Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 188

وَلَا تَأۡكُلُوٓاْ أَمۡوَٰلَكُم بَيۡنَكُم بِٱلۡبَٰطِلِ وَتُدۡلُواْ بِهَآ إِلَى ٱلۡحُكَّامِ لِتَأۡكُلُواْ فَرِيقٗا مِّنۡ أَمۡوَٰلِ ٱلنَّاسِ بِٱلۡإِثۡمِ وَأَنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Na msile mali zenu baina yenu kwa batili na kuzipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali ya watu kwa dhambi na ilhali mnajua



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 161

وَمَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَغُلَّۚ وَمَن يَغۡلُلۡ يَأۡتِ بِمَا غَلَّ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفۡسٖ مَّا كَسَبَتۡ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ

Na haiwezekani kwa Nabii yeyote kufanya khiyana, na atakayefanya khiyana atayaleta aliyoyafanyia khiyana Siku ya Kiama kisha kila nafsi italipwa kwa iliyoyachuma kwa ukamilifu, nao hawatadhulumiwa



Surah: ANNISAI 

Ayah : 2

وَءَاتُواْ ٱلۡيَتَٰمَىٰٓ أَمۡوَٰلَهُمۡۖ وَلَا تَتَبَدَّلُواْ ٱلۡخَبِيثَ بِٱلطَّيِّبِۖ وَلَا تَأۡكُلُوٓاْ أَمۡوَٰلَهُمۡ إِلَىٰٓ أَمۡوَٰلِكُمۡۚ إِنَّهُۥ كَانَ حُوبٗا كَبِيرٗا

Na wapeni Yatima mali zao, na msibadilishe kibaya kwa kizuri na msile mali zao (kwa kuzichanganya) katika mali zenu. Kwa hakika, hilo limekuwa dhambi kubwa kabisa



Surah: ANNISAI 

Ayah : 29

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَأۡكُلُوٓاْ أَمۡوَٰلَكُم بَيۡنَكُم بِٱلۡبَٰطِلِ إِلَّآ أَن تَكُونَ تِجَٰرَةً عَن تَرَاضٖ مِّنكُمۡۚ وَلَا تَقۡتُلُوٓاْ أَنفُسَكُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِكُمۡ رَحِيمٗا

Enyi mlioamini, msile mali zenu baina yenu kwa batili, isipokuwa tu kama mali hizo ni biashara (inayofanyika) kwa maridhiano yenu. Na msijiue. Hakika, Allah ni mwenye rehema kwenu



Surah: ANNISAI 

Ayah : 30

وَمَن يَفۡعَلۡ ذَٰلِكَ عُدۡوَٰنٗا وَظُلۡمٗا فَسَوۡفَ نُصۡلِيهِ نَارٗاۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرًا

Na atakayefanya hayo kwa uadui na dhuluma, basi huyo tutamuingiza Motoni, na hilo kwa Allah ni jepesi sana



Surah: ANNISAI 

Ayah : 162

لَّـٰكِنِ ٱلرَّـٰسِخُونَ فِي ٱلۡعِلۡمِ مِنۡهُمۡ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَ يُؤۡمِنُونَ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبۡلِكَۚ وَٱلۡمُقِيمِينَ ٱلصَّلَوٰةَۚ وَٱلۡمُؤۡتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ أُوْلَـٰٓئِكَ سَنُؤۡتِيهِمۡ أَجۡرًا عَظِيمًا

Lakini waliobobea katika elimu miongoni mwao, na waumini wanaamini yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako na wenye kusimamisha Swala na wenye kutoa Zaka na wenye kumuamini Allah na Siku ya Mwisho. Hao tutawapa malipo makubwa sana



Surah: AL-MAIDA 

Ayah : 42

سَمَّـٰعُونَ لِلۡكَذِبِ أَكَّـٰلُونَ لِلسُّحۡتِۚ فَإِن جَآءُوكَ فَٱحۡكُم بَيۡنَهُمۡ أَوۡ أَعۡرِضۡ عَنۡهُمۡۖ وَإِن تُعۡرِضۡ عَنۡهُمۡ فَلَن يَضُرُّوكَ شَيۡـٔٗاۖ وَإِنۡ حَكَمۡتَ فَٱحۡكُم بَيۡنَهُم بِٱلۡقِسۡطِۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُقۡسِطِينَ

(Hao ni) Wasikilizaji sana wa uwongo, walaji sana wa haramu. Basi wakikujia, wahukumu baina yao au wapuuze[1]. Na ukiwapuuza, katu hawatakudhuru kitu chochote. Na ukihukumu, basi hukumu baina yao kwa uadilifu. Hakika, Allah anawapenda waadilifu


1- - Amri hii ya kupuuza imefutwa kwa Aya ya 49 ya Sura hii hii ya Almaida (5) inayolazimisha kutekelezwa kwa hukumu bila ya kuwa na hiari ya kupuuza.


Surah: AL-MAIDA 

Ayah : 62

وَتَرَىٰ كَثِيرٗا مِّنۡهُمۡ يُسَٰرِعُونَ فِي ٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡعُدۡوَٰنِ وَأَكۡلِهِمُ ٱلسُّحۡتَۚ لَبِئۡسَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Na utawaona wengi kati yao wanakimbilia kwenye dhambi na uadui na ulaji wao wa vya haramu. Kwa yakini kabisa, ni maovu mno hayo waliyokuwa wanayatenda



Surah: AL-MAIDA 

Ayah : 63

لَوۡلَا يَنۡهَىٰهُمُ ٱلرَّبَّـٰنِيُّونَ وَٱلۡأَحۡبَارُ عَن قَوۡلِهِمُ ٱلۡإِثۡمَ وَأَكۡلِهِمُ ٱلسُّحۡتَۚ لَبِئۡسَ مَا كَانُواْ يَصۡنَعُونَ

Mbona wachamungu (wao) na wanazuoni (wao) hawawakatazi kusema maneno ya dhambi na ulaji wao wa vya haramu? Kwa yakini kabisa, ni maovu mno hayo waliyokuwa wanayafanya



Surah: AL-MAIDA 

Ayah : 78

لُعِنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۢ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ عَلَىٰ لِسَانِ دَاوُۥدَ وَعِيسَى ٱبۡنِ مَرۡيَمَۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَواْ وَّكَانُواْ يَعۡتَدُونَ

Wamelaaniwa waliokufuru miongoni mwa Wana wa Israili kupitia ulimi wa Daudi na Issa Mwana wa Mariamu. Hayo ni kwasababu waliasi na walikuwa wanachupa mipaka



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 34

۞يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِنَّ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلۡأَحۡبَارِ وَٱلرُّهۡبَانِ لَيَأۡكُلُونَ أَمۡوَٰلَ ٱلنَّاسِ بِٱلۡبَٰطِلِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِۗ وَٱلَّذِينَ يَكۡنِزُونَ ٱلذَّهَبَ وَٱلۡفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ فَبَشِّرۡهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٖ

Enyi mlioamini, kwa hakika kabisa watawa na makuhani wengi wanakula mali za watu kwa batili na wanazuia (watu kufuata) Njia ya Allah (Uislamu). Na wale wanaolimbikiza dhahabu na fedha na hawazitumii katika Njia ya Allah, wabashirie (waonye) adhabu iumizayo mno



Surah: AL-KAHF 

Ayah : 79

أَمَّا ٱلسَّفِينَةُ فَكَانَتۡ لِمَسَٰكِينَ يَعۡمَلُونَ فِي ٱلۡبَحۡرِ فَأَرَدتُّ أَنۡ أَعِيبَهَا وَكَانَ وَرَآءَهُم مَّلِكٞ يَأۡخُذُ كُلَّ سَفِينَةٍ غَصۡبٗا

Ama lile jahazi lilikuwa la masikini wafanyao kazi baharini. Nilitaka kuliharibu, kwani nyuma yao alikuwako mfalme anaghusubu (anapora) majahazi yote



Surah: AL-FAJRI 

Ayah : 19

وَتَأۡكُلُونَ ٱلتُّرَاثَ أَكۡلٗا لَّمّٗا

Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa,



Surah: AL-FAJRI 

Ayah : 20

وَتُحِبُّونَ ٱلۡمَالَ حُبّٗا جَمّٗا

Na mnapenda mali mapenzi ya kupita kiasi