Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 8

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَقُولُ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَبِٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَمَا هُم بِمُؤۡمِنِينَ

Na miongoni mwa watu wapo wanaosema[1] kuwa: “Tumemuamini Allah na Siku ya Mwisho” na[2] sio waumini (wa kweli)


1- - Kwa maneno tu.


2- - Ukweli ni kwamba…


Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 9

يُخَٰدِعُونَ ٱللَّهَ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَمَا يَخۡدَعُونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمۡ وَمَا يَشۡعُرُونَ

Wanamhadaa Allah na wale walioamini. Na hawahadai isipokuwa nafsi zao tu na wao hawatambui



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 10

فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ فَزَادَهُمُ ٱللَّهُ مَرَضٗاۖ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمُۢ بِمَا كَانُواْ يَكۡذِبُونَ

Ndani ya nyoyo zao kuna ugonjwa, na Allah akawaongezea ugonjwa. Na wanastahiki adhabu kali kwa uongo waliokuwa wanaufanya



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 44

۞أَتَأۡمُرُونَ ٱلنَّاسَ بِٱلۡبِرِّ وَتَنسَوۡنَ أَنفُسَكُمۡ وَأَنتُمۡ تَتۡلُونَ ٱلۡكِتَٰبَۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ

Je, mnaamrisha watu kutenda wema na mnajisahau, na ilhali nyinyi mnakisoma kitabu? Je, hamtumii akili?



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 96

وَلَتَجِدَنَّهُمۡ أَحۡرَصَ ٱلنَّاسِ عَلَىٰ حَيَوٰةٖ وَمِنَ ٱلَّذِينَ أَشۡرَكُواْۚ يَوَدُّ أَحَدُهُمۡ لَوۡ يُعَمَّرُ أَلۡفَ سَنَةٖ وَمَا هُوَ بِمُزَحۡزِحِهِۦ مِنَ ٱلۡعَذَابِ أَن يُعَمَّرَۗ وَٱللَّهُ بَصِيرُۢ بِمَا يَعۡمَلُونَ

Na kwa hakika kabisa, utawakuta wao (Wayahudi) ndio wanaojali mno uhai[1] kuliko watu wote, na miongoni mwa washirikishaji (pia utakuta nao wako hivyo); anatamani mmoja wao angalau apewe umri wa miaka elfu moja. Na kupewa kwake umri mrefu hakutamuepushia adhabu, na Allah ni Mwenye kuyaona wanayoyatenda


1- - Katika maisha ya duniani


Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 118

وَقَالَ ٱلَّذِينَ لَا يَعۡلَمُونَ لَوۡلَا يُكَلِّمُنَا ٱللَّهُ أَوۡ تَأۡتِينَآ ءَايَةٞۗ كَذَٰلِكَ قَالَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِم مِّثۡلَ قَوۡلِهِمۡۘ تَشَٰبَهَتۡ قُلُوبُهُمۡۗ قَدۡ بَيَّنَّا ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يُوقِنُونَ

Na walisema wasiojua (kitu kwamba): Kwanini Allah asituambie wenyewe, au usitujie muujiza!? Kama hivyo walisema waliokuwa kabla yao mfano wa kauli yao hiyo. Zimefanana nyoyo zao. Hakika tumebainisha miujiza mbalimbali kwa watu wanaoamini



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 165

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ ٱللَّهِ أَندَادٗا يُحِبُّونَهُمۡ كَحُبِّ ٱللَّهِۖ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَشَدُّ حُبّٗا لِّلَّهِۗ وَلَوۡ يَرَى ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓاْ إِذۡ يَرَوۡنَ ٱلۡعَذَابَ أَنَّ ٱلۡقُوَّةَ لِلَّهِ جَمِيعٗا وَأَنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعَذَابِ

Na miongoni mwa watu kuna wanaofanya washirika badala ya (kumuamini) Allah (pekee); wanawapenda kama wampendavyo Allah. Na walioamini wanampenda zaidi Allah. Na laiti waliodhulumu wangejua watakapoiona adhabu kwamba, nguvu zote ni za Allah, na kwamba, Allah ni mkali wa kuadhibu[1]


1- - Wasingethubutu kumfanyia Allah washirika.


Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 200

فَإِذَا قَضَيۡتُم مَّنَٰسِكَكُمۡ فَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ كَذِكۡرِكُمۡ ءَابَآءَكُمۡ أَوۡ أَشَدَّ ذِكۡرٗاۗ فَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَقُولُ رَبَّنَآ ءَاتِنَا فِي ٱلدُّنۡيَا وَمَا لَهُۥ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ مِنۡ خَلَٰقٖ

Mtakapomaliza ibada zenu, basi mtajeni Allah, kama mnavyowataja baba zenu au zaidi. Na miongoni mwa watu wapo wanaosema: “Ewe Mola wetu tupe katika dunia, na hawatakuwa na fungu lolote Akhera



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 201

وَمِنۡهُم مَّن يَقُولُ رَبَّنَآ ءَاتِنَا فِي ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗ وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِ حَسَنَةٗ وَقِنَا عَذَابَ ٱلنَّارِ

Na baadhi yao wapo wanaosema: Ewe Mola wetu, tupe katika dunia wema, na Akhera wema na utukinge na adhabu ya Moto



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 204

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يُعۡجِبُكَ قَوۡلُهُۥ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَيُشۡهِدُ ٱللَّهَ عَلَىٰ مَا فِي قَلۡبِهِۦ وَهُوَ أَلَدُّ ٱلۡخِصَامِ

Na miongoni mwa watu wapo ambao zinakuvutia kauli zao katika maisha ya dunia, na wanamshuhudisha Allah juu ya yaliyo moyoni mwake hali yeye ni mpingaji mno



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 205

وَإِذَا تَوَلَّىٰ سَعَىٰ فِي ٱلۡأَرۡضِ لِيُفۡسِدَ فِيهَا وَيُهۡلِكَ ٱلۡحَرۡثَ وَٱلنَّسۡلَۚ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ ٱلۡفَسَادَ

Na anapoondoka (kwako) anahangaika huku na kule ardhini ili kufanya ufisadi humo na kuangamiza mimea na vizazi. Na Allah hapendi ufisadi



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 206

وَإِذَا قِيلَ لَهُ ٱتَّقِ ٱللَّهَ أَخَذَتۡهُ ٱلۡعِزَّةُ بِٱلۡإِثۡمِۚ فَحَسۡبُهُۥ جَهَنَّمُۖ وَلَبِئۡسَ ٱلۡمِهَادُ

Na wanapoambiwa; Muogopeni Allah hupandwa na mori wa kufanya uovu. Basi kitakachowatosha ni Jahanamu na ni makazi mabaya mno



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 207

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَشۡرِي نَفۡسَهُ ٱبۡتِغَآءَ مَرۡضَاتِ ٱللَّهِۚ وَٱللَّهُ رَءُوفُۢ بِٱلۡعِبَادِ

Na miongoni mwa watu wapo ambao huuza nafsi zao kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah na Allah ni Mpole sana kwa waja



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 273

لِلۡفُقَرَآءِ ٱلَّذِينَ أُحۡصِرُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ لَا يَسۡتَطِيعُونَ ضَرۡبٗا فِي ٱلۡأَرۡضِ يَحۡسَبُهُمُ ٱلۡجَاهِلُ أَغۡنِيَآءَ مِنَ ٱلتَّعَفُّفِ تَعۡرِفُهُم بِسِيمَٰهُمۡ لَا يَسۡـَٔلُونَ ٱلنَّاسَ إِلۡحَافٗاۗ وَمَا تُنفِقُواْ مِنۡ خَيۡرٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ بِهِۦ عَلِيمٌ

(Heri na sadaka hizo) Wapewe mafakiri waliofungwa katika njia ya Allah wasioweza kusafiri katika ardhi (kwa kujitafutia riziki), asiyewajua huwadhania ni wakwasi kwa kujizuia kuomba. Utawatambua kwa alama zao, hawawaombi watu kwa ung’ang’anizi. Na heri yoyote mnayoitoa, basi kwa hakika Allah anaijua sana



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 173

ٱلَّذِينَ قَالَ لَهُمُ ٱلنَّاسُ إِنَّ ٱلنَّاسَ قَدۡ جَمَعُواْ لَكُمۡ فَٱخۡشَوۡهُمۡ فَزَادَهُمۡ إِيمَٰنٗا وَقَالُواْ حَسۡبُنَا ٱللَّهُ وَنِعۡمَ ٱلۡوَكِيلُ

Ambao watu waliwaambia wao: hakika kundi la watu limekukusanyikieni basi waogopeni, hilo likawazidishia imani na wakasema: Allah anatutosha na ndiye mbora wa wenye kutegemewa



Surah: ANNISAI 

Ayah : 37

ٱلَّذِينَ يَبۡخَلُونَ وَيَأۡمُرُونَ ٱلنَّاسَ بِٱلۡبُخۡلِ وَيَكۡتُمُونَ مَآ ءَاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ مِن فَضۡلِهِۦۗ وَأَعۡتَدۡنَا لِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٗا مُّهِينٗا

Ambao wanaofanya ubahili na wanawaamuru watu wawe mabahili, na wanaficha fadhila alizowapa Allah. Na tumewaandalia makafiri adhabu inayodhalilisha



Surah: ANNISAI 

Ayah : 38

وَٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمۡوَٰلَهُمۡ رِئَآءَ ٱلنَّاسِ وَلَا يُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَلَا بِٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۗ وَمَن يَكُنِ ٱلشَّيۡطَٰنُ لَهُۥ قَرِينٗا فَسَآءَ قَرِينٗا

Na ambao wanatoa mali zao kwa kujionesha (na kujitangaza) kwa watu, na hawamuamini Allah na Siku ya Mwisho. Na yeyote atakayemfanya shetani kuwa rafiki yake, basi (ajue kuwa huyo ni) rafiki mbaya sana



Surah: ANNISAI 

Ayah : 108

يَسۡتَخۡفُونَ مِنَ ٱلنَّاسِ وَلَا يَسۡتَخۡفُونَ مِنَ ٱللَّهِ وَهُوَ مَعَهُمۡ إِذۡ يُبَيِّتُونَ مَا لَا يَرۡضَىٰ مِنَ ٱلۡقَوۡلِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِمَا يَعۡمَلُونَ مُحِيطًا

Wanajificha wasionekane na watu na wala hawamstahi Allah kuwaona (wanapofanya dhambi) ilhali yeye yuko pamoja nao wakati wanapopanga njama usiku za (kusema) kauli zisizoridhiwa (na Allah). Na Allah anayajua vilivyo yote wayafanyayo



Surah: AL-MAIDA 

Ayah : 82

۞لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ ٱلنَّاسِ عَدَٰوَةٗ لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱلۡيَهُودَ وَٱلَّذِينَ أَشۡرَكُواْۖ وَلَتَجِدَنَّ أَقۡرَبَهُم مَّوَدَّةٗ لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّا نَصَٰرَىٰۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّ مِنۡهُمۡ قِسِّيسِينَ وَرُهۡبَانٗا وَأَنَّهُمۡ لَا يَسۡتَكۡبِرُونَ

Hakika kabisa, utakuta watu walio na uadui mkubwa na Waislamu ni Wayahudi na washirikishaji (wanaomfanyia ushirika Allah). Na kwa hakika kabisa, utakuta (watu) walio karibu nao zaidi ni wale wanaosema: Sisi ni Wanaswara (Wakristo). Hayo ni kwasababu miongoni mwao wapo Makasisi na Watawa, na kwasababu wao hawafanyi kiburi (katika kuifuata haki)



Surah: AL-MAIDA 

Ayah : 83

وَإِذَا سَمِعُواْ مَآ أُنزِلَ إِلَى ٱلرَّسُولِ تَرَىٰٓ أَعۡيُنَهُمۡ تَفِيضُ مِنَ ٱلدَّمۡعِ مِمَّا عَرَفُواْ مِنَ ٱلۡحَقِّۖ يَقُولُونَ رَبَّنَآ ءَامَنَّا فَٱكۡتُبۡنَا مَعَ ٱلشَّـٰهِدِينَ

Na wanaposikia yaliyoteremshwa kwa Mtume utaona macho yao yanabubujika machozi kwasababu ya haki waliyoitambua. Wanasema: Ewe Mola wetu Mlezi, tumeamini; basi tuandike (tuwe) pamoja na wanaoshuhudia (Uungu wako, upekee wako na kuabudiwa kwako)



Surah: AL-MAIDA 

Ayah : 84

وَمَا لَنَا لَا نُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَمَا جَآءَنَا مِنَ ٱلۡحَقِّ وَنَطۡمَعُ أَن يُدۡخِلَنَا رَبُّنَا مَعَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلصَّـٰلِحِينَ

Na kwanini tusimuamini Allah na haki iliyotujia (Qur’an) Na hali tunatumai Mola wetu Mlezi atuingize pamoja na watu wema?



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 164

وَإِذۡ قَالَتۡ أُمَّةٞ مِّنۡهُمۡ لِمَ تَعِظُونَ قَوۡمًا ٱللَّهُ مُهۡلِكُهُمۡ أَوۡ مُعَذِّبُهُمۡ عَذَابٗا شَدِيدٗاۖ قَالُواْ مَعۡذِرَةً إِلَىٰ رَبِّكُمۡ وَلَعَلَّهُمۡ يَتَّقُونَ

Na (kumbuka) wakati kundi miongoni mwao liliposema (kwamba): Kwa nini mnawapa mawaidha watu ambao Allah ni Mwenye kuwaangamiza au kuwaadhibu adhabu kali? Walisema: (Tunawapa mawaidha) Ili uwe udhuru kwa Mola wenu na huwenda nao wakawa wachaMungu



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 6

وَإِنۡ أَحَدٞ مِّنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ ٱسۡتَجَارَكَ فَأَجِرۡهُ حَتَّىٰ يَسۡمَعَ كَلَٰمَ ٱللَّهِ ثُمَّ أَبۡلِغۡهُ مَأۡمَنَهُۥۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ قَوۡمٞ لَّا يَعۡلَمُونَ

Na iwapo yeyote katika washirikina (makafiri) wakikuomba ujirani (na ulinzi na amani kwenye himaya yako), basi mpe ujirani (ukae naye) ili apate kuyasikia maneno ya Allah. Kisha mfikishe mahali pake pa amani (sehemu atakayokuwa salama). Hiyo ni kwa kuwa hao ni watu wasiojua (Uislamu)



Surah: AL-ANBIYAA 

Ayah : 1

ٱقۡتَرَبَ لِلنَّاسِ حِسَابُهُمۡ وَهُمۡ فِي غَفۡلَةٖ مُّعۡرِضُونَ

Imewakaribikia watu hesabu yao, na ilihali wao wakiwa wameghafilika na kupuuza



Surah: AL-ANBIYAA 

Ayah : 2

مَا يَأۡتِيهِم مِّن ذِكۡرٖ مِّن رَّبِّهِم مُّحۡدَثٍ إِلَّا ٱسۡتَمَعُوهُ وَهُمۡ يَلۡعَبُونَ

Hayawafikii mawaidha mapya kutoka kwa Mola wao Mlezi ila huyasikiliza na huku wanafanya mchezo



Surah: AL-ANBIYAA 

Ayah : 3

لَاهِيَةٗ قُلُوبُهُمۡۗ وَأَسَرُّواْ ٱلنَّجۡوَى ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ هَلۡ هَٰذَآ إِلَّا بَشَرٞ مِّثۡلُكُمۡۖ أَفَتَأۡتُونَ ٱلسِّحۡرَ وَأَنتُمۡ تُبۡصِرُونَ

Zimeghafilika nyoyo zao. Na wale walio dhulumu hunong’onezana kwa siri: Ni nani ati huyu isipo kuwa ni binaadamu tu kama nyinyi! Mnauendea uchawi hali nanyi mnaona?



Surah: AL-HAJJ 

Ayah : 3

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يُجَٰدِلُ فِي ٱللَّهِ بِغَيۡرِ عِلۡمٖ وَيَتَّبِعُ كُلَّ شَيۡطَٰنٖ مَّرِيدٖ

Na miongoni mwa watu wapo wanao bishana juu ya Allah bila ya elimu, na wanamfuata kila shetani aliyeasi



Surah: AL-HAJJ 

Ayah : 8

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يُجَٰدِلُ فِي ٱللَّهِ بِغَيۡرِ عِلۡمٖ وَلَا هُدٗى وَلَا كِتَٰبٖ مُّنِيرٖ

Na katika watu wapo wanao bishana juu ya Allah bila ya elimu, wala uongofu, wala Kitabu chenye nuru



Surah: AL-HAJJ 

Ayah : 9

ثَانِيَ عِطۡفِهِۦ لِيُضِلَّ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِۖ لَهُۥ فِي ٱلدُّنۡيَا خِزۡيٞۖ وَنُذِيقُهُۥ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ عَذَابَ ٱلۡحَرِيقِ

Anaye geuza shingo yake ili kupoteza watu waache Njia ya Allah. Duniani atapata fedheha, na Siku ya Kiyama tutamwonjesha adhabu ya kuungua



Surah: AL-HAJJ 

Ayah : 11

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَعۡبُدُ ٱللَّهَ عَلَىٰ حَرۡفٖۖ فَإِنۡ أَصَابَهُۥ خَيۡرٌ ٱطۡمَأَنَّ بِهِۦۖ وَإِنۡ أَصَابَتۡهُ فِتۡنَةٌ ٱنقَلَبَ عَلَىٰ وَجۡهِهِۦ خَسِرَ ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةَۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡخُسۡرَانُ ٱلۡمُبِينُ

Na katika watu wapo wanao muabudu Allah kwa ukingoni. Ikimfikia kheri hutulia kwayo, na ukimfikia msukosuko hugeuza uso wake. Amepata hasara dunia na Akhera; hiyo ndiyo hasara iliyo wazi