Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 173

إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡمَيۡتَةَ وَٱلدَّمَ وَلَحۡمَ ٱلۡخِنزِيرِ وَمَآ أُهِلَّ بِهِۦ لِغَيۡرِ ٱللَّهِۖ فَمَنِ ٱضۡطُرَّ غَيۡرَ بَاغٖ وَلَا عَادٖ فَلَآ إِثۡمَ عَلَيۡهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ

Yeye tu amekuharamishieni mzoga na damu na nyama ya nguruwe na kilichochinjwa kwa kutaja jina lisiliokuwa la Allah. Lakini, aliyefikwa na dharura bila ya kutamani wala kupitiliza kiasi, hana dhambi[1]. Hakika, Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu


1- - Kula katika hivyo vilivyo haramishwa.


Surah: AL-MAIDA 

Ayah : 3

حُرِّمَتۡ عَلَيۡكُمُ ٱلۡمَيۡتَةُ وَٱلدَّمُ وَلَحۡمُ ٱلۡخِنزِيرِ وَمَآ أُهِلَّ لِغَيۡرِ ٱللَّهِ بِهِۦ وَٱلۡمُنۡخَنِقَةُ وَٱلۡمَوۡقُوذَةُ وَٱلۡمُتَرَدِّيَةُ وَٱلنَّطِيحَةُ وَمَآ أَكَلَ ٱلسَّبُعُ إِلَّا مَا ذَكَّيۡتُمۡ وَمَا ذُبِحَ عَلَى ٱلنُّصُبِ وَأَن تَسۡتَقۡسِمُواْ بِٱلۡأَزۡلَٰمِۚ ذَٰلِكُمۡ فِسۡقٌۗ ٱلۡيَوۡمَ يَئِسَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن دِينِكُمۡ فَلَا تَخۡشَوۡهُمۡ وَٱخۡشَوۡنِۚ ٱلۡيَوۡمَ أَكۡمَلۡتُ لَكُمۡ دِينَكُمۡ وَأَتۡمَمۡتُ عَلَيۡكُمۡ نِعۡمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ ٱلۡإِسۡلَٰمَ دِينٗاۚ فَمَنِ ٱضۡطُرَّ فِي مَخۡمَصَةٍ غَيۡرَ مُتَجَانِفٖ لِّإِثۡمٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Mmeharamishiwa (kula) mzoga[1] na damu na nyama ya nguruwe na (mnyama) aliyechinjwa pasina (kutajwa jina la) Allah na (mnyama) aliyekufa kwa kusongeka koo (kujinyonga) na aliyekufa kwa kupigwa na aliyekufa kwa kuporomoka na aliyekufa kwa kupigwa pembe (na mwenzake) na aliyeliwa (kwa kushambuliwa) na mnyama mkali ila (mliyemuwahi akiwa hai) mkamchinja. Na (pia mmeharamishiwa kula nyama ya mnyama) aliyechinjwa katika (sehem yalipo) masanamu.[2] Na (mmeharamishiwa) kutaka kujua mambo yaliyopangwa (na Allah ikiwemo kupiga ramli na mfano wa hilo) kwa kutumia mbao. Ilivyo ni kwamba hayo (yote) ni uovu. Leo waliokufuru wameikatia tamaa dini yenu, basi msiwaogope (isipokuwa) niogopeni Mimi. Leo nimekukamilishieni dini yenu na kukutimizieni neema yangu na nimeuchagua Uislamu uwe dini yenu. Na mwenye kushikwa na dhiki ya njaa kali pasipo na kukusudia dhambi (anaruhusiwa kula hivyo vilivyoharamishwa kwa sababu) hakika, Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa huruma


1- - Mzoga ni mnyama aliyekufa mwenyewe au amechinjwa bila ya kufuata taratibu za sheria ya Kiislamu; kibudu, nyamafu.


2- - Mnyama aliyechinjwa katika sehemu za masanamu, mizimu, makaburini nk. Ni haramu kula nyama yake.


Surah: AL-MAIDA 

Ayah : 6

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا قُمۡتُمۡ إِلَى ٱلصَّلَوٰةِ فَٱغۡسِلُواْ وُجُوهَكُمۡ وَأَيۡدِيَكُمۡ إِلَى ٱلۡمَرَافِقِ وَٱمۡسَحُواْ بِرُءُوسِكُمۡ وَأَرۡجُلَكُمۡ إِلَى ٱلۡكَعۡبَيۡنِۚ وَإِن كُنتُمۡ جُنُبٗا فَٱطَّهَّرُواْۚ وَإِن كُنتُم مَّرۡضَىٰٓ أَوۡ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوۡ جَآءَ أَحَدٞ مِّنكُم مِّنَ ٱلۡغَآئِطِ أَوۡ لَٰمَسۡتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَلَمۡ تَجِدُواْ مَآءٗ فَتَيَمَّمُواْ صَعِيدٗا طَيِّبٗا فَٱمۡسَحُواْ بِوُجُوهِكُمۡ وَأَيۡدِيكُم مِّنۡهُۚ مَا يُرِيدُ ٱللَّهُ لِيَجۡعَلَ عَلَيۡكُم مِّنۡ حَرَجٖ وَلَٰكِن يُرِيدُ لِيُطَهِّرَكُمۡ وَلِيُتِمَّ نِعۡمَتَهُۥ عَلَيۡكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ

Enyi mlioamini, mnaposimama kwenda kuswali[1], basi (tawadheni) osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka viwikoni na pakeni (maji) vichwa vyenu na (osheni) miguu yenu mpaka vifundoni[2]. Na mkiwa wenye Janaba basi jitwaharisheni (kwa kuoga au kutayamamu ikishindikana kuoga). Na mkiwa wagonjwa au mpo safarini au mmoja wenu ametoka msalani au mmegusana (mmejamiiana) na wanawake (wake zenu)[3] na hamkupata maji, basi tayamamuni (kusudieni) mchanga ulio safi[4] na mpake nyuso zenu na mikono yenu kwa mchanga huo[5]. Allah hataki kukuwekeeni tabu yoyote (uzito na usumbufu kwa kulazimisha kujitwaharisha kwa maji wakati maji hayapo au haiwezekani kuyatumia kwasababu ya ugonjwa au baridi kali); bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake kwenu ili mpate kushukuru.[6]


1- - Hii ina maana hata kwa anayeswali kwa kuketi au kwa kulala ujumbe na utaratibu huu unamhusu pia.


2- - Kwenye Aya hii kuna visomo vikuu viwili vinavyokubalika: “Arjulakum” kwa Nasbu. Na kisomo cha pili ni “Arjulikum” kwa Jarri. Hii inamaanisha kwamba, kwa mujibu wa Qur’an na Suna sahihi za Mtume wa Allah uoshaji wa miguu una hukumu za aina mbili: (a) Kama miguu ikiwa wazi (haijavikwa kitu) faradhi yake ni kuoshwa kwa maji. (b) Kama miguu imevikwa khofu/soksi faradhi yake ni kupakwa maji.


3- - Muradi wa kugusana hapa ni kujamiiana. Kugusana tu kwa Ngozi na Ngozi hakulazimishi kutawadha.


4- - Kitendo hiki cha kutumia mchanga ulio safi na kupaka vumbi lake usoni na mikononi kinaitwa Tayamamu katika sheria ya Kiislamu.


5- - Kwa pigo la kwanza pakeni usoni na kwa pigo la pili pakeni mikononi.


6- - Aya hapa inaonesha kuwa ni lazima Muislamu kila anapotaka kuswali atawadhe. Lakini ulazima huu ni kwa yule ambaye hana Udhu. Ama mtu mwenye Udhu halazimiki kutawadha, lakini ni jambo zuri kama
atatawadha tena.


Surah: AL-MAIDA 

Ayah : 31

فَبَعَثَ ٱللَّهُ غُرَابٗا يَبۡحَثُ فِي ٱلۡأَرۡضِ لِيُرِيَهُۥ كَيۡفَ يُوَٰرِي سَوۡءَةَ أَخِيهِۚ قَالَ يَٰوَيۡلَتَىٰٓ أَعَجَزۡتُ أَنۡ أَكُونَ مِثۡلَ هَٰذَا ٱلۡغُرَابِ فَأُوَٰرِيَ سَوۡءَةَ أَخِيۖ فَأَصۡبَحَ مِنَ ٱلنَّـٰدِمِينَ

Basi hapo Allah akampeleka kunguru anayefukua ardhini ili amuoneshe namna ya kusitiri (kuzika) mwili wa nduguye. Akasema: “Ole wangu! Hivi nimeshindwa kuwa kama huyu kunguru nikasitiri mwili wa ndugu yangu?”. Basi akawa ni miongoni mwa wenye kujuta



Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 145

قُل لَّآ أَجِدُ فِي مَآ أُوحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَىٰ طَاعِمٖ يَطۡعَمُهُۥٓ إِلَّآ أَن يَكُونَ مَيۡتَةً أَوۡ دَمٗا مَّسۡفُوحًا أَوۡ لَحۡمَ خِنزِيرٖ فَإِنَّهُۥ رِجۡسٌ أَوۡ فِسۡقًا أُهِلَّ لِغَيۡرِ ٱللَّهِ بِهِۦۚ فَمَنِ ٱضۡطُرَّ غَيۡرَ بَاغٖ وَلَا عَادٖ فَإِنَّ رَبَّكَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Sema: Katika yale niliyofunuliwa (niliyopewa Wahyi) sipati kilichoharamishwa kwa mlaji anayekila isipokuwa tu kama kitakuwa nyamafu au damu yenye kuchirizika au nyama ya nguruwe, kwa sababu hivyo ni najisi, au kilichochinjwa kwa minajili ya kutajwa asiyekuwa Allah katika kuchinjwa kwake.[1] Basi aliyeshikika pasipo kupenda wala kuchupa mipaka (anaruhusiwa kula hivyo vilivyoharamishwa kwakuwa) Mola wako Mlezi ni Msamehevu sana, Mwenye kurehemu


1- - Hapa Qur’ani imemtaka Mtume ataje baadhi ya vitu vilivyoharamishwa. Hivi ni baadhi tu. Vingine amevitaja Mtume kupitia Hadithi zake. Watu wa Suna na Jamaa (Suna) wanavikubali vilivyotajwa na Mtume kupitia maagizo ya Allah kwamba, anayotuagiza Mtume tuyafuate na anayotukataza tuyaache. Rejea Aya ya 7 ya Sura Alhashri (59).


Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 31

۞يَٰبَنِيٓ ءَادَمَ خُذُواْ زِينَتَكُمۡ عِندَ كُلِّ مَسۡجِدٖ وَكُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ وَلَا تُسۡرِفُوٓاْۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُسۡرِفِينَ

Enyi wanadamu, chukueni mapambo yenu kila muendapo msikitini (kila mnaposwali)[1] na kuleni na kunyweni na msifanye ubadhirifu. Hakika, yeye (Allah) hawapendi wabadhirifu


1- - Aya hii ndio iliyoweka sharti la Muislamu kujisitiri kwa kuvaa nguo za heshima na sitara katika Swala. Na sio kuvaa nguo tu, lakini kuvaa nguo ya sitara, safi na inayopendeza. Kwa msingi huu, sio vyema kwa Muislamu kuswali akiwa amevaa nguo chafu au zenye michoro, picha na mandishi yasiyokuwa na lazima.


Surah: ANNAHLI 

Ayah : 69

ثُمَّ كُلِي مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِ فَٱسۡلُكِي سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلٗاۚ يَخۡرُجُ مِنۢ بُطُونِهَا شَرَابٞ مُّخۡتَلِفٌ أَلۡوَٰنُهُۥ فِيهِ شِفَآءٞ لِّلنَّاسِۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّقَوۡمٖ يَتَفَكَّرُونَ

Kisha kula kila aina ya matunda, na zifuate kwa unyenyekevu njia za Mola wako mlezi. Kinatoka katika matumbo yao kinywaji chenye rangi mbalimbali. Ndani yake kuna shifaa kwa watu. Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wenye kutafakari (na kuzingatia)



Surah: MARYAM 

Ayah : 25

وَهُزِّيٓ إِلَيۡكِ بِجِذۡعِ ٱلنَّخۡلَةِ تُسَٰقِطۡ عَلَيۡكِ رُطَبٗا جَنِيّٗا

Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu



Surah: AL-HAJJ 

Ayah : 29

ثُمَّ لۡيَقۡضُواْ تَفَثَهُمۡ وَلۡيُوفُواْ نُذُورَهُمۡ وَلۡيَطَّوَّفُواْ بِٱلۡبَيۡتِ ٱلۡعَتِيقِ

Kisha wajisafishe taka zao, na waondoe nadhiri zao, na waizunguke Nyumba ya Kale