Surah: ANNISAI 

Ayah : 97

إِنَّ ٱلَّذِينَ تَوَفَّىٰهُمُ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ ظَالِمِيٓ أَنفُسِهِمۡ قَالُواْ فِيمَ كُنتُمۡۖ قَالُواْ كُنَّا مُسۡتَضۡعَفِينَ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ قَالُوٓاْ أَلَمۡ تَكُنۡ أَرۡضُ ٱللَّهِ وَٰسِعَةٗ فَتُهَاجِرُواْ فِيهَاۚ فَأُوْلَـٰٓئِكَ مَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُۖ وَسَآءَتۡ مَصِيرًا

Hakika, wale ambao Malaika wamewafisha (wamewatoa roho) ilhali wamezidhulumu nafsi zao, (Malaika) watawauliza: Je, mlikuwa na nini nyinyi? Watasema: Tulikuwa wayonge katika ardhi (duniani). (Malaika) Watawaambia: Hivi Ardhi ya Allah haikuwa yenye wasaa mkahama humo? Basi hao makazi yao ni Jahanamu, na marejeo mabaya mno ni hayo.[1]


1- - Aya hii inawataka Waislamu kutoridhika na mazingira ambayo sio rafiki katika kutekeleza majukumu ya dini yao na pia mambo yao ya kimaendeleo. Wanatakiwa kupambana na ikishindikana wahame na kwenda eneo jingine lenye mazingira rafiki.


Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 61

وَهُوَ ٱلۡقَاهِرُ فَوۡقَ عِبَادِهِۦۖ وَيُرۡسِلُ عَلَيۡكُمۡ حَفَظَةً حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَ أَحَدَكُمُ ٱلۡمَوۡتُ تَوَفَّتۡهُ رُسُلُنَا وَهُمۡ لَا يُفَرِّطُونَ

Na yeye tu ndiye Mwenye nguvu kubwa juu ya waja wake, na anatuma kwenu (Malaika) waangalizi (wanaowalinda binadamu na kutunza kumbukumbu za matendo yao)[1], mpaka kinapomfikia mmoja wenu kifo wajumbe wetu wanamfisha, na hawafanyi uzembe


1- - Rejea Aya ya 11, Sura Arraad (13).


Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 93

وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوۡ قَالَ أُوحِيَ إِلَيَّ وَلَمۡ يُوحَ إِلَيۡهِ شَيۡءٞ وَمَن قَالَ سَأُنزِلُ مِثۡلَ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُۗ وَلَوۡ تَرَىٰٓ إِذِ ٱلظَّـٰلِمُونَ فِي غَمَرَٰتِ ٱلۡمَوۡتِ وَٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ بَاسِطُوٓاْ أَيۡدِيهِمۡ أَخۡرِجُوٓاْ أَنفُسَكُمُۖ ٱلۡيَوۡمَ تُجۡزَوۡنَ عَذَابَ ٱلۡهُونِ بِمَا كُنتُمۡ تَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ غَيۡرَ ٱلۡحَقِّ وَكُنتُمۡ عَنۡ ءَايَٰتِهِۦ تَسۡتَكۡبِرُونَ

Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyemzushia Allah uongo (kuwa amempa Utume) au aliyesema kuwa: Nimeletewa Wahyi na ilhali hakuletewa Wahyi wowote? Na (ni nani dhalimu zaidi kuliko) yule aliyesema kuwa: Nitateremsha mfano wa aliyoteremsha Allah? Na lau ungeona wakati madhalimu wamo katika mahangaiko ya mauti na Malaika wamenyoosha mikono yao (wakiwa tayari kuchukua roho zao wakiwaambia): Zitoeni (ziokoeni) roho zenu (kutoka mikononi mwetu kama mnaweza kwa sababu) leo mtalipwa adhabu ya fedheha kwa sababu ya yale yasiyokuwa ya haki mliyomsingizia Allah, na mlikuwa mnazifanyia kiburi Aya zake



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 37

فَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوۡ كَذَّبَ بِـَٔايَٰتِهِۦٓۚ أُوْلَـٰٓئِكَ يَنَالُهُمۡ نَصِيبُهُم مِّنَ ٱلۡكِتَٰبِۖ حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَتۡهُمۡ رُسُلُنَا يَتَوَفَّوۡنَهُمۡ قَالُوٓاْ أَيۡنَ مَا كُنتُمۡ تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِۖ قَالُواْ ضَلُّواْ عَنَّا وَشَهِدُواْ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ أَنَّهُمۡ كَانُواْ كَٰفِرِينَ

Basi, ni nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyemzushia uwongo Allah au kuzikadhibisha Aya zake? Hao itawapata sehemu ya maandiko (aliyowaandikia Allah) mpaka watakapowafikia Wajumbe wetu wakiwatoa roho watasema: Wako wapi mliokuwa mkiwaomba (mukiwaabudu) badala ya Allah watasema: “Wametupotea” na wamejishuhudia wenyewe kwamba walikuwa makafiri



Surah: AN-FAL 

Ayah : 50

وَلَوۡ تَرَىٰٓ إِذۡ يَتَوَفَّى ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ يَضۡرِبُونَ وُجُوهَهُمۡ وَأَدۡبَٰرَهُمۡ وَذُوقُواْ عَذَابَ ٱلۡحَرِيقِ

Na laiti (ewe Muhammad ungekuwa) unaona wakati Malaika wanawaua makafiri huku wakizipiga nyuso zao na migongo yao na (kuwaambia): Onjeni adhabu ya kuungua (ungeona jambo kubwa la kutisha)



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 28

ٱلَّذِينَ تَتَوَفَّىٰهُمُ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ ظَالِمِيٓ أَنفُسِهِمۡۖ فَأَلۡقَوُاْ ٱلسَّلَمَ مَا كُنَّا نَعۡمَلُ مِن سُوٓءِۭۚ بَلَىٰٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمُۢ بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Wale ambao Malaika wame-wafisha ilhali wamedhulumu nafsi zao. Nawakajisalimisha kwa Allah (wakisema): hatukuwa tukifanya uovu wowote. Naam, hakika Allah anajua sana mliyokuwa mkiyatenda



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 32

ٱلَّذِينَ تَتَوَفَّىٰهُمُ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ طَيِّبِينَ يَقُولُونَ سَلَٰمٌ عَلَيۡكُمُ ٱدۡخُلُواْ ٱلۡجَنَّةَ بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Wale ambao Malaika wame-wafisha wakiwa vizuri (Malaika watawaambia) Assalamu alaykum (amani iwe juu yenu!) Ingieni Peponi kwasababu ya yale mliyokuwa mkiyatenda



Surah: ASSAJDAH 

Ayah : 11

۞قُلۡ يَتَوَفَّىٰكُم مَّلَكُ ٱلۡمَوۡتِ ٱلَّذِي وُكِّلَ بِكُمۡ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمۡ تُرۡجَعُونَ

Sema: Atakufisheni Malaika wa mauti aliye wakilishwa juu yenu; kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu Mlezi



Surah: MUHAMMAD 

Ayah : 27

فَكَيۡفَ إِذَا تَوَفَّتۡهُمُ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ يَضۡرِبُونَ وُجُوهَهُمۡ وَأَدۡبَٰرَهُمۡ

Basi itakuwaje Malaika watakapo wafisha wakawa wanawapiga nyuso zao na migongo yao!