Surah: NUUH 

Ayah : 20

لِّتَسۡلُكُواْ مِنۡهَا سُبُلٗا فِجَاجٗا

Ili mtembee humo katika njia zilizo pana



Surah: ALMURSALAAT 

Ayah : 25

أَلَمۡ نَجۡعَلِ ٱلۡأَرۡضَ كِفَاتًا

Je, kwani Hatukufanya ardhi kuwa ni chombo cha kukusanya?



Surah: ALMURSALAAT 

Ayah : 26

أَحۡيَآءٗ وَأَمۡوَٰتٗا

Walio hai na maiti (na waliokufa)?



Surah: ALMURSALAAT 

Ayah : 27

وَجَعَلۡنَا فِيهَا رَوَٰسِيَ شَٰمِخَٰتٖ وَأَسۡقَيۡنَٰكُم مَّآءٗ فُرَاتٗا

Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tuna-kunywesheni maji matamu?



Surah: ANNABAI 

Ayah : 6

أَلَمۡ نَجۡعَلِ ٱلۡأَرۡضَ مِهَٰدٗا

Je, kwani hatukuifanya ardhi (kama) tandiko?



Surah: ANNABAI 

Ayah : 7

وَٱلۡجِبَالَ أَوۡتَادٗا

Na milima kuwa (kama) vigingi?



Surah: A’BASA

Ayah : 26

ثُمَّ شَقَقۡنَا ٱلۡأَرۡضَ شَقّٗا

Kisha Tukaipasua ardhi mipasuko



Surah: A’BASA

Ayah : 27

فَأَنۢبَتۡنَا فِيهَا حَبّٗا

Kisha tukaotesha humo nafaka mbali mbali



Surah: A’BASA

Ayah : 28

وَعِنَبٗا وَقَضۡبٗا

Na mizabibu na mimea ya mboga (ikatwayo ikamea tena)



Surah: A’BASA

Ayah : 29

وَزَيۡتُونٗا وَنَخۡلٗا

Na mizaituni na mitende



Surah: A’BASA

Ayah : 30

وَحَدَآئِقَ غُلۡبٗا

Na mabustani yaliyositawi na kusongamana miti yake



Surah: A’BASA

Ayah : 31

وَفَٰكِهَةٗ وَأَبّٗا

Na matunda na majani ya malisho ya wanyama



Surah: A’BASA

Ayah : 32

مَّتَٰعٗا لَّكُمۡ وَلِأَنۡعَٰمِكُمۡ

Ni manufaa kwenu na kwa wanyama wenu wa mifugo



Surah:  AL-GHAASHIYAH 

Ayah : 20

وَإِلَى ٱلۡأَرۡضِ كَيۡفَ سُطِحَتۡ

Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa?