Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 83

وَإِذۡ أَخَذۡنَا مِيثَٰقَ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ لَا تَعۡبُدُونَ إِلَّا ٱللَّهَ وَبِٱلۡوَٰلِدَيۡنِ إِحۡسَانٗا وَذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينِ وَقُولُواْ لِلنَّاسِ حُسۡنٗا وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ ثُمَّ تَوَلَّيۡتُمۡ إِلَّا قَلِيلٗا مِّنكُمۡ وَأَنتُم مُّعۡرِضُونَ

Na (kumbukeni) Tulipochukua ahadi kwa Wana wa Israeli kwamba, hamtamuabudu yeyote Ila Allah tu, na mtawatendea wema wazazi, na ndugu na yatima na maskini, na mseme na watu kwa maneno mazuri. Na simamisheni Swala na toeni Zaka, kisha mkakengeuka isipokuwa wachache tu kati yenu, na ilhali nyinyi mnapuuza



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 220

فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۗ وَيَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلۡيَتَٰمَىٰۖ قُلۡ إِصۡلَاحٞ لَّهُمۡ خَيۡرٞۖ وَإِن تُخَالِطُوهُمۡ فَإِخۡوَٰنُكُمۡۚ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ ٱلۡمُفۡسِدَ مِنَ ٱلۡمُصۡلِحِۚ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَأَعۡنَتَكُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٞ

(Ili mtafakari) duniani na akhera. Na wanakuuliza kuhusu Mayatima. Sema: Kuwatengenezea vizuri mambo yao ni jambo la heri, na mkijichanganya nao basi hao ni ndugu zenu. Na Allah anamjua mharibifu na mtengenezaji. Na Allah lau angetaka (kukupatisheni tabu) angekupatisheni tabu. Kwa hakika Allah ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima mno



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 233

۞وَٱلۡوَٰلِدَٰتُ يُرۡضِعۡنَ أَوۡلَٰدَهُنَّ حَوۡلَيۡنِ كَامِلَيۡنِۖ لِمَنۡ أَرَادَ أَن يُتِمَّ ٱلرَّضَاعَةَۚ وَعَلَى ٱلۡمَوۡلُودِ لَهُۥ رِزۡقُهُنَّ وَكِسۡوَتُهُنَّ بِٱلۡمَعۡرُوفِۚ لَا تُكَلَّفُ نَفۡسٌ إِلَّا وُسۡعَهَاۚ لَا تُضَآرَّ وَٰلِدَةُۢ بِوَلَدِهَا وَلَا مَوۡلُودٞ لَّهُۥ بِوَلَدِهِۦۚ وَعَلَى ٱلۡوَارِثِ مِثۡلُ ذَٰلِكَۗ فَإِنۡ أَرَادَا فِصَالًا عَن تَرَاضٖ مِّنۡهُمَا وَتَشَاوُرٖ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡهِمَاۗ وَإِنۡ أَرَدتُّمۡ أَن تَسۡتَرۡضِعُوٓاْ أَوۡلَٰدَكُمۡ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ إِذَا سَلَّمۡتُم مَّآ ءَاتَيۡتُم بِٱلۡمَعۡرُوفِۗ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ

Na wazazi wanawake wan-yonyeshe watoto wao miaka miwili kamili, kwa anayetaka kutimiza kunyonyesha. Na ni juu ya baba chakula chao (mama na mtoto) na kivazi chao kwa wema. Nafsi haikalifishwi (kufanya jambo) isipokuwa lililo ndani ya uwezo wake tu. Mama asidhuriwe kwa sababu ya mwanawe, na baba asidhuriwe kwa sababu ya mwanawe. Na ni wajibu juu ya mrithi (wa mtoto kufanya hayo). Na si vibaya kwa wawili hao (baba na mama) wakitaka kumwachisha ziwa (mtoto chini ya miaka miwili) kwa kushauriana na kuridhiana. Na mkitaka kuwapatia watoto wenu mama wa kuwanyonyesha, basi hapana ubaya kwenu mkitoa kile mlichowapa kwa njia ya wema. Na mcheni Allah na jueni kwamba Allah ni mwenye kuyaona sana yote myatendayo



Surah: ANNISAI 

Ayah : 2

وَءَاتُواْ ٱلۡيَتَٰمَىٰٓ أَمۡوَٰلَهُمۡۖ وَلَا تَتَبَدَّلُواْ ٱلۡخَبِيثَ بِٱلطَّيِّبِۖ وَلَا تَأۡكُلُوٓاْ أَمۡوَٰلَهُمۡ إِلَىٰٓ أَمۡوَٰلِكُمۡۚ إِنَّهُۥ كَانَ حُوبٗا كَبِيرٗا

Na wapeni Yatima mali zao, na msibadilishe kibaya kwa kizuri na msile mali zao (kwa kuzichanganya) katika mali zenu. Kwa hakika, hilo limekuwa dhambi kubwa kabisa



Surah: ANNISAI 

Ayah : 6

وَٱبۡتَلُواْ ٱلۡيَتَٰمَىٰ حَتَّىٰٓ إِذَا بَلَغُواْ ٱلنِّكَاحَ فَإِنۡ ءَانَسۡتُم مِّنۡهُمۡ رُشۡدٗا فَٱدۡفَعُوٓاْ إِلَيۡهِمۡ أَمۡوَٰلَهُمۡۖ وَلَا تَأۡكُلُوهَآ إِسۡرَافٗا وَبِدَارًا أَن يَكۡبَرُواْۚ وَمَن كَانَ غَنِيّٗا فَلۡيَسۡتَعۡفِفۡۖ وَمَن كَانَ فَقِيرٗا فَلۡيَأۡكُلۡ بِٱلۡمَعۡرُوفِۚ فَإِذَا دَفَعۡتُمۡ إِلَيۡهِمۡ أَمۡوَٰلَهُمۡ فَأَشۡهِدُواْ عَلَيۡهِمۡۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ حَسِيبٗا

Na wapeni majaribio Yatima[1] mpaka wafikiapo (umri wa) kuoa, na kama mtajiridhisha kwao ukomavu (wa kufanya matumizi), basi wapeni mali zao na msizile mali hizo kwa fujo na kuwahi kabla wenyewe kuwa wakubwa. Na yeyote aliye na uwezo aache (kuzitumia) na yeyote aliye fakiri basi na ale kwa uzuri. Na pindi mtapowapa mali zao wawekeeni ushahidi, na inatosha Allah kuwa mwenye kuhesabu


1- - Iili kujua uwezo wao wa kuweza kujiendesha kimaisha endapo watakabidhiwa mali zao.


Surah: ANNISAI 

Ayah : 8

وَإِذَا حَضَرَ ٱلۡقِسۡمَةَ أُوْلُواْ ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينُ فَٱرۡزُقُوهُم مِّنۡهُ وَقُولُواْ لَهُمۡ قَوۡلٗا مَّعۡرُوفٗا

Na kama (katika kikao cha) kugawa watahudhuria ndugu na Yatima na masikini basi waruzukuni humo chochote, na waambieni kauli nzuri



Surah: ANNISAI 

Ayah : 10

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَأۡكُلُونَ أَمۡوَٰلَ ٱلۡيَتَٰمَىٰ ظُلۡمًا إِنَّمَا يَأۡكُلُونَ فِي بُطُونِهِمۡ نَارٗاۖ وَسَيَصۡلَوۡنَ سَعِيرٗا

Hakika wale wanaokula mali za Yatima kwa dhulma kwa hakika wanakula moto (kutia) matumboni mwao na watauingia Motoni



Surah: ANNISAI 

Ayah : 26

يُرِيدُ ٱللَّهُ لِيُبَيِّنَ لَكُمۡ وَيَهۡدِيَكُمۡ سُنَنَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ وَيَتُوبَ عَلَيۡكُمۡۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ

Allah anataka kukubainishieni na kukuongozeni katika njia za wale waliokuwepo kabla yenu, na kukusameheni. Na Allah ni Mjuzi mno, Mwenye hekima



Surah: ANNISAI 

Ayah : 127

وَيَسۡتَفۡتُونَكَ فِي ٱلنِّسَآءِۖ قُلِ ٱللَّهُ يُفۡتِيكُمۡ فِيهِنَّ وَمَا يُتۡلَىٰ عَلَيۡكُمۡ فِي ٱلۡكِتَٰبِ فِي يَتَٰمَى ٱلنِّسَآءِ ٱلَّـٰتِي لَا تُؤۡتُونَهُنَّ مَا كُتِبَ لَهُنَّ وَتَرۡغَبُونَ أَن تَنكِحُوهُنَّ وَٱلۡمُسۡتَضۡعَفِينَ مِنَ ٱلۡوِلۡدَٰنِ وَأَن تَقُومُواْ لِلۡيَتَٰمَىٰ بِٱلۡقِسۡطِۚ وَمَا تَفۡعَلُواْ مِنۡ خَيۡرٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِهِۦ عَلِيمٗا

Na wanakuuliza Fat’wa[1] kuhusu wanawake. Sema: Allah anakupeni Fat`wa kuhusu wao na (kuhusu) yale yanayosomwa kwenu katika kitabu (hiki) kuhusu Yatima wanawake ambao hamuwapi kile kilicho wajibu kupewa na mnatamani kuwaoa, na (Fat’wa kuhusu) wale wanyonge miongoni mwa watoto na kwamba muwasimamie Yatima kwa uadilifu. Na kheri yoyote mnayoifanya basi hakika Allah anaijua sana


1- - Fat’wa katika Uislamu ni kutoa maelezo ya hukumu ya sheria, kwa maana ya kufafanua na sio kulazimisha. Anayefanya hivi anaitwa Mufti. Kadhi na Mufti wanatofautiana kwamba kazi ya Kadhi ni kutoa hukumu na kulazimisha utekelezwaji wa hukumu hiyo wakati kauli ya Mufti na ufafanuzi wa hukumu yake sio lazima kutekelezwa. Rejea kitabu cha Al-Ahkaamus Sultwaaniyyah cha Imamu Almaawardi, Allah amrehemu.


Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 139

وَقَالُواْ مَا فِي بُطُونِ هَٰذِهِ ٱلۡأَنۡعَٰمِ خَالِصَةٞ لِّذُكُورِنَا وَمُحَرَّمٌ عَلَىٰٓ أَزۡوَٰجِنَاۖ وَإِن يَكُن مَّيۡتَةٗ فَهُمۡ فِيهِ شُرَكَآءُۚ سَيَجۡزِيهِمۡ وَصۡفَهُمۡۚ إِنَّهُۥ حَكِيمٌ عَلِيمٞ

Na (Washirikina) wamesema: Vilivyomo ndani ya matumbo ya wanyama hawa (mimba zao) ni mahususi (halali) kwa wanaume wetu na ni haramu kwa wake zetu. Na kama (Wanyama hao) wakiwa wamekufa (nyamafu) basi wao ni washirika kwenye hilo (ni halali kwa wake na waume). (Allah) Atawalipa wasifu wao (wanaoustahiki). Hakika yeye (Allah) ni Mwenye hekima, Mjuzi mno



Surah: AN-FAL 

Ayah : 41

۞وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّمَا غَنِمۡتُم مِّن شَيۡءٖ فَأَنَّ لِلَّهِ خُمُسَهُۥ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينِ وَٱبۡنِ ٱلسَّبِيلِ إِن كُنتُمۡ ءَامَنتُم بِٱللَّهِ وَمَآ أَنزَلۡنَا عَلَىٰ عَبۡدِنَا يَوۡمَ ٱلۡفُرۡقَانِ يَوۡمَ ٱلۡتَقَى ٱلۡجَمۡعَانِۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Na jueni ya kwamba, ngawira[1] yoyote mnayoipata, basi khumsi (moja ya tano 1/5) ni ya Allah na Mtume na jamaa (wa Mtume) na mayatima na masikini na msafiri, ikiwa nyinyi mmemuamini Allah na tuliyoyateremsha kwa mja wetu siku ya upambanuzi (siku ya vita vya Badri), siku yalipokutana majeshi mawili. Na Allah ni Muweza wa kila kitu


1- - Ngawira ni mali ya makafiri itekwayo na wapiganaji wa Kiislamu katika vita vya Jihadi na ambayo
hugawanya mafungu matano, mafungu manne ni ya wapiganaji na fungu la tano “Khumsi” ndio la Allah
na Mtumewe na ambalo hugawanywa mafungu matano...


Surah: AL-ISRAA 

Ayah : 24

وَٱخۡفِضۡ لَهُمَا جَنَاحَ ٱلذُّلِّ مِنَ ٱلرَّحۡمَةِ وَقُل رَّبِّ ٱرۡحَمۡهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرٗا

Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni



Surah: AL-ISRAA 

Ayah : 31

وَلَا تَقۡتُلُوٓاْ أَوۡلَٰدَكُمۡ خَشۡيَةَ إِمۡلَٰقٖۖ نَّحۡنُ نَرۡزُقُهُمۡ وَإِيَّاكُمۡۚ إِنَّ قَتۡلَهُمۡ كَانَ خِطۡـٔٗا كَبِيرٗا

Wala msiwauwe watoto wenu kwa kuogopa umasikini. Sisi tunawaruzuku wao na nyinyi. Hakika kuwaua hao ni hatia (kosa) kubwa sana



Surah: AL-KAHF 

Ayah : 82

وَأَمَّا ٱلۡجِدَارُ فَكَانَ لِغُلَٰمَيۡنِ يَتِيمَيۡنِ فِي ٱلۡمَدِينَةِ وَكَانَ تَحۡتَهُۥ كَنزٞ لَّهُمَا وَكَانَ أَبُوهُمَا صَٰلِحٗا فَأَرَادَ رَبُّكَ أَن يَبۡلُغَآ أَشُدَّهُمَا وَيَسۡتَخۡرِجَا كَنزَهُمَا رَحۡمَةٗ مِّن رَّبِّكَۚ وَمَا فَعَلۡتُهُۥ عَنۡ أَمۡرِيۚ ذَٰلِكَ تَأۡوِيلُ مَا لَمۡ تَسۡطِع عَّلَيۡهِ صَبۡرٗا

Na ama ukuta, huo ulikuwa ni wa vijana wawili mayatima kule mjini. Na chini yake ilikuwepo hazina yao; na Baba yao alikuwa ni mtu mwema. Basi Mola wako Mlezi alitaka wafikie utu uzima na wajitolee hazina yao wenyewe, kuwa ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Wala mimi sikutenda hayo kwa amri yangu. Hiyo ndiyo tafsiri ya hayo ambayo wewe hukuweza kuyasubiria



Surah: MARYAM 

Ayah : 7

يَٰزَكَرِيَّآ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَٰمٍ ٱسۡمُهُۥ يَحۡيَىٰ لَمۡ نَجۡعَل لَّهُۥ مِن قَبۡلُ سَمِيّٗا

(Akaambiwa): Ewe Zakariya! Hakika Sisi tunakubashiria mwana; jina lake ni Yahya. Hatujapata kumpa jina hilo yeyote kabla yake



Surah: LUQMAAN 

Ayah : 19

وَٱقۡصِدۡ فِي مَشۡيِكَ وَٱغۡضُضۡ مِن صَوۡتِكَۚ إِنَّ أَنكَرَ ٱلۡأَصۡوَٰتِ لَصَوۡتُ ٱلۡحَمِيرِ

Na ushike mwendo wa katikati, na teremsha sauti yako. Hakika katika sauti mbaya zote bila ya shaka iliyo zidi ni sauti ya punda



Surah: ATTUR 

Ayah : 26

قَالُوٓاْ إِنَّا كُنَّا قَبۡلُ فِيٓ أَهۡلِنَا مُشۡفِقِينَ

Watasema hakika sisi tulikua kabla ya hapa kwa watu wetu wenye kuwafanyia upole



Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 7

مَّآ أَفَآءَ ٱللَّهُ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡقُرَىٰ فَلِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينِ وَٱبۡنِ ٱلسَّبِيلِ كَيۡ لَا يَكُونَ دُولَةَۢ بَيۡنَ ٱلۡأَغۡنِيَآءِ مِنكُمۡۚ وَمَآ ءَاتَىٰكُمُ ٱلرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَىٰكُمۡ عَنۡهُ فَٱنتَهُواْۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۖ إِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ

Ngawira Aliyotoa Allah kwa Mtume Wake kutoka kwa watu wa hivi vijiji ni kwa ajili ya Allah na kwaajili ya Mtume na kwa ajili ya jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini na msafiri aliyeharibikiwa, ili isiwe yakizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu. Na lolote analokupeni Mtume basi lichukueni, na analokukatazeni, basi acheni. Na mcheni Allah. Hakika Allah ni Mkali wa kudhiabu



Surah: AL-INSAAN

Ayah : 8

وَيُطۡعِمُونَ ٱلطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِۦ مِسۡكِينٗا وَيَتِيمٗا وَأَسِيرًا

Na wanalisha chakula, pamoja na kukipenda kwake, (wanawalisha) masikini na mayatima na mateka



Surah: ADH-DHUHAA 

Ayah : 9

فَأَمَّا ٱلۡيَتِيمَ فَلَا تَقۡهَرۡ

Basi yatima usimwonee!