Surah: AL-FAATIHA 

Ayah : 4

مَٰلِكِ يَوۡمِ ٱلدِّينِ

Mmiliki wa Siku ya Malipo



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 48

وَٱتَّقُواْ يَوۡمٗا لَّا تَجۡزِي نَفۡسٌ عَن نَّفۡسٖ شَيۡـٔٗا وَلَا يُقۡبَلُ مِنۡهَا شَفَٰعَةٞ وَلَا يُؤۡخَذُ مِنۡهَا عَدۡلٞ وَلَا هُمۡ يُنصَرُونَ

Na iogopeni siku ambayo nafsi haitaisaidia chochote nafsi nyingine, na wala hautakubaliwa uombezi wowote kwa nafsi hiyo (kumuombea mwengine), na wala haitachukuliwa fidia yoyote kwa nafsi hiyo, nao hawatanusuriwa



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 113

وَقَالَتِ ٱلۡيَهُودُ لَيۡسَتِ ٱلنَّصَٰرَىٰ عَلَىٰ شَيۡءٖ وَقَالَتِ ٱلنَّصَٰرَىٰ لَيۡسَتِ ٱلۡيَهُودُ عَلَىٰ شَيۡءٖ وَهُمۡ يَتۡلُونَ ٱلۡكِتَٰبَۗ كَذَٰلِكَ قَالَ ٱلَّذِينَ لَا يَعۡلَمُونَ مِثۡلَ قَوۡلِهِمۡۚ فَٱللَّهُ يَحۡكُمُ بَيۡنَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فِيمَا كَانُواْ فِيهِ يَخۡتَلِفُونَ

Na Wayahudi wamesema: Manaswara hawa na kitu (chochote cha maana). Na Manaswara wame-sema: Wayahudi hawana kitu (chochote cha maana), na wao (wote) wanasoma Kitabu (kitakatifu kitokacho kwa Mola wao). Kama hivyo, wale ambao hawajui kitu wamesema mfano wa maneno yao. Basi Allah atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyokuwa wakitafautiana



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 123

وَٱتَّقُواْ يَوۡمٗا لَّا تَجۡزِي نَفۡسٌ عَن نَّفۡسٖ شَيۡـٔٗا وَلَا يُقۡبَلُ مِنۡهَا عَدۡلٞ وَلَا تَنفَعُهَا شَفَٰعَةٞ وَلَا هُمۡ يُنصَرُونَ

Na iogopeni siku ambayo nafsi haitaifaa nafsi nyingine (kwa) chochote, na haitakubaliwa nafsi hiyo fidia wala kuombewa msamaha na kamwe hawatanusuriwa



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 281

وَٱتَّقُواْ يَوۡمٗا تُرۡجَعُونَ فِيهِ إِلَى ٱللَّهِۖ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفۡسٖ مَّا كَسَبَتۡ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ

Na iogopeni siku ambayo mtarejeshwa kwa Allah, kisha kila mtu atalipwa kikamilifu aliyoyachuma, nao hawatadhulumiwa



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 9

رَبَّنَآ إِنَّكَ جَامِعُ ٱلنَّاسِ لِيَوۡمٖ لَّا رَيۡبَ فِيهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُخۡلِفُ ٱلۡمِيعَادَ

Ewe Mola wetu, hakika wewe ni mwenye kuwakusanya watu katika siku isiyokuwa na shaka. Hakika, Allah havunji ahadi



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 30

يَوۡمَ تَجِدُ كُلُّ نَفۡسٖ مَّا عَمِلَتۡ مِنۡ خَيۡرٖ مُّحۡضَرٗا وَمَا عَمِلَتۡ مِن سُوٓءٖ تَوَدُّ لَوۡ أَنَّ بَيۡنَهَا وَبَيۡنَهُۥٓ أَمَدَۢا بَعِيدٗاۗ وَيُحَذِّرُكُمُ ٱللَّهُ نَفۡسَهُۥۗ وَٱللَّهُ رَءُوفُۢ بِٱلۡعِبَادِ

Siku ambayo kila nafsi itakuta kheri iliyoitenda ikiwa imehudhurishwa, na pia ubaya iliyoutenda. Itapenda lau kungekuwepo masafa marefu kati yake na ubaya huo. Na Allah anakutahadharisheni nafsi yake. Na Allah ni Mpole mno kwa waja (wake)



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 185

كُلُّ نَفۡسٖ ذَآئِقَةُ ٱلۡمَوۡتِۗ وَإِنَّمَا تُوَفَّوۡنَ أُجُورَكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۖ فَمَن زُحۡزِحَ عَنِ ٱلنَّارِ وَأُدۡخِلَ ٱلۡجَنَّةَ فَقَدۡ فَازَۗ وَمَا ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَآ إِلَّا مَتَٰعُ ٱلۡغُرُورِ

Kila nafsi itaonja kifo, si vingine malipo yenu mtapewa yakiwa kamili siku ya kiyama, atakaye epushwa na kuwekwa mbali na Moto na akaingizwa Peponi basi huyo amefanikiwa, na haikua maisha ya dunia ila ni starehe zenye kudanganya



Surah: ANNISAI 

Ayah : 87

ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۚ لَيَجۡمَعَنَّكُمۡ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ لَا رَيۡبَ فِيهِۗ وَمَنۡ أَصۡدَقُ مِنَ ٱللَّهِ حَدِيثٗا

Allah, hakuna mwenye haki ya kuabudiwa ispokuwa yeye tu. Kwa yakini kabisa, atakukusanyeni katika Siku ya Kiyama isiyokuwa na shaka yoyote. Na ni nani mkweli sana wa maneno kuliko Allah?



Surah: ANNISAI 

Ayah : 141

ٱلَّذِينَ يَتَرَبَّصُونَ بِكُمۡ فَإِن كَانَ لَكُمۡ فَتۡحٞ مِّنَ ٱللَّهِ قَالُوٓاْ أَلَمۡ نَكُن مَّعَكُمۡ وَإِن كَانَ لِلۡكَٰفِرِينَ نَصِيبٞ قَالُوٓاْ أَلَمۡ نَسۡتَحۡوِذۡ عَلَيۡكُمۡ وَنَمۡنَعۡكُم مِّنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۚ فَٱللَّهُ يَحۡكُمُ بَيۡنَكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ وَلَن يَجۡعَلَ ٱللَّهُ لِلۡكَٰفِرِينَ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ سَبِيلًا

Ambao wanakuvizieni. Mkipata ushindi unaotoka kwa Allah wanasema: Si tulikuwa pamoja na nyinyi? Na ikiwa makafiri wamepata sehemu ndogo ya ushindi wanasema: Si tulikusimamieni na kukukingeni dhidi ya Waislamu? Basi Allah atahukumu baina yenu Siku ya Kiama. Na Allah hatawapa makafiri njia (ya kuwashinda) Waislamu



Surah: YUNUS 

Ayah : 28

وَيَوۡمَ نَحۡشُرُهُمۡ جَمِيعٗا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشۡرَكُواْ مَكَانَكُمۡ أَنتُمۡ وَشُرَكَآؤُكُمۡۚ فَزَيَّلۡنَا بَيۡنَهُمۡۖ وَقَالَ شُرَكَآؤُهُم مَّا كُنتُمۡ إِيَّانَا تَعۡبُدُونَ

Na (kumbuka) siku tutakayo-wakusanya wote, kisha tutawaambia wale washirikina (makafiri kuwa): Simameni hapo hapo mlipo nyinyi na washirika (Miungu) wenu (mliowashirikisha na Allah), hivyo tutatenganisha baina yao. Na washirika wao watasema: Nyinyi hamkuwa mnatuabudu



Surah: YUNUS 

Ayah : 29

فَكَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدَۢا بَيۡنَنَا وَبَيۡنَكُمۡ إِن كُنَّا عَنۡ عِبَادَتِكُمۡ لَغَٰفِلِينَ

Basi Allah anatosha kuwa shahidi baina yetu na baina yenu. Hakika sisi tulikuwa hatujui chochote kuhusu ibada yenu



Surah: YUNUS 

Ayah : 30

هُنَالِكَ تَبۡلُواْ كُلُّ نَفۡسٖ مَّآ أَسۡلَفَتۡۚ وَرُدُّوٓاْ إِلَى ٱللَّهِ مَوۡلَىٰهُمُ ٱلۡحَقِّۖ وَضَلَّ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ

Huko, kila mtu atayatafuta matendo yake aliyoyatanguliza (kuyafanya; yawe ya kheri au ya shari), na watarudishwa kwa (Allah) Mola wao wa haki, na yatawapotea yale waliyokuwa wakiyazusha



Surah: YUNUS 

Ayah : 93

وَلَقَدۡ بَوَّأۡنَا بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ مُبَوَّأَ صِدۡقٖ وَرَزَقۡنَٰهُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَٰتِ فَمَا ٱخۡتَلَفُواْ حَتَّىٰ جَآءَهُمُ ٱلۡعِلۡمُۚ إِنَّ رَبَّكَ يَقۡضِي بَيۡنَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فِيمَا كَانُواْ فِيهِ يَخۡتَلِفُونَ

Na, kwa hakika kabisa, tuliwaweka Wana wa Israili makazi ya ukweli (sahihi na mazuri), na tuliwaruzuku vilivyo vizuri. Basi hawakutofautiana mpaka ilipowafikia elimu. Hakika, Mola wako Mlezi atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyokuwa wanatofautiana



Surah: IBRAHIM 

Ayah : 44

وَأَنذِرِ ٱلنَّاسَ يَوۡمَ يَأۡتِيهِمُ ٱلۡعَذَابُ فَيَقُولُ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ رَبَّنَآ أَخِّرۡنَآ إِلَىٰٓ أَجَلٖ قَرِيبٖ نُّجِبۡ دَعۡوَتَكَ وَنَتَّبِعِ ٱلرُّسُلَۗ أَوَلَمۡ تَكُونُوٓاْ أَقۡسَمۡتُم مِّن قَبۡلُ مَا لَكُم مِّن زَوَالٖ

Na waonye watu siku itapowajia adhabu, na waseme waliodhulumu: Ewe Mola wetu Mlezi, tupe muhula (muda kidogo angalau) tuitikie wito wako na tuwafuate Mitume. (Watajibiwa kwa shere) Kwani nyinyi si mliapa zamani kwamba hamtaondolewa (duniani na kurejeshwa Akhera)?



Surah: IBRAHIM 

Ayah : 47

فَلَا تَحۡسَبَنَّ ٱللَّهَ مُخۡلِفَ وَعۡدِهِۦ رُسُلَهُۥٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٞ ذُو ٱنتِقَامٖ

Basi usimdhanie Allah kuwa ni mwenye kukhalifu ahadi zake (kwa) Mitume wake. Hakika Allah ni Mwenye nguvu sana, (na) ni Mwenye kulipiza (dhidi ya maadui wake)



Surah: IBRAHIM 

Ayah : 48

يَوۡمَ تُبَدَّلُ ٱلۡأَرۡضُ غَيۡرَ ٱلۡأَرۡضِ وَٱلسَّمَٰوَٰتُۖ وَبَرَزُواْ لِلَّهِ ٱلۡوَٰحِدِ ٱلۡقَهَّارِ

(Malipo yatakuwa) Siku itapogeuzwa ardhi iwe ardhi nyingine, na mbingu pia. Nao watahudhuria mbele ya Allah, Mwenye nguvu mno



Surah: IBRAHIM 

Ayah : 49

وَتَرَى ٱلۡمُجۡرِمِينَ يَوۡمَئِذٖ مُّقَرَّنِينَ فِي ٱلۡأَصۡفَادِ

Na utawaona wahalifu siku hiyo wamefungwa katika minyororo



Surah: IBRAHIM 

Ayah : 50

سَرَابِيلُهُم مِّن قَطِرَانٖ وَتَغۡشَىٰ وُجُوهَهُمُ ٱلنَّارُ

Mavazi yao yatakuwa ya lami (nyeusi tii na yananuka), na nyuso zao zitagubikwa na Moto



Surah: IBRAHIM 

Ayah : 51

لِيَجۡزِيَ ٱللَّهُ كُلَّ نَفۡسٖ مَّا كَسَبَتۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ

(Watu watatoka makaburini) ili Allah ailipe kila nafsi kwa yale iliyo yachuma. Hakika Allah ni Mwepesi wa kuhesabu



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 111

۞يَوۡمَ تَأۡتِي كُلُّ نَفۡسٖ تُجَٰدِلُ عَن نَّفۡسِهَا وَتُوَفَّىٰ كُلُّ نَفۡسٖ مَّا عَمِلَتۡ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ

Siku ambayo kila nafsi itakuja kujitetea yenyewe, na kila nafsi itapewa sawa na iliyoyafanya, nao hawatadhulumiwa



Surah: AL-ISRAA 

Ayah : 13

وَكُلَّ إِنسَٰنٍ أَلۡزَمۡنَٰهُ طَـٰٓئِرَهُۥ فِي عُنُقِهِۦۖ وَنُخۡرِجُ لَهُۥ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ كِتَٰبٗا يَلۡقَىٰهُ مَنشُورًا

Na kila mtu tumemfungia a’mali yake shingoni mwake. Na Siku ya Kiyama tutamtolea kitabu atakacho kikuta kiwazi kimekunjuliwa



Surah: AL-ISRAA 

Ayah : 14

ٱقۡرَأۡ كِتَٰبَكَ كَفَىٰ بِنَفۡسِكَ ٱلۡيَوۡمَ عَلَيۡكَ حَسِيبٗا

Ataambiwa: Soma kitabu chako! Nafsi yako inakutosha leo kukuhesabu



Surah: MARYAM 

Ayah : 37

فَٱخۡتَلَفَ ٱلۡأَحۡزَابُ مِنۢ بَيۡنِهِمۡۖ فَوَيۡلٞ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن مَّشۡهَدِ يَوۡمٍ عَظِيمٍ

Lakini makundi yakakhitalifiana wao kwa wao. Basi ole wao hao walio kufuru kwa kuhudhuria Siku iliyo kuu



Surah: MARYAM 

Ayah : 38

أَسۡمِعۡ بِهِمۡ وَأَبۡصِرۡ يَوۡمَ يَأۡتُونَنَا لَٰكِنِ ٱلظَّـٰلِمُونَ ٱلۡيَوۡمَ فِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٖ

Watasikia na wataona vizuri vilioje Siku watakayo tufikia! Lakini madhalimu sasa wamo katika upotofu ulio dhaahiri



Surah: MARYAM 

Ayah : 39

وَأَنذِرۡهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡحَسۡرَةِ إِذۡ قُضِيَ ٱلۡأَمۡرُ وَهُمۡ فِي غَفۡلَةٖ وَهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ

Na waonye siku ya majuto itakapo tolewa amri. Nao wamo katika ghafla, wala hawaamini



Surah: MARYAM 

Ayah : 40

إِنَّا نَحۡنُ نَرِثُ ٱلۡأَرۡضَ وَمَنۡ عَلَيۡهَا وَإِلَيۡنَا يُرۡجَعُونَ

Hakika Sisi tutairithi ardhi na walio juu yake. Na kwetu watare-jeshwa



Surah: MARYAM 

Ayah : 85

يَوۡمَ نَحۡشُرُ ٱلۡمُتَّقِينَ إِلَى ٱلرَّحۡمَٰنِ وَفۡدٗا

Siku tutakayo wakusanya wacha Mungu kuwapeleka kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema kuwa ni wageni wake



Surah: MARYAM 

Ayah : 86

وَنَسُوقُ ٱلۡمُجۡرِمِينَ إِلَىٰ جَهَنَّمَ وِرۡدٗا

Na tukawachunga waovu kuwapeleka Jahannamu hali ya kuwa wana kiu



Surah: MARYAM 

Ayah : 87

لَّا يَمۡلِكُونَ ٱلشَّفَٰعَةَ إِلَّا مَنِ ٱتَّخَذَ عِندَ ٱلرَّحۡمَٰنِ عَهۡدٗا

Hawatakuwa na mamlaka ya uombezi ila wale walio chukua ahadi kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema