Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 38

وَمَا مِن دَآبَّةٖ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا طَـٰٓئِرٖ يَطِيرُ بِجَنَاحَيۡهِ إِلَّآ أُمَمٌ أَمۡثَالُكُمۚ مَّا فَرَّطۡنَا فِي ٱلۡكِتَٰبِ مِن شَيۡءٖۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِمۡ يُحۡشَرُونَ

Na hakuna kiumbe yeyote anayetembea ardhini wala ndege anayeruka kwa mbawa zake, isipokuwa tu ni mataifa mfano wenu. Hatukuzembea (hatukuacha) kitu chochote katika (hiki) Kitabu (cha Qur’ani). Kisha watakusanywa kwa Mola wao tu (Siku ya Kiyama)



Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 59

۞وَعِندَهُۥ مَفَاتِحُ ٱلۡغَيۡبِ لَا يَعۡلَمُهَآ إِلَّا هُوَۚ وَيَعۡلَمُ مَا فِي ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِۚ وَمَا تَسۡقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعۡلَمُهَا وَلَا حَبَّةٖ فِي ظُلُمَٰتِ ٱلۡأَرۡضِ وَلَا رَطۡبٖ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِي كِتَٰبٖ مُّبِينٖ

Na ziko kwake yeye (Allah) tu funguo (hazina) za Ghaibu; hakuna azijuaye isipokuwa yeye tu. Na anajua kilichopo nchi kavu na baharini. Na halidondoki jani lolote ila analijua. Na (haidondoka) punje yoyote katika giza la ardhini na kibichi na kikavu isipokuwa kipo katika kitabu kinachobainisha (kila kitu)



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 36

إِنَّ عِدَّةَ ٱلشُّهُورِ عِندَ ٱللَّهِ ٱثۡنَا عَشَرَ شَهۡرٗا فِي كِتَٰبِ ٱللَّهِ يَوۡمَ خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ مِنۡهَآ أَرۡبَعَةٌ حُرُمٞۚ ذَٰلِكَ ٱلدِّينُ ٱلۡقَيِّمُۚ فَلَا تَظۡلِمُواْ فِيهِنَّ أَنفُسَكُمۡۚ وَقَٰتِلُواْ ٱلۡمُشۡرِكِينَ كَآفَّةٗ كَمَا يُقَٰتِلُونَكُمۡ كَآفَّةٗۚ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلۡمُتَّقِينَ

Hakika, idadi ya miezi kwa Allah ni miezi kumi na miwili katika kitabu cha Allah[1] tangu alipoumba mbingu na ardhi. Katika hiyo ipo (miezi) minne mitukufu[2]. Hiyo ndio Dini iliyo sawa. Basi msidhulumu nafsi zenu humo (ndani ya hiyo miezi minne kwa kufanya mambo yasiyomridhisha Allah). Na piganeni na washirikina (makafiri) wote kama wao wanavyopigana nanyi nyote. Na jueni kuwa Allah yupo pamoja na wenye takwa (uchaMungu)


1- - Hiki ni kitabu kiitwacho Allauhul-Mahfuudh na kinachotunza mambo yote. Kitabu hiki kimetajwa katika Aya ya 22 ya Sura Alburuuj (85).


2- - Miezi hiyo mine mitukufu ni Dhul-qa’adah (Mfungopili), Dhul-hijja (Mfungotatu), Muharram (Mfungonne) na Rajabu (mfungokumi).


Surah: YUNUS 

Ayah : 61

وَمَا تَكُونُ فِي شَأۡنٖ وَمَا تَتۡلُواْ مِنۡهُ مِن قُرۡءَانٖ وَلَا تَعۡمَلُونَ مِنۡ عَمَلٍ إِلَّا كُنَّا عَلَيۡكُمۡ شُهُودًا إِذۡ تُفِيضُونَ فِيهِۚ وَمَا يَعۡزُبُ عَن رَّبِّكَ مِن مِّثۡقَالِ ذَرَّةٖ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا فِي ٱلسَّمَآءِ وَلَآ أَصۡغَرَ مِن ذَٰلِكَ وَلَآ أَكۡبَرَ إِلَّا فِي كِتَٰبٖ مُّبِينٍ

Na huwi katika jambo lolote na husomi chochote katika Qur’ani na hamtendi kitendo chochote isipokuwa kwamba tumekuwa mashahidi kwenu mnapokiendea (mnapofanya). Na haujifichi kwa Mola wako Mlezi uzito wa chembe ndogo ardhini wala mbinguni na hata kidogo zaidi ya hicho au kikubwa isipokuwa kipo katika kitabu chenye kuweka wazi (kila kitu)



Surah: HUUD 

Ayah : 6

۞وَمَا مِن دَآبَّةٖ فِي ٱلۡأَرۡضِ إِلَّا عَلَى ٱللَّهِ رِزۡقُهَا وَيَعۡلَمُ مُسۡتَقَرَّهَا وَمُسۡتَوۡدَعَهَاۚ كُلّٞ فِي كِتَٰبٖ مُّبِينٖ

Na hakuna chochote kitem-beacho ardhini ispokuwa rizki yake ni kwa Allah pekee, na anayajua makazi yake (hapa duniani na baada ya kufa kwake) na sehemu atakapokufa. Hayo yote yapo katika kitabu kinacho bainisha



Surah: AR-RA’D 

Ayah : 39

يَمۡحُواْ ٱللَّهُ مَا يَشَآءُ وَيُثۡبِتُۖ وَعِندَهُۥٓ أُمُّ ٱلۡكِتَٰبِ

Allah hufuta na huthibitisha ayatakayo (katika hukumu zake). Na asili ya hukumu zote ipo kwake



Surah: AL-ISRAA 

Ayah : 58

وَإِن مِّن قَرۡيَةٍ إِلَّا نَحۡنُ مُهۡلِكُوهَا قَبۡلَ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ أَوۡ مُعَذِّبُوهَا عَذَابٗا شَدِيدٗاۚ كَانَ ذَٰلِكَ فِي ٱلۡكِتَٰبِ مَسۡطُورٗا

Na hapana mji wowote ila Sisi tutauteketeza kabla ya Siku ya Kiyama, au tutaupa adhabu kali. Haya yamekwisha andikwa katika Kitabu



Surah: AL-ANBIYAA 

Ayah : 105

وَلَقَدۡ كَتَبۡنَا فِي ٱلزَّبُورِ مِنۢ بَعۡدِ ٱلذِّكۡرِ أَنَّ ٱلۡأَرۡضَ يَرِثُهَا عِبَادِيَ ٱلصَّـٰلِحُونَ

Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya Kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema



Surah: AL-HAJJ 

Ayah : 70

أَلَمۡ تَعۡلَمۡ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا فِي ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِۚ إِنَّ ذَٰلِكَ فِي كِتَٰبٍۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٞ

Je! Hujui kwamba Allah ana-yajua yaliomo mbinguni na katika ardhi? Hakika hayo yamo Kitabuni. Hakika hayo kwa Allah ni mepesi



Surah: ANNAMLI 

Ayah : 75

وَمَا مِنۡ غَآئِبَةٖ فِي ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ إِلَّا فِي كِتَٰبٖ مُّبِينٍ

Na hakuna siri katika mbingu na ardhi ila imo katika Kitabu kinacho bainisha



Surah: AL-AHZAAB 

Ayah : 6

ٱلنَّبِيُّ أَوۡلَىٰ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ مِنۡ أَنفُسِهِمۡۖ وَأَزۡوَٰجُهُۥٓ أُمَّهَٰتُهُمۡۗ وَأُوْلُواْ ٱلۡأَرۡحَامِ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلَىٰ بِبَعۡضٖ فِي كِتَٰبِ ٱللَّهِ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُهَٰجِرِينَ إِلَّآ أَن تَفۡعَلُوٓاْ إِلَىٰٓ أَوۡلِيَآئِكُم مَّعۡرُوفٗاۚ كَانَ ذَٰلِكَ فِي ٱلۡكِتَٰبِ مَسۡطُورٗا

Nabii ni bora zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao. Na wake zake ni mama zao. Na jamaa ni karibu wao kwa wao katika Kitabu cha Allah kuliko Waumini wengine na Wahamiaji. Ila muwe mnawafanyia wema marafiki zenu. Haya yamekwisha andikwa Kitabuni



Surah: SABAA 

Ayah : 3

وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَا تَأۡتِينَا ٱلسَّاعَةُۖ قُلۡ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتَأۡتِيَنَّكُمۡ عَٰلِمِ ٱلۡغَيۡبِۖ لَا يَعۡزُبُ عَنۡهُ مِثۡقَالُ ذَرَّةٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَلَا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَآ أَصۡغَرُ مِن ذَٰلِكَ وَلَآ أَكۡبَرُ إِلَّا فِي كِتَٰبٖ مُّبِينٖ

Na walisema walio kufuru: Haitatufikia Saa (ya Kiyama). Sema: Kwani? Hapana shaka itakufikieni, naapa kwa haki ya Mola wangu Mlezi, Mwenye kujua ya ghaibu! Hapana kinacho fichikana kwake hata chenye uzito wa chembe tu, si katika mbingu wala katika ardhi, wala kilicho kidogo kuliko hivyo, wala kikubwa zaidi; ila vyote hivyo vimo katika Kitabu chake chenye kubainisha



Surah: FAATWIR 

Ayah : 11

وَٱللَّهُ خَلَقَكُم مِّن تُرَابٖ ثُمَّ مِن نُّطۡفَةٖ ثُمَّ جَعَلَكُمۡ أَزۡوَٰجٗاۚ وَمَا تَحۡمِلُ مِنۡ أُنثَىٰ وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلۡمِهِۦۚ وَمَا يُعَمَّرُ مِن مُّعَمَّرٖ وَلَا يُنقَصُ مِنۡ عُمُرِهِۦٓ إِلَّا فِي كِتَٰبٍۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٞ

Na Allah amekuumbeni kutokana na udongo. Kisha kwa tone la manii. Kisha akakufanyeni mwanamume na mwanamke. Na mwanamke yeyote hachukui mimba, wala hazai, ila kwa elimu yake.(Allah) Na wala hapewi umri mwenye umri mrefu, wala hapunguziwi katika umri wake, ila yamo hayo katika Kitabu. Hakika hayo ni mepesi kwa Allah



Surah: AZZUKHRUF 

Ayah : 4

وَإِنَّهُۥ فِيٓ أُمِّ ٱلۡكِتَٰبِ لَدَيۡنَا لَعَلِيٌّ حَكِيمٌ

Na hakika kitabu hicho katika Kitabu Mama kilichopo kwetu, kwa yakini kabisa, ni kitukufu, chenye hekima nyingi



Surah: QAAF 

Ayah : 4

قَدۡ عَلِمۡنَا مَا تَنقُصُ ٱلۡأَرۡضُ مِنۡهُمۡۖ وَعِندَنَا كِتَٰبٌ حَفِيظُۢ

Hakika, sisi tumejua kila ambacho ardhi inakipunguza kwao[1] na tunacho Kitabu kinachohifadhi barabara


1- - Kinachokusudiwa hap ani kwamba, kwa Allah hakipotei kitu. Pamoja na kwamba, makafifiri katika Aya iliyopita kabla ya hii wanaona kwamba wakifa na kuzikwa miili yao inaoza ardhini na kwamba si jambo linalowezekana kurejea tena kwenye hali yao ya zamani, Allah anasema hilo kwake ni jepesi na hakuna kitakachopotea.


Surah: ATTUR 

Ayah : 2

وَكِتَٰبٖ مَّسۡطُورٖ

Na kwa kitabu kilichoandikwa



Surah: AL-WAAQIA’H 

Ayah : 78

فِي كِتَٰبٖ مَّكۡنُونٖ

Katika Kitabu kilichohifadhiwa



Surah: AL-HADIID

Ayah : 22

مَآ أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٖ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا فِيٓ أَنفُسِكُمۡ إِلَّا فِي كِتَٰبٖ مِّن قَبۡلِ أَن نَّبۡرَأَهَآۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٞ

Hautokei msiba wowote katika ardhi au katika nafsi zenu isipokuwa umo katika Kitabu kabla hatuja utokezesha (hatujauumba). Hakika hayo kwa Allah ni mepesi



Surah: AL-BURUJI 

Ayah : 22

فِي لَوۡحٖ مَّحۡفُوظِۭ

Katika Ubao Ulio Hifadhiwa