَ مِنۡهُ وَهُوَ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ
Na yeyote atakayetaka dini isiyokuwa Uislamu, hatakubaliwa na Akhera atakuwa miongoni mwa wenye hasara
قُلۡ صَدَقَ ٱللَّهُۗ فَٱتَّبِعُواْ مِلَّةَ إِبۡرَٰهِيمَ حَنِيفٗاۖ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ
Sema: Allah amesema kweli. Basi ifuateni mila ya Ibrahimu aliyejiepusha na itikadi potofu, na hakuwa miongoni mwa washirikina
وَمَنۡ أَحۡسَنُ دِينٗا مِّمَّنۡ أَسۡلَمَ وَجۡهَهُۥ لِلَّهِ وَهُوَ مُحۡسِنٞ وَٱتَّبَعَ مِلَّةَ إِبۡرَٰهِيمَ حَنِيفٗاۗ وَٱتَّخَذَ ٱللَّهُ إِبۡرَٰهِيمَ خَلِيلٗا
Na hakuna aliye na dini iliyo nzuri (sahihi) sana kuliko yule aliyeusalimisha uso wake kwa Allah (kwa kumtii), naye akawa mwenye kufanya mazuri na akafuata dini ya Ibrahimu akijitenga na Shirki. Na Allah amemfanya Ibrahimu kipenzi (chake)
قُلۡ إِنَّنِي هَدَىٰنِي رَبِّيٓ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ دِينٗا قِيَمٗا مِّلَّةَ إِبۡرَٰهِيمَ حَنِيفٗاۚ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ
Sema: Kwa hakika, mimi ameniongoza Mola wangu Mlezi kwenye njia iliyo nyooka; dini iliyo sawa kabisa, mila ya Ibrahimu aliyeacha itikadi zote potofu na hakuwa miongoni mwa washirikina
وَٱتَّبَعۡتُ مِلَّةَ ءَابَآءِيٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَإِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَۚ مَا كَانَ لَنَآ أَن نُّشۡرِكَ بِٱللَّهِ مِن شَيۡءٖۚ ذَٰلِكَ مِن فَضۡلِ ٱللَّهِ عَلَيۡنَا وَعَلَى ٱلنَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَشۡكُرُونَ
Na nilifuata mila (dini) ya Baba zangu, Ibrahim na Is-hak na Yakubu. Sisi hatukuwa na haki ya kumshirikisha Allah kwa chochote. Hayo ni katika fadhila za Allah kwetu na kwa watu (wengine) lakini watu wengi sana hawashukuru
ثُمَّ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ أَنِ ٱتَّبِعۡ مِلَّةَ إِبۡرَٰهِيمَ حَنِيفٗاۖ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ
Kisha tukakufunulia (ewe Muhammad) kwamba ufuate mila (dini) ya Ibrahimu (aliyekuwa) mtiifu kamili, wala hakuwa miongoni mwa washirikina
وَجَٰهِدُواْ فِي ٱللَّهِ حَقَّ جِهَادِهِۦۚ هُوَ ٱجۡتَبَىٰكُمۡ وَمَا جَعَلَ عَلَيۡكُمۡ فِي ٱلدِّينِ مِنۡ حَرَجٖۚ مِّلَّةَ أَبِيكُمۡ إِبۡرَٰهِيمَۚ هُوَ سَمَّىٰكُمُ ٱلۡمُسۡلِمِينَ مِن قَبۡلُ وَفِي هَٰذَا لِيَكُونَ ٱلرَّسُولُ شَهِيدًا عَلَيۡكُمۡ وَتَكُونُواْ شُهَدَآءَ عَلَى ٱلنَّاسِۚ فَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱعۡتَصِمُواْ بِٱللَّهِ هُوَ مَوۡلَىٰكُمۡۖ فَنِعۡمَ ٱلۡمَوۡلَىٰ وَنِعۡمَ ٱلنَّصِيرُ
Na piganeni jihadi katika njia ya Allah kama inavyo stahiki jihadi yake. Yeye amekuteueni. Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya Baba yenu Ibrahim. Yeye (Allah) alikuiteni Waislamu tangu zamani, na katika hii (Qur’ani) pia, ili Mtume awe shahidi juu yenu, na nyinyi muwe mashahidi kwa watu. Basi shikeni Sala na toeni Zaka na shikamaneni na Allah. Yeye ndiye Mlinzi wenu, Mlinzi bora kabisa, na Msaidizi bora kabisa
۞شَرَعَ لَكُم مِّنَ ٱلدِّينِ مَا وَصَّىٰ بِهِۦ نُوحٗا وَٱلَّذِيٓ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ وَمَا وَصَّيۡنَا بِهِۦٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَىٰٓۖ أَنۡ أَقِيمُواْ ٱلدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُواْ فِيهِۚ كَبُرَ عَلَى ٱلۡمُشۡرِكِينَ مَا تَدۡعُوهُمۡ إِلَيۡهِۚ ٱللَّهُ يَجۡتَبِيٓ إِلَيۡهِ مَن يَشَآءُ وَيَهۡدِيٓ إِلَيۡهِ مَن يُنِيبُ
Amekuamrisheni Dini ile ile aliyo muusia Nuhu na tuliyo kufunulia wewe, na tuliyo wausia Ibrahim na Mussa na Issa, kwamba shikeni Dini wala msifarakane kwayo. Ni magumu kwa washirikina hayo unayo waitia. Allah humteua amtakaye, na humwongoa aelekeaye
قَدۡ كَانَتۡ لَكُمۡ أُسۡوَةٌ حَسَنَةٞ فِيٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَٱلَّذِينَ مَعَهُۥٓ إِذۡ قَالُواْ لِقَوۡمِهِمۡ إِنَّا بُرَءَـٰٓؤُاْ مِنكُمۡ وَمِمَّا تَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ كَفَرۡنَا بِكُمۡ وَبَدَا بَيۡنَنَا وَبَيۡنَكُمُ ٱلۡعَدَٰوَةُ وَٱلۡبَغۡضَآءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ وَحۡدَهُۥٓ إِلَّا قَوۡلَ إِبۡرَٰهِيمَ لِأَبِيهِ لَأَسۡتَغۡفِرَنَّ لَكَ وَمَآ أَمۡلِكُ لَكَ مِنَ ٱللَّهِ مِن شَيۡءٖۖ رَّبَّنَا عَلَيۡكَ تَوَكَّلۡنَا وَإِلَيۡكَ أَنَبۡنَا وَإِلَيۡكَ ٱلۡمَصِيرُ
Hakika, nyinyi mna mfano mzuri wa kuiga kwa (Mtume) Ibrahim na wale waliokuwa pamoja naye wakati walipowaambia watu wao kwamba: Hakika, sisi ni wenye kujitenga nanyi na (pia ni wenye kujitenga na) hao (Miungu masanamu) mnaowaabudu badala ya Allah. Tumekukataeni na umekwishadhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapomuamini Allah pekee. Isipokuwa kauli ya Ibrahim ya kumwambia baba yake kwamba: Hakika, nitakuombea msamaha na si miliki chochote kwa Allah kwa ajili yako. Ewe Mola wetu, tumekutegemea wewe tu, na tumetubu kwako tu, na kwako tu ndio marejeo (ya wote)
رَبَّنَا لَا تَجۡعَلۡنَا فِتۡنَةٗ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ وَٱغۡفِرۡ لَنَا رَبَّنَآۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ
Ee Mola wetu! Usitujaalie kuwa mtihani kwa wale waliokufuru, na Utusamehe Ee Mola wetu; Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima
لَقَدۡ كَانَ لَكُمۡ فِيهِمۡ أُسۡوَةٌ حَسَنَةٞ لِّمَن كَانَ يَرۡجُواْ ٱللَّهَ وَٱلۡيَوۡمَ ٱلۡأٓخِرَۚ وَمَن يَتَوَلَّ فَإِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡغَنِيُّ ٱلۡحَمِيدُ
Kwa yakini imekuwa kwenu kigezo kizuri katika mwenendo wao kwa mwenye kumtaraji Allah na Siku ya Mwisho. Na mwenye kugeuka basi hakika Allah ni Mwenye kujitosha, Msifiwa