Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 155

وَلَنَبۡلُوَنَّكُم بِشَيۡءٖ مِّنَ ٱلۡخَوۡفِ وَٱلۡجُوعِ وَنَقۡصٖ مِّنَ ٱلۡأَمۡوَٰلِ وَٱلۡأَنفُسِ وَٱلثَّمَرَٰتِۗ وَبَشِّرِ ٱلصَّـٰبِرِينَ

Na kwa yakini kabisa, tutakutieni katika mtihani mdogo wa hofu na njaa na upungufu wa mali na uhai na matunda. Na wape bishara wenye uvumilivu



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 188

وَلَا تَأۡكُلُوٓاْ أَمۡوَٰلَكُم بَيۡنَكُم بِٱلۡبَٰطِلِ وَتُدۡلُواْ بِهَآ إِلَى ٱلۡحُكَّامِ لِتَأۡكُلُواْ فَرِيقٗا مِّنۡ أَمۡوَٰلِ ٱلنَّاسِ بِٱلۡإِثۡمِ وَأَنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Na msile mali zenu baina yenu kwa batili na kuzipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali ya watu kwa dhambi na ilhali mnajua



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 261

مَّثَلُ ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمۡوَٰلَهُمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ كَمَثَلِ حَبَّةٍ أَنۢبَتَتۡ سَبۡعَ سَنَابِلَ فِي كُلِّ سُنۢبُلَةٖ مِّاْئَةُ حَبَّةٖۗ وَٱللَّهُ يُضَٰعِفُ لِمَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٌ

Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Allah ni kama mfano wa punje iliyotoa mashuke saba, ikawa katika kila shuke mna punje mia. Na Allah humuongezea amtakaye, Na Allah ni Mwingi wa fadhila, Mjuzi mno



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 262

ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمۡوَٰلَهُمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ ثُمَّ لَا يُتۡبِعُونَ مَآ أَنفَقُواْ مَنّٗا وَلَآ أَذٗى لَّهُمۡ أَجۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡ وَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Wale wanaotoa mali zao katika njia ya Allah, kisha wasifuatishe yale waliyoyatoa kwa masimbulizi wala maudhi, wana malipo yao kwa Mola wao, wala hawatakuwa na hofu na hawatahuzunika



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 263

۞قَوۡلٞ مَّعۡرُوفٞ وَمَغۡفِرَةٌ خَيۡرٞ مِّن صَدَقَةٖ يَتۡبَعُهَآ أَذٗىۗ وَٱللَّهُ غَنِيٌّ حَلِيمٞ

Kauli njema na kusamehe ni bora kuliko sadaka inayofuatishwa na maudhi, na Allah ni Mkwasi sana, Mpole mno



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 264

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تُبۡطِلُواْ صَدَقَٰتِكُم بِٱلۡمَنِّ وَٱلۡأَذَىٰ كَٱلَّذِي يُنفِقُ مَالَهُۥ رِئَآءَ ٱلنَّاسِ وَلَا يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۖ فَمَثَلُهُۥ كَمَثَلِ صَفۡوَانٍ عَلَيۡهِ تُرَابٞ فَأَصَابَهُۥ وَابِلٞ فَتَرَكَهُۥ صَلۡدٗاۖ لَّا يَقۡدِرُونَ عَلَىٰ شَيۡءٖ مِّمَّا كَسَبُواْۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Enyi mlioamini, msizibatilishe sadaka zenu kwa masimbulizi na maudhi, kama yule anayetoa mali yake kwa kuwaonesha watu, na hamuamini Allah na Siku ya Mwisho. Basi mfano wake ni kama jiwe lenye kuteleza ambalo juu yake kuna mchanga, kisha likanyeshewa na mvua kubwa na ikaliacha tupu. Basi hawatakuwa na uwezo juu ya chochote katika walicho kichuma, na Allah hawaongozi watu makafiri



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 265

وَمَثَلُ ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمۡوَٰلَهُمُ ٱبۡتِغَآءَ مَرۡضَاتِ ٱللَّهِ وَتَثۡبِيتٗا مِّنۡ أَنفُسِهِمۡ كَمَثَلِ جَنَّةِۭ بِرَبۡوَةٍ أَصَابَهَا وَابِلٞ فَـَٔاتَتۡ أُكُلَهَا ضِعۡفَيۡنِ فَإِن لَّمۡ يُصِبۡهَا وَابِلٞ فَطَلّٞۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٌ

Na mfano wa wale wanaotoa mali zao kwa kuzitafuta radhi za Allah kwa uthabiti na yakini wa nafsi zao, ni kama mfano wa bustani iliyo katika muinuko, ipatayo mvua nyingi, na ikatoa matunda yake maradufu, na isiponyeshewa na mvua nyingi, mvua chache (hutosha) na Allah anayajua mnayoyatenda



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 266

أَيَوَدُّ أَحَدُكُمۡ أَن تَكُونَ لَهُۥ جَنَّةٞ مِّن نَّخِيلٖ وَأَعۡنَابٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ لَهُۥ فِيهَا مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِ وَأَصَابَهُ ٱلۡكِبَرُ وَلَهُۥ ذُرِّيَّةٞ ضُعَفَآءُ فَأَصَابَهَآ إِعۡصَارٞ فِيهِ نَارٞ فَٱحۡتَرَقَتۡۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمُ ٱلۡأٓيَٰتِ لَعَلَّكُمۡ تَتَفَكَّرُونَ

Je, anapenda mmoja wenu kuwa na bustani ya mitende na mizabibu, itiririkayo mito chini yake, naye humo hupata matunda ya kila namna, na ukamfikia uzee, na ana watoto dhaifu, mara kimbunga chenye moto kikaikumba bustani hiyo na ikaungua. Hivyo ndivyo Allah anavyo kubainishieni Aya zake ili mpate kufikiri



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 267

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَنفِقُواْ مِن طَيِّبَٰتِ مَا كَسَبۡتُمۡ وَمِمَّآ أَخۡرَجۡنَا لَكُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِۖ وَلَا تَيَمَّمُواْ ٱلۡخَبِيثَ مِنۡهُ تُنفِقُونَ وَلَسۡتُم بِـَٔاخِذِيهِ إِلَّآ أَن تُغۡمِضُواْ فِيهِۚ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ غَنِيٌّ حَمِيدٌ

Enyi mlioamini, toeni katika vitu vizuri mlivyovichuma, na katika vile tulivyowatoleeni kutoka katika ardhi. Na msikusudie (kutoa) kibaya na hali nyinyi hamkuwa ni wenye kukipokea (kama mtapewa) ila kwa kukifumbia macho, najueni kwamba, Allah ni Mkwasi, Mwenye kuhimidiwa mno



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 268

ٱلشَّيۡطَٰنُ يَعِدُكُمُ ٱلۡفَقۡرَ وَيَأۡمُرُكُم بِٱلۡفَحۡشَآءِۖ وَٱللَّهُ يَعِدُكُم مَّغۡفِرَةٗ مِّنۡهُ وَفَضۡلٗاۗ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٞ

Shetani anakutieni hofu ya ufukara na anakuamrisheni uovu, na Allah anakuahidini msamaha utokao kwake na ziada, na Allah ni Mwenye wasaa sana, Mwenye kujua mno



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 269

يُؤۡتِي ٱلۡحِكۡمَةَ مَن يَشَآءُۚ وَمَن يُؤۡتَ ٱلۡحِكۡمَةَ فَقَدۡ أُوتِيَ خَيۡرٗا كَثِيرٗاۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّآ أُوْلُواْ ٱلۡأَلۡبَٰبِ

Humpa hekima amtakaye. Na aliyepewa hekima bila shaka amepewa heri nyingi, na hawakumbuki ila wenye akili



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 270

وَمَآ أَنفَقۡتُم مِّن نَّفَقَةٍ أَوۡ نَذَرۡتُم مِّن نَّذۡرٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُهُۥۗ وَمَا لِلظَّـٰلِمِينَ مِنۡ أَنصَارٍ

Na chochote mkitoacho au nadhiri yoyote muiwekayo kwa hakika Allah anaijua, na madhalimu hawana yeyote wa kuwanusuru



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 271

إِن تُبۡدُواْ ٱلصَّدَقَٰتِ فَنِعِمَّا هِيَۖ وَإِن تُخۡفُوهَا وَتُؤۡتُوهَا ٱلۡفُقَرَآءَ فَهُوَ خَيۡرٞ لَّكُمۡۚ وَيُكَفِّرُ عَنكُم مِّن سَيِّـَٔاتِكُمۡۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ

Iwapo mtadhihirisha sadaka ni vizuri sana, na kama mtatoa kwa siri na kuwapa mafukara basi hilo ni bora zaidi kwenu na atakufutieni baadhi ya maovu yenu na Allah anayajua mno mnayoyatenda



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 274

ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمۡوَٰلَهُم بِٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِ سِرّٗا وَعَلَانِيَةٗ فَلَهُمۡ أَجۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡ وَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Wale watoao mali zao usiku na mchana, kwa siri na kwa dhahiri, basi wana malipo yao kwa Mola wao, na hawatakuwa na hofu yoyote na hawatahuzunika



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 275

ٱلَّذِينَ يَأۡكُلُونَ ٱلرِّبَوٰاْ لَا يَقُومُونَ إِلَّا كَمَا يَقُومُ ٱلَّذِي يَتَخَبَّطُهُ ٱلشَّيۡطَٰنُ مِنَ ٱلۡمَسِّۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ قَالُوٓاْ إِنَّمَا ٱلۡبَيۡعُ مِثۡلُ ٱلرِّبَوٰاْۗ وَأَحَلَّ ٱللَّهُ ٱلۡبَيۡعَ وَحَرَّمَ ٱلرِّبَوٰاْۚ فَمَن جَآءَهُۥ مَوۡعِظَةٞ مِّن رَّبِّهِۦ فَٱنتَهَىٰ فَلَهُۥ مَا سَلَفَ وَأَمۡرُهُۥٓ إِلَى ٱللَّهِۖ وَمَنۡ عَادَ فَأُوْلَـٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Wale wanaokula riba, hawatai-nuka isipokuwa kama anavyoinuka ambaye amepagawa kwa kukumbwa na Shetani. Hayo ni kwa sababu walisema kuwa biashara ni kama riba, na Allah ameihalalisha biashara na ameiharamisha riba. Basi ambaye amefikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake na akaacha, basi yake ni yale yaliyokwishapita, na jambo lake lipo kwa Allah. Na watakaorejea, basi hao ndio watu wa Motoni, wao watakaa humo milele



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 276

يَمۡحَقُ ٱللَّهُ ٱلرِّبَوٰاْ وَيُرۡبِي ٱلصَّدَقَٰتِۗ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ

Allah huiondolea baraka riba na huzibariki sadaka, na Allah hampendi kila kafiri mno mwingi wa dhambi



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 277

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَوُاْ ٱلزَّكَوٰةَ لَهُمۡ أَجۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡ وَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Hakika wale walioamini na kutenda vitendo vizuri na kusimamisha Swala na kutoa Zaka, wanamalipo mema mbele ya Mola wao, na hawana hofu yoyote, na hawahuzuniki



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 278

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَذَرُواْ مَا بَقِيَ مِنَ ٱلرِّبَوٰٓاْ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Enyi mlioamini, mcheni Allah, na acheni yaliyobakia katika riba ikiwa ninyi ni waumini



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 279

فَإِن لَّمۡ تَفۡعَلُواْ فَأۡذَنُواْ بِحَرۡبٖ مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦۖ وَإِن تُبۡتُمۡ فَلَكُمۡ رُءُوسُ أَمۡوَٰلِكُمۡ لَا تَظۡلِمُونَ وَلَا تُظۡلَمُونَ

Na msipofanya (hivyo) basi tangazeni vita na Allah na Mtume wake, na kama mkitubu, basi ni stahiki yenu rasilimali zenu, hamtadhulumu wala hamtadhulumiwa



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 280

وَإِن كَانَ ذُو عُسۡرَةٖ فَنَظِرَةٌ إِلَىٰ مَيۡسَرَةٖۚ وَأَن تَصَدَّقُواْ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Na kama (mdeni) ni mwenye hali ngumu, basi (mdai) angoje mpaka wakati wa uwezo. Na kulifanya sadaka (hilo deni) ni heri kwenu (kuliko kungoja mpaka mdaiwa kupata uwezo), ikiwa mnajua



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 10

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَن تُغۡنِيَ عَنۡهُمۡ أَمۡوَٰلُهُمۡ وَلَآ أَوۡلَٰدُهُم مِّنَ ٱللَّهِ شَيۡـٔٗاۖ وَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمۡ وَقُودُ ٱلنَّارِ

Hakika, waliokufuru, katu hazitawasaidia chochote mali zao wala watoto wao kwa Allah, na hao ndio kuniza Motoni



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 116

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَن تُغۡنِيَ عَنۡهُمۡ أَمۡوَٰلُهُمۡ وَلَآ أَوۡلَٰدُهُم مِّنَ ٱللَّهِ شَيۡـٔٗاۖ وَأُوْلَـٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Hakika, wale waliokufuru kamwe hazitawanufaisha chochote kwa Allah mali zao na watoto wao. Na hao ni watu wa Motoni, watakaa humo milele



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 117

مَثَلُ مَا يُنفِقُونَ فِي هَٰذِهِ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا كَمَثَلِ رِيحٖ فِيهَا صِرٌّ أَصَابَتۡ حَرۡثَ قَوۡمٖ ظَلَمُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ فَأَهۡلَكَتۡهُۚ وَمَا ظَلَمَهُمُ ٱللَّهُ وَلَٰكِنۡ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ

Mfano wawavitoavyo katika maisha haya ya duniani (na kutaraji kupata malipo mema Akhera) ni kama upepo wenye baridi kali uliolikumba shamba la watu waliodhulumu nafsi zao (kwa kumuasi Allah) ukaliangamiza shamba hilo (na wakakosa kufaidika na mazao waliyoyapanda kwa kuwa yameteketea). Na Allah hakuwadhulumu lakini wanajidhulumu wenyewe



Surah: ANNISAI 

Ayah : 2

وَءَاتُواْ ٱلۡيَتَٰمَىٰٓ أَمۡوَٰلَهُمۡۖ وَلَا تَتَبَدَّلُواْ ٱلۡخَبِيثَ بِٱلطَّيِّبِۖ وَلَا تَأۡكُلُوٓاْ أَمۡوَٰلَهُمۡ إِلَىٰٓ أَمۡوَٰلِكُمۡۚ إِنَّهُۥ كَانَ حُوبٗا كَبِيرٗا

Na wapeni Yatima mali zao, na msibadilishe kibaya kwa kizuri na msile mali zao (kwa kuzichanganya) katika mali zenu. Kwa hakika, hilo limekuwa dhambi kubwa kabisa



Surah: ANNISAI 

Ayah : 5

وَلَا تُؤۡتُواْ ٱلسُّفَهَآءَ أَمۡوَٰلَكُمُ ٱلَّتِي جَعَلَ ٱللَّهُ لَكُمۡ قِيَٰمٗا وَٱرۡزُقُوهُمۡ فِيهَا وَٱكۡسُوهُمۡ وَقُولُواْ لَهُمۡ قَوۡلٗا مَّعۡرُوفٗا

Na msiwape Masafihi (wapuuzi) mali zenu ambazo Allah amezifanya kwenu muhimili wa maisha yenu, na wapatieni mahitaji yao ndani ya mali hizo na wapatieni mavazi na zungumzeni nao lugha mzuri



Surah: ANNISAI 

Ayah : 6

وَٱبۡتَلُواْ ٱلۡيَتَٰمَىٰ حَتَّىٰٓ إِذَا بَلَغُواْ ٱلنِّكَاحَ فَإِنۡ ءَانَسۡتُم مِّنۡهُمۡ رُشۡدٗا فَٱدۡفَعُوٓاْ إِلَيۡهِمۡ أَمۡوَٰلَهُمۡۖ وَلَا تَأۡكُلُوهَآ إِسۡرَافٗا وَبِدَارًا أَن يَكۡبَرُواْۚ وَمَن كَانَ غَنِيّٗا فَلۡيَسۡتَعۡفِفۡۖ وَمَن كَانَ فَقِيرٗا فَلۡيَأۡكُلۡ بِٱلۡمَعۡرُوفِۚ فَإِذَا دَفَعۡتُمۡ إِلَيۡهِمۡ أَمۡوَٰلَهُمۡ فَأَشۡهِدُواْ عَلَيۡهِمۡۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ حَسِيبٗا

Na wapeni majaribio Yatima[1] mpaka wafikiapo (umri wa) kuoa, na kama mtajiridhisha kwao ukomavu (wa kufanya matumizi), basi wapeni mali zao na msizile mali hizo kwa fujo na kuwahi kabla wenyewe kuwa wakubwa. Na yeyote aliye na uwezo aache (kuzitumia) na yeyote aliye fakiri basi na ale kwa uzuri. Na pindi mtapowapa mali zao wawekeeni ushahidi, na inatosha Allah kuwa mwenye kuhesabu


1- - Iili kujua uwezo wao wa kuweza kujiendesha kimaisha endapo watakabidhiwa mali zao.


Surah: ANNISAI 

Ayah : 7

لِّلرِّجَالِ نَصِيبٞ مِّمَّا تَرَكَ ٱلۡوَٰلِدَانِ وَٱلۡأَقۡرَبُونَ وَلِلنِّسَآءِ نَصِيبٞ مِّمَّا تَرَكَ ٱلۡوَٰلِدَانِ وَٱلۡأَقۡرَبُونَ مِمَّا قَلَّ مِنۡهُ أَوۡ كَثُرَۚ نَصِيبٗا مَّفۡرُوضٗا

(Watoto) wanaume wana fungu kutokana na kile alichoacha (mmoja wa) wazazi wawili na ndugu wa karibu (pia wanafungu). Na wanawake wanafungu kutokana na alichoacha (mmoja wa) wazazi wawili na ndugu wa karibu (sawa) kiwe kingi au kichache ni fungu lililofaradhishwa



Surah: ANNISAI 

Ayah : 8

وَإِذَا حَضَرَ ٱلۡقِسۡمَةَ أُوْلُواْ ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينُ فَٱرۡزُقُوهُم مِّنۡهُ وَقُولُواْ لَهُمۡ قَوۡلٗا مَّعۡرُوفٗا

Na kama (katika kikao cha) kugawa watahudhuria ndugu na Yatima na masikini basi waruzukuni humo chochote, na waambieni kauli nzuri



Surah: ANNISAI 

Ayah : 9

وَلۡيَخۡشَ ٱلَّذِينَ لَوۡ تَرَكُواْ مِنۡ خَلۡفِهِمۡ ذُرِّيَّةٗ ضِعَٰفًا خَافُواْ عَلَيۡهِمۡ فَلۡيَتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلۡيَقُولُواْ قَوۡلٗا سَدِيدًا

Na waogope wale ambao lau kuwa na wao wangeacha nyuma yao kizazi (watoto) wanyonge wakiwahofia (kudhulumiwa na kunyanyaswa), basi wamuogope Allah na waseme neno la kweli



Surah: ANNISAI 

Ayah : 10

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَأۡكُلُونَ أَمۡوَٰلَ ٱلۡيَتَٰمَىٰ ظُلۡمًا إِنَّمَا يَأۡكُلُونَ فِي بُطُونِهِمۡ نَارٗاۖ وَسَيَصۡلَوۡنَ سَعِيرٗا

Hakika wale wanaokula mali za Yatima kwa dhulma kwa hakika wanakula moto (kutia) matumboni mwao na watauingia Motoni