وَتَرَكۡنَا فِيهَآ ءَايَةٗ لِّلَّذِينَ يَخَافُونَ ٱلۡعَذَابَ ٱلۡأَلِيمَ
Na Tukaacha Humo Ishara Kwa Wale Ambao wanaoiogopa Adhabu Iumizayo
Share :
وَفِي مُوسَىٰٓ إِذۡ أَرۡسَلۡنَٰهُ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ بِسُلۡطَٰنٖ مُّبِينٖ
Na katika khabari za mussa pale tulipompeleka kwa Firauni kwa hoja za wazi
وَفِي عَادٍ إِذۡ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمُ ٱلرِّيحَ ٱلۡعَقِيمَ
Na katika khabari za Adi pale tulipowapelekea upepo wa kukata uzazi
وَفِي ثَمُودَ إِذۡ قِيلَ لَهُمۡ تَمَتَّعُواْ حَتَّىٰ حِينٖ
Na katika khabari za Thamud pale walipoambiwa stareheni hadi muda ufike
وَحَمَلۡنَٰهُ عَلَىٰ ذَاتِ أَلۡوَٰحٖ وَدُسُرٖ
Na Tukambeba kwenye ile (jahazi) yenye mbao na misumari
تَجۡرِي بِأَعۡيُنِنَا جَزَآءٗ لِّمَن كَانَ كُفِرَ
Kikienda haraka tukikitazama kwa macho yetu ikiwa ni malipo kwa ambaye alikuwa amekufuru
وَلَقَد تَّرَكۡنَٰهَآ ءَايَةٗ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ
Na kwa yakini Tumeiacha iwe ni mazingatio, Je, basi yuko yeyote mwenye kuwaidhika?