Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 169

إِنَّمَا يَأۡمُرُكُم بِٱلسُّوٓءِ وَٱلۡفَحۡشَآءِ وَأَن تَقُولُواْ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ

Yeye anakuamrisheni mambo mabaya na machafu tu na …kumsingizia Allah msiyoyajua



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 30

يَوۡمَ تَجِدُ كُلُّ نَفۡسٖ مَّا عَمِلَتۡ مِنۡ خَيۡرٖ مُّحۡضَرٗا وَمَا عَمِلَتۡ مِن سُوٓءٖ تَوَدُّ لَوۡ أَنَّ بَيۡنَهَا وَبَيۡنَهُۥٓ أَمَدَۢا بَعِيدٗاۗ وَيُحَذِّرُكُمُ ٱللَّهُ نَفۡسَهُۥۗ وَٱللَّهُ رَءُوفُۢ بِٱلۡعِبَادِ

Siku ambayo kila nafsi itakuta kheri iliyoitenda ikiwa imehudhurishwa, na pia ubaya iliyoutenda. Itapenda lau kungekuwepo masafa marefu kati yake na ubaya huo. Na Allah anakutahadharisheni nafsi yake. Na Allah ni Mpole mno kwa waja (wake)



Surah: ANNISAI 

Ayah : 22

وَلَا تَنكِحُواْ مَا نَكَحَ ءَابَآؤُكُم مِّنَ ٱلنِّسَآءِ إِلَّا مَا قَدۡ سَلَفَۚ إِنَّهُۥ كَانَ فَٰحِشَةٗ وَمَقۡتٗا وَسَآءَ سَبِيلًا

Na msiwaoe wale walio olewa na baba zenu ispokuwa yaliyopita, tendo hilo ni baya na bughdha na ni njia mbaya



Surah: ANNISAI 

Ayah : 79

مَّآ أَصَابَكَ مِنۡ حَسَنَةٖ فَمِنَ ٱللَّهِۖ وَمَآ أَصَابَكَ مِن سَيِّئَةٖ فَمِن نَّفۡسِكَۚ وَأَرۡسَلۡنَٰكَ لِلنَّاسِ رَسُولٗاۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدٗا

(Jambo) Zuri lolote lililokupata limetoka kwa Allah, na (jambo) lolote baya lililokupata limetokana na wewe mwenyewe. Na tumekupeleka kwa watu ukiwa Mtume, na yatosha kwamba Allah ni shahidi



Surah: ANNISAI 

Ayah : 84

فَقَٰتِلۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ لَا تُكَلَّفُ إِلَّا نَفۡسَكَۚ وَحَرِّضِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۖ عَسَى ٱللَّهُ أَن يَكُفَّ بَأۡسَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْۚ وَٱللَّهُ أَشَدُّ بَأۡسٗا وَأَشَدُّ تَنكِيلٗا

Basi pigana katika njia ya Allah. Hukalifishwi isipokuwa nafsi yako tu, na wahamasishe waumini, huenda Allah akayazuia mashambulizi ya waliokufuru. Na Allah ni Mkali sana wa kushambulia na Mkali wa kuadhibu



Surah: ANNISAI 

Ayah : 148

۞لَّا يُحِبُّ ٱللَّهُ ٱلۡجَهۡرَ بِٱلسُّوٓءِ مِنَ ٱلۡقَوۡلِ إِلَّا مَن ظُلِمَۚ وَكَانَ ٱللَّهُ سَمِيعًا عَلِيمًا

Allah hapendi kudhihirisha kauli ovu isipokuwa kwa mwenye kudhulumiwa. Na Allah ni Mwenye kusikia sana, Mjuzi sana.[1]


1- - Aya inamkataza Muislamu kuwa na hulka na tabia ya kutoa kauli zisizofaa na zisizokuwa na staha. Lakini mbele ya mamlaka au mbele ya vyombo vya sheria na maamuzi, Muislamu ambaye amedhulumiwa haki yake anaruhusiwa kuwasilisha madai na, ikibidi kutamka maneno halisi ili madai yake yaeleweke, hata kama maneno ni makali. Anaruhusiwa kufanya hivyo ili apate haki yake na ili dhalimu aadhibiwe kwa kupewa adhabu anayostahiki.


Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 31

قَدۡ خَسِرَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِلِقَآءِ ٱللَّهِۖ حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَتۡهُمُ ٱلسَّاعَةُ بَغۡتَةٗ قَالُواْ يَٰحَسۡرَتَنَا عَلَىٰ مَا فَرَّطۡنَا فِيهَا وَهُمۡ يَحۡمِلُونَ أَوۡزَارَهُمۡ عَلَىٰ ظُهُورِهِمۡۚ أَلَا سَآءَ مَا يَزِرُونَ

Hakika, wamepata hasara wale waliopinga kukutana na Allah, hadi kitakapowajia Kiyama ghafla watasema: Eee! Majuto ni yetu kwa (sababu ya) yale tuliyoyafanyia uzembe humo (duniani), na huku wanabeba mizigo (makosa) yao migongoni mwao. Elewa kwamba, ni mabaya mno hayo (madhambi) wanayoyabeba



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 9

ٱشۡتَرَوۡاْ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ ثَمَنٗا قَلِيلٗا فَصَدُّواْ عَن سَبِيلِهِۦٓۚ إِنَّهُمۡ سَآءَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Wamezibadilisha Aya za Allah kwa thamani duni mno, na wakaizuia Njia yake (kwa kuiwekea vikwazo ili watu wasiifuate). Hakika ni jambo ovu sana walilokuwa wanalifanya



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 98

وَمِنَ ٱلۡأَعۡرَابِ مَن يَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ مَغۡرَمٗا وَيَتَرَبَّصُ بِكُمُ ٱلدَّوَآئِرَۚ عَلَيۡهِمۡ دَآئِرَةُ ٱلسَّوۡءِۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٞ

Na miongoni mwa Mabedui wapo wanaochukulia (wanadhani) vile wanavyovitoa (katika njia ya Allah) ni kazi bure (hasara), na wanakuvizieni mpate majanga. Majanga mabaya yawashukie wao. Na Allah ni Mwenye kusikia sana, Mwenye kujua mno



Surah: YUNUS 

Ayah : 11

۞وَلَوۡ يُعَجِّلُ ٱللَّهُ لِلنَّاسِ ٱلشَّرَّ ٱسۡتِعۡجَالَهُم بِٱلۡخَيۡرِ لَقُضِيَ إِلَيۡهِمۡ أَجَلُهُمۡۖ فَنَذَرُ ٱلَّذِينَ لَا يَرۡجُونَ لِقَآءَنَا فِي طُغۡيَٰنِهِمۡ يَعۡمَهُونَ

Na lau kama Allah angewaha-rakishia watu shari kama wao wanavyoharakisha kheri, bila shaka muda wao (wa kuishi) ungekatishwa (wangekuwa wameangamizwa zamani). Basi tunawaacha wale wasioamini kukutana nasi (Siku ya Kiyama) wakitangatanga katika upotevu wao



Surah: HUUD 

Ayah : 114

وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ طَرَفَيِ ٱلنَّهَارِ وَزُلَفٗا مِّنَ ٱلَّيۡلِۚ إِنَّ ٱلۡحَسَنَٰتِ يُذۡهِبۡنَ ٱلسَّيِّـَٔاتِۚ ذَٰلِكَ ذِكۡرَىٰ لِلذَّـٰكِرِينَ

Na simamisha swala katika ncha mbili za mchana na nyakati za usiku. Hakika mema huondoa maovu. Huo ni ukumbusho kwa wale wanaokumbuka



Surah: YUSUF 

Ayah : 53

۞وَمَآ أُبَرِّئُ نَفۡسِيٓۚ إِنَّ ٱلنَّفۡسَ لَأَمَّارَةُۢ بِٱلسُّوٓءِ إِلَّا مَا رَحِمَ رَبِّيٓۚ إِنَّ رَبِّي غَفُورٞ رَّحِيمٞ

(Yusuf aliendelea kusema) Nami siisafishi nafsi yangu (sijitoi lawamani). Kwa hakika nafsi inaamrisha mno maovu, isipokuwa ile tu aliyoirehemu Mola wangu Mlezi. Hakika, Mola wangu Mlezi ni Msamehevu, mwingi wa rehema



Surah: IBRAHIM 

Ayah : 26

وَمَثَلُ كَلِمَةٍ خَبِيثَةٖ كَشَجَرَةٍ خَبِيثَةٍ ٱجۡتُثَّتۡ مِن فَوۡقِ ٱلۡأَرۡضِ مَا لَهَا مِن قَرَارٖ

Na mfano wa neno ovu (neno la ukafiri) ni kama mti muovu, uliong’olewa juu ya ardhi. Hauna uimara



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 25

لِيَحۡمِلُوٓاْ أَوۡزَارَهُمۡ كَامِلَةٗ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَمِنۡ أَوۡزَارِ ٱلَّذِينَ يُضِلُّونَهُم بِغَيۡرِ عِلۡمٍۗ أَلَا سَآءَ مَا يَزِرُونَ

Ili (mwisho) wabebe madhambi yaokamili Siku ya Kiyama, na sehemu ya madhambi ya wale wanaowapoteza bila ya kujua. Sikilizeni! Ni mabaya sana wanayobeba



Surah: AL-ISRAA 

Ayah : 10

وَأَنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ أَعۡتَدۡنَا لَهُمۡ عَذَابًا أَلِيمٗا

Na yakwamba wale wasio iamini Akhera tumewaandalia adhabu chungu



Surah: AL-ISRAA 

Ayah : 32

وَلَا تَقۡرَبُواْ ٱلزِّنَىٰٓۖ إِنَّهُۥ كَانَ فَٰحِشَةٗ وَسَآءَ سَبِيلٗا

Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya



Surah: AL-ISRAA 

Ayah : 38

كُلُّ ذَٰلِكَ كَانَ سَيِّئُهُۥ عِندَ رَبِّكَ مَكۡرُوهٗا

Haya yote ubaya wake ni wenye kuchukiza kwa Mola wako Mlezi



Surah: AL-ISRAA 

Ayah : 83

وَإِذَآ أَنۡعَمۡنَا عَلَى ٱلۡإِنسَٰنِ أَعۡرَضَ وَنَـَٔا بِجَانِبِهِۦ وَإِذَا مَسَّهُ ٱلشَّرُّ كَانَ يَـُٔوسٗا

Na mwanaadamu tunapo mneemesha hugeuka na kujitenga kando. Na inapo mgusa shari hukata tamaa



Surah: AL-ANBIYAA 

Ayah : 35

كُلُّ نَفۡسٖ ذَآئِقَةُ ٱلۡمَوۡتِۗ وَنَبۡلُوكُم بِٱلشَّرِّ وَٱلۡخَيۡرِ فِتۡنَةٗۖ وَإِلَيۡنَا تُرۡجَعُونَ

Kila nafsi itaonja mauti; na tunakujaribuni kwa mtihani wa shari na kheri. Na kwetu Sisi mtarejeshwa



Surah: ALMUUMINUUN 

Ayah : 96

ٱدۡفَعۡ بِٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُ ٱلسَّيِّئَةَۚ نَحۡنُ أَعۡلَمُ بِمَا يَصِفُونَ

Kinga maovu kwa kutenda yaliyo mema zaidi. Sisi tunajua wayasemayo



Surah: ARRUUM 

Ayah : 36

وَإِذَآ أَذَقۡنَا ٱلنَّاسَ رَحۡمَةٗ فَرِحُواْ بِهَاۖ وَإِن تُصِبۡهُمۡ سَيِّئَةُۢ بِمَا قَدَّمَتۡ أَيۡدِيهِمۡ إِذَا هُمۡ يَقۡنَطُونَ

Na watu tunapo waonjesha rehema huifurahia, na ukiwasibu uovu kwa iliyo yatanguliza mikono yao wenyewe, mara wanakata tamaa



Surah: FAATWIR 

Ayah : 43

ٱسۡتِكۡبَارٗا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَكۡرَ ٱلسَّيِّيِٕۚ وَلَا يَحِيقُ ٱلۡمَكۡرُ ٱلسَّيِّئُ إِلَّا بِأَهۡلِهِۦۚ فَهَلۡ يَنظُرُونَ إِلَّا سُنَّتَ ٱلۡأَوَّلِينَۚ فَلَن تَجِدَ لِسُنَّتِ ٱللَّهِ تَبۡدِيلٗاۖ وَلَن تَجِدَ لِسُنَّتِ ٱللَّهِ تَحۡوِيلًا

Kwa kutakabari kwao katika nchi, na kufanya vitimbi vya uovu. Na vitimbi viovu havimsibu ila mwenyewe aliye vifanya. Hebu hawangojei yalio wasibu watu wa kale? Basi hutapata mabadiliko katika mtindo wa Allah. Wala hutapata mageuko katika mwendo wa Allah



Surah: FUSSWILAT 

Ayah : 34

وَلَا تَسۡتَوِي ٱلۡحَسَنَةُ وَلَا ٱلسَّيِّئَةُۚ ٱدۡفَعۡ بِٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُ فَإِذَا ٱلَّذِي بَيۡنَكَ وَبَيۡنَهُۥ عَدَٰوَةٞ كَأَنَّهُۥ وَلِيٌّ حَمِيمٞ

Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako na baina yake pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu



Surah: AZZILZAAL 

Ayah : 8

وَمَن يَعۡمَلۡ مِثۡقَالَ ذَرَّةٖ شَرّٗا يَرَهُۥ

Na anaye tenda chembe ya uovu atauona!



Surah: AL-FALAQ

Ayah : 1

قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلۡفَلَقِ

Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko



Surah: AL-FALAQ

Ayah : 2

مِن شَرِّ مَا خَلَقَ

(Najikinga) Dhidi ya shari ya alivyoviumba



Surah: AL-FALAQ

Ayah : 3

وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ

Na (najikinga) dhidi ya shari ya giza la usiku liingiapo



Surah: AL-FALAQ

Ayah : 4

وَمِن شَرِّ ٱلنَّفَّـٰثَٰتِ فِي ٱلۡعُقَدِ

Na (najikinga) dhidi ya shari ya (wanawake) wanaopulizia mafundoni



Surah: AL-FALAQ

Ayah : 5

وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ

Na (najikinga) dhidi ya shari ya hasidi anapo husudu



Surah: ANNAAS

Ayah : 1

قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلنَّاسِ

Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa watu