Surah: AZZUKHRUF 

Ayah : 71

يُطَافُ عَلَيۡهِم بِصِحَافٖ مِّن ذَهَبٖ وَأَكۡوَابٖۖ وَفِيهَا مَا تَشۡتَهِيهِ ٱلۡأَنفُسُ وَتَلَذُّ ٱلۡأَعۡيُنُۖ وَأَنتُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Watakuwa wanapitishiwa sahani za dhahabu na vikombe; na vitakuwamo ambavyo nafsi zinavipenda na macho yanavifurahia, na nyinyi mtakaa humo milele



Surah: AL-JAATHIYA 

Ayah : 22

وَخَلَقَ ٱللَّهُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّ وَلِتُجۡزَىٰ كُلُّ نَفۡسِۭ بِمَا كَسَبَتۡ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ

Na Allah ameziumba mbingu na ardhi kwa haki, na ili kila nafsi ilipwe yale iliyo yachuma. Nao hawatadhulumiwa



Surah: QAAF 

Ayah : 21

وَجَآءَتۡ كُلُّ نَفۡسٖ مَّعَهَا سَآئِقٞ وَشَهِيدٞ

Na kila nafsi itakuja pamoja nayo mcungaji na shahidi



Surah: QAAF 

Ayah : 22

لَّقَدۡ كُنتَ فِي غَفۡلَةٖ مِّنۡ هَٰذَا فَكَشَفۡنَا عَنكَ غِطَآءَكَ فَبَصَرُكَ ٱلۡيَوۡمَ حَدِيدٞ

(Aambiwe): Kwa yakini ulikuwa umeghafilika na haya! Basi Tumekuondoshea kifuniko chako (pazia lako), basi kuona kwako leo ni kukali



Surah: ATTUR 

Ayah : 21

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَٱتَّبَعَتۡهُمۡ ذُرِّيَّتُهُم بِإِيمَٰنٍ أَلۡحَقۡنَا بِهِمۡ ذُرِّيَّتَهُمۡ وَمَآ أَلَتۡنَٰهُم مِّنۡ عَمَلِهِم مِّن شَيۡءٖۚ كُلُّ ٱمۡرِيِٕۭ بِمَا كَسَبَ رَهِينٞ

Na wale walioamini na wakafuatwa na dhuriya wao kwa Imani Tutawakutanisha nao dhuriya wao na Hatutawapunguzia katika ‘amali zao kitu chochote. Kila mtu lazima atapata alicho kichuma



Surah: ALMUDDATH-THIR 

Ayah : 38

كُلُّ نَفۡسِۭ بِمَا كَسَبَتۡ رَهِينَةٌ

Kila nafsi iko katika rehani kwa yale iliyoyachuma.[1]


1- - Kila nafsi itashikwa kwa iliyo yatenda.


Surah: ATTAK-WIIR 

Ayah : 14

عَلِمَتۡ نَفۡسٞ مَّآ أَحۡضَرَتۡ

Kila nafsi itajua ilicho kihudhurisha



Surah: AL-INFITWAAR 

Ayah : 5

عَلِمَتۡ نَفۡسٞ مَّا قَدَّمَتۡ وَأَخَّرَتۡ

Hapo kila nafsi itajua ilichotanguliza, na ilicho bakisha nyuma



Surah: AL-FAJRI 

Ayah : 27

يَـٰٓأَيَّتُهَا ٱلنَّفۡسُ ٱلۡمُطۡمَئِنَّةُ

Ewe nafsi iliyo tua!