لَّيۡسَ عَلَى ٱلضُّعَفَآءِ وَلَا عَلَى ٱلۡمَرۡضَىٰ وَلَا عَلَى ٱلَّذِينَ لَا يَجِدُونَ مَا يُنفِقُونَ حَرَجٌ إِذَا نَصَحُواْ لِلَّهِ وَرَسُولِهِۦۚ مَا عَلَى ٱلۡمُحۡسِنِينَ مِن سَبِيلٖۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Hakuna dhambi kwa wanyonge na wagonjwa na wasiokuwa na cha kutoa, iwapo wanamsafia nia Allah na Mtume wake. Hakuna njia ya kuwalaumu wanaofanya mazuri. Na Allah ni Mwenye kusamehe, mwenye Rehemu
وَلَا عَلَى ٱلَّذِينَ إِذَا مَآ أَتَوۡكَ لِتَحۡمِلَهُمۡ قُلۡتَ لَآ أَجِدُ مَآ أَحۡمِلُكُمۡ عَلَيۡهِ تَوَلَّواْ وَّأَعۡيُنُهُمۡ تَفِيضُ مِنَ ٱلدَّمۡعِ حَزَنًا أَلَّا يَجِدُواْ مَا يُنفِقُونَ
Na wala (hawana dhambi) wale (Answari) ambao walipokujia ili uwachukue (uwawezeshe na uwape vipando vya kwendea jihadi) ulisema: Sina kipando cha kukuchukueni (cha kukupeni) waliondoka na ilhali macho yao yanatiririka machozi kwa huzuni ya kukosa cha kutoa
۞إِنَّمَا ٱلسَّبِيلُ عَلَى ٱلَّذِينَ يَسۡتَـٔۡذِنُونَكَ وَهُمۡ أَغۡنِيَآءُۚ رَضُواْ بِأَن يَكُونُواْ مَعَ ٱلۡخَوَالِفِ وَطَبَعَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ
Kwa hakika kabisa, njia (ya kulaumu na kuwachukulia hatua) ipo kwa wale wanaokuomba ruhusa (ili wasiende vitani) na ilhali wao ni wakwasi. Wameridhia kuwa pamoja na wabakiao nyuma (kwa udhuru kama vile watoto, wagonjwa, wazee, wanawake, walemavu n.k.) na Allah amewapiga chapa kwenye nyoyo zao. Kwa hivyo hawajui (lililo na manufaa na wao)
يَعۡتَذِرُونَ إِلَيۡكُمۡ إِذَا رَجَعۡتُمۡ إِلَيۡهِمۡۚ قُل لَّا تَعۡتَذِرُواْ لَن نُّؤۡمِنَ لَكُمۡ قَدۡ نَبَّأَنَا ٱللَّهُ مِنۡ أَخۡبَارِكُمۡۚ وَسَيَرَى ٱللَّهُ عَمَلَكُمۡ وَرَسُولُهُۥ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَٰلِمِ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
(Wanafiki) Watakutoleeni udhuru mtakaporejea kwao. Sema (uwaambie): “Msitoe udhuru; hatutakuaminini tena. Allah ameshatueleza habari zenu. Na Allah na Mtume wake wataviona vitendo vyenu (kwamba mtatubu na kuacha unafiki au mtaendelea). Kisha mtarudishwa kwa (Allah) Mjuzi wa ya siri na ya dhahiri; naye atakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda”
سَيَحۡلِفُونَ بِٱللَّهِ لَكُمۡ إِذَا ٱنقَلَبۡتُمۡ إِلَيۡهِمۡ لِتُعۡرِضُواْ عَنۡهُمۡۖ فَأَعۡرِضُواْ عَنۡهُمۡۖ إِنَّهُمۡ رِجۡسٞۖ وَمَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُ جَزَآءَۢ بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ
Watakuapieni kwa Allah mtaka-porudi kwao ili msiwaulize. Basi wapuuzeni. Hakika hao ni Najisi (wa imani), na makazi yao ni Jahanamu ikiwa ni malipo kwa sababu ya waliyokuwa wanayachuma
يَحۡلِفُونَ لَكُمۡ لِتَرۡضَوۡاْ عَنۡهُمۡۖ فَإِن تَرۡضَوۡاْ عَنۡهُمۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يَرۡضَىٰ عَنِ ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡفَٰسِقِينَ
Wanakuapieni ili muwe radhi nao. Basi hata mkiwaridhia, kwa hakika Allah hawaridhii watu waovu
ٱلۡأَعۡرَابُ أَشَدُّ كُفۡرٗا وَنِفَاقٗا وَأَجۡدَرُ أَلَّا يَعۡلَمُواْ حُدُودَ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ عَلَىٰ رَسُولِهِۦۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ
Mabedui[1] ni washupavu mno katika ukafiri na unafiki (kuliko watu wa mijini) na ni kawaida sana (ya) kutoijua mipaka ya yale aliyoyateremsha Allah kwa Mtume wake[2]. Na Allah ni Mjuzi mno, Mwenye hekima sana
1- - Bedui ni mkazi wa mashambani; iwe jangwani au sehemu yoyote ya nje ya mji.
2- - Mabedui wamepewa sifa hizi kutokana na uchache wa maingiliano na kuchanganyika na watu wengine na pia kutokana na wao kuwa mbali na vyanzo vya elimu na maarifa. Aya pamoja na kuwa imetaja Mabedui kwa jumla yao lakini sio wote. Ni baadhi tu wenye sifa hizo. Katika lugha hii ni kawaida; kutaja jumla lakini ikakusudiwa baadhi, kama ilivyotajwa katika Aya ya 67 ya Sura Al-israi (17) kwamba “…na mwanadamu amekuwa kafiri sana (wa kumkataa Allah na kukanusha neema zake)”. Sio kwamba kila mwanadamu ana sifa hii. Ni baadhi tu. Na katika suala la Mabedui ni hivyo hivyo. Sio wote wana sifa za ukafiri na unafiki mkali. Ni baadhi tu. Ni kwa sababu hii, Allah katika Aya ya 99 ya Sura hii ya Attauba (9) ametaja kuwa wapo Mabedui wenye maadili mazuri na Imani sahihi.
وَمِنَ ٱلۡأَعۡرَابِ مَن يَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ مَغۡرَمٗا وَيَتَرَبَّصُ بِكُمُ ٱلدَّوَآئِرَۚ عَلَيۡهِمۡ دَآئِرَةُ ٱلسَّوۡءِۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٞ
Na miongoni mwa Mabedui wapo wanaochukulia (wanadhani) vile wanavyovitoa (katika njia ya Allah) ni kazi bure (hasara), na wanakuvizieni mpate majanga. Majanga mabaya yawashukie wao. Na Allah ni Mwenye kusikia sana, Mwenye kujua mno
وَمِنَ ٱلۡأَعۡرَابِ مَن يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَيَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ قُرُبَٰتٍ عِندَ ٱللَّهِ وَصَلَوَٰتِ ٱلرَّسُولِۚ أَلَآ إِنَّهَا قُرۡبَةٞ لَّهُمۡۚ سَيُدۡخِلُهُمُ ٱللَّهُ فِي رَحۡمَتِهِۦٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Na katika Mabedui wapo wanaomuamini Allah na Siku ya Mwisho na wanachukulia (wanaamini) kuwa wanavyovitoa (katika njia ya Allah) ni ibada zinazowasogeza kwa Allah na maombi ya Mtume. Zindukeni na mjue kwamba, hizo ni (ibada) zinazowasogeza (kwa Allah) kwa faida yao. Allah atawaingiza katika rehema zake. Hakika, Allah ni Mwenye kusamehe, mwenye kurehemu
لَّقَد تَّابَ ٱللَّهُ عَلَى ٱلنَّبِيِّ وَٱلۡمُهَٰجِرِينَ وَٱلۡأَنصَارِ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوهُ فِي سَاعَةِ ٱلۡعُسۡرَةِ مِنۢ بَعۡدِ مَا كَادَ يَزِيغُ قُلُوبُ فَرِيقٖ مِّنۡهُمۡ ثُمَّ تَابَ عَلَيۡهِمۡۚ إِنَّهُۥ بِهِمۡ رَءُوفٞ رَّحِيمٞ
Kwa hakika kabisa, Allah alishamsamehe Nabii (baada ya kuwaruhusu waliotoa udhuru wa uongo wa kutokwenda kupigana Jihadi) na (aliwasamehe pia) Muhajirina na Answari waliomfuata Mtume katika kipindi kigumu, baada ya nyoyo za baadhi yao kukaribia kugeuka (kwa kutamani kuacha kwenda vitani katika kipindi cha joto kali na mazingira magumu), kisha (Allah) akapokea Toba zao. Hakika, Yeye kwao ni Mpole mno, Mwenye kurehemu
وَعَلَى ٱلثَّلَٰثَةِ ٱلَّذِينَ خُلِّفُواْ حَتَّىٰٓ إِذَا ضَاقَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلۡأَرۡضُ بِمَا رَحُبَتۡ وَضَاقَتۡ عَلَيۡهِمۡ أَنفُسُهُمۡ وَظَنُّوٓاْ أَن لَّا مَلۡجَأَ مِنَ ٱللَّهِ إِلَّآ إِلَيۡهِ ثُمَّ تَابَ عَلَيۡهِمۡ لِيَتُوبُوٓاْۚ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ
Na (pia Allah amekubali Toba ya wale watu) watatu walioachwa nyuma (waliokataa kwenda Jihadi kwa uvivu[1] ambao Mtume hakuikubali toba yao kwa wepesi na aliwawekea vikwazo) mpaka dunia walipoiona finyu kwao pamoja na upana wake, na nafsi zao zikadhikika na wakawa na yakini kuwa hakuna pa kumkimbia Allah isipokuwa kwake Yeye tu. Kisha Allah aliwasamehe (baada ya kubainika ni waumini kweli aliwawezesha kujirudi) ili watubu. Hakika, Allah tu ndiye Mwenye kupokea sana Toba, Mwenye kurehemu
1- - Hawa ni Kaabi bin Malik, Hilal bin Umaya na Murara bin Rabii.
مَا كَانَ لِأَهۡلِ ٱلۡمَدِينَةِ وَمَنۡ حَوۡلَهُم مِّنَ ٱلۡأَعۡرَابِ أَن يَتَخَلَّفُواْ عَن رَّسُولِ ٱللَّهِ وَلَا يَرۡغَبُواْ بِأَنفُسِهِمۡ عَن نَّفۡسِهِۦۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ لَا يُصِيبُهُمۡ ظَمَأٞ وَلَا نَصَبٞ وَلَا مَخۡمَصَةٞ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلَا يَطَـُٔونَ مَوۡطِئٗا يَغِيظُ ٱلۡكُفَّارَ وَلَا يَنَالُونَ مِنۡ عَدُوّٖ نَّيۡلًا إِلَّا كُتِبَ لَهُم بِهِۦ عَمَلٞ صَٰلِحٌۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Haikupasa kwa watu wa Madina na (Mabedui) walioko pembezoni mwao kubakia nyuma wasitoke na Mtume wa Allah, wala kujipendelea nafsi zao kuliko yeye. Hayo ni kwa sababu hawapati kiu, wala uchovu wala njaa katika Njia ya Allah, wala hawakanyagi mahali panapo wachukiza makafiri, wala hawapati chochote cha kupata kwa maadui (ngawira, kuuawa au kutekwa), ila kwa hayo huandikwa kuwa ni kitendo chema kwao. Hakika, Allah haupotezi ujira wa wanaofanya mazuri
وَلَا يُنفِقُونَ نَفَقَةٗ صَغِيرَةٗ وَلَا كَبِيرَةٗ وَلَا يَقۡطَعُونَ وَادِيًا إِلَّا كُتِبَ لَهُمۡ لِيَجۡزِيَهُمُ ٱللَّهُ أَحۡسَنَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Na hawatoi cha kutoa; kidogo wala kikubwa, wala hawavuki bonde (wawapo njiani), ila huandikiwa (mema) ili Allah awalipe mazuri zaidi ya waliyokuwa wakiyatenda
۞وَمَا كَانَ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ لِيَنفِرُواْ كَآفَّةٗۚ فَلَوۡلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرۡقَةٖ مِّنۡهُمۡ طَآئِفَةٞ لِّيَتَفَقَّهُواْ فِي ٱلدِّينِ وَلِيُنذِرُواْ قَوۡمَهُمۡ إِذَا رَجَعُوٓاْ إِلَيۡهِمۡ لَعَلَّهُمۡ يَحۡذَرُونَ
Na hawakutakiwa Waumini watoke wote (kwenda vitani). Basi kwa nini hawatoki baadhi katika kila kundi miongoni mwao, wakajifunze vyema Dini, na kisha waje kuwaonya wenzao watakaporejea kwao, ili nao wapate kujihadhari?