قُتِلَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡأُخۡدُودِ
Wameangamizwa watu wa mahandaki
Share :
ٱلنَّارِ ذَاتِ ٱلۡوَقُودِ
Yenye moto wenye kuni nyingi,
إِذۡ هُمۡ عَلَيۡهَا قُعُودٞ
Walipo kuwa wamekaa hapo,
وَهُمۡ عَلَىٰ مَا يَفۡعَلُونَ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ شُهُودٞ
Na wao ni mashahidi wa yale waliyo kuwa wakiwafanyia Waumini
وَمَا نَقَمُواْ مِنۡهُمۡ إِلَّآ أَن يُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَمِيدِ
Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Allah, Mwenye nguvu, Msifiwa,
ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدٌ
Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Allah ni shaahidi wa kila kitu
إِنَّ ٱلَّذِينَ فَتَنُواْ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ ثُمَّ لَمۡ يَتُوبُواْ فَلَهُمۡ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمۡ عَذَابُ ٱلۡحَرِيقِ
Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua