وَإِذۡ نَجَّيۡنَٰكُم مِّنۡ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ يَسُومُونَكُمۡ سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِ يُذَبِّحُونَ أَبۡنَآءَكُمۡ وَيَسۡتَحۡيُونَ نِسَآءَكُمۡۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَآءٞ مِّن رَّبِّكُمۡ عَظِيمٞ
Na (kumbukeni) tulipokuokoeni kutoka kwenye mateso ya Firauni na watu wake waliokupeni adhabu mbaya kabisa; wakiwauwa watoto wenu wanaume kwa kuwachinjachinja na wakiwaacha hai watoto wenu wanawake. Na katika hayo kuna mtihani mkubwa sana kwenu kutoka kwa Mola wenu
وَإِذۡ فَرَقۡنَا بِكُمُ ٱلۡبَحۡرَ فَأَنجَيۡنَٰكُمۡ وَأَغۡرَقۡنَآ ءَالَ فِرۡعَوۡنَ وَأَنتُمۡ تَنظُرُونَ
Na (kumbukeni) tulipokut-enganishieni bahari tukakuokoeni na tukawazamisha watu wa Firauni na nyinyi mkitazama
ثُمَّ بَعَثۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِم مُّوسَىٰ بِـَٔايَٰتِنَآ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦ فَظَلَمُواْ بِهَاۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُفۡسِدِينَ
Kisha tulimtuma Musa kwa Aya zetu baada yao, aende kwa Firauni na kundi lake la mamwinyi, basi wakazidhulumu (wakazipinga) Aya hizo. Basi ona namna ulivyokuwa mwisho wa waharibifu
وَقَالَ مُوسَىٰ يَٰفِرۡعَوۡنُ إِنِّي رَسُولٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Na Musa akasema: Ewe Firauni, hakika mimi ni Mtume kutoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote
حَقِيقٌ عَلَىٰٓ أَن لَّآ أَقُولَ عَلَى ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡحَقَّۚ قَدۡ جِئۡتُكُم بِبَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّكُمۡ فَأَرۡسِلۡ مَعِيَ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ
Ni haki kwangu kutomsemea Allah ila lile la haki tu. Hakika, nimekujieni na hoja za wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi (zinazothibitisha ukweli wangu). Basi waachie Wana wa Israili (wawe huru) wawe pamoja na mimi (kwenda kwenye mji wa baba zao)
قَالَ إِن كُنتَ جِئۡتَ بِـَٔايَةٖ فَأۡتِ بِهَآ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ
(Firauni) Akasema: Kama umekuja na hoja basi ilete kama wewe ni miongoni mwa wasemao kweli
فَأَلۡقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعۡبَانٞ مُّبِينٞ
Basi (Musa) akaitupa chini fimbo yake na ghafla ikawa nyoka wa dhahiri
وَنَزَعَ يَدَهُۥ فَإِذَا هِيَ بَيۡضَآءُ لِلنَّـٰظِرِينَ
Na akautoa kwa nguvu mkono wake (kutoka katika nguo yake) na ghafla ukawa mweupe kwa wanaotazama
قَالَ ٱلۡمَلَأُ مِن قَوۡمِ فِرۡعَوۡنَ إِنَّ هَٰذَا لَسَٰحِرٌ عَلِيمٞ
Mamwinyi katika watu wa Firauni wakasema: Hakika, huyu ni mchawi mjuzi sana
يُرِيدُ أَن يُخۡرِجَكُم مِّنۡ أَرۡضِكُمۡۖ فَمَاذَا تَأۡمُرُونَ
Anataka kukutoeni katika ardhi (nchi) yenu (kwa uchawi wake). Basi mnaniamuru (mnanishauri nifanye) nini?
قَالُوٓاْ أَرۡجِهۡ وَأَخَاهُ وَأَرۡسِلۡ فِي ٱلۡمَدَآئِنِ حَٰشِرِينَ
Wakasema: Mpe muda yeye (Musa) na ndugu yake na tuma katika miji yote (watu) watakaofanya kazi ya kukusanya (wachawi)
يَأۡتُوكَ بِكُلِّ سَٰحِرٍ عَلِيمٖ
Wakuletee kila mchawi mahiri sana
وَجَآءَ ٱلسَّحَرَةُ فِرۡعَوۡنَ قَالُوٓاْ إِنَّ لَنَا لَأَجۡرًا إِن كُنَّا نَحۡنُ ٱلۡغَٰلِبِينَ
Na wachawi walikuja kwa Firauni wakasema: Hivi sisi tutalipwa endapo tutashinda?
قَالَ نَعَمۡ وَإِنَّكُمۡ لَمِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ
(Firauni) Akasema: Ndio, na kwa hakika kabisa, nyinyi mtakuwa miongoni mwa watu wangu wa karibu sana
قَالُواْ يَٰمُوسَىٰٓ إِمَّآ أَن تُلۡقِيَ وَإِمَّآ أَن نَّكُونَ نَحۡنُ ٱلۡمُلۡقِينَ
(Wachawi) Wakasema: Ewe Musa, ama tupa (toa wewe uchawi wako) au sisi tuwe wa mwanzo kutupa (kutoa)
قَالَ أَلۡقُواْۖ فَلَمَّآ أَلۡقَوۡاْ سَحَرُوٓاْ أَعۡيُنَ ٱلنَّاسِ وَٱسۡتَرۡهَبُوهُمۡ وَجَآءُو بِسِحۡرٍ عَظِيمٖ
(Musa) Akasema: Tupeni (Toeni). (Wachawi) Walipotupa (walipotoa uchawi wao) waliyaroga macho ya watu na waliwatisha na walikuja na uchawi mkubwa sana!
۞وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنۡ أَلۡقِ عَصَاكَۖ فَإِذَا هِيَ تَلۡقَفُ مَا يَأۡفِكُونَ
Na tulimfunulia Musa Wahyi kwamba: Tupa fimbo yako, na ghafla ikawa inameza vyote wanavyovizusha
فَوَقَعَ ٱلۡحَقُّ وَبَطَلَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Basi haki ikathibiti na vikabatilika vyote walivyokuwa wanafanya
فَغُلِبُواْ هُنَالِكَ وَٱنقَلَبُواْ صَٰغِرِينَ
Basi (wachawi) hapo wakashindwa na wakabadilika wakawa wanyonge!
وَأُلۡقِيَ ٱلسَّحَرَةُ سَٰجِدِينَ
Na wachawi wakaporomoka chini kumsujudia (Allah)
قَالُوٓاْ ءَامَنَّا بِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Wakasema: Tumeamuamini Mola Mlezi wa walimwengu wote
رَبِّ مُوسَىٰ وَهَٰرُونَ
Mola Mlezi wa Musa na Haruna
قَالَ فِرۡعَوۡنُ ءَامَنتُم بِهِۦ قَبۡلَ أَنۡ ءَاذَنَ لَكُمۡۖ إِنَّ هَٰذَا لَمَكۡرٞ مَّكَرۡتُمُوهُ فِي ٱلۡمَدِينَةِ لِتُخۡرِجُواْ مِنۡهَآ أَهۡلَهَاۖ فَسَوۡفَ تَعۡلَمُونَ
Firauni akasema: Hivi mmemuamini kabla mimi sijakupeni idhini? Kwa hakika kabisa, hii ni njama mliyoipanga mjini ili muwatoe humo watu wake. Basi mtatambua (nitakachokufanyeni)!
لَأُقَطِّعَنَّ أَيۡدِيَكُمۡ وَأَرۡجُلَكُم مِّنۡ خِلَٰفٖ ثُمَّ لَأُصَلِّبَنَّكُمۡ أَجۡمَعِينَ
Kwa hakika kabisa, nitaikatakata mikono yenu na miguu yenu kwa kupishanisha, kisha nitakutundikeni misalabani nyote
قَالُوٓاْ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ
Wakasema: Hakika, sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi
وَمَا تَنقِمُ مِنَّآ إِلَّآ أَنۡ ءَامَنَّا بِـَٔايَٰتِ رَبِّنَا لَمَّا جَآءَتۡنَاۚ رَبَّنَآ أَفۡرِغۡ عَلَيۡنَا صَبۡرٗا وَتَوَفَّنَا مُسۡلِمِينَ
Na hakuna kosa linalopelekea ututese isipokuwa tu huku kuamini kwetu Aya za Mola wetu Mlezi zilipotufikia. (Ewe) Mola wetu Mlezi, tujaze subira na tufishe tukiwa Waislamu
وَقَالَ ٱلۡمَلَأُ مِن قَوۡمِ فِرۡعَوۡنَ أَتَذَرُ مُوسَىٰ وَقَوۡمَهُۥ لِيُفۡسِدُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَيَذَرَكَ وَءَالِهَتَكَۚ قَالَ سَنُقَتِّلُ أَبۡنَآءَهُمۡ وَنَسۡتَحۡيِۦ نِسَآءَهُمۡ وَإِنَّا فَوۡقَهُمۡ قَٰهِرُونَ
Na mamwinyi katika watu wa Firauni wakasema (kumwambia Firauni): Hivi unamuacha Musa na watu wake wafanye uharibifu katika ardhi (nchi yetu) na akuache wewe na Miungu yako? (Firauni) Akasema: Tutawaua vibaya watoto wao wanaume na tutawaacha hai watoto wao wanawake, nasi tuna uwezo mkubwa wa kuwashinda!
قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِ ٱسۡتَعِينُواْ بِٱللَّهِ وَٱصۡبِرُوٓاْۖ إِنَّ ٱلۡأَرۡضَ لِلَّهِ يُورِثُهَا مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦۖ وَٱلۡعَٰقِبَةُ لِلۡمُتَّقِينَ
Musa akawaambia watu wake: Ombeni msaada kwa Allah na vumilieni[1]. Hakika, ardhi ni ya Allah tu anamrithisha amtakaye miongoni mwa waja wake. Na mwisho mwema ni wa wachaMungu tu
1- - Hapa kuna fundisho kwa Waislamu. Mtume Musa, kwa wakati huo, aliona udhaifu wa waumini na kutokuwa na maandalizi na uwezo wa kupambana. Kwa mantiki hiyo, hakuwashauri kuingia katika mapambano, lakini aliwaelekeza kuomba msaada kwa Allah na kuwa na Subira na uvumilivu na kuwaliwaza na pia kuwakumbusha ahadi ya Allah kuwa ushindi kwa waumini ni lazima pale Allah atakaporuhusu mazingira ya ushindi.
قَالُوٓاْ أُوذِينَا مِن قَبۡلِ أَن تَأۡتِيَنَا وَمِنۢ بَعۡدِ مَا جِئۡتَنَاۚ قَالَ عَسَىٰ رَبُّكُمۡ أَن يُهۡلِكَ عَدُوَّكُمۡ وَيَسۡتَخۡلِفَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرَ كَيۡفَ تَعۡمَلُونَ
Wakasema: Tumefanyiwa maudhi kabla ya wewe kutujia na baada ya kutujia. (Musa) Akasema: Huenda Mola wenu Mlezi akamuangamiza adui yenu na akakuwekeni nyinyi badala yao katika ardhi ili aangalie: Mtafanya nini?
وَلَقَدۡ أَخَذۡنَآ ءَالَ فِرۡعَوۡنَ بِٱلسِّنِينَ وَنَقۡصٖ مِّنَ ٱلثَّمَرَٰتِ لَعَلَّهُمۡ يَذَّكَّرُونَ
Na kwa hakika kabisa, tuliwashika (tuliwatia adabu) watu wa Firauni kwa miaka ya shida mbali mbali na upungufu wa matunda (vyakula) ili waonyeke