Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 65

وَلَقَدۡ عَلِمۡتُمُ ٱلَّذِينَ ٱعۡتَدَوۡاْ مِنكُمۡ فِي ٱلسَّبۡتِ فَقُلۡنَا لَهُمۡ كُونُواْ قِرَدَةً خَٰسِـِٔينَ

Na, kwa hakika kabisa, mmewajua waliovuka mipaka miongoni mwenu katika (siku ya) Jumamosi, tukawaambia: Kuweni nyani dhalili



Surah: ANNISAI 

Ayah : 154

وَرَفَعۡنَا فَوۡقَهُمُ ٱلطُّورَ بِمِيثَٰقِهِمۡ وَقُلۡنَا لَهُمُ ٱدۡخُلُواْ ٱلۡبَابَ سُجَّدٗا وَقُلۡنَا لَهُمۡ لَا تَعۡدُواْ فِي ٱلسَّبۡتِ وَأَخَذۡنَا مِنۡهُم مِّيثَٰقًا غَلِيظٗا

Na tulinyanyua (mlima) Turi juu yao kwa makubaliano nao na kuwaambia: Ingieni lango (la mji wenu) mkiwa mmeinama. Na tuliwaambia: Msivunje mwiko (wa kuiheshimu) siku ya Jumamosi (Sabato). Na tulichukua kwao ahadi nzito



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 163

وَسۡـَٔلۡهُمۡ عَنِ ٱلۡقَرۡيَةِ ٱلَّتِي كَانَتۡ حَاضِرَةَ ٱلۡبَحۡرِ إِذۡ يَعۡدُونَ فِي ٱلسَّبۡتِ إِذۡ تَأۡتِيهِمۡ حِيتَانُهُمۡ يَوۡمَ سَبۡتِهِمۡ شُرَّعٗا وَيَوۡمَ لَا يَسۡبِتُونَ لَا تَأۡتِيهِمۡۚ كَذَٰلِكَ نَبۡلُوهُم بِمَا كَانُواْ يَفۡسُقُونَ

Na waulize kuhusu mji uliokuwepo kando ya bahari walipokiuka (heshima ya siku ya) Jumamosi wakati samaki wao walipokuwa wanawajia nje nje siku yao ya mapumziko, na siku wasiyopumzika (samaki) hawawajii. Kama hivyo tunawajaribu (tunawapa mtihani) kwa vile walivyokuwa wakifanya uasi



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 164

وَإِذۡ قَالَتۡ أُمَّةٞ مِّنۡهُمۡ لِمَ تَعِظُونَ قَوۡمًا ٱللَّهُ مُهۡلِكُهُمۡ أَوۡ مُعَذِّبُهُمۡ عَذَابٗا شَدِيدٗاۖ قَالُواْ مَعۡذِرَةً إِلَىٰ رَبِّكُمۡ وَلَعَلَّهُمۡ يَتَّقُونَ

Na (kumbuka) wakati kundi miongoni mwao liliposema (kwamba): Kwa nini mnawapa mawaidha watu ambao Allah ni Mwenye kuwaangamiza au kuwaadhibu adhabu kali? Walisema: (Tunawapa mawaidha) Ili uwe udhuru kwa Mola wenu na huwenda nao wakawa wachaMungu



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 165

فَلَمَّا نَسُواْ مَا ذُكِّرُواْ بِهِۦٓ أَنجَيۡنَا ٱلَّذِينَ يَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلسُّوٓءِ وَأَخَذۡنَا ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ بِعَذَابِۭ بَـِٔيسِۭ بِمَا كَانُواْ يَفۡسُقُونَ

Basi walipoyasahau yale waliyokumbushwa tuliwaokoa waliokuwa wanakataza maovu na tuliwachukulia hatua ambao wamedhulumu (nafsi zao kwa kuasi) kwa (kuwapa) adhabu mbaya kwa walivyokuwa wanafanya uasi



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 166

فَلَمَّا عَتَوۡاْ عَن مَّا نُهُواْ عَنۡهُ قُلۡنَا لَهُمۡ كُونُواْ قِرَدَةً خَٰسِـِٔينَ

Basi walipoyapuuza yale waliyokatazwa tuliwaambia: Kuweni manyani dhalili



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 124

إِنَّمَا جُعِلَ ٱلسَّبۡتُ عَلَى ٱلَّذِينَ ٱخۡتَلَفُواْ فِيهِۚ وَإِنَّ رَبَّكَ لَيَحۡكُمُ بَيۡنَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فِيمَا كَانُواْ فِيهِ يَخۡتَلِفُونَ

Hakika siku ya Sabato (jumamosi) iliwekwa kwa wale waliohitilafiana kuhusu yeye (Ibrahimu) na dini yake. Na kwa hakika Mola wako atahukumu baina yao Siku ya Kiyama kuhusu yale waliyokuwa wakihitilafiana