Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 178

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُتِبَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡقِصَاصُ فِي ٱلۡقَتۡلَىۖ ٱلۡحُرُّ بِٱلۡحُرِّ وَٱلۡعَبۡدُ بِٱلۡعَبۡدِ وَٱلۡأُنثَىٰ بِٱلۡأُنثَىٰۚ فَمَنۡ عُفِيَ لَهُۥ مِنۡ أَخِيهِ شَيۡءٞ فَٱتِّبَاعُۢ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَأَدَآءٌ إِلَيۡهِ بِإِحۡسَٰنٖۗ ذَٰلِكَ تَخۡفِيفٞ مِّن رَّبِّكُمۡ وَرَحۡمَةٞۗ فَمَنِ ٱعۡتَدَىٰ بَعۡدَ ذَٰلِكَ فَلَهُۥ عَذَابٌ أَلِيمٞ

Enyi mlioamini, mmeandikiwa kulipa kisasi katika waliouawa; muungwana kwa muungwana na mtumwa kwa mtumwa na mwanamke kwa mwanamke. Na aliyesamehewa jambo na ndugu yake (mtendewa jinai) basi fidia ifuatiliwe kwa wema na atekelezewe kwa uzuri. Hiyo ni tahafifu itokayo kwa Mola wenu na ni rehema. Na atakayekiuka baada ya hayo, basi yeye atapata adhabu iumizayo



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 190

وَقَٰتِلُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ ٱلَّذِينَ يُقَٰتِلُونَكُمۡ وَلَا تَعۡتَدُوٓاْۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُعۡتَدِينَ

Na piganeni na wanaokupigeni katika njia ya Allah, na msivuke mipaka (mkawashambulia wasiohusika), kwa sababu Allah hawapendi wavukao mipaka



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 194

ٱلشَّهۡرُ ٱلۡحَرَامُ بِٱلشَّهۡرِ ٱلۡحَرَامِ وَٱلۡحُرُمَٰتُ قِصَاصٞۚ فَمَنِ ٱعۡتَدَىٰ عَلَيۡكُمۡ فَٱعۡتَدُواْ عَلَيۡهِ بِمِثۡلِ مَا ٱعۡتَدَىٰ عَلَيۡكُمۡۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلۡمُتَّقِينَ

Mwezi mtukufu kwa mwezi mtukufu. Na kila kilicho kitukufu kitalipiwa kisasi. Na yeyote atakaye fanya uadui juu yenu, basi mlipeni sawa na uadui alioufanya kwenu. Na mcheni Allah na jueni kwamba Allah yupamoja na wamchao



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 213

كَانَ ٱلنَّاسُ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗ فَبَعَثَ ٱللَّهُ ٱلنَّبِيِّـۧنَ مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ وَأَنزَلَ مَعَهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ بِٱلۡحَقِّ لِيَحۡكُمَ بَيۡنَ ٱلنَّاسِ فِيمَا ٱخۡتَلَفُواْ فِيهِۚ وَمَا ٱخۡتَلَفَ فِيهِ إِلَّا ٱلَّذِينَ أُوتُوهُ مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَتۡهُمُ ٱلۡبَيِّنَٰتُ بَغۡيَۢا بَيۡنَهُمۡۖ فَهَدَى ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لِمَا ٱخۡتَلَفُواْ فِيهِ مِنَ ٱلۡحَقِّ بِإِذۡنِهِۦۗ وَٱللَّهُ يَهۡدِي مَن يَشَآءُ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٍ

Watu walikuwa umma mmoja. Allah akatuma Mitume wakitoa habari njema na wakitoa maonyo na aliteremsha vitabu pamoja nao kwa haki ili ahukumu kati ya watu katika yale ambayo wametofatiana. Na hawakutofautiana katika hayo isipokuwa wale tu waliopewa vitabu hivyo, baada ya kuwafikia hoja za waziwazi kwa sababu tu ya uovu walionao. Basi Allah akawaongoza wale ambao wameamini kwenye haki kwa idhini yake na Allah anamuongoza amtakaye kwenye njia iliyo nyooka



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 19

إِنَّ ٱلدِّينَ عِندَ ٱللَّهِ ٱلۡإِسۡلَٰمُۗ وَمَا ٱخۡتَلَفَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَهُمُ ٱلۡعِلۡمُ بَغۡيَۢا بَيۡنَهُمۡۗ وَمَن يَكۡفُرۡ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ فَإِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ

Hakika, dini (inayokubalika) kwa Allah ni Uislamu tu. Na wale waliopewa Kitabu hawakutofautiana isipokuwa tu baada ya kuwa elimu imewafikia kwa sababu ya uovu uliokuwepo kati yao. Na yeyote anayezikataa Aya za Allah, basi hakika Allah ni Mwepesi mno wa kuhesabu



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 112

ضُرِبَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلذِّلَّةُ أَيۡنَ مَا ثُقِفُوٓاْ إِلَّا بِحَبۡلٖ مِّنَ ٱللَّهِ وَحَبۡلٖ مِّنَ ٱلنَّاسِ وَبَآءُو بِغَضَبٖ مِّنَ ٱللَّهِ وَضُرِبَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلۡمَسۡكَنَةُۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ كَانُواْ يَكۡفُرُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَيَقۡتُلُونَ ٱلۡأَنۢبِيَآءَ بِغَيۡرِ حَقّٖۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَواْ وَّكَانُواْ يَعۡتَدُونَ

Wamepigwa chapa ya udhalili popote wanapokutwa, isipokuwa (kama) watakuwa wameshika kamba (dini) ya Allah au kamba (misaada) ya watu (wengine). Na wamestahiki ghadhabu za Allah na pia wamepigwa chapa ya umaskini. Hiyo ni kwasababu walikuwa wakizikataa Aya za Allah na kuua Mitume pasina haki yoyote. Hiyo ni kwa sababu ya uasi wao na walikuwa wakichupa mipaka ya sheria (za Allah)



Surah: ANNISAI 

Ayah : 24

۞وَٱلۡمُحۡصَنَٰتُ مِنَ ٱلنِّسَآءِ إِلَّا مَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُكُمۡۖ كِتَٰبَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡۚ وَأُحِلَّ لَكُم مَّا وَرَآءَ ذَٰلِكُمۡ أَن تَبۡتَغُواْ بِأَمۡوَٰلِكُم مُّحۡصِنِينَ غَيۡرَ مُسَٰفِحِينَۚ فَمَا ٱسۡتَمۡتَعۡتُم بِهِۦ مِنۡهُنَّ فَـَٔاتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ فَرِيضَةٗۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ فِيمَا تَرَٰضَيۡتُم بِهِۦ مِنۢ بَعۡدِ ٱلۡفَرِيضَةِۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمٗا

Na (ni haramu kwenu) wanawake walio katika ndoa isipokuwa wale mliowamiliki kwa mikono yenu ya kuume[1], (hili) Allah ameandika kwenu, na mmehalalishiwa (wanawake) wasiokuwa hawa mtake kwa mali zenu, kujilinda na kutofanya zinaa. Na wale (wake) mliokaa nao faragha (baada ya ndoa) kati ya hao, wapeni mahari yao ni lazima. Na si vibaya kwenu kwa mliyoridhiana katika yale yaliyotajwa[2]baada ya kutimiza wajibu, hakika Allah ni mjuzi mwenye hekima


1- - Ni haramu kumuoa mwanamke aliye katika ndoa isipokuwa kafiri endapo atatekwa katika vita ya jihadi ni halali baada ya kukaa wa kusubiria hali ya tumbo lake kuwa si mja mzito


2- - Amesema shekhe Siidy alipotafsiri aya hii wanazuoni waliyo wengi wamesema kuwa; Mwanamke kupunguza sehemu ya waliokubaliana au mwanaume kutoa zaidi ya walichoafikiana


Surah: AL-MAIDA 

Ayah : 87

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تُحَرِّمُواْ طَيِّبَٰتِ مَآ أَحَلَّ ٱللَّهُ لَكُمۡ وَلَا تَعۡتَدُوٓاْۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُعۡتَدِينَ

Enyi mlioamini, msiharimishe vizuri alivyokuhalalishieni Allah, na msikiuke mipaka. Hakika, Allah hawapendi wakiukao mipaka



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 33

قُلۡ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ ٱلۡفَوَٰحِشَ مَا ظَهَرَ مِنۡهَا وَمَا بَطَنَ وَٱلۡإِثۡمَ وَٱلۡبَغۡيَ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّ وَأَن تُشۡرِكُواْ بِٱللَّهِ مَا لَمۡ يُنَزِّلۡ بِهِۦ سُلۡطَٰنٗا وَأَن تَقُولُواْ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ

Sema: Hakika, ilivyo ni kwamba, Mola wangu Mlezi ameharamisha (mambo) machafu; ya dhahiri katika hayo na ya siri na dhambi na dhuluma bila ya haki yoyote,[1] na kuvishirikisha na Allah vitu ambavyo hakuviteremshia dalili (hoja) yoyote na (pia Allah ameharamisha) kumsemea Allah msiyoyajua


1- - Dhuluma bila ya haki ni dhuluma isiyokuwa na msingi wa kisheria. Ama kutekeleza haki kwa msingi wa sheria sio dhuluma wala ukandamizaji, ila tu limetumika neno dhuluma kwa ulinganifu wa lugha. Inayo onekana kama ni dhuluma kwenye macho ya wapingaji wa sheria za Allah ni kama kuuawa kwa mtu aliyethibitika kuua, kukatwa mkono mtu aliyethibitika kuiba n.k. Lakini hii sio dhuluma ila ni haki kwa sababu ni utekelezaji wa sheria.


Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 155

وَٱخۡتَارَ مُوسَىٰ قَوۡمَهُۥ سَبۡعِينَ رَجُلٗا لِّمِيقَٰتِنَاۖ فَلَمَّآ أَخَذَتۡهُمُ ٱلرَّجۡفَةُ قَالَ رَبِّ لَوۡ شِئۡتَ أَهۡلَكۡتَهُم مِّن قَبۡلُ وَإِيَّـٰيَۖ أَتُهۡلِكُنَا بِمَا فَعَلَ ٱلسُّفَهَآءُ مِنَّآۖ إِنۡ هِيَ إِلَّا فِتۡنَتُكَ تُضِلُّ بِهَا مَن تَشَآءُ وَتَهۡدِي مَن تَشَآءُۖ أَنتَ وَلِيُّنَا فَٱغۡفِرۡ لَنَا وَٱرۡحَمۡنَاۖ وَأَنتَ خَيۡرُ ٱلۡغَٰفِرِينَ

Na Musa aliteua katika watu wake wanaume sabini kwa ajili ya miadi yetu. Basi lilipowachukua tetemeko (la ardhi) alisema: Ewe Mola wangu Mlezi, lau kama ulitaka (kuwaangamiza) si ungewaangamiza wao na mimi kabla (ya leo)?[1] Hivi unatuangamiza kwa (sababu ya) waliyofanya wapuuzi miongoni mwetu? Haya si chochote isipokuwa tu ni mtihani wako. Kwa mtihani huo unamuacha umtakaye apotee na unamuongoza umtakaye. Wewe ndiye mwandani wetu. Basi tusamehe na turehemu, na wewe ni bora zaidi ya wenye kusamehe makosa


1- - Nabii Musa aliwachagua wanaume sabini katika watu bora miongoni mwa watu wake kwa ajili ya miadi na Mola wao. Walipofika katika eneo ambalo Musa aliahidiwa na Mola wake, wale watu sabini walimwambia Musa kuwa: Hatutakuamini wewe Musa hadi tumuone Allah bayana. Si unadai umeongea naye, basi tuoneshe sasa? likawakumba tetemeko la ardhi na kuwaangamiza. Nabii Musa alipozinduka akawa anamwambia Mola wake kuwa, atakwenda kusema nini akirudi kwa watu wake kwa kuwashirikisha viongozi wao bora? Ingekuwa vyema, kwa maoni yake, kwamba wangeangamizwa pale mwanzo walipoabudu ndama.


Surah: ATTAUBA 

Ayah : 10

لَا يَرۡقُبُونَ فِي مُؤۡمِنٍ إِلّٗا وَلَا ذِمَّةٗۚ وَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُعۡتَدُونَ

(Makafiri wapo kwenye vita dhidi ya Uislamu na Waislamu muda wote) Hawatazami (hawajali) kwa Muumini udugu wala ahadi, na hao ndio wavukao mipaka



Surah: YUNUS 

Ayah : 23

فَلَمَّآ أَنجَىٰهُمۡ إِذَا هُمۡ يَبۡغُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّۗ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنَّمَا بَغۡيُكُمۡ عَلَىٰٓ أَنفُسِكُمۖ مَّتَٰعَ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۖ ثُمَّ إِلَيۡنَا مَرۡجِعُكُمۡ فَنُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Basi (Allah) alipowaokoa, ghafla wakawa wanafanya uovu katika ardhi bila ya haki. Enyi watu, hakika uasi wenu ni hasara kwenu; ni anasa (fupi) za maisha ya duniani. Kisha kwetu tu ndio marejeo yenu, kwa hiyo tutakuambieni yote mliyokuwa mkiyafanya



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 90

۞إِنَّ ٱللَّهَ يَأۡمُرُ بِٱلۡعَدۡلِ وَٱلۡإِحۡسَٰنِ وَإِيتَآيِٕ ذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَيَنۡهَىٰ عَنِ ٱلۡفَحۡشَآءِ وَٱلۡمُنكَرِ وَٱلۡبَغۡيِۚ يَعِظُكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ

Kwa hakika Allah anaamuru uadilifu, na ihsani, na kuwapa (sadaka) ndugu wa karibu na anakataza uchafu, na uovu, na uasi. Anawanasihini ili mpate kukumbuka



Surah: AL-HAJJ 

Ayah : 60

۞ذَٰلِكَۖ وَمَنۡ عَاقَبَ بِمِثۡلِ مَا عُوقِبَ بِهِۦ ثُمَّ بُغِيَ عَلَيۡهِ لَيَنصُرَنَّهُ ٱللَّهُۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَعَفُوٌّ غَفُورٞ

Ndio namna hivi. Na anaye lipiza mfano wa alivyo adhibiwa, kisha akadhulumiwa, basi hapana shaka Allah atamsaidia. Hakika Allah ni Msamehevu (tena) ni Mwingi wa msamaha



Surah: AL-QASWAS 

Ayah : 76

۞إِنَّ قَٰرُونَ كَانَ مِن قَوۡمِ مُوسَىٰ فَبَغَىٰ عَلَيۡهِمۡۖ وَءَاتَيۡنَٰهُ مِنَ ٱلۡكُنُوزِ مَآ إِنَّ مَفَاتِحَهُۥ لَتَنُوٓأُ بِٱلۡعُصۡبَةِ أُوْلِي ٱلۡقُوَّةِ إِذۡ قَالَ لَهُۥ قَوۡمُهُۥ لَا تَفۡرَحۡۖ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلۡفَرِحِينَ

Hakika Qaruni alikuwa katika watu wa Musa, lakini aliwafanyia dhulma. Na tulimpa khazina ambazo funguo zake zinawachosha watu wenye nguvu kuzichukua. Walipo mwambia watu wake: Usijigambe! Hakika Allah hawapendi wanao jigamba



Surah: SWAAD 

Ayah : 22

إِذۡ دَخَلُواْ عَلَىٰ دَاوُۥدَ فَفَزِعَ مِنۡهُمۡۖ قَالُواْ لَا تَخَفۡۖ خَصۡمَانِ بَغَىٰ بَعۡضُنَا عَلَىٰ بَعۡضٖ فَٱحۡكُم بَيۡنَنَا بِٱلۡحَقِّ وَلَا تُشۡطِطۡ وَٱهۡدِنَآ إِلَىٰ سَوَآءِ ٱلصِّرَٰطِ

Walipoingia kwa Daudi, naye akawaogopa. Wakasema: Usiogope! Sisi ni wagombanao wawili, mmoja wetu amemdhulumu mwenziwe. Basi tuhukumu kwa haki, wala usipendelee. Na utuongoe kwenye njia iliyo sawa



Surah: SWAAD 

Ayah : 24

قَالَ لَقَدۡ ظَلَمَكَ بِسُؤَالِ نَعۡجَتِكَ إِلَىٰ نِعَاجِهِۦۖ وَإِنَّ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلۡخُلَطَآءِ لَيَبۡغِي بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٍ إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ وَقَلِيلٞ مَّا هُمۡۗ وَظَنَّ دَاوُۥدُ أَنَّمَا فَتَنَّـٰهُ فَٱسۡتَغۡفَرَ رَبَّهُۥ وَخَرَّۤ رَاكِعٗاۤ وَأَنَابَ۩

Akasema: Kweli amekudhulumu kwa kumtaka kondoo wako mmoja kuongezea kwenye kondoo wake. Na hakika washirika wengi hudhulumiana wao kwa wao, isipo kuwa walio amini na wakatenda mema. Na hao ni wachache. Na Daudi akajua kuwa tumemfanyia mtihani. Basi akamwomba msamaha Mola wake Mlezi, na akaanguka kusujudu na kutubia



Surah: ASH-SHUURAA 

Ayah : 14

وَمَا تَفَرَّقُوٓاْ إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَهُمُ ٱلۡعِلۡمُ بَغۡيَۢا بَيۡنَهُمۡۚ وَلَوۡلَا كَلِمَةٞ سَبَقَتۡ مِن رَّبِّكَ إِلَىٰٓ أَجَلٖ مُّسَمّٗى لَّقُضِيَ بَيۡنَهُمۡۚ وَإِنَّ ٱلَّذِينَ أُورِثُواْ ٱلۡكِتَٰبَ مِنۢ بَعۡدِهِمۡ لَفِي شَكّٖ مِّنۡهُ مُرِيبٖ

Na hawakufarakana ila baada ya kuwajia elimu kwasababu ya husuda iliyo kuwa baina yao. Na lau kuwa haikwisha tangulia kauli kutoka kwa Mola wako Mlezi ya kuakhirisha mpaka muda maalumu, basi bila ya shaka pangelihukumiwa baina yao. Na hakika waliorithishwa Kitabu baada yao wanakitilia shaka inayo wahangaisha



Surah: ASH-SHUURAA 

Ayah : 27

۞وَلَوۡ بَسَطَ ٱللَّهُ ٱلرِّزۡقَ لِعِبَادِهِۦ لَبَغَوۡاْ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَٰكِن يُنَزِّلُ بِقَدَرٖ مَّا يَشَآءُۚ إِنَّهُۥ بِعِبَادِهِۦ خَبِيرُۢ بَصِيرٞ

Na lau kuwa Allah angeliwa-kunjulia riziki waja wake, basi bila ya shaka wangelikuwa na kiburi katika ardhi. Lakini anaiteremsha kwa kipimo akitakacho. Hakika Yeye anawajua vyema waja wake na anawaona



Surah: ASH-SHUURAA 

Ayah : 39

وَٱلَّذِينَ إِذَآ أَصَابَهُمُ ٱلۡبَغۡيُ هُمۡ يَنتَصِرُونَ

Na ambao wanapo fanyiwa jeuri hujitetea



Surah: ASH-SHUURAA 

Ayah : 42

إِنَّمَا ٱلسَّبِيلُ عَلَى ٱلَّذِينَ يَظۡلِمُونَ ٱلنَّاسَ وَيَبۡغُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّۚ أُوْلَـٰٓئِكَ لَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ

Bali lawama ipo kwa wale wanao wadhulumu watu, na wanafanya jeuri katika nchi bila ya haki. Hao watapata adhabu iliyo chungu



Surah: AL-JAATHIYA 

Ayah : 17

وَءَاتَيۡنَٰهُم بَيِّنَٰتٖ مِّنَ ٱلۡأَمۡرِۖ فَمَا ٱخۡتَلَفُوٓاْ إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَهُمُ ٱلۡعِلۡمُ بَغۡيَۢا بَيۡنَهُمۡۚ إِنَّ رَبَّكَ يَقۡضِي بَيۡنَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فِيمَا كَانُواْ فِيهِ يَخۡتَلِفُونَ

Na tukawapa maelezo ya wazi ya amri. Basi hawakukhitilafiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa ajili ya uhasidi uliokuwa baina yao. Hakika Mola wako Mlezi atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika mambo waliyo kuwa wakikhitilafiana



Surah: AL-HUJURAAT 

Ayah : 9

وَإِن طَآئِفَتَانِ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ٱقۡتَتَلُواْ فَأَصۡلِحُواْ بَيۡنَهُمَاۖ فَإِنۢ بَغَتۡ إِحۡدَىٰهُمَا عَلَى ٱلۡأُخۡرَىٰ فَقَٰتِلُواْ ٱلَّتِي تَبۡغِي حَتَّىٰ تَفِيٓءَ إِلَىٰٓ أَمۡرِ ٱللَّهِۚ فَإِن فَآءَتۡ فَأَصۡلِحُواْ بَيۡنَهُمَا بِٱلۡعَدۡلِ وَأَقۡسِطُوٓاْۖ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُقۡسِطِينَ

Na endapo makundi mawili yamepigana basi wasuluhisheni kati yao na endapo litaasi moja ya makundi hayo juu ya lingine basi lipigeni ambalo linaasi hadi lirudi kwenye amri ya Allah na endapo litarudi basi wasuluhisheni kati yao kiuadilifu na fanyeni usawa hakika Allah anapenda wenye kutenda usawa



Surah: QAAF 

Ayah : 25

مَّنَّاعٖ لِّلۡخَيۡرِ مُعۡتَدٖ مُّرِيبٍ

Mzuiaji wa kheri, mwenye kuruka mipaka, mwenye kutia shaka



Surah: AL-QALAM 

Ayah : 12

مَّنَّاعٖ لِّلۡخَيۡرِ مُعۡتَدٍ أَثِيمٍ

Mwingi wa kuzuia ya kheri, aliyependukia katika kuwadhulumu (Watu) mwingi wa kutenda dhambi



Surah: AL-MUTWAFFIFIIN 

Ayah : 12

وَمَا يُكَذِّبُ بِهِۦٓ إِلَّا كُلُّ مُعۡتَدٍ أَثِيمٍ

Wala haikadhibishi (siku hiyo) isipokuwa kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi