Surah: AL-FAATIHA 

Ayah : 4

مَٰلِكِ يَوۡمِ ٱلدِّينِ

Mmiliki wa Siku ya Malipo



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 112

بَلَىٰۚ مَنۡ أَسۡلَمَ وَجۡهَهُۥ لِلَّهِ وَهُوَ مُحۡسِنٞ فَلَهُۥٓ أَجۡرُهُۥ عِندَ رَبِّهِۦ وَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Naam, wenye kujisalimisha kwa Allah na ilhali wanatenda yaliyo mazuri, basi watapata malipo yao kwa Mola wao, na hawatakuwa na hofu na hawatahuzunika



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 261

مَّثَلُ ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمۡوَٰلَهُمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ كَمَثَلِ حَبَّةٍ أَنۢبَتَتۡ سَبۡعَ سَنَابِلَ فِي كُلِّ سُنۢبُلَةٖ مِّاْئَةُ حَبَّةٖۗ وَٱللَّهُ يُضَٰعِفُ لِمَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٌ

Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Allah ni kama mfano wa punje iliyotoa mashuke saba, ikawa katika kila shuke mna punje mia. Na Allah humuongezea amtakaye, Na Allah ni Mwingi wa fadhila, Mjuzi mno



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 262

ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمۡوَٰلَهُمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ ثُمَّ لَا يُتۡبِعُونَ مَآ أَنفَقُواْ مَنّٗا وَلَآ أَذٗى لَّهُمۡ أَجۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡ وَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Wale wanaotoa mali zao katika njia ya Allah, kisha wasifuatishe yale waliyoyatoa kwa masimbulizi wala maudhi, wana malipo yao kwa Mola wao, wala hawatakuwa na hofu na hawatahuzunika



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 274

ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمۡوَٰلَهُم بِٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِ سِرّٗا وَعَلَانِيَةٗ فَلَهُمۡ أَجۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡ وَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Wale watoao mali zao usiku na mchana, kwa siri na kwa dhahiri, basi wana malipo yao kwa Mola wao, na hawatakuwa na hofu yoyote na hawatahuzunika



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 277

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَوُاْ ٱلزَّكَوٰةَ لَهُمۡ أَجۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡ وَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Hakika wale walioamini na kutenda vitendo vizuri na kusimamisha Swala na kutoa Zaka, wanamalipo mema mbele ya Mola wao, na hawana hofu yoyote, na hawahuzuniki



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 57

وَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ فَيُوَفِّيهِمۡ أُجُورَهُمۡۗ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Na ama walioamini na wakatenda mema, basi (Allah) atawalipa malipo yao kamili, na Allah hawapendi madhalimu



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 136

أُوْلَـٰٓئِكَ جَزَآؤُهُم مَّغۡفِرَةٞ مِّن رَّبِّهِمۡ وَجَنَّـٰتٞ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ وَنِعۡمَ أَجۡرُ ٱلۡعَٰمِلِينَ

Hao malipo yao ni msamaha wa Mola wao Mlezi na bustani zipitazo mito chini yake, watadumu humo milele, naujira bora kwawanaotenda (mema) ni huo



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 145

وَمَا كَانَ لِنَفۡسٍ أَن تَمُوتَ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِ كِتَٰبٗا مُّؤَجَّلٗاۗ وَمَن يُرِدۡ ثَوَابَ ٱلدُّنۡيَا نُؤۡتِهِۦ مِنۡهَا وَمَن يُرِدۡ ثَوَابَ ٱلۡأٓخِرَةِ نُؤۡتِهِۦ مِنۡهَاۚ وَسَنَجۡزِي ٱلشَّـٰكِرِينَ

Na nafsi yoyote haifi isipokuwa kwa idhini ya Allah tu ikiwa ni jambo lililoandikwa (na lenye) muda maalum. Na yeyote anayetaka malipo ya duniani tunampa humo, na mwenye kutaka malipo ya Akhera tutampa huko. Na tutawalipa wenye kushukuru



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 148

فَـَٔاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ ثَوَابَ ٱلدُّنۡيَا وَحُسۡنَ ثَوَابِ ٱلۡأٓخِرَةِۗ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Basi (Allah) akawapa malipo ya duniani na thawabu nzuri za Akhera, na Allah anawapenda wafanyao mazuri



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 171

۞يَسۡتَبۡشِرُونَ بِنِعۡمَةٖ مِّنَ ٱللَّهِ وَفَضۡلٖ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Wanawapa bishara ya neema zitokanazo kwa Mola wao na fadhila na hakika Allah hapotezi malipo ya waumini



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 172

ٱلَّذِينَ ٱسۡتَجَابُواْ لِلَّهِ وَٱلرَّسُولِ مِنۢ بَعۡدِ مَآ أَصَابَهُمُ ٱلۡقَرۡحُۚ لِلَّذِينَ أَحۡسَنُواْ مِنۡهُمۡ وَٱتَّقَوۡاْ أَجۡرٌ عَظِيمٌ

Ambao walimuitikia Allah na Mtume baada ya kupatwa na majeraha, kwa wale ambao waliofanya wema miongoni mwao na wakamcha Allah watakuwa na ujira mkubwa



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 195

فَٱسۡتَجَابَ لَهُمۡ رَبُّهُمۡ أَنِّي لَآ أُضِيعُ عَمَلَ عَٰمِلٖ مِّنكُم مِّن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰۖ بَعۡضُكُم مِّنۢ بَعۡضٖۖ فَٱلَّذِينَ هَاجَرُواْ وَأُخۡرِجُواْ مِن دِيَٰرِهِمۡ وَأُوذُواْ فِي سَبِيلِي وَقَٰتَلُواْ وَقُتِلُواْ لَأُكَفِّرَنَّ عَنۡهُمۡ سَيِّـَٔاتِهِمۡ وَلَأُدۡخِلَنَّهُمۡ جَنَّـٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ ثَوَابٗا مِّنۡ عِندِ ٱللَّهِۚ وَٱللَّهُ عِندَهُۥ حُسۡنُ ٱلثَّوَابِ

Mola wao akawajibu: Mimi sipotezi tendo la mtendaji yeyote miongoni mwenu awe mwanaume au mwanamke nyinyi kwa nyinyi, basi wale waliohama na wakatolewa majumbani mwao na wakaudhiwa na kukerwa katika njia yangu, na wakapigana na wakauliwa naapa nitawafutia makosa yao na naapa nitawaingiza katika Pepo inayotiririka chini yake mito ikiwa malipo kutoka kwa Allah, na kwa Allah ndiko kuliko na malipo mazuri



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 199

وَإِنَّ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ لَمَن يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكُمۡ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيۡهِمۡ خَٰشِعِينَ لِلَّهِ لَا يَشۡتَرُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ ثَمَنٗا قَلِيلًاۚ أُوْلَـٰٓئِكَ لَهُمۡ أَجۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ

Na kwa hakika katika Watu wa kitabu wapo wanaomuamini Allah hasa na kilichoteremshwa kwenu na kilichoteremshwa kwao, huku wakinyenyekea kwa Allah. Hawauzi Aya za Allah kwa thamani ndogo (ya dunia). Hao malipo yao yako kwa Mola wao mlezi, hakika Allah ni mwepesi mno wa kuhesabu



Surah: ANNISAI 

Ayah : 40

إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَظۡلِمُ مِثۡقَالَ ذَرَّةٖۖ وَإِن تَكُ حَسَنَةٗ يُضَٰعِفۡهَا وَيُؤۡتِ مِن لَّدُنۡهُ أَجۡرًا عَظِيمٗا

Hakika, Allah Hadhulumu uzito wa punje. Na kama (uzito huo wa punje) ni jambo zuri analizidisha na anatoa ujira mkubwa kabisa kutoka kwake



Surah: ANNISAI 

Ayah : 74

۞فَلۡيُقَٰتِلۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ ٱلَّذِينَ يَشۡرُونَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا بِٱلۡأٓخِرَةِۚ وَمَن يُقَٰتِلۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ فَيُقۡتَلۡ أَوۡ يَغۡلِبۡ فَسَوۡفَ نُؤۡتِيهِ أَجۡرًا عَظِيمٗا

Basi wapigane katika njia ya Allah wale ambao wanauza uhai (wao) wa duniani kwa Akhera. Na yeyote anayepigana katika njia ya Allah kisha akauliwa au akashinda, basi ni punde tu tutampa malipo makubwa



Surah: ANNISAI 

Ayah : 100

۞وَمَن يُهَاجِرۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ يَجِدۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُرَٰغَمٗا كَثِيرٗا وَسَعَةٗۚ وَمَن يَخۡرُجۡ مِنۢ بَيۡتِهِۦ مُهَاجِرًا إِلَى ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ ثُمَّ يُدۡرِكۡهُ ٱلۡمَوۡتُ فَقَدۡ وَقَعَ أَجۡرُهُۥ عَلَى ٱللَّهِۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمٗا

Na yeyote anayehama katika njia ya Allah atapata faida nyingi ardhini na ukunjufu. Na yeyote anayetoka nyumbani kwake akahama kwa ajili ya Allah na Mtume wake, kisha kifo kikamfika, hakika ujira wake umeshathibiti kwa Allah. Na Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu



Surah: ANNISAI 

Ayah : 134

مَّن كَانَ يُرِيدُ ثَوَابَ ٱلدُّنۡيَا فَعِندَ ٱللَّهِ ثَوَابُ ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ سَمِيعَۢا بَصِيرٗا

Anayetaka malipo ya dunia, basi kwa Allah yapo malipo ya dunia na Akhera. Na Allah ni Mwenye kusikia sana, Mwenye kuona



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 170

وَٱلَّذِينَ يُمَسِّكُونَ بِٱلۡكِتَٰبِ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُصۡلِحِينَ

Na ambao wanakishika vilivyo kitabu (bila ya kukipuuza au kukifanyia mzaha) na wakadumisha Swala, hakika sisi hatupotezi ujira wa watengenezao (mambo ya kumridhisha Allah)



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 21

يُبَشِّرُهُمۡ رَبُّهُم بِرَحۡمَةٖ مِّنۡهُ وَرِضۡوَٰنٖ وَجَنَّـٰتٖ لَّهُمۡ فِيهَا نَعِيمٞ مُّقِيمٌ

Mola wao Mlezi anawabashiria rehema zitokazo kwake na radhi na Pepo (mbalimbali) ambazo humo watapata neema za kudumu



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 22

خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عِندَهُۥٓ أَجۡرٌ عَظِيمٞ

Watadumu humo milele. Hakika kwa Allah yapo malipo (ya aina mbalimbali tena) makubwa mno



Surah: HUUD 

Ayah : 115

وَٱصۡبِرۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Na subiri (kuwa mvumilivu), kwani Allah hapotezi ujira wa wafanyao wema



Surah: YUSUF 

Ayah : 56

وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِي ٱلۡأَرۡضِ يَتَبَوَّأُ مِنۡهَا حَيۡثُ يَشَآءُۚ نُصِيبُ بِرَحۡمَتِنَا مَن نَّشَآءُۖ وَلَا نُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Na kama hivyo tulimmakinisha Yusuf (na kumpa cheo katika nchi); akawa anakaa humo popote anapopenda. Tunamfikishia rehema zetu tumtakaye, na hatupotezi malipo ya wafanyao mazuri



Surah: YUSUF 

Ayah : 57

وَلَأَجۡرُ ٱلۡأٓخِرَةِ خَيۡرٞ لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَكَانُواْ يَتَّقُونَ

Na kwa hakika kabisa, malipo ya Akhera ni bora zaidi kwa walioamini na wakawa wanamcha Allah



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 41

وَٱلَّذِينَ هَاجَرُواْ فِي ٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ مَا ظُلِمُواْ لَنُبَوِّئَنَّهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗۖ وَلَأَجۡرُ ٱلۡأٓخِرَةِ أَكۡبَرُۚ لَوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ

Na wale waliohama kwa ajili ya Allah baada ya kudhulumiwa, bila shaka tutawakalisha katika dunia kwa wema na ujira wa Akhera ni mkubwa zaidi; laiti wangekuwa wanajua!



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 96

مَا عِندَكُمۡ يَنفَدُ وَمَا عِندَ ٱللَّهِ بَاقٖۗ وَلَنَجۡزِيَنَّ ٱلَّذِينَ صَبَرُوٓاْ أَجۡرَهُم بِأَحۡسَنِ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Mlivyo navyo vitakwisha na vilivyoko kwa Allah ndivyo vibakiavyo; na kwa yakini sisi tutawapa waliosubiri ujira wao sawa na matendo mazuri waliyokuwa wakiyatenda



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 97

مَنۡ عَمِلَ صَٰلِحٗا مِّن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَلَنُحۡيِيَنَّهُۥ حَيَوٰةٗ طَيِّبَةٗۖ وَلَنَجۡزِيَنَّهُمۡ أَجۡرَهُم بِأَحۡسَنِ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Atakayefanya mema, mwana-mume au mwanamke, ilhali ni muumini, basi kwa hakika tutampa maisha mema na kwa yakini tutawapa ujira wao kwa uzuri zaidi kuliko yale waliokuwa wakiyatenda



Surah: AL-KAHF 

Ayah : 30

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجۡرَ مَنۡ أَحۡسَنَ عَمَلًا

Hakika wale walio amini na wakatenda mema - hakika Sisi hatupotezi ujira wa anaye tenda mema



Surah: TWAHA 

Ayah : 75

وَمَن يَأۡتِهِۦ مُؤۡمِنٗا قَدۡ عَمِلَ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ فَأُوْلَـٰٓئِكَ لَهُمُ ٱلدَّرَجَٰتُ ٱلۡعُلَىٰ

Na atakayemjia naye ni Muumini aliye tenda mema, basi hao ndio wenye vyeo vya juu



Surah: TWAHA 

Ayah : 76

جَنَّـٰتُ عَدۡنٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ وَذَٰلِكَ جَزَآءُ مَن تَزَكَّىٰ

Bustani za milele zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Na hayo ni malipo ya mwenye kujitakasa